Jenerali Ulimwengu amponda JK na wanachama wa SAIGON!!

Tuna exaggerate mambo?.

Saigon is gone. Kilikua kijiwe cha fitina kwenye siasa za Dar na mpira wa soka Simba na Yanga na "FAT". Wazee wamezeeka hakuna vijana.

Hawana nguvu wala hawajamweka JK madarakani. Wote tunamjua kingmaker ni nani na baadaye King akajiweka mwenyewe na familia yake. PERIOD

Mkuu punguza maneno makali (just kidin') si unajua Watanzania wanvyopenda kutengeneza vinyago halafu vinawatisha wenyewe!! Ni kama zile hadithi za chunusi au joka kubwa kwenye mti fulani......woga mtupu
 
kamanda heshima kwako kwanza,maana long time hatujakutana humu.Kiufupi Didas kampeni yote alipigiwa na saigon japo kweli sio member hata jerry pia,na si mara ya kwanza saigon kumpigia debe mtu asiekua member,utaratibu ni kwamba mtu akishikwa mkono akapelekwa pale na mtu wa pale anaeheshimika na wakamuelewa wanambeba tu,Didas na Jerry waliletwa na Idd simba ambae nadhani kila mtu anaujua uhusiano wa simba wa ilala na saigon


Kim za masiku aisee?
ulipotelea wapi?

sasa kuhusu hii ishu unasemaje pale wana daerasalaam pamoja na wana Saigon
walipoacha mwana Daresalaama mtoto wao Kleist Sykes akikosa hata udiwani na kuvuliwa
umeya na mtu wa kuja Kimbisa?
ulikuwepo?
nini kilitokea?
 
Huwezi ukawa Meya Dar bila kupitia Saigon,huyo Maaburi muulize atakwambia nani alimpeleka Saigon yeye pamoja na Jerry na mpaka Saigon iligawanyika kimtazamo kuhusu nani wamuunge mkono, maana kulikua na mtu ambae anaheshimika sana saigon ambae nae alikua akigombea na Didas.

Llakini Didas kuna mambo aliwaahidi Saigon na mpunga akawapa pia,sheikh zuberi wa msikiti wa mtoro kariakoo ni member anaeheshimika pale, akawakaza kitako wana Saigon akawaeleza hao watu wanaowajua toka wameanza kuwaunga mkono na kuwapa nafasi ya umeya wamefanya kipi cha maana kwa saigon na kwa jiji?

kukawa hakuna majibu akawaambia acheni upuuzi, huyu mtu sio mwenzetu(Didas)katambua uwepo wetu kaja kwa heshima zote kwetu kwa kuwa anajua umuhimu wetu tumpeni huyu...mambo mengi yakafanyika i can't share but ushindi wa Didas na Jerry Saigon wanahusika sana kupitia kwa Idd Simba aliyewapeka kina Didas Saigon
.
 
Kim za masiku aisee?
ulipotelea wapi?

sasa kuhusu hii ishu unasemaje pale wana daerasalaam pamoja na wana Saigon
walipoacha mwana Daresalaama mtoto wao Kleist Sykes akikosa hata udiwani na kuvuliwa
umeya na mtu wa kuja Kimbisa?
ulikuwepo?
nini kilitokea?

Well,ni hivi Kleist alijiponza mwenyewe,nimedokeza hapo juu kisa cha sheikh zuberi na wenzake kuhusu uungaji wa mkono wa mgombea wa umeya wa ilala na dar nzima ambayo ndio maeneo ya kujidai ya wazee wa saigon,kleist kuna mambo aliahidi lakini alipopata umeya akavimba kichwa hata club akawa hakanyagi yeye yuko busy na kina Ami mpungwe na huyu ulimwengu kule British legion club matokeo yake akaangushwa na kimbisa uchaguzi wa nyuma zaidi sio huu wa kina Didas na hata majina ya didas na kina tarimba yalipoletwa ikaja hoja ya uislam na udarisalama lakini sheikh zuberi na wenzake wakajenga hoja zao za kupinga uislam na udarisalama wakiutumia vyema mfano wa sykes,ambae alikua na sifa zote hizo,kwanza muislam pili mdarisalama kwelikweli tena mkariakoo haswa lakini hakuwafaa wazee ikaonekana bora hawa wakuja kina jerry na didas watakua na nidhamu kama wakiwapa kuliko mtu wanemjua na yeye anawajua,atawadharau akipata chakula
 
wandugu,

..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.

..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.

..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.

..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.








..Jenerali anaendelea zaidi hapa:



makala nzima ipo hapa:
Raia Mwema - Tumekuwa watu wa
kama vile mnajichanganya? kama mnajua haiwezekani kwa miaka 5 inakuwaje leo mnategemea kikwete awaletee maisha bora overnight (within 5years) wakati akina nyerere wameshindwa kwa miaka 45? ujinga. tatizo letu mnapenda sana njia za mkato na poyoyo nyiiiingi kuliko kufanya kazi. ujinga.
 
kama vile mnajichanganya? kama mnajua haiwezekani kwa miaka 5 inakuwaje leo mnategemea kikwete awaletee maisha bora overnight (within 5years) wakati akina nyerere wameshindwa kwa miaka 45? ujinga. tatizo letu mnapenda sana njia za mkato na poyoyo nyiiiingi kuliko kufanya kazi. ujinga.

