Jengo la kitengo cha ukimwi Muhimbili laungua.

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Jengo la kitengo cha ukimwi Muhimbili lililopo jirani kabisa na Richmond Tower linawaka moto sasahivi.

Mwenye habari zaidi aweke hapa.
 
Last edited by a moderator:
Jengo la kitengo cha ukimwi Muhimbili lililopo jirani kabisa na Richmond Tower linawaka moto sasahivi.

Mwenye habari zaidi aweke hapa.

Ebwana hizo habari unazitoa wapi, wakati shy anasema kuna mtu yuko hatua kama 10 kutoka hapo na hamna kitu kama hicho?
 
Kuna mtu nimeongea nae yuko hatua 10 toka jengo hilo anasema hamna kitu

Mke wangu anahudhuria semina kwenye jengo hilo, kanipigia simu saa mbili na dak. 32 asubuhi ya leo kwamba wamekimbilia nje baada ya jengo kuanza kuungua moto.
 
Shy usianze ku chenji stori sasa, umesema jengo haliungui.

Halafu unaanza kuleta za jengo zima vs. kipande. Toka lini jengo likalipuka lote kwa mpigo ? Hata kama ni stoo inawaka moto, bado tutasema the damn building is on fire! Sasa come correct with your darn info.
 
Moto umezimwa, bahati nzuri fire briged wako karibu, wameweza kuwahi. Hata hivyo kwa wale waliokuwa kwenye semina kwenye jengo hilo wameahirisha mpaka j3 ili kupisha uchunguzi wa chanzo cha moto.

Shy, mtu wako aliyeko mita kumi kutoka hapo anasemaje?
 
Great Mkuu,

I can rely on this!
 
Mke wangu anahudhuria semina kwenye jengo hilo, kanipigia simu saa mbili na dak. 32 asubuhi ya leo kwamba wamekimbilia nje baada ya jengo kuanza kuungua moto.
Sina nia kabisa ya kukukorofisha na mkeo ndugu yangu Kashaija, ila inawezekana kabisa mkeo hayupo hapo, yupo sehemu nyingine nyeti, anataka tu usiwe shingo feni, ukazie macho Muhimbili near Richmond Tower.
 
Fataki, ieleweke wazi kwamba hoja hapa si kujadili mke wangu, hoja ni jengo kuungua moto. Suala la mke wangu na mimi halikuhusu.

Hata hivyo kama wewe ni mstaarabu, nategemea angalau baada ya kusoma habari hizi kwenye magazeti ya mchana utarudi hapa hapa na kunitaka radhi.
 
Sina nia kabisa ya kukukorofisha na mkeo ndugu yangu Kashaija, ila inawezekana kabisa mkeo hayupo hapo, yupo sehemu nyingine nyeti, anataka tu usiwe shingo feni, ukazie macho Muhimbili near Richmond Tower.

Fataki...jina linakufaa kweli.

Hebu jamani usilete vumbi ndani ya nyumba ya mwenzio...
 
Hii imethibitishwa na Gazeti la Dar leo

Last Updated on: 21.11.2008 0236 EAT (1802 GMT)
•
Moto wazua tafrani Chuo Kikuu Muhimbili
Na Waandishi Wetu, Muhimbili
CHUO Kikuu cha Muhimbili sehemu ya Utafiti wa UKIMWI kimenusurika kuteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme iliyozuka ghafla na kuzua tafrani kwa wanafunzi wa chuo hicho.

Moto huo umezuka leo asubuhi ambapo imedaiwa kuwa ulianzia kwenye 'main switch' .

Kitengo hicho kinachojihusisha na masuala ya UKIMWI kinaendeshwa kwa ushirikiano na na Chuo Kikuu cha Havard cha Marekeni.

Waandishi wa gazeti hili walifika eneo la tukio na kukuta Kikosi cha Zima Moto cha Kampuni ya Ultimate Security wakizima moto huo.

Baadhi ya magari ya kampuni hiyo yaliyofika eneo la tukio T 328 ATU, T 689 AGA ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo walifanya kila jitihada za kuzima moto huo.

Baada ya kupita dakika kadhaa ndipo Kikosi cha zima moto cha Halmashauri ya jiji kilifika eneo la tukio ambapo walikuta tayari moto huo umezimwa.
 
Kuna mtu nimeongea nae yuko hatua 10 toka jengo hilo anasema hamna kitu

Dogo Shy ana serious mental illness!! hawezi tokea kuja kutetea huyo aliyeongea naye akiwa hatua 10 toka jengo hilo, Shy kama huna cha kuchangia acha kusumbua keyboard!! £$ZXYZNS VU
 
Back
Top Bottom