Jenerali Ulimwengu: Hata kwenye upuuzi tuko dhaifu!

Kuna watu wakiongea kitu unajuwa wanamaanisha0„3* Ulimwengu ni mtu ambae siku zote yuko within logic and reason. Hio article nimeisoma, ina ujumbe mzito BUT nimeona niiangalie more like a critique than tu kuikubali kama ilivo kwa mimi kuweza elewa na faidika nayo. Huwa nasoma makala zake once in a while na huwa hazinipi shida katika kumpata0„3*

Kwa maelezo yako ulotoa (hasa paragraph ya pili); imeonesha kuwa nimeelewa vema kama wewe pia umeelewa hivo. Kama ulivosema na nakubaliana nawewe kuwa hajatumia neno zuri. Hata hivo nadhani shida sana sio kuendekeza kwa hayo mambo; shida ni kitendo cha kuwa na audacity ya ku-entertain vitu kama entertainment in a time ambayo taifa inakumbana na matatizo kila Nyanja, kila sector, ndani/nje and between hizo Nyanja na sector0„3* Sad.

Tukija upande wa mfano wako wa Kanumba... Lets just not go there! Words can not suffice at the moment.

Ninatatizika na unachosema wewe na wanachosema baadhi ya wachangiaji kwamba katumia neno 'baya,lisiloleta hisia chanya' miongoni mwetu. Lakn ninachokiona hapa ni watu kuangalia neno moja tu ''upuuzi'' na kujaribu kuonyesha kwamba makala nzima imepotoka. Ni vema wasomaji waliangalie neno 'upuuzi' kwa kina na kulielewa umaana wake kabla hatujajaribu kutoa ctitique kwa kitu ambacho bado hatujakiangalia deep.Jenerali,unapomsikiliza au kusoma makala zake,unahitaji jicho na sikio la ziada kupata anajaribu kukipresent.
 
Ninatatizika na unachosema wewe na wanachosema baadhi ya wachangiaji kwamba katumia neno 'baya,lisiloleta hisia chanya' miongoni mwetu. Lakn ninachokiona hapa ni watu kuangalia neno moja tu ''upuuzi'' na kujaribu kuonyesha kwamba makala nzima imepotoka. Ni vema wasomaji waliangalie neno 'upuuzi' kwa kina na kulielewa umaana wake kabla hatujajaribu kutoa ctitique kwa kitu ambacho bado hatujakiangalia deep.Jenerali,unapomsikiliza au kusoma makala zake,unahitaji jicho na sikio la ziada kupata anajaribu kukipresent.


Almasi you have a point... Hata hivo sijaelewa nani hasa umeona hajaelewa vema neno 'upuuzi' limetumika vipi. Ni kweli kuwa baadhi yetu tumekazania utumiaji wa hilo neno moja tu... Ila tambua ni neno moja ambalo limetumika kufikisha ujumbe kwa njia ya msisitizo wa kulitaja neno lenyewe. Na hata hivo kidogo sijaelewa ni kwanini wewe pia umeelema katika utumiaji tu wa neno hilo na hujaangalia upande wa pili wa shilling...

So far sijamsoma mtu yeyote aliyekataa kuwa hii makala haina ujumbe mzito na wa kuzingatiwa. Personally nakubaliana na mawazo ya Ulimwengu ila sikubaliani na utumiaji wa neno upuuzi juu ya kundi alilolenga.
 
Nimekumbuka vitabu kama Nyota ya Rehema Duniani kuna Watu nk kwa miundo na misamiati ya Kiswahili
 
Tatizo tumekubali akili ndogo itawale akili kubwa,bungeni kuna maprofesa ambao wana uwezo wa kuibadilisha nchi yetu ,but still wamebaki kupiga makofi kuunga hoja ambazo kimsingi hazimsaidii mtanzania,hii ni just another drama ambayo inabidi tukubali changes katika uchaguzi huu.
 
eh hakika tunaelekea kwenye Nchi kuifanya ya kipuuzi, hivi kweli watu walio makini ; kwa mfano Bunge ndicho chombo cha kutunga sheria ambayo ndio muongozo, sasa eti sifa ya kumpata huyo mtunga sheria ni kujua kuandika na kusoma, kama si upuuzi ninini.........?
Nimeipenda makala ya Generali Ulimwengu ya week hii....

