Jenerali Ulimwengu na makala zake

Kitila na wengine,

David Brooks wa New York Times katoa maana moja poa sana na inabidi tuangalie kama inawiana na Siasa za Afrika na hasa sisi kwetu Tanzania.

Namnukuu



http://www.nytimes.com/2008/05/09/opinion/09brooks.html
Rev.,
the quality and the real meaning of life can only be realized when we are all humane.That is why I believe humanity stands out as an ideal philosophy of mankind not only politically but socially as well as in economic and technolohical development.
 
Ulimwengu roots for action against leaders misusing national resources

2008-07-07 09:45:50
By Nasser Kigwangallah


Veteran journalist Jenerali Ulimwengu has called upon civil society organisations and the public in general to join hands in fighting corruption and the constant misuse of national resources by bigwigs in the government circles.

He made the remarks in Dar es Salaam on Saturday night at a party organised by the Legal and Human Rights Centre (LHRC) to bid farewell to its long serving executive director, Helen Kijo-Bisimba.

She will be living for the United Kingdom to pursue a three-year doctorate degree at Warwick University.

The function was an opportunity to also welcome the acting executive director, Francis Kiwanga.

Ulimwengu said in order to preserve the existing peace and tranquility, there is a need to fight corruption by all means.

``Corruption is an endemic which if not tackled early, could make the government machinery to collapse,`` he said.

He urged human right activists in the country to continue with the same zeal and vigor in protecting the majority poor.

Ulimwengu congratulated Bisimba for her relentless efforts in fighting violation of human rights, which according to him have enabled human right issues in the country to become known.

``I have worked with Helen in various capacities and I can testify her to be a woman different from others, she is courageous and does not fear anyone in fighting human rights abuses,`` he said.

For his part, Bishop Elinaza Sendoro, the LHRC chairperson said Helen has been in office for twelve years and she has identified herself to be a true human rights activist of her own calibre.

He said they were proud of her dedication and would continue honouring her contributions for many years to come.

Speaking at the occasion, Kijo-Bisimba, said human rights issues can be a reality to the people of Tanzania if everyone of us begins to think of them and act accordingly.

She added that LHRC`s challenges are to ensure that people are able to experience and view human rights as a reality and not as a mere illusion.

``Everyday the Centre gets an opportunity to sharpen its expertise, overcome challenges or barriers, address unexpected issues and grow even further,`` Helen said.

SOURCE: Guardian
 
Mchango wangu kwako ulimwengu Jenerali

Nimesoma sehemu kubwa ya sheria zako kumi za elimu. Natoa mawazo yangu kuhusu suala la kufundisha maadili mema kwa lengo la kujenaga uhusiano mwema. Ni wazo zuri kujenga uhusiano mwema kwa vile pengine ni kichocheo cha maendeleo. Watu licha ya mifumo ya jamii inayowapa changamoto kadhaa za maisha wanatofautiana katiaka haiba zao. Kufundisha maadili mema kunaweza kuishia darasani tu kama yalivyo mambo mengi tuliyoyaingiza kwenye mtaala. Hapa sichambui dhana ya maadili mema, sisi walimu tunapofundisha tuanajali Nyanja zote za elimu. Ukiondoa maarifa kwa sababu tunaweza kupima kwa mtihani, Nyanja nyingine ina uamuzi wake zaidi kwa kuamagalia maisha yake na jamii kwa ujumla. Ni sawa na kufundisha njia bora za kilimo katika ngazi zote za elimu, anyway uzalishaji bado ni mdogo ukilinganisha na rasilimali za asili zilizo nchini.

Nimegusia haiba hapo juu (sijui na wewe Ulimwengu unajua kuwa haiba ni kuvaa nguo za heshima au la?) nikiwa na maana kuwa wapo watu hata bila kusoma wanaweza kujifunza au kuishi yaliyo mema kama wanavyopenda iwe. Lakini pia wapo wale wanaofundishwa ndipo wahishi hivyo. Makundi haya ya watu ni magumu kuyatambua na kwa sababu ya kazi chache za kutafiti, labda itakuwa ngumu kuona uhuisano wa kufundisha maadili(mema) na uraia mwema na utakuwa fisadi (ulimwengu) kama utasema upo ushahidi wa utafiti na unausoma peke yako tu na hujali kama wengine wamesoma au la.

