Elections 2010 Jengo la Machinga ni hatari kwa binadamu: Wakaguzi

Mi niko tofauti kidogo na hili! Kuhusu Machinga complex, tumechelewa sana tena sana maana hizi zinatakiwa kama ishirini kwa Dar pekee yake ili kuboost uchumi.

erikali inatakiwa ibuni vyanzo vya mapato ikiwemo miradi kama hii, nimeenda Indonesia mwaka jana jiji moja linaitwa Surabaya kuna sehemu kama hizi yaani safi zina bei nzuri wafanyabiashara wanalipa kodi zao vizuri, Mamantilie wanasehemu zao nzuri, hakuna tatizo zikiwemo nyingi za kutosha, chukulia pale mwenge ziwepo, Buguruni, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi, Tabata zitatutoa kwenye uchumu tegemezi, bajeti tegemezi. Inakuwa fujo mtu kuanza safari ya kwenda kariakoo. Hata wakulima watakuwa wanasehemu maalumu za kuuza vitu vyao sio kama sasa.

Mtu akienda kule analake jambo.

Sema viongozi wetu wanatamaa, wanataka kila kitu wawepo wao na 10% ndo kabisa. Tatizo kubwa ni usimamizi na hizi tamaa za viongozi.
 
Boss naomba nitofautiane na wewe kuhusiana na Machinga complex.

Mfumo wa biashara huwa una chain ndefu saaana kutokea kwa manufacturer mpaka kwa mteja mwenyewe. Na chain hiyo mara nyingi hutegema aina bidhaa.

Pia kumbuka Machinga Complex imekuja kwa lengo la kurasimisha mfumo wa biashara za mitumbo na wakati huohuo kuhakikisha mpangilio wa jiji unakuwa sasa. Kwahiyo nadhani tuipime machinga kwa malengo haya, je yanafikiwa au yatafikiwa?

Ila kwa ujumla si potevu wa fedha tena kama zimetumika ipasavya.

Unaweza ukawa na point nzuri... lakini kumbuka wateja wa wauza biashara ndogondogo ni impulse shopppers na siyo watu wanaopangilia kwenda kununua vitu hivyo hadi wafunge safari kufuata vitu fulani machinga complex. Pia kumbuka kero ya foleni za Dar, nani atapoteza muda kwenda huko?

Kama alivyosema Boss, hata mimi namuunga mkono kuwa mradi mzima haukupangwa kwa kufanyiwa tathmini/ feasibility study ya uhakika - kama ilifanyika basi kwa maoni yangu ilifanyika kama prcedure tu lakini sidhani kama ilionyesha kuleta tija mwisho wa siku.Halafu ukiangalia hata mpangilio wa hivyo viota humo ndani ni maajabu maana ni vidogo mno.

Nimewahi kuona similar complexes Bangkok na Indonesia. Huko ndio ni jengo kubwa sana kwa wafanya biashara hasa za traditional wear, crafts nk. Maana yake ni kuwa mtu ukihitaji mavazi au crafts badi unajua where to go. Sasa hili la machinga complex yetu naliona liki fail hata kabla ya kuanza!
 
Hii machinga complex iko sehemu gani? au mnamaanisha lile jengo pale karume stadium limenjengewa fences huko ndani kama banda la kufugia kuku?
 
kwanza, waliopata nafasi sio hao wamachinga waliokusudiwa. pengine tulipe jina jingine, lakini sio machinga complex.
 
kwanza, waliopata nafasi sio hao wamachinga waliokusudiwa. pengine tulipe jina jingine, lakini sio machinga complex.

Hivi hao machinga kweli waliamini kuwa wataona ndani kwenye jengo hili?! Lakini wakumbuke kuwa amnyimae punda adesi...... Tuliyaona soko la Makumbusho. Yatajirudia tena kwenye hili jengo.

Amandla.....
 
Unaweza ukawa na point nzuri... lakini kumbuka wateja wa wauza biashara ndogondogo ni impulse shopppers na siyo watu wanaopangilia kwenda kununua vitu hivyo hadi wafunge safari kufuata vitu fulani machinga complex. Pia kumbuka kero ya foleni za Dar, nani atapoteza muda kwenda huko?

Kama alivyosema Boss, hata mimi namuunga mkono kuwa mradi mzima haukupangwa kwa kufanyiwa tathmini/ feasibility study ya uhakika - kama ilifanyika basi kwa maoni yangu ilifanyika kama prcedure tu lakini sidhani kama ilionyesha kuleta tija mwisho wa siku.Halafu ukiangalia hata mpangilio wa hivyo viota humo ndani ni maajabu maana ni vidogo mno.