Mkuu mjinga hapa ni nani? Huyo aliyeahidi maendeleo overnight au walioahidiwa?
 
JK sio mtu wa Saigon JK maskani yake ni Magomeni Mapipa (Shibamu).
 
Kijiwe bila mipango na maono kinaishia kuwa kijiwe tu..na products zake ni hizo hizo. Maneno meeeengi, vitendo hakuna! Sound mpaka huko Ikulu.
 
Mbona na Julius alikuwa mwana kijiwe pia? pia kuna home alone camp mwananyamala, Kwa msisiri mwananyamala, mpira pesa, sheibany magomeni mapipa, kiembe mbuzi vijiwe vipo vingi jamani hapa town msijitafutie sababu za kujitisha na kuogopa wenyewe.

Wengine wanavijiwe kwenye nyumba zao za ibada, sema tu majina tofauti ila vyote ni vijiwe kama saigon au mahala kwingine. Unaweza ita vijiwe, jumuhiya, vikundi na kadhalika. Sema tu wabongo mnachagua nani kafanya nini, watu wa mjini wengi wanakutana vijiweni.

Sio kweli watu vijiweni hawana maendeleo, Mbona Bakhresa anatoka kijiwe hiko hiko na Jenerali yupo anambwela mbwela miaka yote na habari corporation ilizidiwa na mwananchi kama yeye kichwa mpaka akasepa na mbona partner wake ni Rostam ambaye analalamikiwa mpaka basi katika printing, tamaduni za kiafrika ni kupambana to outsmart each other kila kukicha.
 
Kuendesha nchi si mchezo si sawa na kuendesha biashara ya duka la reja reja.Maelekezo ya kuongoza nchi yakitokea Saigon basi usishangae siku moja mkuu akatangaza na kusema leo tuna wafukuza machinga wote waende wakalime makwao bila kuwaandalia mazingira ya kilimo wakiwa huko makwao
 
saigon kwanza si nasikia imegawanyika imekua vipande vipande,wengine wamehamia pale livingstone kwenye baraza moja ya muuza kahawa na wengine wapo pale narung'ombe kwenye nyumba ambayo bakhresa anaitumia kama stoo yake ya kuhifadhia maji ya uhai,naomba ufafanuzi zaidi
 
Saigon ndo type hizo, kina Kitwana Kondo, marehemu kaka Dito (best man wa Kikwete) na Kikwete. Ukija na usomisomi wako utaulizwa "mjini umekuja lini? unajua kula chapati kwa mchuzi wewe?"

Kumbe ndio sababu hawapendi Wanyakyu......... sababu ya usomi wao!! Halafu watu wanashangaa mambo yanayowakuta wakina Mwakyembe, Mwaikusa etc.!!!!
 
Kuna msemo wa waswahili kuwa ukiwa muongo ni vyema usiwe msahaulifu. Sasa Kikwete wakati alipobadilisha baraza lake la mawaziri hivi karibuni aliwaambia wananchi kuwa baada ya kuwaondoa hao mawaziri kutoka wizara husika angewageukia makatibu wakuu na watendaji wengine wa hizo wizara ambao mara nyingi husababisha utendaji mbovu wa hizo wizara.

Lakini mpaka hivi leo na bunge la bajeti limekwisha kitambo jamaa ameisha sahau kama aliyasema maneno hayo. Anangojea ushauri toka Saigon.
 
kiranga -hivi utadhani kikwete ndo akuandalie timu ya vijana na mipango yote? wewe umefanya nini kufikia mafanikio unayoyatamani mpaka sasa? au ndo wale wenye kudandia na kulaumu kila jambo kwa kuwa wewe ni kinyume na JK? Mbona humsemi tenga ambaye ana dhamana ya kujenga mfumo wa mpira hapa TZ? Itakuwa nchi ya ajabu iwapo tunataka rais afanye kila kitu-alileta kocha wa kigeni baada ya kumuuliza tenga tutakwenda Ghana? maana yake si kwenda leo au kesho bali alitaka Tenga aweke mfumo wa kutuwezesha kufika huko baada ya kuwa na kocha wa kigeni-usiwe mwenye kulaum kila jambo jiulize wewe umefanya nini kufikia hapo unapotutaka tufike.
 
Kuchelewa si kusahau-serikali haibadilishwi kama vile unavyobadili nguo zako kila asubuhi-mambo yanakwenda kwa taratibu-ujue pia kuwa uteuzi na ubadilishaji wa makatibu na wakuregenzi si suala la kisiasa-ni la kitaaluma zaidi-unahitaji kuwa na uhakikia kuwa yule unayemweka badala ya awali ni bora kuliko nayeondoka-naamini wewe ukipewa utaanza pia kuangalia maslahi yako kwanza -si bora yule aliyepo kwa ubovu wake huo mdogo kuliko wewe ujae kwa ubovu mkubwa. Si lazima kila mabadiliko ya kitaaluma yanapofanywa yatangazwe kama ya kisiasa ndugu Ndinani
 
ufafanuzi RON PAUL kutoka kwa nani wakati wrewe ndo umesikia? Kama huna uhakikia ungenyamaza mpaka uupate ukweli ndo useme:director:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom