Jenerali Ulimwengu amfananisha Pinda na mbwa wa PAVLOV

Wakuu tunatakiwa kuvaa viatu vya Pinda, kabla ya kuanza kum-judge.
Ndugu yangu kama unayosema ni kweli basi huyo Pinda hafai, hafai na hafai. Mathalani tuseme hakubaliani na hali ilivyo, kwa nini kakubali kuvaa viatu vinavyompwaya ? Pinda kama walivyo viongozi wenzake wengi anatawaliwa na ulafi baada ya kuonja asali na mlafi hana budi kuwa mnafiki vinginevyo mate yatajaa mdomoni kama mbwa wa PAVLOV.
Can you imagine cabinet yetu ya sasa? try to compare it with that of Ben. Hao ndio watu anaofanya nao kazi Pinda, angalia JK na vision yake kwa Tanzania ( kama ipo), kama hakuna watu kwenye timu, kama hakuna malengo na strategy utafanya nini uwanjani, inabidi uwe unajifurahisha tu.
Kama nitakuwa naelewa sawa cabinet inateuliwa na Raisi kwa kushauriana na Waziri Mkuu hivyo kama kupwaya kwa cabinet wa kulaumiwa ni Kikwete na msaidizi wake Pinda. Kama Pinda angekuwa tofauti na viongozi wengine kutoka CCM na mtu mwenye msimamo asiyetawaliwa na unafiki, hiyo tabia ya ulafi hangekuwa nao kama mbwa wa PAVLOV.
Tusije tukadhani kuwa walioko serikalini ni wajinga sana, wanaona zaidi kuliko sisi tulio nje, lakini wamebanwa au hawataki kuonesha uzalendo kwa nchi, wanathamini chama zaidi.
Halafu bila aibu unasema kuna watu serikalini unaodai si wajinga na wanaona zaidi kuliko sisi tulio nje lakini kwa kubanwa au kutokutaka kuonesha uzalendo wanathamini chama zaidi. OMG ! kwa nini hatuiti koleo kwa jina lake ? Hawa watu kinachowabana ni matumbo yao, ulafi unaowafanya watokwe mate ovyo kama mbwa wa PAVLOV !
 
Alichokisema Ulimwengu si kwamba watanzania hatukifahamu ama hatuyafahamu.Tatizo letu kubwa ni kufurahi tu kwasababu kuna mtu ameandika yale tunayoyafahamu kwa namna ya kuvutia.Makala za kina Bagenda,Ulimwengu nk nilikuwa nikizisoma toka nikiwa bwana mdogo kabisa.

Nilikuwa nikizipenda makala hizo kwasababu ilikuwa ni faraja kutambua kuwa kuna watu ambao hawapendezwi na utawala na kwamba kumbe na wao wanafahamu upuuzi unaoendelea.Wlisaidia sana mageuzi na hata ndiyo maana Mrema alipata sapoti kubwa kipindi cha nyuma.Yote pia yalichangiwa na watu kama kina Ulimwengu.Vijana wadogo wanawasoma sana pia.

Hata hivyo sasa imeshakuwa kama utamaduni,kufurahia tu makala zenye kutuelezea yale tunayoyafahamu kwa namna ya kusisimua.Msisimko ukishazoeleka,basi inakuwa ni kama watu wanasubiri nyimbo ama albamu mpya ili waendelee kusisimka.

Nawasapoti wapambanaji hawa.Hatahivyo ni wakati wa kubadili namna ya kukabiliana na mafisadi na ujambazi dhidi ya mali za Taifa.Naamini ni wakati wa vitendo.Wengine tumechoshwa,we want to do something other than just analyzing on how bad the things are and how bad these people are....
We want to do something about those things and ofcourse something about those people.

Mambo kama haya yakishazoeleka inakuwa ni kama versions za filamu tu.Kinachofuatia ni mijadala tu na kubishana kuhusu versions hizo za makala.
 
Kuvimbiwa kwa watawala: Jibu si kuvua gamba

Jenerali Ulimwengu
22 Jun 2011
Toleo na 191

Wahitaji kula haluli kusafisha tumbo

SI kazi rahisi kwa yeyote miongoni mwetu kujaribu kueleza, na akaeleweka kuhusu nini kinatendeka hivi sasa katika siasa za nchi yetu, hususan kuhusu nafasi ya chama ambacho kimeliongoza Taifa hili kwa nusu karne sasa.

Yapo mambo mengi sana, ikiwa ni pamoja na matendo na matamko ambayo yanaashiria kwamba ndani ya chama hicho mchoko umefikia viwango vya kushangaza kwa wale wasiojua umetokea wapi.

Wapo watu wachache wanaojua, angalau kidogo, mchoko huo umetokea wapi, na nasaba yake ni nini, na wanajua jinsi ulivyoanza na jinsi ulivyoanza kukua ndani ya chama hicho hadi kufikia hali tunayoishuhudia leo, yaani hali ya mchoko wa hoi-bin-taaban.