Mapendedezo yangu ni kwamba ujenzi wa uraia mwema uanze kwa kuwafundisha maadili viongozi wa ngazi zote kwa sababu kwa jamii hii yenye wasomi wachache mno itasaidia kundi kubwa la watu wanojifunza au kuishi kwa sababu viongozi wanaishi hivyo(kuiga). “Stable” jamii inazaa maadili mema “automatically” bila hata kufundisha mashuleni.
Nina wasiwasi kwa vile pale panapotokea “lets say” jambo fulani basi wazo la kwanza ni kuliweka kwenye mtaala pengine bila kuangalia gharama zake hasa kwenye huu mfumo wetu. Wazazi “of course no need to consider”- kama ambavyo tumezoea licha ya kuwa wao ndo wamiliki wa mtaala, angalia TIE, NECTA, WEMU (vyuo vya ualimu, walimu na wanafunzi) na wadau wengine kama wewe na haki elimu kwa mfano.

Lakini wakati mwingine sio muhimu sana kujali gharama. yapo mengi tumeingiza kwenye mtaala kama elimu ya ukimwi, mazingira, uzazi wa mpango, lakini jenerali unaweza kusimama na kuwaambia watu kwa kiasi gani kwa kuwepo kwenye mtaala yamefaidisha jamii? Nadhani hili ni swali gumu sana kwa sababu pengine hata hujui hali ilikuwaje kabla ya kuingizwa kwenye mtaala. Nnavyokufahamu unaweza kukomaa na kusema kuna mabadiliko, si unayaona bwana!? Utafiti wa nini! Lakini unajua kama yanafundishwa au la? Umewahi kusikia mzazi akihimiza mtoto wake kuhusu suala la utunzaji wa mazingira?

Labda a counterbalance is needed kwa wadau wote wa elimu, wafeel, hasa wazazi na wanafunzi kuwa jambo hilo ni la muhimu.

Wanayoyapenda muwafanyie hamjadili na hamuwatekelezei kama vile ubora wa walimu na ikama yao. Anyway presha toka juu inaweza kuleta mafanikio na watu wakaona umuhimu wake baadaye kama ilivyokuwa pale tulipobadili masomo na kuyaweka yale ya maarifa ya jamii na stadi za kazi-hapo ndo tuliona manufaa ya yale mawazo yako, nadhani unawashangaa hawa wengine wanaotaka kubadilisha tena au umeshiriki nini?(of course wamebadilisha).

Nini kimetokea mtaani mpaka mwaleta mabadiliko. Of course itakuwa hasara ambayo hamtaweza kuniambia mmeijuaje sasa (mapema mno) na hamkuiona kabla. Hasara ya mabadilikomabadiliko ya mara tusomeshe hili mara lile. Kumbe uwaziri ni kazi rahisi sana! Kwa kushirikiana na wewe, mnabadilisha tu. Kama unaona wanakuzidi nguvu na wewe gombea uwaziri!ili ukabadili au ukaongeze vya kwako. Kwa taarifa yako sijui kama tunajua kufundisha.

Kwa hili ningekushauri utumie wataalam wako kufanya utafiti kwa sababu ndo njia rahisi ya maana ya kusikiliza sauti ya wazazi. ili watu waone mafanikio ya haya mambo ambayo tayari tumeshayaingiza kwenye mtaala na wanaweza kumotishika kwa hilo.

Hivi ulimwengu unajua ni mambo gani muhimu yanafundishwa mashuleni? Ni heri ufundishe walugulu kuhusu milima ya ulugulu kuliko kuwafundisha warufiji juu ya milima ya ulugulu. haijawahi kutokea warufiji kwenda kuishi kwenye milima hata kama utawasomeshea milimani. Haya ndo mambo ya maana kwangu. Kama hutaki basi! Labda umejiundia maana yako ya elimu ya kujitegemea.

Asilimia 95% ya watu wanaoishi vijijini haichanganyi jumuia hamiaji kwa kiasi kikubwa. Ona sasa nashindwa hata kusema haichanganyi kwa asilimia ngapi kwa sababu hata wewe Ulimwengu huwa unasema kuwa zaidi ya 80% ya watu wanaishi vijijini bila kujua mchanguo wao japo wachaga wapo wangapi, wenyeji wangapi na labda waha ni wangapi? Mwenzio nina chanzo changu (jono) kinachonionesha kuwa wenyeji ni wengi kuliko wahamiaji tena nimeipata mtandaoni (ntawaprintia rafiki zangu watanzania waione).

