Jenereta na solar power

Chereko

Member
Jul 20, 2009
54
16
Wakati nchi ilipata dhoruba ya ukame, tuliagiza majenereta, makampuni mengi yanatumia jenereta wakati umeme unakatika
  1. Pale DSM mjini kelele kila mtaaa; huu si ni uharibifu wa mazingira kwa maana ya kelele?
  2. Hewa chafu wanayoita "Green gas" (sijui kwa nini "green") aghalabu utaziba pua usivute hewa chafu mtaani
  3. Hutumia mafuta ambayo in gharama kubwa kuendesha
  4. Ajali za moto tumezisikia ambazo zimetokana na majenereta
Wizara husika ihamasishe matumizi ya solar energy. Kwenye maofisi zifungwe solar panel na kwa kweli kwa ujumla mahitaji ya ile TANESCO wanaita National GRID yatapungua kwa kiasi kikubwa.

Wizara iweke ushuru mkubwa kuagiza jenereta ndogo ndogo na pia iweke kodi kubwa kumiliki jenereta hizo na wakati huo huo iondoe ushuru kwa uingizaji wa vifaa vya solar ikiwezekana kumwita mwekezaji vifaa hivyo vitengenezwe hapa nchini
 
Back
Top Bottom