Jenerali Ulimwengu: Waafrika bado tunajidhalilisha wenyewe kwa kuendeleza 'utumwa'

Yap, halafu na Jenerali mwenyewe anajitahidi kuandika kiingereza flani ili aonekane nae "amekwenda shule". Anajisahau kuwa hiyo pia ni dalili ya utumwa wa kimawazo. Makala zake zingewasaidia wengi kama zingeandikwa kwa lugha ya kiswahili. Wengi wanaoweza kusoma kiinglishi chake wanayajua yote anayotaka kuzungumza kwa hiyo haisaidii sana katika kumkomboa mtu "wa kawaida". Hii ya Black Skin White Masks ilishachambuliwa vizuri sana na Frantz Fanon miaka zaidi ya hamsini iliyopita (enzi zile tulipokuwa vijana)!

Ndugu yangu unaishi mchi gani. anaandika haya haya kwa Kiswahili -- katika gazeti lake la RAIA MWEMA -Rai ya Jeneralii. Pia aliwahi kuwa anaandika katika gazeti lake la awali la RAI. Na ndo maana alikosana na watu wa magamba na kunyang'anywa uraia.

Siamini kama wewe upo humu Tz!!!
 
Back
Top Bottom