Soma mwenyewe hapa CLICK HERE Kwa nini tunataka ‘kuizairesha’ nchi?: Katika upuuzi tutakuwa wapuuzi dhaifu

NIMESEMA mara nyingi kwamba tunahitaji kupunguza upuuzi katika maisha yetu na shughuli zetu kama jamii na kama taifa. Hii ina maana kwamba tunaenenda kipuuzi mno na ndiyo sababu kubwa ya kukosa maendeleo ambayo tunaweza kujivunia, tukiacha hayo maendeleo tunayolazimishwa tuyaangalie na wale wanaojisifu kwa kazi nzuri ambayo haionekani.
Upuuzi kwa kiasi fulani ni jambo jema. Kila mtu anayo haki ya kufanya upuuzi kidogo kama njia ya kujipumzisha, kujiliwaza na kujiburudisha baada ya kazi ngumu, ama ya mwili ama ya akili. Ndiyo maana hata katika jamii zilizoendelea sana katika ujenzi wa uchumi wapo watu ambao wanalipwa kwa mabilioni ya dola ili wapangilie upuuzi utakaowaburudisha wenzao waliotoka kwenye migodi na kazi nyingine za ngwamba. Kwa Marekani wengi wa watu wa aina hii wako Hollywood. Bara Hindi wako Bollywood.

Hata sisi hapa nchini tunao watu wa aina hiyo, hata kama sanaa yao haijakua kiasi cha kuzikaribia Hollywood na Bollywood. Na ni kweli kwamba wanatuburudisha na kutufurahisha kwa kiwango chao. Ni watu muhimu katika jamii kama ambavyo tulikumbushwa si muda mrefu uliopita alipofariki Kanumba.
Hata hivyo, hatutakiwi sote kuwa waburudishaji na watumbuizaji. Wengine hawana budi kufanya kazi nyingine ili taifa lisonge mbele, liweze kujilisha na kujilimbikizia amali kwa siku zijazo, kwa ajili ya vizazi vijavyo. Tukiwa sote ni watumbuizaji ni nani atatulisha, atatuvisha, atatujengea nyumba? Nasema, tunahitaji upuuzi kidogo, na tena huu ni upuuzi uliopangiliwa vyema, lakini upuuzi hautakiwi uwe ndiyo shughuli kuu ya jamii nzima.

Tukitaka kuangalia jamii iliyofanya upuuzi ukawa ndiyo shughuli kuu katika maisha yake, hatuhitaji kwenda mbali sana; tuiangalie Kongo, ambayo Joseph Mobutu aliita Zaire kwa kipindi kirefu akiwa mtawala wake. Kongo imejipambanua kwamba nchi ya upuuzi kabla ya uhuru wake mwaka 1960. Ilipoingiliwa na wazungu ilifanywa kuwa shamba binafsi la Mfalme Leopold II wa Ubelgiji, ambaye alichimba na kuchuma kila alichokitaka na alifanya kila aina ya unyama bila kuulizwa siyo tu na Wakongo bali pia hata Bunge la nchi yake. Kongo haikuwa koloni la Ubelgiji; lilikuwa ni kihamba cha Leopold.
Baada ya uhuru wanasiasa wapuuzi wakalumbana, wakazodoana, wakafukuzana, wakauana, hadi alipoibuka mshindi wa kinyanga’anyiro hicho kwa sura ya Jospeh Mobutu, ambaye aliboresha mbinu za wizi, uporaji, unyang’anyi, udhalimu na uuaji kiasi kwamba ikawa inajulikana kwamba hayo ndiyo maisha ya nchi ya Zaire na huo ndio utamaduni wake. Hiki ndicho kilikuja kujulikana kama Mobutism, u-Mobutu.

Kwa wananchi wa kawaida, hii ndiyo ilikuwa hali ya maisha, nao wakaichukulia hivyo ilivyokuwa na wakajichimbia katika wizi wao na unyang’anyi wao mdogo mdogo (small scakle thievery) ambao ulikuwa ni kiungo muhimu katika kufanikisha wizi mkubwa (large scale thievery) ya Mobutu na genge lake.

