Zawadi Madawili: Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kuwa Brigedia Jenerali

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,538
19,388
Maj. Gen Zawadi Madawili ni mwanamke ambaye binafsi nimekuwa namheshimu sana maisha yangu yote tangu nimfahamu wakati aliopongoza mbio za mwenge mwaka 1975 akiwa luteni wa jeshi la wananchi wa Tanzania. Baada ya mimi binafsi kupitia mafunzo ya kijeshi ndipo nilipozidi kumheshimu sana mama huyo.

Serikali ya Tanzania ingefanya jambo moja la maana sana kwa kumpa nafasi pekee Jenerali Madawili baada ya kustaafu kwake jeshini awe na jukumu kubwa sana katika nchi hii kuhusu haki za wanawake.

Wanawake wengi Tanzania wanaonewa sana kijinsia na waajiri wao ama kabla ya kupewa kazi au baada ya kupewa kazi. Ingawa mama Madawili siyo mwanasheria, ana jina kubwa sana ambalo angeweza kulitumia kwa kusaidiwa na wanasheria kuhakikisha kuwa wanawake wote wa Tanzania wanapewa haki na heshima kama binadamu wengine.
 
Mimi naomba nitofautiane na wewe!

Namheshimu sana pia Mama Zawadi Madawili!

Kuwa na Mwanamke Mjeshi kwenye nafasi ya juu uraiani hakutafanya vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake vikome!

Kitakachowaokoa wanawake ni Elimu tu!... Unaelewa kwanini wanawake wengi wasomi hawaolewi(chunguza huko Botswana)?....the thing is just that they went to school and can take care of themselves without needing some flag-career pals!

Kama ni misimamo wanayo akina Ananilea Nkya bana! Pamoja na kazi zao, do you see any significant difference though?
 
Wapo wengi mkuu ila wamestaafu na wameachwa tu.............!!

Mfano mwingine ni Maj. Gen Samwel Kitundu ........!!

Huyu bado ni nguvu kazi katika nyanja za kibalozi.....!! na ana uzoefu kem kem...

Alishaliwakilisha Jeshi la Tanzania kama Muambata huko China kwa Miaka 7..............!!!
 
Sure huyu mama General ana elimu gani? Au ni wale walipata vyeo zamani kwa kulenga shabaha na kuhudhuria Monduli?

Kama hakufunguka akaingia darasani basi atabaki na cheo chake hicho kwa sasa!!! Angepewa say ubalozi atauweza? Maana itahitaji tena aajiriwe mkalimali kwa ajili yake (double cost).

Kwa kweli sijamsikia kabisa mama mkubwa huyu, au tuseme wanaume wa vyeo kama chake wanamfunika? Anatakiwa afurukute pia si kubebwa tu!!!

Mbebaji mwenyewe 2015 hatakuwepo tena.
 
Back
Top Bottom