Jenerali Ulimwengu amponda JK na wanachama wa SAIGON!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
wandugu,

..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.

..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.

..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.

..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.

Katika mahojiano ya kipindi cha KITIMOTO nilikumbana na mashabiki waliotoka Saigon ambao walikuwa wamekuja studio kusema upuuzi ule ule : Leta kocha wa kizungu, waweke vijana kambini miezi sita, tunawachapa hawa Waganda na Wakenya bila taabu yo yote, kisha tunakwenda kucheza Kombe la Dunia.

Nilichokuwa nashauri ni kwamba hatuna budi kufanya maandalizi katika ngazi kadhaa tukianzia na watoto wa umri wa miaka mitano na kuendelea kadri umri unavyopanda (U-14 ; U-17 ; U-21 na kadhalika) kwa kuwawekea madaraja hadi wawe wapevu, tukiwekeza bila kuchoka, tukitaraji kwamba vijana tulioanza nao wakiwa na miaka mitano watakuwa na miaka 20 baada ya miaka 15, na hawa wawe ndio tumaini la kwenda Kombe la Dunia.

Mashabiki wa Saigon wakapiga kelele : nani angojee miaka 15, bwana wewe ? Wewe leta kocha mzungu, weka vijana kambini…

Ajabu ni kwamba walikwisha kusahau kwamba tulikwisha kuwa na makocha wazungu (akina Celebic, Trautmann, Hudson nk) ambao hawakutupa matokeo kama ya akina Marijani Shaaban, Paul West Gwivaha na Joel Bendera). Kumbukumbu mara nyingi huwakimbia watu wasiojisumbua kuzitafuta.

..Jenerali anaendelea zaidi hapa:

Rais Jakaya Kikwete alipomuuliza Leodgar Tenga kama iwapo yeye (Kikwete) angemleta kocha wa kigeni na kumlipa, Tenga angetupeleka Ghana (mashindano ya CAN) na Tenga akajibu ‘Ndiyo'. Tulichokuwa tunakishuhudia ni ushabiki wa mkuu (kuamini kwamba kocha wa kigeni ndilo suluhisho) na soni ya mdogo (kulazimika kuitikia jambo asiloliamini kwa sababu kamera za TV zilikuwa zinatiririka).

Kocha mgeni alikuja, na mkuu akalipa, lakini hatukwenda Ghana, na inavyoelekea kwa muda mrefu ujao tutakuwa tunawasikia na kuwatazama wenzetu wanaokwenda CAN.

Hapa ndipo wanapokutana wale mashabiki wangu wa Saigon na wakuu wa nchi wanaoamini kwamba mambo yanaweza kufanywa haraka haraka na yakazaa matunda wakati hakuna mkakati endelevu wa kujenga hatua kwa hatua.

Tumekuwa watu wa " fasta fasta " na watu wa kuambiwa " kuwa mjanja " badala ya watu wa tafakuri na mipango inayolenga mbali.

makala nzima ipo hapa:
http://raiamwema.co.tz/tumekuwa-watu-wa-‘fasta-fasta’-tunafundishwa-‘kuwa-wajanja’
 
Rais mwenyewe anachagua mawaziri kwa mtindo wa Vodafasta, Ikulu inatumia email ya Yahoo -maana yake vi engineer vya Yahoo vikitaka kuchungulia emails za Ikulu yetu vinaweza- unategemea nini?

Kikwete si dhaifu tu -kuwa mwanadamu ni kuwa dhaifu kwa namna moja au nyingine- huyu ni goigoi.

Na huu utamaduni wa kutaka vitu harakaharaka tumeusema sana hapa. Bora Ulimwengu katumia kalamu yake kutuonyesha uzito wa tatizo.
 
wandugu,

..Jenerali angeweza kutumia mfano wa kijiwe chochote kile maana viko vingi, lakini ameamua kutaja kjiwe cha Saigon.

..kama mnavyoelewa JK amejitambulisha kama mwanachama wa kijiwe hicho.

..sasa katika makala hii, reading btn the lines, utaona Jenerali anadai nchi haisongi mbele kwasababu JK anaongozwa na mawazo na mitizamo toka kijiweni Saigon.

..kwa kweli JK anapaswa kujitafakari ktk kipindi hicho cha kuelekea mwisho wa utawala wake.

..Jenerali anaendelea zaidi hapa:

makala nzima ipo hapa:
Raia Mwema - Tumekuwa watu wa

Bila SAIGON Kikwete asinge panda juu hadi kufikiriwa kuwa RAIS... Kikwete ni MTOTO WA SAIGON; MZEE KITWANA KONDO

alikuwa Mmoja wa watu WA SAIGON ndio aliyependekeza JINA la KIKWETE kwa RAIS MWINYI...
 
mambo yakijiweni ya baki kijiweni ndio maaba nchi haiongozi vizuri maana anaokota mawazo kutoka kijiweni
 
Bila SAIGON Kikwete asinge panda juu hadi kufikiriwa kuwa RAIS... Kikwete ni MTOTO WA SAIGON; MZEE KITWANA KONDO

alikuwa Mmoja wa watu WA SAIGON ndio aliyependekeza JINA la KIKWETE kwa RAIS MWINYI...