Waswahili husema usiangalie ulipoangukia bali chunguza ni wapi ulipojikwaa, kwani anguko lako ni matokeo ya kujikwaa kwako, ambako usipoangalia unaweza ukakusahau ukiangalia tu pale ulipoangukia. Gharama mojawapo inayolipwa na mwangukaji asiyejua ni wapi alipojikwaa ni kuiona ardhi alipoangukia kama ndilo tatizo lake.

Siwezi kudai kwamba mimi binafsi nina uelewa mkubwa kuliko wa watu wengi kuhusu chanzo cha mchoko tunaouona, lakini ninaweza nikachanga mawazo yangu ambayo yanaweza, kwa kuchakatwa pamoja na ya wenzangu, yakatoa mwanga kidogo katika hili ninalolijadili sasa.

Naamini kwamba zoezi hili lina umuhimu wake kama tunataka kuepukana na zahma za kutupiana lawama, na hata kuumizana, kwa sababu ama hatutaki, ama hatuwezi kufanya tafakuri ya masafa marefu, na hamasa zetu zisizo na mafunzo zinatutuma kutafuta majibu mepesi mepesi na majibizano yasiyosumbua akili.

Kwa kuwa mjadala huu hauna budi kuingia katika mijadala mipana inayoendelea kuhusu umuhimu wa kubadili kwa kina namna tunavyoendesha shughuli zetu za kitaifa, masuala kama vile ya Katiba mpya na mipangilio mipya ya kisiasa na kiutawala, bila shaka yataibuka mara kwa mara, na hivyo ndivyo ilivyo katika mjadala wo wote ambao unaangalia masuala kwa mtazamo kamilifu (holistic). Kwa jinsi hii tuanweza tukatambua mti mmoja mmoja na pia tukatambua msitu ambamo ndani yake ndimo inapatikana miti hiyo.

Uvuaji gamba

Leo hii ningependa nijiunge na wale wanaojadili suala la chama-tawala kufanya kila kilichopachikwa jina la ‘kuvua gamba’. Nisingependa kuingilia mijadala ya kishabiki na mabezo mengi yaliyotolewa katika vyombo vya habari kuhusu uteuzi wa nahau ya kuvua gamba, ambayo imeelekezwa moja kwa moja upande wa silka ya nyoka. Nitaliacha hilo, kwa sababu naamini halina uzito mkubwa kwani ni utelezi wa ulimi ambao naamini katika miezi ijayo hatutausikia sana.

Mimi nitakwenda katika dhana yenyewe ya kutaka kujisafisha kwa kuwaondoa katika nafasi za uongozi wanachama watatu,au watano, au 10, au 20, au 40, au hata 100. Nimekuwa nikifuatilia mijadala (nyingi zikiwa ni kelele) kuhusu ‘mapacha’ ambao wanatakiwa ‘watoswe’ ili ‘kukinusuru chama.’

Inaelekea mantiki iliyotumika ni kwamba hawa watu wamekipa chama-tawala jina baya machoni mwa Watanzania kwa sababu wao ndio wanaosemwa sana kwamba wanahusika na ufisadi, na kwa hiyo ikiwezekana ‘kuwatosa’ chama kitakuwa kimejitakasa mbele ya wananchi, nao wananchi wataanza kutuamini tena na kuturuhusu tuwaongoze.

Utaalamu wangu mdogo wa masuala ya kisiasa haunipi taswira ya chama ambacho kwa kuwaondoa watu watatu au wanne, au hata 100, kinakuwa kimejisafisha kwa kufanya hilo tu. Sijasikia chama hicho kikijadili au kupendekeza mapitio ya misingi ya kifalsafa na kiitikadi ndani ya chama hicho; mijadala ya programu za kisiasa; marejeo ya sera za chama kuhusu utekelezaji wa programu hizo za kisiasa; wala miundo yake itakuwa ipi ili kubeba programu hizo na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika inavyopasa; wala maandalizi ya makada wenye uangavu wa msimamo unaowawezesha kutekeleza programu hizo.

Ninachosikia, na ambacho kinachosha kama walivyochoka wanaokiendeleza, ni ‘kuvua gamba’, ni kupambana hadi ‘tone la mwisho la damu’ na mambo mengine ambayo, kusema kweli, mimi nayaona ni ya kipuuzi. Hao ‘mapacha’ wana nguvu gani ndani ya chama ambayo wamejilimbikizia kwa kuipora bila wanachama na mifumo ya chama hicho kujua?

Ni lini hasa walipoanza kuwa na nguvu hii, na wenzao ndani ya chama walikuwa wanafanya nini wakati wote huo, na leo ndiyo wanatanabahi wakati ‘mapacha’ wamekwisha kukiteka chama kizima kiasi kwamba nusura ya chama ni kwa hao ‘mapacha’ kuondoka?

Hebu tujiulize, hicho ni chama cha siasa kinachoongoza serikali au ni chama cha wacheza dhumna? Hata wacheza dhumna, pale Saigon mathalan, huwezi kuchezea chama chao kwa muda wa wiki mbili, ukafanya mambo yanayowaudhi wanachama wengime, halafu ukawa salama na wakakuachia uendelee kuendesha shughuli za chama chao.