Nimewahi kuona similar complexes Bangkok na Indonesia. Huko ndio ni jengo kubwa sana kwa wafanya biashara hasa za traditional wear, crafts nk. Maana yake ni kuwa mtu ukihitaji mavazi au crafts badi unajua where to go. Sasa hili la machinga complex yetu naliona liki fail hata kabla ya kuanza!
WoS, binafsi naamini tathmini yakinifu ilifanyika juu ya Machinga Complex na kwahilo km usimamizi utakuwa ni bora, basi hayo ni miongoni mwa mafanikio ya serikali. Km utakumbuka vyema, Machinga Complex ni mradi wa kwanza lakini malengo ni kuwa na mradi kama huo katika kila Wilaya. Pia si kweli kuwa wanaonunua ni wale wapita njia. Sina hakika ya sample yako lakini binafsi nafaham watu wengi ambao hutenga siku kabisa kwa ajili ya kwenda kutafuta vivazi huko. Kwamaana nyingine hizo pia ni km Malls nyingine kwa baadhi ya class katika jamii yetu.
Dhana ya kuhamisha ingezua lawama zaidi kuliko uhalisia wa sasa hivi. Hawa wauzaji wanapatikana sehem ambayo kuna wateja na kama hakuna wateja nao huondoka. Kuna ushahidi mwingi wa kutosha ni namna gani baadhi ya masoko hayajafanikiwa kwa sababu hayafikiwi na wateja. Suala la foleni ni la kimiundombinu zaidi.
 
tUKO PAMOJA MKUU!
Ila hapo kwenye bold..huoni miradi yetu mingi ina shindwa kwa sababu hakuna miundo mbinu ku support dhana au intervention? Huoni kama kukosekana infrastructural support by itself is poor planning of most of our projects?

Ukiniambia niende machinga complex Ilala siku ya jumamosi ati kwamba ni Mall concept, walahi sitakanyaga huko hata kwa kiboko.Kama concept ilikuwa hiyo na siyo afterthought, kwanini basi hawakujenga nje kidogo ya jiji?Feasibility ilifanyika to this effect?
 
Monday, 18 October 2010 07:53

bkikwete.jpg
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Kikwete, akinyoosha kadi ya chama hicho tayari kumkabidhi aliyekuwa mbunge wa chama cha CUF jimbo la Chakechake Pemba, Fatma Magimbi, aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi. Picha na Silvan Kiwale

Hussein Issa
MGOMBEA urais wa CCM, Jakaya Kikwete jana alihamishia kampeni zake jijini Dar es salaam ambako aliahidi kuwajengea wafanyabiashara ndogondogo majengo ya kufanyia shughuli zao kwenye wilaya zote, huku akiahidin chanjo ya saratani kwa wanawake.Tayari wafanyabiashara hao wameshajengewa jengo kubwa la ghorofa pacha linaloitwa Machinga Complex ambalo liko Mtaa wa Lindi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo ambao wameshaanza kulitumia, ingawa biashara bado haijapamba moto.
Akihutubia mkutano wa hadhara jana jijini Dar es salaam, Kikwete alisema wamachinga wataendelea kupata neema kwa kuwa atawajengea majengo mengine kama hilo lililo eneo la Karume ambalo ni kwa ajili ya wilaya.
“Hii ni ahadi yangu naitoa tena na tena... tayari tumeshapata wafadhili kutoka China ambao watatoa Sh100 bilioni za kujengea majengo hayo na kila wilaya, tutayajenga mawili,” alisema Kikwete.
Kikwete alitaja maeneo ambayo yatajengwa majengo hayo kuwa ni eneo la soko la Buguruni kwa ajili ya jengo jingine la wilayani Ilala, Tazara na eneo la Temeke Stereo kwa ajili ya wilaya ya Temeke wakati wilayani Kinondoni majengo hayo yatajengwa maeneo ya Magomeni Kondoa na Mbezi Luis, akibainisha kuwa kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 7,000.
Kwa kuangalia uywezo wa mejngo hayo matano na lile la Mtaa wa Lindi, majengo yote yataweza kuchukua wafanyabiashara 35,000 kwa wakati mmoja.
Tayari Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilishasema kuwa majengo hayo yako kwenye mpango wake na kwamba lilikuwa linasubiri maombi kutoka halmashauri za wilaya za Dar es salaam ili lipate baraka za kuendelea na mradi huo.
Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili ya miaka mitano, pia aliahidi kusimamia ugawaji wa maeneo hayo ya biashara mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa majengo hayo akitaka kudhibiti ubabaishaji ambao ulijitokeza kwenye jengo la Machinga Complex.
Kikwete alisema kwamba katika ugawaji wa maeneo kwenye jengo la Machinga, watu wasio na sifa walipewa nafasi kutokana na kuwa na undugu ama urafiki na wagawaji.
“Ndiyo maana ugawaji ulichelewa sana kipindi kile eneo lile la Ilala kwa kuwa niligundua kuna ujanja unaoendelea pale lakini nilisimama kidete wakapata wahusika,” alisisitiza Kikwete.
Kuhusu wanawake, Kikwete aliahidi kuwa watapatiwa chanjo ya saratani nchi nzima ifikapo mwakani baada ya kuliona tatizo hilo kuwa linazidi kuwa sugu.
Alisema kwa sasa serikali inatoa chanjo kwa kutumia hospitali ya Ocean Road ili kupunguza tatizo hilo hapa nchini.
“Hili ni tatizo ambalo limeshakuwa sugu kwa kuwa saratani zipo aina tatu; kuna ya koo, matiti, na ngozi, sasa imegundulika kuwa akina mama ndio wanaopata saratani kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Tunaanza nao mwakani kwa kutoa chanjo nchi nzima," alisema mgombea huyo.
Kikwete pia alisema kuwa katika kuboresha elimu nchini, serikali ijayo itahakikisha inatilia mkazo masomo ya sayansi na kwamba kila mwanafunzi atapata kitabu chake.
Alifafanua kwamba tayari vitabu vimeshaagizwa kwa ajili ya kutatua tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za sekondari zenye mchepuo wa sayansi.
Kikwete pia aliahidi kujenga miundombinu kwenye eneo la Tazara wilaya Temeke ambako wafanyabiashara ndogondogo wapatao 40,000 wataweza kujenga viwanda vidogodogo.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Huyu jamaa naona kadri siku zinavyokwenda anazidi kudata. Kumbukumbu zangu zinaniambia ya kwamba ile Machinga Complex ya Ilala ilijengwa ili kuondoa ufanyaji biashara holela na kuzungusha bidhaa mikononi. Lakini sasa tatizo halizungumzwi na haieleweki kama kufanya hivyo kunaondoa tatizo, yeye anakurupukia kujenga hizo machinga complex zingine tano. Bidhaa za machinga 99% imported.