Isitoshe, katika kujiliwaza na kujisahaulisha madhila waliyoyapata muda wote, wakiwa ni shamba la Leopold na wakiwa ni shamba la Mobutu, wananchi wa nchi hiyo yenye utajiri kama El Dorado wakaingia katika shughuli ya kujitumbuiza kwa muziki na ngoma. Na hii ikawa ndiyo shughuli yao kubwa. Kongo ikajulikana kwa mambo manne makubwa: moja, utajiri mkubwa uliomnufaisha Mobutu na mafisi waliomzunguka, lakini hasa uliowanufaisha wazungu; pili, vita, fujo na vurumai zisizoisha; tatu, udhaifu wa serikali ambayo haikuonekana majimboni isipokuwa kwa uwapo wa askari wanaopora ili kupata ujira wao; nne, muziki, ngoma na burudani kama soka na ngono.
Taswira hii ya Kongo haijabadilika sana. Mwaka 1997 nilikuwa katika msafara wa Mwalimu Julius Nyerere aliyekwenda Kinshasa kwa mazungumzo na Rais Laurent Kabila. Katika wiki moja tuliyokaa Kinshasa jambo moja kubwa alilobaini ni kwamba Kabila na genge lake walikuwa wamefanikiwa kumfurusha madarakani Mobutu lakini wakabakiza u-Mobutu katika utawala wao. Kabila alikuwa ni Mobutu baada ya Mobutu, mrithi halali wa Leopold. Hadi leo hali haijabadilika sana, baada ya Kabila mdogo kumrithi baba yake aliyeuawa katika mazingira ya kunyang’anyana mali.

Pamoja na yote, K0ngo/Zaire ilipata mafanikio makubwa sana katika upuuzi uliopangiliwa. Haiwezekani kuzungumzia muziki barani Afrika bila kuitaja Kongo/Zaire; hata barani Uropa, wapenzi wa muziki ambao hawana asili ya Afrika wanatafuta muziki wa Kongo/Zaire. Aidha Wakongo ni wasanii katika mambo mengine pia, kama ushonaji wa nguo, ushonaji wa viatu, uchoraji na uchongaji. Pia ni wanasoka wazuri wanaosifika Ulaya ambako wanacheza katika ligi kubwa.
Mobutu, pamoja na kwamba alikuwa mshenzi, alifanya kazi kubwa ya kuhifadhi urithi wa kimuziki wa Kongo. Katika miaka ya 1970 nilikwenda mara kadhaa mjini Kinshasa na nikaweza kujikusanyia albamu kadhaa ya wanamuziki wa zamani wa Kongo, akina, Kabasele, Wendo na Boukaka, yote kwa sababu Mobutu alikuwa amefadhili kazi ya kukusanya nyimbo za zamani na kuziweka katika sahani za santuri.
Uhamasishaji wa vikundi vya ngoma na mapambio ya kumsifu Mobutu ulifikia viwango vya juu kabisa, kiasi kwamba watawala wa nchi nyingine, kama Gnassinbe Eyadema wa Togo, walianza kuiga walichokuwa wakifanya Wazaire katika kumsifu Mobutu. Hata sisi hapa nchini tulivutika na upuuzi huo kiasi kwamba wimbo wa “chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi” ulichukua mahadhi ya wimbo wa kumsifu Mobutu, “Tokobongisa Mobutu Sesse Seko.”
Mobutu alifanikisha upuuzi kwa kiwango cha juu sana, na akaifanya nchi yake kuwa ya kipuuzi ambamo rasilimali za nchi zinaporwa na wageni wakisaidiwa na watawala wa nchi, huku wananchi wakiimba na kukata viuno wakimsifu Bwana Mkubwa. Nchi tajiri kwa rasilimali kuliko nchi nyingi duniani (ardhi nzuri yenye rutuba, misitu, maji, madini ya kila aina) lakini yenye wananchi siyo tu masikini lakini wasiokuwa na amani kutokana na vita za kila mara; lakini wanacheza ngoma, wanafurahi.

Wakichoka kuishi katika vurumai za nchini mwao wanaondoka, wanahamia katika nchi nyingine Afrika na ng’ambo ambako wanakwenda kuimba na kupiga muziki wa dansi, kushona nguo, na kusuka nywele. Kwa jinsi hii wamejipatia umaarufu mkubwa katika upuuzi wao. Laiti wangekuwa ni wapiga muziki mahiri, wanasanaa wakubwa na wasusi wa nywele wa kimataifa na papo hapo wakaiendeleza nchi yao katika kilimo na viwanda, tungelazimika kuwaheshimu kwa yote hayo na mimi nisingethubutu kuwaita wapuuzi ; kwa walivyo, ni wapuuzi waliofanikisha upuuzi wao kwa kiwango cha juu.