Seuze kwa chama kinachoongoza serikali. Wote wanaozungumzwa hivi leo wamewahi kuwa na nyadhifa kubwa katika chama-tawala, na wengine katika serikali. Hao wanaotaka tuamini kwamba hawa ni watu hatari kiasi hicho hawana budi waseme pia ni kwa nini wananchi wa Tanzania waendelee kukiamini chama hicho ambacho kinafanya kazi kama kimelala usingizi hadi kizinduke miaka kadhaa baada ya mambo kuwa yamekwenda hovyo.

Msimamo wangu

Nieleze msimamo wangu kuhusu hao ‘mapacha’ maarufu. Kwanza sidhani miongoni mwao yupo hata mmoja ambaye anazo sifa za kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania, kama tunaitakia mema nchi hii.

Niseme ukweli wangu: Naamini hadi sasa, na hili nitaliamini hadi kufa, kwamba, kwa jinsi nchi ilvyovurugika, tunahitaji Julius Nyerere mpya, ambaye nitamweleza baadaye, ambaye ataongoza mapambano ya ukombozi mpya wa nchi hii na wananchi wake.

Katika hao wanaotajwa hakuna mtu wa aina hiyo, na kwangu mimi ye yote mwenye njozi za aina hiyo angefanya vyema kutia tamati na afanye mambo mengine.

Lakini si lazima waondoke katika chama-tawala kwa ajili eti ya kukisafisha. Kwa kuwa kwa njia hiyo hakisafishiki. Muasisi wa chama hicho, Mwalimu Nyerere alikwisha kukiona chama chake kwamba kimechafuka mno kiasi kwamba sababu moja iliyomsukuma kufanya kampeni ya kurejesha mfumo wa vyama vingi (aliokuwa ameukomesha mwenyewe) ilikuwa ni kupata vyama vya kukizindua chama-tawala kutoka usingizi wa pono kiliokuwa kimelala.

Badala ya chama-tawala kuuelewa msimamo wa Kambarage na kufanya marekebisho ndani yake kwa kunoa falsafa yake na kutakasa itikadi yake, kikazidi kujichimbia katika kila aina ya uovu na kukaribisha kila aina ya wanachama wasio na nasaba yo yote na chama hicho.

Chama cha makabwela (Baba kabwela UNO- kumbuka) kikageuka, kikawa ni chama cha wenye ‘vijisenti.’ Naye Mwalimu aliwauliza warithi wake katika utawala: Tumefanya mambo mengi mabaya, lakini pia tumefanya machache mazuri. Mbona inaelekea nyiye mnang’ang’ania mabaya yetu na mazuri yetu hamyataki?

Hali hii haikutokea ghafla, na wala haikusababishwa na hao mapacha maarufu. Pia si kweli kwamba hakukuwa na watu wa kutahadharisha kuhusu hatari ya chama kutekwa na siasa zisizokuwa zake. Wale waliokuwa ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kati ya miaka 1992 na 1997 watakumbuka kwamba baadhi yetu tulisema, tukazomewa na wajumbe wachovu waliokuwa na haraka ya kuwahi kula nyama-choma mnadani Dodoma. Wenye kumbukumbu na wakumbuke.

Nayaandika haya leo, na (Insha Allah) nitayaandika mengine mengi katika kipindi hiki, kwa sababu miaka inakwenda, tunazidi kuwa watu wazima, wengi miongoni mwetu wanaondoka, nasi tu njiani pasi na shaka. Nayaandika haya, ili angalau wale ambao bado wangali hai, waseme kama huu ni uongo.

Baadhi yetu tulifadhaika kuona chama kilichoanzishwa chini ya siasa ya utu na udugu wa binadamu wote kikigeuka kuwa chama cha manyang’au wasiojali watu bali wanajali vitu, chama kilichosimamia misingi ya haki kwa wote kikigeuka chombo cha utetezi wa wenye nguvu dhidi ya wanyonge.

Chama kilichonasibika Afrika na dunia nzima kuwa ngao ya kutetea nchi na mali zake kikibadilika na kuwa chama-na-serikali-dalali cha kuuza nchi na rasilimali zake kila kinapopata fursa ya kufanya hivyo.

Sasa, na aseme mtu kwamba haya yote wamefanya mapacha wetu maarufu, na wakiondoka ndani ya chama hicho, chama kitarejea misingi yake ya kale, nami nitajiunga na maandamano ya kuwang’oa hao mapacha maarufu.Wenyewe wanajua lakini wanajifanya hamnazo.

Ni kweli baadhi ya mambo yaliyofanywa na mapacha maarufu ni ya hovyo, na mengi hayahitaji mjadala, lakini je, ni wao peke yao? Tukiisha ‘kuwatosa’ (Waswahili kwa kupenda kutosana!) ndiyo tutakuwa tumemaliza kazi?

Hao ‘watosaji’ na wanaovua magamba bila mpangilio wanajua kwamba kwa muda mrefu chama chao na serikali yao vimetekeleza sera za ugawaji (‘uuzaji’ wanasema wasiojua Kiswahili) mali za Taifa kwa bure, bure! Mifano ni mingi: madini yetu na Benki ya Taifa, na sasa ardhi kwa ajili ya kilimo cha petroli. Nyerere alipopiga kelele kuhusu kuigawa benki yetu kwa Makaburu alipuuzwana kudharauliwa ungedhani aliyesema Jenerali miye.Kisa, wakubwa wa Washington wamesema, na watawala wetu wakiambiwa na wakuu hao ‘Ruka!’ wanachouliza watawala wetu ni ‘Hadi wapi?’

