Jengo la Mahakama ya Kazi (Picha) tufanyeje?

Vipi wale walemavu waishio kwenye nyumba za udongo?

kama ni nyumba zao nadhani wanazitengeneza wapendavyo, lakini kwenye public accommodation nadhani kuna haja ya kuhakikisha kunakuwa na minimum standard of constructing these places.
 
Haya majengo ni ya miaka mingi kabla haki za walemavu hazijapigiwa kelele na kuwekewa mikakati maalum.Hata hivyo bado wangeweza kuweka provision kuwajali walemavu.Majengo mengi mapya wanajitahidi kuwafikiria pia walemavu kwa kuwawekea ramp au lift n.k.

....No....kabla hiyo ofisi kufunguliwa hilo Jengo lilifanyiwa ukarafati (ukarabati) mkubwa........ni incompetence tu........
 
Vipi wale walemavu waishio kwenye nyumba za udongo?

Majengo ya udongo ya asili hayana kikwazo kwa mlemavu kwa vile hayana ngazi wala threshhold za kuitisha. Sakafu zake za kukandikwa ni nzuri kwa kutambaa na hazitunzi baridi kama zinavyofanya hizi sakafu zetu za kisasa za ceramic tiles! Nyumba za asili vitanda vyake kama vipo, vinakuwa katika urefu ambao mlemavu ni rahisi kufikia. Majiko ya mafiga ni rahisi kwa mlemavu kutumia kuliko haya majiko yetu ya kisasa ambayo yanamlazima aidha asimame au atumie gari la magurumu. Kata, mitugi, mbuzi za kukunia, vigoda vyote vinaweza kutumiwa kirahisi na mlemavu kuliko haya majokofu yetu na makabati ya juu ya jikoni!

Kwa msingi huyo, mlemavu anayeishi katika nyumba ya asilia ana afueni kuliko huyo anayeishi katika losheni ya kisasa! Mlemavu ninaye mzungumzia ni yule wa miguu.
 
Watu wa kulaumiwa hapa ni ma'architecture' (samahani MKJJ, wahandisi nafasi yao ni ndogo sana katika hii ishu hususan tukiangalia majengo). Wao ndio wanaobuni na kudesign majengo na inawabidi wafikirie watumiaji wote ( walemavu wa miguu, vipofu, viziwi, mama waja wazito, watu wa makamu, watoto wadogo n.k.) Hili mara nyingi hawafanyi. Pamoja na hao ni manispaa na vyombo vya serikali vinavyotoa vibali vya ujenzi. Hawa wanapaswa kushinikiza hadi regulations zinazotumika zibadilishwe na kuingiza kipengele cha accessibility kwa jamii nzima kwenye public buildings ( si ya serikali peke yake)

I stand to be corrected, lakini ninavyofahamu mimi building regulations tunazozitumia ni zile tulizorithi kutoka kwa waingereza na kuzitia vilaka. Sidhani kama moja ya kilaka kinahusu accessibility kwa watu wote! Ramp kama zinawekwa ni kama mawazo ya baadae lakini ni mara chache sana kupewa uzito tokeahatua za mwanzo. Ni majengo mangapi ya public ( ya serikali, bar, hoteli, kumbi za mikutano, vituo vya reli, vituo vya mabasi, airport, makanisa, misikiti n.k) vyenye vyoo kwa ajili ya walemavu? Ukweli ni kwamba hatuwajali na tunawaona ni kero.

Huyo muungwana aliyesimama kushoto unaweza kukuta ni wakili wa huyo mlemavu na anaona anamchelewesha!

Tuna safari ndefu lakini......Amandla.................!
 
Mambo ni mabaya zaidi kwenye majengo ya mahakama za mwanzo vijijini, majengo ya shule za msingi, nyumba za walimu,....NSSF wamekazania kujenga maghorofa na kuyapa majina ya akina Mkapa!
 
Serikali yetu ni very reactive... inangoja shida au maafa yatokee ndipo wajifanye wanachukua hatua... mifano michache ni hii:
1.Mgonjwa wa akili kuua wagonjwa wenzake Muhimbili
2.Kuunda tume kuchunguza maafa ya watoto kule Tabora
3.Kuwasimamisha Trafiki waliopokea Rushwa kwa kupigwa picha ya TV wakati kila siku Trafiki Rushwa ni kwenda mbele
4.Kuunda tume kuchunguza jengo lililoanguka pale Kisutu, wakati lilikuwa katika hali ya hasara kwa muda mrefu tu...

Yaani hakuna proactive programs zozote zinazofanywa ili kujitoa katika matatizo yatakayotokea baadaye. Usingizi ni mzito kwakweli!
 
