Jenerali Ulimwengu amponda JK na wanachama wa SAIGON!!

jmushi1
Ukisikia wazee wa Dae -es Salaam basi sii wengine isipokuwa wana Saigon ambapo hata mwalimu alikuwa kijiwe hicho..hawa ndio wanaamini kuwa chimbuko la TAA,TANU hadi CCM...

Mkuu labda ungetufafanulia sifa za kuwa member kwenye hicho chama. Je mikutano wanafanya, na wanafinyia wapi.? Na wananguvu kiasi gani kwenye siasa za nchi hii.? Mwisho nini ajenda yao kuu ndani ya nchi hii.??
 
Wakuu kwani mnazungumzia saigon hii ya hapa NARUNG'OMBE / LIVINGSTONE? Mbona ofisi yenyewe imechoka sana ,tena kunakipindi walikatiwa umeme,,mimi niliwahi kujichanganya siku moja kipindi rage amefungwa jela jamaa wakikuw wanajipanga kwenda kumbembelezea kwa mkulu.
 
Ndugu Mkandara ameshakuja hapa,kama una swali lolote kuhusiana na hilo,basi nina uhakika anaweza kukupatia jibu.Kama alivyosema hapo nyuma,hao inaonekana ni very powerful,kama alivyosema,mwalimu naye alikuwa member.Hilo kwakweli sikuwa nafahamu Mkandara endelea kutufahamisha zaidi mkuu,kuna rais aliyewahi kuchukuwa nchi bila sapoti yao?
Undani wake siwezi kuujua maana sisi ktk makuzi yetu tumeikuta Saigon huwezi kuingia pasipo kuwa introduced.. Ila nachofahamu watu wa Saigon ni kama Cartel ni CCM damu hawawezi kuhama chama na hawa ndio pia chimbuko la Mpira nchini toka Simba hadi Yanga enzi za marehemu Karume rais wa kwanza wa Zanzibar. Hawa walikuwa wanakula na kulala kwa Mpira na Siasa..

Kwa hiyo mapenzi ya mwalimu Nyerere na mpira nayo hayakuanza alipokuwa rais, na ndio maana tulifanya vizuri sana wakati wa mwalimu na Ujamaa kwa sababu tulicheza Mpira kwa mapenzi ya mchezo na Uzalendo. Leo hii sisi tumeachwa nyuma kwa sababu bado tunatumia fikra za Kijamaa wakati Mpira leo ni sehemu kubwa ya Ajira..Hivyo vijana huandaliwa kama sehemu ya maandalizi ya ajira ikiwa pamoja na sanaa na michezo. Tanzania bado tunachukulia haya kuwa ni anasa na mapenzi ya mtu. Kwa Tanzania hatuna sababu yoyote wala uwezo wa kuandaa kwa madaraja mpira wa miguu, isipokuwa shule zetu ndizo zinatakiwa kuwa chimbuko la wanamichezo bora nchini toka shule za msingi hadi Vyuo kabla ya kuingia legue kuu.

Shule zote zipewe daraja la juu kulingana na ushiriki wake kt michezo hasa mpira, riadha na sanaa. Shule hizi zipewe fedha zaidi ya zile zisizoshiriki yaani kuwepo na madaraja ya shule kulingana na ushiriki wake. hatuwezi kuandaa watu 28 walichaguliwa team ya taifa ili kwenda World cup au Olimpiki isipokuwa pale tunapoweza kuongeza nguvu ya ushindani ndani na kuwapa mafunzo ya juu zaidi..

Kuhusu mwalimu Mzungu au Mweusi halina maana yoyote ikiwa mmoja wao hana elimu ya juu ktk mchezo husika maana kama shule zetu Mwalimu atathaminika zaidi kwa uwezo wake wa kufundisha na sio rangi yake lakini pia mwalimu lazima awe kaelimika (kwa kusoma vitabu vya wazungu) kuhusu somo analofundisha. Hivyo kama kweli makocha wetu wameelimika vizuri ktk ngazi ya Ukocha na wamefikia daraja la juu kuwa Profesa basi bila shaka atafundisha timu ya taifa maana ni ujinga mkubwa kumwajiri lecture asiyekuwa na digrii ya juu kufundisha University.
 
Wakuu kwani mnazungumzia saigon hii ya hapa NARUNG'OMBE / LIVINGSTONE? Mbona ofisi yenyewe imechoka sana ,tena kunakipindi walikatiwa umeme,,mimi niliwahi kujichanganya siku moja kipindi rage amefungwa jela jamaa wakikuw wanajipanga kwenda kumbembelezea kwa mkulu.
Nasikia nyumba yenyewe imevunjwa sasa sielewi ni ktk kuijenga Saigon mpya au ndio wamesambaratika..
 
Ndugu Mkandara ameshakuja hapa,kama una swali lolote kuhusiana na hilo,basi nina uhakika anaweza kukupatia jibu.Kama alivyosema hapo nyuma,hao inaonekana ni very powerful,kama alivyosema,mwalimu naye alikuwa member.Hilo kwakweli sikuwa nafahamu Mkandara endelea kutufahamisha zaidi mkuu,kuna rais aliyewahi kuchukuwa nchi bila sapoti yao?