Yamesemwa mengi, nami sina haja ya kuyarejea yote, kwani wakati mwingine yanatia kinyaa... rada, ndege, ma-green na ma-meremeta, nyumba za serikali walizogawiwa maofisa waliochaguana katika wizi wa mchana ambao haujawahi kutokea, hata Nigeria.

Mwenyekiti wa chama-tawala wakati huo aliamua kwenda mbali zaidi kwa kujizawadia mgodi mzima wa serikali, kama mjasiriamali-mamboleo. Chama chake, kimya! Najiuliza hilo gamba wanalosema wanajivua ni gamba lipi, mbona yako mengi? Na wakitaka kutafuta mapacha wa ‘kuwatosa’ si itawabidi wapange mafungu kadhaa ya mapacha, halafu waanze kuwatosa kwa zamu, kila fungu na msimu wake wa ‘kutoswa?’ Na hawatawamaliza, jinsi walivyo wengi na walivyokikamata chama chao.

Ubanaji posho za vikao

Sasa hebu tuangalie namna ya kujivua gamba hili jingine. Kama alivyotabiri Kambarage, kumbuka, chama kikuu cha upinzani kimeamua kuitikisa misingi mibovu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuasisi wazo la kubana posho za vikao ambazo kinadhani si halali hata kama zinalipwa kwa utaratibu uliowekwa kisheria (kumbuka kila kinachofanyika kisherria si lazima kiwe halali; ndiyo tofauti kati ya legal au lawful na legitimate).

Jinsi alivyolileta Kabwe Zitto suala hili lilizua malumbano kana kwamba ni tatizo kati yake na Ofisi ya Spika, lakini baadaye ikaonekana kwamba ni sera ya CHADEMA ambayo inaambatana na mahesabu ya bajeti ambamo wanapendekeza kuokoa shilingi bilioni 900 kwa kufuta posho zisizokuwa na maelezo isipokuwa mazoea ya kula bila kufikiri, zoezi ambalo wanapendekeza liguse ngazi zote za serikali.

Mjadala haujafanyika kuhusu hili, lakini kinachosikika ni kelele zaidi, kwani inaelekea chama-tawala hakijaamua kifanye nini kuhusu hili, na hapa napo kimechelewa, kinafuata yale yanayosemwa na wengine, kama kinadhani yanawavutia wananchi, badala ya kuongoza. Na kama kawaida yao, inaelekea hawajakubaliana miongoni mwao: msemaji wa chama anasema lake, kiongozi wa serikali anasema lake.

Lakini ni msemaji wa serikali aliyenivutia. Waziri Mkuu Mizengo Pinda anasema kwamba hizi ni posho za kawaida tu, na wala mtu asije akataka kuwaambia wananchi kwamba wabunge wanawaibia. Sawa, wabunge hawaibi kwa sababu kisheria posho hizi zimepangwa. Hata hivyo, nadhani wanachosema CHADEMA, kama nimeelewa vyema, si kwamba wabunge wanaiba, la hasha, bali kwamba hizi posho hazina uhalali kwa sababu tayari wabunge wanalipwa mishahara na posho stahili na maridhawa, na kwamba fedha zinazoweza kuokolewa kwa kufuta hizi kodi zingekuwa na manufaa kwa wananchi.

Hapa tena niseme kwamba nashindwa kuelewa ugumu wa kulielewa hili unatoka wapi. Kama mbunge analipwa mshahara wa mwezi, kisha analipwa masurufu ya kuwa kazini nje ya kituo chake, posho ya kikao, ambacho ndiyo kazi yake ni ya nini? Ni nini cha zaidi anachofanya kuliko kuhudhuria kikao cha Bunge ambacho ndicho kimempeleka Dodoma na ambacho kwacho amelipwa per diem?

Maneno mengine hayapendezi, na si jambo jema kumsuta waziri mkuu, hasa kwa sababu Pinda ninamheshimu sana. Lakini haipendezi kusema eti hata hao wabunge wa Upinzani “wanazimezeamezea mate fedha hizo, lakini wafanyeje?” Nini maana yake? Kwamba wangekuwa huru kusema wangesema wapewe hizo fedha lakini labda wamebanwa na uongozi wao? Nini hasa maana yake, kwamba mtu wa kawaida atazimezeamezea mate tu hizo posho hata kama hazina sababu, na kwa hiyo ni halali zilipwe, kwa sababu ya kumezewamezewa mate?

Hapa hakuna msaada wa kujisafisha kitakaopata chama-tawala kupitia njia ya kujivua gamba. Shughuli inayomezewamezewa mate hapa haina uhusiano na gamba la mnyama ye yote, bali inahusu tumbo. Mate ya mbwa wa Pavlov huanza kumdondoka anapopata ishara kwamba mlo wake unakaribia, na mlo wake ukicheleweshwa inabidi ameze mate. Sijui kama hivyo ndivyo wanavyofanya wabunge wa Upinzani.