Hatari ninayoiona ni hii inayotunyemelea: Kwamba tunaelekea kuifanya nchi yetu kuwa Zaire bila kuwa na wanasanaa wa viwango vya Zaire. Tunataka kuwa wapuuzi bila kuwa na uwezo wa kufanya upuuzi ukafikia kiwango cha kutupatia sifa kama wapuuzi. Hii haitakuwa rahisi, na hii ina maana kwamba hata katika upuuzi tutakuwa wapuuzi dhaifu; hatutawafikia Wazaire kwa upuuzi.
Hii ni kwa sababu nchi yetu inayo misingi ya kitaifa iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Misingi hiyo inakataa nchi yetu kugeuzwa kihamba cha mtu au watu wachache; ni kihamba chetu sote, na wala si chetu kiasi hicho, kwani tumepewa dhamana tu ya kukihifadhi na kukiendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwa niaba ya Watanzania tusiowajua, kwa sababu hawajazaliwa.
Tunao watoto tayari ambao kila wakituchunguza tunavyoenenda ki-Zaire hawaoni mustakabali wao na wa watoto wao; wanatuuliza maswali, tunashindwa kuwajibu; wanaasi, hatuelewi.
Tungekuwa na busara ya kusikiliza vyema wanachosema, tungezisikia sauti za watoto watakaozaliwa mwaka 2099, wakisaili: Mbona mnaigeuza nchi yetu Zaire? Tungesikiliza sauti hizo tungekomesha huu Uzaireshaji (Zairesation) wa nchi yetu, tungekuwa watu makini wenye viwango vidogo tu (vile vya lazima) vya upuuzi.
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

Mkuu Eddie
Naona hujamwelewa Jenerali, makala hii inajitosheleza kwa mtu mwenye uelewa.
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

Wa sasa kazidi, angalau Mkapa alikua ananuna, lakini huyu anatabasamu kwa ayafanyayo. Nipo deep, kama hujaingia deep hutonielewa.
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?
Ktk wapuuzi anao ongelea Jenerali nafikiri ww ni mmoja wao. Kuna theory moja nafikiri ni ya somebody Jeriko Nyerere kwamba kama ukiona matendo na maneno yako watu hawayaelewi mshukuru Jah, lkn siku ukiona wameanza kukuelewa jitafakari ulipo anguka maana umeanza kufikiri kama wao.Kitu kama hicho nafikiri siko mbali sana. Ndo maana nasema watu kama ww ni janga la c tu la taifa bali dunia nzima. Jitafakari kama elimu yako kama c darasani basi hata mitaani kama inakutosha ndugu yangu. Je, unaposema fisadi mwenzako Mkapa kwamba alimtesa Jenerali aliambulia nn kama c aibu na na bado huyu mwandishi nguli bado yupo na ataendelea kuwepo kwa sababu hahitaji fadhira za rais yeyote bali uzalendo wake ktk nchi finito! Basi ww usiye mnyarwanda tuambie umeifanyia nn nchi hii kuliko J.Ulimwengu? Mavi yako ww.
 
Ktk wapuuzi anao ongelea Jenerali nafikiri ww ni mmoja wao. Kuna theory moja nafikiri ni ya somebody Jeriko Nyerere kwamba kama ukiona matendo na maneno yako watu hawayaelewi mshukuru Jah, lkn siku ukiona wameanza kukuelewa jitafakari ulipo anguka maana umeanza kufikiri kama wao.Kitu kama hicho nafikiri siko mbali sana. Ndo maana nasema watu kama ww ni janga la c tu la taifa bali dunia nzima. Jitafakari kama elimu yako kama c darasani basi hata mitaani kama inakutosha ndugu yangu. Je, unaposema fisadi mwenzako Mkapa kwamba alimtesa Jenerali aliambulia nn kama c aibu na na bado huyu mwandishi nguli bado yupo na ataendelea kuwepo kwa sababu hahitaji fadhira za rais yeyote bali uzalendo wake ktk nchi finito! Basi ww usiye mnyarwanda tuambie umeifanyia nn nchi hii kuliko J.Ulimwengu? Mavi yako ww.
big up
 
Udhaifu hata katika upuuzi, so interesting! Je vipi udhaifu katika ujuha!?
 