Kuna mzungu mmoja alifanya utafiti hapa bongo. Hata wale wachache wanaohama ni kwa vile umewafundisha kuwa mjini kuna ajira za viwandani na umeme. Tena na migogoro yenu ya umeme unayojadili mara kwa mara-mpaka wanaona kuwa umeme ni kitu cha maana mno kuliko kupalilia mgomba wanayouza mkungu mmoja tsh 1500- huyu mfundishe maadili mema ili ajenge uhusiano mwema na wafanyabiashara uliowapa rungu la soko huru bila mpango.

Lakini Ulimwengu ungewaambia waende mjini baada ya kuwaonesha kuwa wanaweza kuajiri na kuzalisha umeme palepale chijijini. Shauri yako. Mi nakuonea huruma kwa vile unaweza kusema kuwa kwa kuamua kuwafundisha mambo yanayowazunguka utawabana kuvumbua rasilimali za Tanzania hiihii zilizopo upande wa kushoto na juu.

Specialization matters mzee. Amua moja. Si tumesoma mengi kichizi ya South Africa, USSR, North America na Ulaya kwenye jiografia, we unajua hii. Hata mto Mvuha pale Morogoro siwezi kuutepu nimwagilie bustani kwa sababu kuta ni ndefu. We unaujua mto Mngazi? Madini pale Kimberlei, nimesahau hata kuandika vizuri jina la mji wa pale penye dhahabu Afrika Kusini, anyway, hapa kwenye nyumba yangu pana dalili ya madini na siwezi kuyachimba kwa vile watu wenye viwango wanaweza kubinafsisha na haka kanyumba kangu.

Labda kwa stahili hii ningefundishwa maadili mema shuleni ningeshaenda kuwaambia wenye viwango kuwa pana madini hapa kwangu na kuwashauri waje wachimbe kwa ujenzi wa taifa lenye nguvu. I mean maadili mema is automatically yanakuja.

Ulimwengu umewahi kuwaza kuwa mwavuli ulionao, huo wenye rangi rangi kuwa haufai? Umeuona mwavuli wa kisasa? Sasa huo wa kwako hauna dili kwa sababu mvua ikinyesha miguu yako na mgongoni kunalowana. Fundisha watoto matatizo yao kwa namna ya ubunifu watatue matatizo yao hapa hapa kama huyu aliyetengeneza mwavuli huu. Utauona miaka ya mbele sana kwa kwa ushamba wako.
Sina muda mzee. Edit edit kidogo ili usome kwa raha.

Naitwa James Lukes
(kama hutaki kuamini kuwa hilo ni jina langu shauri yako)
 
Hivi kila Mtu mnayemuona yupo Tofauti na Mambo ya serikali mnamuona kuwa ni Chadema?.Basi kwa Mwendo huo Mzee Mwinyi,Prof.Shivji na Judge Bomani wote ni Chadema.

Nafikiri suala zima la Uongozi Mbovu, linaonekana kwa watu wa vyama vyote!Kinachotoa msukumo kuzungumza hapo ni Utanzania na si Itikadi ya vyama vyao.Tuzungumze kama Watanzania na si Ucuf au Uchadema!!

Unasound kiCCM zaidi, ...ni mtazamo wangu tu lakini, naona hutaki wapinzani wapate credit wanayodeserve!!
 
Nimejaribu ku-attach makala kuhusu maelezo ya Jenerali Ulimwengu jana Chuo Kikuu Dar.

i285_Jenerali1.jpg

mKUU NAONA WEWE UMEKAA KUPINGA WANAHARAKATI

mPANGO WAKO TUMEUSHUTUKIA
 
Watamhoji urai wake sasa hivi maana hiyo ndio silaha kuu ya zimwi liitwalo CCM
 
Palipo na uovu lazima pafunuliwe ili uovu uonekane mbele ya jamii. Hicho ndicho anachofanya Ulimwengu. Kwa mantiki hiyo, sioni ajabu kwa vijifisadi koko kama huyu bwana vinavyopingana nae.
Aluta kontinua Generali mpaka haka kachama kalikozeeka kaishiwe pumzi na kutoweka kabisa kwenye uso wa TZ.
 
Palipo na uovu lazima pafunuliwe ili uovu uonekane mbele ya jamii. Hicho ndicho anachofanya Ulimwengu. Kwa mantiki hiyo, sioni ajabu kwa vijifisadi koko kama huyu bwana vinavyopingana nae.
Aluta kontinua Generali mpaka haka kachama kalikozeeka kaishiwe pumzi na kutoweka kabisa kwenye uso wa TZ.