Lakini wale wanaoendelea kutaka kula hicho chakula ambacho wenzao wanakimezea mate ajue kwamba wananchi sasa wamejua kwamba wawakilishi wao wanalipwa masurufu wasiyostahili, hata kama wanalipwa kisheria.

‘Mavyakula’ kama haya hayaathiri afya ya ngozi, bali huathiri tumbo. Kulakula hovyo ni dalili ya ulafi, na ulafi ni mojawapo ya dhambi za mauti, hasa kwa Wakristo. Miongoni mwa mambo mengi wanayolalamikia wananchi wetu, moja kubwa ni ulafi wa watawala wao katika mazingira ya hali mbaya mno za maisha ya watu wa kawaida.

Chama cha upinzani kitakuwa si chama cha upinzani kama kitashindwa kuliona hilo na kuwapiga nalo watawala na kupata kuungwa mkono na wananchi.

Tamko jingine la kushangaza ni lile la Mustafa Mkulo anayesema kwamba wanaokataa posho wanatafuta umaarufu wa kisiasa. Sasa je, ni mwanasiasa gani asiyetafuta umaarufu wa kisiasa? Suala ni kujua umaarufu huo anautafuta kwa mbinu gani, mbinu za kuwaangamiza watu wake au za kuwasaidia?

Kiafya, ulafi husababisha mtu kuvimbiwa, na kuvimbiwa dawa yake si kuvua gamba bali ni kula haluli (laxative) inayosafisha tumbo chafu na kutoa uchafu wote nje. Katika makala ijayo nitaijadili hiyo haluli wanayohitaji watawala wetu.

Asente Jenerali asavali umelonga hii mijitu imeweka nta masikioni
 
Kuvimbiwa kwa watawala: Jibu si kuvua gamba

Jenerali Ulimwengu
22 Jun 2011
Toleo na 191

Wahitaji kula haluli kusafisha tumbo

SI kazi rahisi kwa yeyote miongoni mwetu kujaribu kueleza, na akaeleweka kuhusu nini kinatendeka hivi sasa katika siasa za nchi yetu, hususan kuhusu nafasi ya chama ambacho kimeliongoza Taifa hili kwa nusu karne sasa.

Yapo mambo mengi sana, ikiwa ni pamoja na matendo na matamko ambayo yanaashiria kwamba ndani ya chama hicho mchoko umefikia viwango vya kushangaza kwa wale wasiojua umetokea wapi.

Wapo watu wachache wanaojua, angalau kidogo, mchoko huo umetokea wapi, na nasaba yake ni nini, na wanajua jinsi ulivyoanza na jinsi ulivyoanza kukua ndani ya chama hicho hadi kufikia hali tunayoishuhudia leo, yaani hali ya mchoko wa hoi-bin-taaban.

Waswahili husema usiangalie ulipoangukia bali chunguza ni wapi ulipojikwaa, kwani anguko lako ni matokeo ya kujikwaa kwako, ambako usipoangalia unaweza ukakusahau ukiangalia tu pale ulipoangukia. Gharama mojawapo inayolipwa na mwangukaji asiyejua ni wapi alipojikwaa ni kuiona ardhi alipoangukia kama ndilo tatizo lake.

Siwezi kudai kwamba mimi binafsi nina uelewa mkubwa kuliko wa watu wengi kuhusu chanzo cha mchoko tunaouona, lakini ninaweza nikachanga mawazo yangu ambayo yanaweza, kwa kuchakatwa pamoja na ya wenzangu, yakatoa mwanga kidogo katika hili ninalolijadili sasa.

Naamini kwamba zoezi hili lina umuhimu wake kama tunataka kuepukana na zahma za kutupiana lawama, na hata kuumizana, kwa sababu ama hatutaki, ama hatuwezi kufanya tafakuri ya masafa marefu, na hamasa zetu zisizo na mafunzo zinatutuma kutafuta majibu mepesi mepesi na majibizano yasiyosumbua akili.

Kwa kuwa mjadala huu hauna budi kuingia katika mijadala mipana inayoendelea kuhusu umuhimu wa kubadili kwa kina namna tunavyoendesha shughuli zetu za kitaifa, masuala kama vile ya Katiba mpya na mipangilio mipya ya kisiasa na kiutawala, bila shaka yataibuka mara kwa mara, na hivyo ndivyo ilivyo katika mjadala wo wote ambao unaangalia masuala kwa mtazamo kamilifu (holistic). Kwa jinsi hii tuanweza tukatambua mti mmoja mmoja na pia tukatambua msitu ambamo ndani yake ndimo inapatikana miti hiyo.

Uvuaji gamba

Leo hii ningependa nijiunge na wale wanaojadili suala la chama-tawala kufanya kila kilichopachikwa jina la ‘kuvua gamba'. Nisingependa kuingilia mijadala ya kishabiki na mabezo mengi yaliyotolewa katika vyombo vya habari kuhusu uteuzi wa nahau ya kuvua gamba, ambayo imeelekezwa moja kwa moja upande wa silka ya nyoka. Nitaliacha hilo, kwa sababu naamini halina uzito mkubwa kwani ni utelezi wa ulimi ambao naamini katika miezi ijayo hatutausikia sana.