......SAIGON ina nguvu sana,aliyekuwa meya wa Ilala ABOU JUMA anaifahamu sana..alishikwa mkono na mzee KK-kitwana kondo na kupewa umeya wa jiji wakati huo..alipoupata akwadharau wazee wa kijiwe,akawa haendi tena kusalimia wakimtafuta ansema yuko bize...ikaundwa tume wazee wakamvaa waziri mkuu wakati huo SUMAYE...ikapigwa fitna ya nguvu kwamba jiji chafu,meya Abou kashidwa kazi....hahahaaaa!!!! kilichtokea ni waziri mkuu kuvunja halmashauli ya jiji na kuundwa TUME YA JIJI...mnamkumbuka KEENJA?...mheshimiwa Abou akarudi kijiweni...CHEZA na Saigon wewe....daaa nimeimis sana...wazee wa mujini!!!!
 
wandugu,

..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.

..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.

..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.

..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.

..Jenerali anaendelea zaidi hapa:

makala nzima ipo hapa:
Raia Mwema - Tumekuwa watu wa
mbona website imekufa?
 
Huyu Ulimwengu ni nani?
Ni mwandishi wa habri? Ni mhariri? Ni mwanaharakati?

Hivi karibuni waandishi wa habari kote nchini walifanya maandamano ya amani kulaani kitendo kilichofanywa na Polisi kwa kumuuwa mwandishi wa habari. Ulimwengu ulikuwa wapi? Hukuonekana na hata hukusikika kwa salamu.
 
Enzi za Saigon zinakwisha
Kikwete will be the last Saigon member kuongoza...

sometimes mnawapa credit kuubwa kuliko reality....

Saigon ni kijiwe tu cha kupiga story

na kama kijiwe chochote kila 'kujuana kuna faida zake'

hata huko Marekani kuna vijiwe vile vile....vyenye kujuana na watu kufaidika na kujuana huko......

waliosoma na The Kennedys au 'Harvard connections' na kadhalika
 
Saigon kwa sasa haina nguvu tena....hata ya kuweka Mbunge.....wale watoto wengi wa Mujini Kama kina mzee kitwana kondo,Sykes...et al wamezeeka ,...na wengine Kama kina Ditipile..,Mansour Magram etc....wamefariki..na hapana members vijana credible kuendeleza..
 
Didas Masaburi
sio member na amekuwa Mayor...
na wengi wengineo kina Jerry Silaha na yule alienunua mali za UDA...
Saigon inapewa sifa nyiingi kuliko hali halisi
 
Wakuu kwani mnazungumzia saigon hii ya hapa NARUNG'OMBE / LIVINGSTONE? Mbona ofisi yenyewe imechoka sana ,tena kunakipindi walikatiwa umeme,,mimi niliwahi kujichanganya siku moja kipindi rage amefungwa jela jamaa wakikuw wanajipanga kwenda kumbembelezea kwa mkulu.

Acha uwongo Saigon ni nyumba ya Bakhresa kuna maduka yake ya kuuza maji jumla wazee wamepewa milango miwili ndiyo maskani yao.
 
hahahaaaaaa... !! Michango ya leo imenivunja mbavu! Loh, kuna mambo yalikuwa yanasemwa semwa lakini sasa ukiunga unga unapata ukweli.
Ni kweli kabisa hapo Dar palikuwa na wenyewe. Ndiyo maana kuna ambao hawaamini yanayotokea sasa. Jiji linakuwa pia la wasioweza kula chapati kwa mchuzi.
 
jmushi1
Ukisikia wazee wa Dae -es Salaam basi sii wengine isipokuwa wana Saigon ambapo hata mwalimu alikuwa kijiwe hicho..hawa ndio wanaamini kuwa chimbuko la TAA,TANU hadi CCM...

Japo kwa ufupi lakini si mbaya umetoa picha, hawa jamaa ni kama enzi zile jamaa wa mjini walikuwa wanapenda kukaa Salamander cafe kwa issue mbalimbali za mjini?
 
Acha uwongo Saigon ni nyumba ya Bakhresa kuna maduka yake ya kuuza maji jumla wazee wamepewa milango miwili ndiyo maskani yao.

aliyekwambia si nyumba ya bakhresa nani? usiwe unakurupuka “like a dissatisfied woman!”
nimeuliza ni saigoni ya narung'ombe/livingstone au ipi? sasa uwongo unatoka wapi hapo? au haipo narung'ombe kkoo? think big bwana
 
Pole sn ulimwengu JK sijui kakukosea nn? hii si mara ya kwanza kumuandama, pamoja na kuwaachia uhuru wa kuongea haimaanishi uongee chochote km ajakupa shavu ww kampa mwenzio maana tupo wengi.Lkn nikuulize unaijua vzr SYIGON?????????????? Acheni wivu wa kike JK amefanya mengi sn mazuri tatizo tunaangalia vitu in negative way.
wandugu,

..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.

..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.

..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.

..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.

..Jenerali anaendelea zaidi hapa:

makala nzima ipo hapa:
Raia Mwema - Tumekuwa watu wa
 
Enzi za Saigon zinakwisha
Kikwete will be the last Saigon member kuongoza...

sometimes mnawapa credit kuubwa kuliko reality....

Saigon ni kijiwe tu cha kupiga story

na kama kijiwe chochote kila 'kujuana kuna faida zake'

hata huko Marekani kuna vijiwe vile vile....vyenye kujuana na watu kufaidika na kujuana huko......

waliosoma na The Kennedys au 'Harvard connections' na kadhalika

Umeongea ukweli mtupu.
Saigon ya sasa ni ya madereva wa teksi tu...yaani ushuzi mtupu.
Klabu nayoikubali hapa Dar ni ile ya Nyota nyekundu ambayO wao wana miradi yao na maendeleo kivyao na si kusifiwa kwa fitna...puumbav
 
Back
Top Bottom