Sidhani Tanzania inaweza kulinganishwa na Zaire, sisi tumekuwa na demokrasia japo bado changa, lakini tunaweza kusema, tunakosoa, tunatoa maoni yetu kwa haki, uwazi na bila woga na tukabaki salama, kitu ambacho kwa Mobutu hakikuwepo. Upuuzi huo ambao yeye anaona kama hatari itunyemeleayo haiwezi kukwepeka, ni madiliko ya kiuchumi ndio yanayo sukuma upuuzi huu utokee Tanzania, ambao ulianza kushamiri na kushika kasi miaka ya tisini, upuuzi ambao sasa umegeuka fursa kwa vijana, akumbuke kuwa miaka ya akina Mobutu upuuzi huo ulikuwa kwa ajili ya kujiliwaza tu, starehe na mengineyo, lakini kwa kizazi hiki cha sasa upuuzi huo umekuwa ajira tena yenye tija kubwa kwa "wapuuzi" wenyewe na jamii zinazo wazunguka na hata Taifa pia
 
Kwa mtazamo wa huyu Mnyarwanda muziki ni "upuuzi" na kuthubutu kukashifu tasnia nzima ya burudani kuwa nayo tunashindwa!

Kweli mgema akisifiwa tembo hulitia maji, mwandishi huyu mkongwe kakosa maneno sawia na kuamua kumwaga kashfa na bado anaambiwa yupo "deep!"

Kweli serikali hii ipo "auto pilot" ujinga ujinga kama huu mbona hakumfanyia Mkapa?

Crappp!

Kweli akili za kuazima mbaya sana.......kama hujaelewa alichokisema Jenerali soma tena mstari kwa mstari ndio uje kutoa maoni yako hapa.
 
Jenerali anasema kama leo sera zikiwa mbaya,kesho nchi itakuwa kama zaire na kashfa ya escrow itatokea kila wiki. Neno upuuzi linaleta ubishi. Maneno mengi yangeweza kutumika,ujinga,upumbavu,utoto,kuzubaa. Taabu kupata neno zuri,lakini watu wakifanya mambo haya unayatambua mara moja. Jenerali anasema tu,look before you leap. Chuo Kikuu people are trained to speak,they are trained to think. Tunahitaji patience in dealing with people who have not gone to university ama sivyo itatokea zairesheni. Kuhusu Zaire,yupo diplomat mmoja wa Tanzania aliitwa State Department wakamuomba awape jina moja la mtu central africa ambaye anaweza kulinda maslahi yao,yaani maslahi ya Big Money,wale wanaochimba madini Zaire. Akasema' Nyerere'. Akaambiwa Nyerere usimtaje hapa. Tupe jina lingine. Akasema' Museveni'. Akaambiwa'. Excellent'. Kwa hiyo Museveni akachaguliwa kwa kazi hiyo,na Laurent Kabila akachaguliwa kama Kamanda wa kwenda kumuondoa Mobutu. Kabila alichaguliwa na State Department kwa vile alikuwa ni mmoja wa Nyerere Kindergarten,yaani mmoja wa mlolongo wa wanasiasa waliopigwa msasa na Nyerere. Kwa hiyo wakaanza mapigano halafu baadaye wakaja Msasani kumwona Mwalimu. Walipomaliza kuongea waliposimama wanataka kuondoka wakasema watarudi tena. Kila linalotokea tutakuja kukwambia. Mwalimu Nyerere akasema,'Oh? That will be fine. Kwa sababu itamaanisha kuwa mimi ndio nitakuwa nananihii....,'. Yaani yeye ndiye atakayekuwa Master Mind. Museveni akachaguliwa kulinda maslahi ya hawa watu central africa.
 
Jenerali anasema kazi za 'Kipuuzi' akimaanisha kuwa Ni kazi za 'burudani', sijamwelewa Jenerali hapo, pengine Jenerali angefafanua vyema tumuelewe!!! Kwan burudani ina mchango mkubwa Sana katika kupumzisha akili za watu.
 
Back
Top Bottom