Mimi nitakwenda katika dhana yenyewe ya kutaka kujisafisha kwa kuwaondoa katika nafasi za uongozi wanachama watatu,au watano, au 10, au 20, au 40, au hata 100. Nimekuwa nikifuatilia mijadala (nyingi zikiwa ni kelele) kuhusu ‘mapacha' ambao wanatakiwa ‘watoswe' ili ‘kukinusuru chama.'

Inaelekea mantiki iliyotumika ni kwamba hawa watu wamekipa chama-tawala jina baya machoni mwa Watanzania kwa sababu wao ndio wanaosemwa sana kwamba wanahusika na ufisadi, na kwa hiyo ikiwezekana ‘kuwatosa' chama kitakuwa kimejitakasa mbele ya wananchi, nao wananchi wataanza kutuamini tena na kuturuhusu tuwaongoze.

Utaalamu wangu mdogo wa masuala ya kisiasa haunipi taswira ya chama ambacho kwa kuwaondoa watu watatu au wanne, au hata 100, kinakuwa kimejisafisha kwa kufanya hilo tu. Sijasikia chama hicho kikijadili au kupendekeza mapitio ya misingi ya kifalsafa na kiitikadi ndani ya chama hicho; mijadala ya programu za kisiasa; marejeo ya sera za chama kuhusu utekelezaji wa programu hizo za kisiasa; wala miundo yake itakuwa ipi ili kubeba programu hizo na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika inavyopasa; wala maandalizi ya makada wenye uangavu wa msimamo unaowawezesha kutekeleza programu hizo.

Ninachosikia, na ambacho kinachosha kama walivyochoka wanaokiendeleza, ni ‘kuvua gamba', ni kupambana hadi ‘tone la mwisho la damu' na mambo mengine ambayo, kusema kweli, mimi nayaona ni ya kipuuzi. Hao ‘mapacha' wana nguvu gani ndani ya chama ambayo wamejilimbikizia kwa kuipora bila wanachama na mifumo ya chama hicho kujua?

Ni lini hasa walipoanza kuwa na nguvu hii, na wenzao ndani ya chama walikuwa wanafanya nini wakati wote huo, na leo ndiyo wanatanabahi wakati ‘mapacha' wamekwisha kukiteka chama kizima kiasi kwamba nusura ya chama ni kwa hao ‘mapacha' kuondoka?

Hebu tujiulize, hicho ni chama cha siasa kinachoongoza serikali au ni chama cha wacheza dhumna? Hata wacheza dhumna, pale Saigon mathalan, huwezi kuchezea chama chao kwa muda wa wiki mbili, ukafanya mambo yanayowaudhi wanachama wengime, halafu ukawa salama na wakakuachia uendelee kuendesha shughuli za chama chao.

Seuze kwa chama kinachoongoza serikali. Wote wanaozungumzwa hivi leo wamewahi kuwa na nyadhifa kubwa katika chama-tawala, na wengine katika serikali. Hao wanaotaka tuamini kwamba hawa ni watu hatari kiasi hicho hawana budi waseme pia ni kwa nini wananchi wa Tanzania waendelee kukiamini chama hicho ambacho kinafanya kazi kama kimelala usingizi hadi kizinduke miaka kadhaa baada ya mambo kuwa yamekwenda hovyo.

Msimamo wangu

Nieleze msimamo wangu kuhusu hao ‘mapacha' maarufu. Kwanza sidhani miongoni mwao yupo hata mmoja ambaye anazo sifa za kuwa kiongozi mkuu wa Tanzania, kama tunaitakia mema nchi hii.(Hapa ndio kisu kilipogonga mfupa!)

Niseme ukweli wangu: Naamini hadi sasa, na hili nitaliamini hadi kufa, kwamba, kwa jinsi nchi ilvyovurugika, tunahitaji Julius Nyerere mpya, ambaye nitamweleza baadaye, ambaye ataongoza mapambano ya ukombozi mpya wa nchi hii na wananchi wake.

Katika hao wanaotajwa hakuna mtu wa aina hiyo, na kwangu mimi ye yote mwenye njozi za aina hiyo angefanya vyema kutia tamati na afanye mambo mengine.

Lakini si lazima waondoke katika chama-tawala kwa ajili eti ya kukisafisha. Kwa kuwa kwa njia hiyo hakisafishiki. Muasisi wa chama hicho, Mwalimu Nyerere alikwisha kukiona chama chake kwamba kimechafuka mno kiasi kwamba sababu moja iliyomsukuma kufanya kampeni ya kurejesha mfumo wa vyama vingi (aliokuwa ameukomesha mwenyewe) ilikuwa ni kupata vyama vya kukizindua chama-tawala kutoka usingizi wa pono kiliokuwa kimelala.

Badala ya chama-tawala kuuelewa msimamo wa Kambarage na kufanya marekebisho ndani yake kwa kunoa falsafa yake na kutakasa itikadi yake, kikazidi kujichimbia katika kila aina ya uovu na kukaribisha kila aina ya wanachama wasio na nasaba yo yote na chama hicho.