Yaani badala ya ku-encourage uzalishaji jamaa ana-encorage uchuuzi. Kweli this guy is a big joke!
 
Sure Nyambala imagine hiki ndio kichwa tulikikabidhi nchi 5 years ago hakuna alichofanya kwa ahadi za 2005 anakuja tena kuomba ridhaa na ahadi zisizotamkika. Tunalalamika kwamba hii nchi imegeuzwa kuwa gulio kwa kila kitu toka nje kuanzia toothpicks mpaka toilet papers yeye hilo halimsumbui kabisa maskini. Haya machungwa toka Tanga yanaenda Kenya kukamuliwa na kuwekwa kwenye mabox na kurudishwa nchini kwa bei juu kama juice hilo nalo halimpi shida kiasi kwamba anataka kuongeza complex zingine 5 ili tuuziwe vizuri hizo bidhaa kutoka nje ambazo tunaweza kuzitengeneza wenyewe. Viwanda kwakwe sio priority.

Gharama ya kuwa na huyu mtu tena 5 years nyingine ni KUBWA SANA na kibaya zaidi ni kwamba si kizazi hiki pekee bali na vizazi vingine kadhaa vitapaswa kuilipa hiyo price. Mungu please tusaidie watanzania tuelewe kwamba urais si ushabiki au kumpenda mtu kama big brother bali maamuzi yanayogusa maisha ya watu zaidi ya milioni 40 hivyo yatupasa kuwa serious tunapochagua.
 
The question is in his first season Jk only managed to build only one Machinga Complex then why should we believe him now that he will build five more?

We need to know from JK what stopped him from building five Machinga Complex in his first reign before we can embark to consider believing his new pathetic promises earmarked to hoodwink us to vote in the most unsuitable presidential candidate CCM has ever sponsored?
 
Wakuu, hivi kweli JK ana mpango wa maendeleo kwa nchi hii? Kama jibu ni ndiyo basi atakuwa amekosea sana kufikiria kuendelea na biashara za wamachinga kama shughuli ya msingi katika kuinua uchuni wa nchi yetu. Kwa mtazamo wangu machinga ni biashara lakini si biashara itakayoitoa Tz hapa ilipo. Hivi kweli mmachinga asiyeweza hata kulipa kodi unamfikiria kuboreshea mazingira kwa kujenda Complex za kuuza soksi pair mbili? Kwa nini asifikirie kuanzisha kiwanda au mpango mwingine utakao discourage hii biashara? Au ndiyo maisha yetu yatakuwa ya mitumba milele? Kazi ipo...
 