Mkuu Heshima mbele!
Wakati mwingine huyu jamaa ni controversial, tunakumbuka mwaka 1995 alipoamua kumpigia kampeni ya wazi mgombea wa ccm Mkapa; wakati ule kupitia gazeti lake la Rai lililokuwa likiheshimika. Wapenda mageuzi wengi hawakumwelewa ingawa yeye alidai kuwa anamfahamu na eti ni Mr. Clean, walivyokosana hadi kunyang'anywa uraia hadi leo ni kitendawili.

Siku hizi naona makala zake zimejishikiza kwenye kampeni ya Chadema, inawezekana anaashiria mtizamo wa kisiasa kwa sasa na kujaribu kuhakikisha mauzo ya gazeti lake yasianguke kama ilivyotokea 1995, au bado ana visasi na rafiki zake wa zamani ndani ya ccm?
 
Jenerali Ulimwengu anasimama kati ya Maadili na Ukweli, anasimama kama sauti ya mtu aliae Nyikani , mwenye macho ya kusoma na asome, amekua na msimamo huo kitambo tu, hakuanza leo harakati zake, ameanza kitambo, na daima amekua akipigania Ukweli hata kwa gharama ya kuwaudhi watawala na marafiki zake.
Ukweli ameusimamia sana, huyu alirudisha kadi ya CCM baada ya kuona hakua katika chama sahihi, chenyee mrengo sahihi kwa maendeleo ya Taifa. Yeye si kama wale wanaouma na kupuliza, yeye anauma na kuchoma moto, yeye haumi maneno, kwa umri alioishi , kwa kazi alizofanya, hakuna wakumtisha.Yeye anapambana na wala rushwa kwa msimamo hasa, si wale wanajidai kupambana kwao na wala rushwa ni kumsaidia Kikwete, wakati Kikwete hakuwaomba, wala haitaji kusaidiwa, maana huwezi kumtenganisha Kikwete na wala RUSHWA NDANI YA CCM.
Namuunga mkono katika Hoja zake, nikiona ni kama changamoto ya Kujenga vyama Imara kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
 
Asante Kitila kwa mchango wako lakini hii nukuu ya Jenerali Ulimwengu inanipa wasiwasi yupo wapi nasi kwenye hivi vita dhidi ya dhuluma ambayo CCM inatufanzia:-

Aidha chama hicho kimejenga tabia ya kutamba kwa jeuri ya “chama tawala”, na kinayo haki ya kutamba, sawa sawa na baba alivyo na haki ya kutamba kwa kuwa mkuu wa familia. Pamoja na haki hiyo ya kutamba, chama hicho hakina budi kuelewa kwamba kina majukumu makubwa ya kulipa Taifa hili uongozi makini, sawa na baba alivyo na majukumu mazito ya kuiongoza familia yake na kukidhi mahitaji yake.

Alichotakiwa kusema ni kuwa huyu baba aliyepoteza sifa ya kuwa baba wa familia siyo baba tena na hana haki ya kujiita ni "chama tawala".

Uongozi makini utatoka mahali popote pale siyo lazima CCM tu. Jenerali bado yuko kwenye njozi za Nyerere ambaye alitudanganya pale aliposema na nina nukuu:-

Kiongozi anaweza kutoka popote lakini kiongozi wa kutumainiwa atatoka CCM

Tumeona kwa macho yetu JK siyo kiongozi wa kutumainiwa hata kidogo kwa kuwakumbatia "list of shame".

Vile vile Jenerali ni vyema akaelewa ya kuwa kiongozi makini ni mnyenyekevu na wala siyo mtu mwenye makuu na hapaswi kutamba. Jenerali anapobariki CCM kutamba naona amekalia kaa la moto la kuamini CCM inaweza kujirekebisha wakati haitaweza hadi siku itakaposhindwa uchaguzi mkuu ndipo kiburi chote kitwaishia. Waulize Kanu ambao walidai kuondolewa madarakani kwao ni kugumu kama kuukata mpingo kwa wembe....Leo hakuna hata anayewakumbuka na wamebaki kutajwa kwenye vitabu vya historia tu. CCM ndiko itaishia huko baada ya Oktoba 31. Hakuna dawa hapo hata mwarobaini hautasaidia.

Sikio la kufa la CCM halisikii dawa
 
Back
Top Bottom