Chama cha makabwela (Baba kabwela UNO- kumbuka) kikageuka, kikawa ni chama cha wenye ‘vijisenti.' Naye Mwalimu aliwauliza warithi wake katika utawala: Tumefanya mambo mengi mabaya, lakini pia tumefanya machache mazuri. Mbona inaelekea nyiye mnang'ang'ania mabaya yetu na mazuri yetu hamyataki?

Hali hii haikutokea ghafla, na wala haikusababishwa na hao mapacha maarufu. Pia si kweli kwamba hakukuwa na watu wa kutahadharisha kuhusu hatari ya chama kutekwa na siasa zisizokuwa zake. Wale waliokuwa ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kati ya miaka 1992 na 1997 watakumbuka kwamba baadhi yetu tulisema, tukazomewa na wajumbe wachovu waliokuwa na haraka ya kuwahi kula nyama-choma mnadani Dodoma. Wenye kumbukumbu na wakumbuke.

Nayaandika haya leo, na (Insha Allah) nitayaandika mengine mengi katika kipindi hiki, kwa sababu miaka inakwenda, tunazidi kuwa watu wazima, wengi miongoni mwetu wanaondoka, nasi tu njiani pasi na shaka. Nayaandika haya, ili angalau wale ambao bado wangali hai, waseme kama huu ni uongo.

Baadhi yetu tulifadhaika kuona chama kilichoanzishwa chini ya siasa ya utu na udugu wa binadamu wote kikigeuka kuwa chama cha manyang'au wasiojali watu bali wanajali vitu, chama kilichosimamia misingi ya haki kwa wote kikigeuka chombo cha utetezi wa wenye nguvu dhidi ya wanyonge.

Chama kilichonasibika Afrika na dunia nzima kuwa ngao ya kutetea nchi na mali zake kikibadilika na kuwa chama-na-serikali-dalali cha kuuza nchi na rasilimali zake kila kinapopata fursa ya kufanya hivyo.

Sasa, na aseme mtu kwamba haya yote wamefanya mapacha wetu maarufu, na wakiondoka ndani ya chama hicho, chama kitarejea misingi yake ya kale, nami nitajiunga na maandamano ya kuwang'oa hao mapacha maarufu.Wenyewe wanajua lakini wanajifanya hamnazo.

Ni kweli baadhi ya mambo yaliyofanywa na mapacha maarufu ni ya hovyo, na mengi hayahitaji mjadala, lakini je, ni wao peke yao? Tukiisha ‘kuwatosa' (Waswahili kwa kupenda kutosana!) ndiyo tutakuwa tumemaliza kazi?

Hao ‘watosaji' na wanaovua magamba bila mpangilio wanajua kwamba kwa muda mrefu chama chao na serikali yao vimetekeleza sera za ugawaji (‘uuzaji' wanasema wasiojua Kiswahili) mali za Taifa kwa bure, bure! Mifano ni mingi: madini yetu na Benki ya Taifa, na sasa ardhi kwa ajili ya kilimo cha petroli. Nyerere alipopiga kelele kuhusu kuigawa benki yetu kwa Makaburu alipuuzwana kudharauliwa ungedhani aliyesema Jenerali miye.Kisa, wakubwa wa Washington wamesema, na watawala wetu wakiambiwa na wakuu hao ‘Ruka!' wanachouliza watawala wetu ni ‘Hadi wapi?'

Yamesemwa mengi, nami sina haja ya kuyarejea yote, kwani wakati mwingine yanatia kinyaa... rada, ndege, ma-green na ma-meremeta, nyumba za serikali walizogawiwa maofisa waliochaguana katika wizi wa mchana ambao haujawahi kutokea, hata Nigeria.

Mwenyekiti wa chama-tawala wakati huo aliamua kwenda mbali zaidi kwa kujizawadia mgodi mzima wa serikali, kama mjasiriamali-mamboleo. Chama chake, kimya! Najiuliza hilo gamba wanalosema wanajivua ni gamba lipi, mbona yako mengi? Na wakitaka kutafuta mapacha wa ‘kuwatosa' si itawabidi wapange mafungu kadhaa ya mapacha, halafu waanze kuwatosa kwa zamu, kila fungu na msimu wake wa ‘kutoswa?' Na hawatawamaliza, jinsi walivyo wengi na walivyokikamata chama chao.

Ubanaji posho za vikao

Sasa hebu tuangalie namna ya kujivua gamba hili jingine. Kama alivyotabiri Kambarage, kumbuka, chama kikuu cha upinzani kimeamua kuitikisa misingi mibovu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuasisi wazo la kubana posho za vikao ambazo kinadhani si halali hata kama zinalipwa kwa utaratibu uliowekwa kisheria (kumbuka kila kinachofanyika kisherria si lazima kiwe halali; ndiyo tofauti kati ya legal au lawful na legitimate).

Jinsi alivyolileta Kabwe Zitto suala hili lilizua malumbano kana kwamba ni tatizo kati yake na Ofisi ya Spika, lakini baadaye ikaonekana kwamba ni sera ya CHADEMA ambayo inaambatana na mahesabu ya bajeti ambamo wanapendekeza kuokoa shilingi bilioni 900 kwa kufuta posho zisizokuwa na maelezo isipokuwa mazoea ya kula bila kufikiri, zoezi ambalo wanapendekeza liguse ngazi zote za serikali.