Kwa hiyo anataka vijana wote wa tz wahamie dar kuuza bidhaa ndogondogo?!, is this not a plan to kill our nation?, who will go into production?. Kwa hiyo anataka kizazi chote kiwe chinga?!, how sad !
 
badala ya kufikiria kujenga industries au kufufua viwanda vilivyokuwepo, yeye anafikiria kujenga maduka ya kuuza nguo zilizotumika!, hapo ndipo unapojua uwezo wa jamaa uko wapi, hivi kweli mwanamume mwenye nguvu zake anakaa kutwa nzim kuuza socks mbili na mataulo yaliyotumika baada ya kutafuta jinsi ya kutumia nguvu zake kwa faida yake na faida ya nchi?

toeni huyu jamaa kabisa
 
Wakuu, hivi kweli JK ana mpango wa maendeleo kwa nchi hii? Kama jibu ni ndiyo basi atakuwa amekosea sana kufikiria kuendelea na biashara za wamachinga kama shughuli ya msingi katika kuinua uchuni wa nchi yetu. Kwa mtazamo wangu machinga ni biashara lakini si biashara itakayoitoa Tz hapa ilipo. Hivi kweli mmachinga asiyeweza hata kulipa kodi unamfikiria kuboreshea mazingira kwa kujenda Complex za kuuza soksi pair mbili? Kwa nini asifikirie kuanzisha kiwanda au mpango mwingine utakao discourage hii biashara? Au ndiyo maisha yetu yatakuwa ya mitumba milele? Kazi ipo...

usishangae, social background ya mtu hata kama ni Raisi inachangia sana maamuzi yake. JMK anaelewa maisha ya biashara ya genge ya kuuza nyanya 2, vitunguu 3 na nazi 5 kwa siku. Fikra zake ni finyu ukijumlisha na uwezo mdogo wa kiutendaji alionao, hawezi kuweka dira ya nchi. Anacho weza ni anasa na kutangaza miradi uchwara ambayo ina recycle umasikini wa watanzania (Baba mmachinga ambaye ni maskini ana mrithisha genge mtoto wake na baadae mjukuu wake). Watanzania tuna bahati kwamba aliingia madarakani baada ya Mkapa kuweka miundo mbinu iliyoanza kuboresha uchumi, sijui hali ingekuwaje kama angepokea straight kutoka kwa mzee ruksa! Hapa pia tuna kila sababu ya kumshukuru marehemu Mwl JKN aliyempiga full stop.Tunamwitaji Dr Slaa ili ku -break hii vicious cycle ya umaskini wa watanzania. Chagua Chadema, Chagua Maendeleo ya nchi yako.
 
Wakuu, hivi kweli JK ana mpango wa maendeleo kwa nchi hii? Kama jibu ni ndiyo basi atakuwa amekosea sana kufikiria kuendelea na biashara za wamachinga kama shughuli ya msingi katika kuinua uchuni wa nchi yetu. Kwa mtazamo wangu machinga ni biashara lakini si biashara itakayoitoa Tz hapa ilipo. Hivi kweli mmachinga asiyeweza hata kulipa kodi unamfikiria kuboreshea mazingira kwa kujenda Complex za kuuza soksi pair mbili? Kwa nini asifikirie kuanzisha kiwanda au mpango mwingine utakao discourage hii biashara? Au ndiyo maisha yetu yatakuwa ya mitumba milele? Kazi ipo...

Huyu ni kibaraka wa watu wenye viwanda na mawakala wao ambao ni wafanyabiashara wakubwa watakao tumika kuwanyonya watz. Kamwe nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea uchuuzi wa aina ya machinga...

JK acha porojo na ujenzi wa majengo yasiyo na tija Machinga Complex ni mzigo kwa wafanyakazi na wanachama wa NSSF kwa sababu sidhani kuwa ina returns zinazoweza za kibiashara iko kisiasa zaidi. Juzi nilipita pale Machinga complex hakuna biashara inayoendelea pale ... Hii ni sawa na yale majengo pacha pale chalinze barabara ya morogoro ya PPF ambayo nayo (kama ilivyo Machinga Complex) hayana wapangaji hivyo yanageuka kuwa mizigo kwa wafanyakazi... Ninafanya hima ili nichukue michango yango isije ikafia huko
 
... Hii ni sawa na yale majengo pacha pale chalinze barabara ya morogoro ya PPF ambayo nayo (kama ilivyo Machinga Complex) hayana wapangaji hivyo yanageuka kuwa mizigo kwa wafanyakazi... Ninafanya hima ili nichukue michango yango isije ikafia huko

Hivi ni kweli hayo majengo pacha pale Chalinze hayana wapangaji??? Mbona nikipita maeneo hayo nakuta nguo nyingi tu zimeanikwa kwenye balkony na kamba na magari mawili matatu yapo yamepaki?? Au ni danganya toto??
 
Yale pale ni ya NHC... Yana watu lakini sio waliokusudiwa...
 
Back
Top Bottom