Saigon ndo type hizo, kina Kitwana Kondo, marehemu kaka Dito (best man wa Kikwete) na Kikwete. Ukija na usomisomi wako utaulizwa "mjini umekuja lini? unajua kula chapati kwa mchuzi wewe?"
 
Saigon ndo type hizo, kina Kitwana Kondo, marehemu kaka Dito (best man wa Kikwete) na Kikwete. Ukija na usomisomi wako utaulizwa "mjini umekuja lini? unajua kula chapati kwa mchuzi wewe?"

ha ha ha, yaani hapo umenikumbusha uchaguzi wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam, kipindi kile Ditopile ni RC wa Dar, kitu kama 1994 au 95 hivi, Lutta Nelson alipogombea, Ditopile akaenda kupoiga kampeni akasema sio mnachagua watu hata Dar hawaijui, yaani hata tongotongo za kijijini kwao hazijawatoka, basi Lutta zengwe likamkuta akatoswa kwenye uchaguzi
sijawahi ona kiongozi yeyote toka Saigoni aliyepata kutuletea maendeleo iwe Dar, Mpirani au kitaifa, angalia KK alikuwa meya wa jiji miaka mingi na hakuna la maana alilofanya, Ditopile yeye ni uzinzi mpaka akawa anaitwa ukimuona mzurimzuri mtupie, angalia Ismail Aden Rage, tangu katibu TFF mpaka kwenye timu yangu niipendayo ya Simba, hamna jipya, sana sana atajifanya yeye mtoto wa njini anajua fitina wakati hamna maendeleo, JK nadhani sina la kusema, wote mnajua amekuwa rais wa aina gani,

kifupi members wa Saigon wamefanikiwa sana kupata vyeo mbalimbali hapa bongo na wanajua sana kuwafanyia fitina wenzao na kuwachafua majina lakini inapokuja kwenye sual la uongozi, wameprove failure vibaya
 
mkuu ndio chama gani hicho kinajishughulisha na nini.? Kipo nchi nzima au dar tu? Mtu yoyote anaweza kujiunga.??
Sidhani kama ni "mtu yeyote" anaweza kujiunga.Ngoja hata kuna watu wana fahamu vyema Mkandara atakuja hapa kukuelewesha kama akipenda,kulikuwepo na mjadala wa kuhusu Saigon humu na alionekana anapafahamu vyema na kuna wakati alistop by hapo kama sikosei.

Hicho ni kijiwe na chama at the same time kama sikosei.(mwanzoni kikiwa na mwelekeo wa issue za mpira wa miguu)

JK ndo alijipatia umaarufu hapo kwa kujidai ni mtu wa "kujichanganya"
 
Last edited by a moderator:
Hata Iddi Simba yupo Saigon, yeye ndiye aliyemshika mkono Didas Masaburi, kumpeleka kwa 'hao wenye mji'....
 
haaaaaaaaaaaaaa?SAIGON? yale malori yaliyoandsaigon ndo mali ya hicho kijiwe?THE HEGUE INAWASUBILIA
 
Sidhani kama ni "mtu yeyote" anaweza kujiunga.Ngoja hata kuna watu wana fahamu vyema Mkandara atakuja hapa kukuelewesha kama akipenda,kulikuwepo na mjadala wa kuhusu Saigon humu na alionekana anapafahamu vyema na kuna wakati alistop by hapo kama sikosei.

Hicho ni kijiwe na chama at the same time kama sikosei.(mwanzoni kikiwa na mwelekeo wa issue za mpira wa miguu)

JK ndo alijipatia umaarufu hapo kwa kujidai ni mtu wa "kujichanganya"

Asante kwa majibu hayo maana yamejibu maswali kadhaa niliyokuwa nayo.

Tunamwomba mkuu Mkandara afike hapa kibarazani atupe masimulizi kodigo ya hako ka ikulu kadogo.
 
Sidhani kama ni "mtu yeyote" anaweza kujiunga.Ngoja hata kuna watu wana fahamu vyema Mkandara atakuja hapa kukuelewesha kama akipenda,kulikuwepo na mjadala wa kuhusu Saigon humu na alionekana anapafahamu vyema na kuna wakati alistop by hapo kama sikosei.

Hicho ni kijiwe na chama at the same time kama sikosei.(mwanzoni kikiwa na mwelekeo wa issue za mpira wa miguu)

JK ndo alijipatia umaarufu hapo kwa kujidai ni mtu wa "kujichanganya"

mkuu asante kwa kunipa mwanga, ngoja waje wadau nadhani watatufafanulia zaidi...manake inaonekana hilo kundi/chama lina nguvu sana kwenye maamuzi serikalini.
 
Last edited by a moderator:
mkuu asante kwa kunipa mwanga, ngoja waje wadau nadhani watatufafanulia zaidi...manake inaonekana hilo kundi/chama lina nguvu sana kwenye maamuzi serikalini.
Ndugu Mkandara ameshakuja hapa,kama una swali lolote kuhusiana na hilo,basi nina uhakika anaweza kukupatia jibu.Kama alivyosema hapo nyuma,hao inaonekana ni very powerful,kama alivyosema,mwalimu naye alikuwa member.Hilo kwakweli sikuwa nafahamu Mkandara endelea kutufahamisha zaidi mkuu,kuna rais aliyewahi kuchukuwa nchi bila sapoti yao?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom