Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Jenerali Ulimwengu ameweka vyama vyote kwenye kapu ikiwemo vya upinzani kuwa havina falsafa wala itakadi:
http://www.raiamwema.co.tz/08/04/23/4.php
Hebu mlio karibu na Raia Mwema mumwambia asome hapa:
http://www.chadema.net/maoni/kijue.php
ili wiki ijayo aendelee kujadili kama CHADEMA nao hawana falsafa wala itikadi?
Asha
Asha:
Kwa maoni yangu binafsi naona Jenerali Ulimwegu anachemsha BIG TIME.
Vyama vya siasa katika nchi zilizoendelea vina Itikadi lakini Itikadi hizo sio zao la mawazo ya mtu mmoja bali ni matokeo ya kisiasa na mabadiliko ya kijamii yalizozikumba nchi hizo.
Pamoja na nchi zilizoendelea kuwa na vyama vya kisiasa vyenye itikadi, malengo makubwa yanabakia ni kutoa viongozi mbalimbali watakaoongoza nchi. Na viongozi hawa wanapokuwa madarakani, wanaongoza nchi kwa kufuata ukweli wa mambo na sio itikadi ya vyama vyao. Hivyo itikadi mara nyingi inatumika katika kupatia kura za uchaguzi.
Kama lengo la vyama vya kisiasa ni kutoa viongozi wa kutawala nchi sioni sababu ya ulazima wa vyama vya kisiasa vya Tanzania kuwa na itikadi za kusimamia na kupigania. Inatosha kwa chama cha kisiasa kuonyesha ni mambo gani watayafanyia kazi wakiwa madarakani na vilevile inatosha kwa vyama vya siasa kutoa upinzani pale chama kilichopo madarakani kinakosea (CHECK AND BALANCE).
Siasa sio rocket science na tusijaribu kuifanya hivyo.