Like a typical pauper, we are maintaining our governmental abodes poorly while flashing the dignitaries in the ever depreciating overpriced ecologicaly profane if fancy gas-guzzlers!

Picturing a judge embarking from a VX into this sorry excuse for a government building, a judiciary palace nonetheless, fills me with contempt of the despicable squalor, booth mental and physical.

Duh,......Mkuu Pundit naweeeeee!!
 
Majengo ya udongo ya asili hayana kikwazo kwa mlemavu kwa vile hayana ngazi wala threshhold za kuitisha. Sakafu zake za kukandikwa ni nzuri kwa kutambaa na hazitunzi baridi kama zinavyofanya hizi sakafu zetu za kisasa za ceramic tiles! Nyumba za asili vitanda vyake kama vipo, vinakuwa katika urefu ambao mlemavu ni rahisi kufikia. Majiko ya mafiga ni rahisi kwa mlemavu kutumia kuliko haya majiko yetu ya kisasa ambayo yanamlazima aidha asimame au atumie gari la magurumu. Kata, mitugi, mbuzi za kukunia, vigoda vyote vinaweza kutumiwa kirahisi na mlemavu kuliko haya majokofu yetu na makabati ya juu ya jikoni!

Kwa msingi huyo, mlemavu anayeishi katika nyumba ya asilia ana afueni kuliko huyo anayeishi katika losheni ya kisasa! Mlemavu ninaye mzungumzia ni yule wa miguu.

Sasa kwa nini tusiendelee kujenga majengo hayo ya "asilia"? Kwa sababu kwa maelezo yako hapo juu majengo hayo "asilia" yana accomodate vizuri tu hao walemavu....
 
kama ni nyumba zao nadhani wanazitengeneza wapendavyo, lakini kwenye public accommodation nadhani kuna haja ya kuhakikisha kunakuwa na minimum standard of constructing these places.

Sidhani kama wanazitengeneza 'wapendavyo'. Ni kwamba hawana uwezo wa kujenga/kutengeneza zile za 'kisasa'.
 
Sasa kwa nini tusiendelee kujenga majengo hayo ya "asilia"? Kwa sababu kwa maelezo yako hapo juu majengo hayo "asilia" yana accomodate vizuri tu hao walemavu....

Jamii si walemavu peke yao. na majengo haya yana mapungufu mengine ( ventilation, hatari ya moto n.k.) ambayo hayaendane na mazingira ya sasa hasa kwenye miji. Majengo haya asilia yanahitaji sehemu kubwa kwa sabau kila matumizi yana jengo lake, choo jengo lake, jiko jengo lake, kila mke jengo lake n.k. ni vigumu kupata nafasi kama hii katika miji yetu. Maisha yetu ya wakati yanahitaji vile vile majengo yanayoweza kuchukua watu wengi kwa pamoja,k.m. maofisi, stadium za michezo, sehemu za burudani, n.k. vitu ambavyo hizi nyumba zetu asilia haziwezi kumudu. Lakini kama una kashamba kako mahali, nakushauri ungeangalia upya namna waliotangulia walivyokuwa wakijenga. Utajifunza mengi kama utaondoa bias tuliyowekewa kuwa kila kitu asilia ni primitive.
 
serkali yetu haiko makini. they didn't consider walemavu during designing and building a lot of majengos in town. hata mahakam kuu ni hivyohivyo
 
serkali yetu haiko makini. they didn't consider walemavu ...

Sio serikali peke yake. Na wengine wote tunafanya hayo hayo. Hapa mlemavu ana nafasi kweli ?

5-2.jpg
 
this is jus sad sad indeed. itz funny cause nowadays tanzania has a lot of architects who had studied abroad where handicap accesibility codes are strictly followed and adhered to. in tanzania accesibility and safety codes hazifatiliwi kabisa. buildings have no handicap ramps or lifts; no handicap toilets/bathrooms; mojority of bldg corridors can't be accesible by handicap in a wheelchair; no handicap parking etc.

itz really sad to see the architectural profession doesn't take into consideration the well being of handicaps and all they think is aesthetic aspect of buildings and their commissions forgeting about the conscience part of architecture.
 
Vipi wale walemavu waishio kwenye nyumba za udongo?

kwenye nyumba ya udongo (adobe mud houses) mlemavu ana-access to all corners of the house. therz no starcase to climb to etc. also, if one belives on sustainable architecture one can see that a mud house is one of the best piece of architecture ever seen. its wide use can be attributed to its simplicity of design and make, and the cheapness thereby in creating it. adobe structures are extremely durable and account for the oldest extant buildings on the planet. in hot climates, compared to wooden buildings or cmu brick, adobe buildings offer significant advantages due to their greater thermal mass.
 
Back
Top Bottom