Mjadala haujafanyika kuhusu hili, lakini kinachosikika ni kelele zaidi, kwani inaelekea chama-tawala hakijaamua kifanye nini kuhusu hili, na hapa napo kimechelewa, kinafuata yale yanayosemwa na wengine, kama kinadhani yanawavutia wananchi, badala ya kuongoza. Na kama kawaida yao, inaelekea hawajakubaliana miongoni mwao: msemaji wa chama anasema lake, kiongozi wa serikali anasema lake.

Lakini ni msemaji wa serikali aliyenivutia. Waziri Mkuu Mizengo Pinda anasema kwamba hizi ni posho za kawaida tu, na wala mtu asije akataka kuwaambia wananchi kwamba wabunge wanawaibia. Sawa, wabunge hawaibi kwa sababu kisheria posho hizi zimepangwa. Hata hivyo, nadhani wanachosema CHADEMA, kama nimeelewa vyema, si kwamba wabunge wanaiba, la hasha, bali kwamba hizi posho hazina uhalali kwa sababu tayari wabunge wanalipwa mishahara na posho stahili na maridhawa, na kwamba fedha zinazoweza kuokolewa kwa kufuta hizi kodi zingekuwa na manufaa kwa wananchi.

Hapa tena niseme kwamba nashindwa kuelewa ugumu wa kulielewa hili unatoka wapi. Kama mbunge analipwa mshahara wa mwezi, kisha analipwa masurufu ya kuwa kazini nje ya kituo chake, posho ya kikao, ambacho ndiyo kazi yake ni ya nini? Ni nini cha zaidi anachofanya kuliko kuhudhuria kikao cha Bunge ambacho ndicho kimempeleka Dodoma na ambacho kwacho amelipwa per diem?

Maneno mengine hayapendezi, na si jambo jema kumsuta waziri mkuu, hasa kwa sababu Pinda ninamheshimu sana. Lakini haipendezi kusema eti hata hao wabunge wa Upinzani "wanazimezeamezea mate fedha hizo, lakini wafanyeje?" Nini maana yake? Kwamba wangekuwa huru kusema wangesema wapewe hizo fedha lakini labda wamebanwa na uongozi wao? Nini hasa maana yake, kwamba mtu wa kawaida atazimezeamezea mate tu hizo posho hata kama hazina sababu, na kwa hiyo ni halali zilipwe, kwa sababu ya kumezewamezewa mate?

Hapa hakuna msaada wa kujisafisha kitakaopata chama-tawala kupitia njia ya kujivua gamba. Shughuli inayomezewamezewa mate hapa haina uhusiano na gamba la mnyama ye yote, bali inahusu tumbo. Mate ya mbwa wa Pavlov huanza kumdondoka anapopata ishara kwamba mlo wake unakaribia, na mlo wake ukicheleweshwa inabidi ameze mate. Sijui kama hivyo ndivyo wanavyofanya wabunge wa Upinzani.

Lakini wale wanaoendelea kutaka kula hicho chakula ambacho wenzao wanakimezea mate ajue kwamba wananchi sasa wamejua kwamba wawakilishi wao wanalipwa masurufu wasiyostahili, hata kama wanalipwa kisheria.

‘Mavyakula' kama haya hayaathiri afya ya ngozi, bali huathiri tumbo. Kulakula hovyo ni dalili ya ulafi, na ulafi ni mojawapo ya dhambi za mauti, hasa kwa Wakristo. Miongoni mwa mambo mengi wanayolalamikia wananchi wetu, moja kubwa ni ulafi wa watawala wao katika mazingira ya hali mbaya mno za maisha ya watu wa kawaida.

Chama cha upinzani kitakuwa si chama cha upinzani kama kitashindwa kuliona hilo na kuwapiga nalo watawala na kupata kuungwa mkono na wananchi.

Tamko jingine la kushangaza ni lile la Mustafa Mkulo anayesema kwamba wanaokataa posho wanatafuta umaarufu wa kisiasa. Sasa je, ni mwanasiasa gani asiyetafuta umaarufu wa kisiasa? Suala ni kujua umaarufu huo anautafuta kwa mbinu gani, mbinu za kuwaangamiza watu wake au za kuwasaidia?

Kiafya, ulafi husababisha mtu kuvimbiwa, na kuvimbiwa dawa yake si kuvua gamba bali ni kula haluli (laxative) inayosafisha tumbo chafu na kutoa uchafu wote nje. Katika makala ijayo nitaijadili hiyo haluli wanayohitaji watawala wetu.

Jenerali Ulimwengu, what a cruel truth... wenye macho na waone na wenye masikio wasikie... Lakini kama kawaida yao watajifanya "hamnazo!"
 
Inaonyesha tuna tatizo kubwa sana wabongo,sasa hizo kauli hapo juu zinasadia nini?Haya mmejua,whats next?Ama mna uhakika mliikuwa hamjui hayo yote aliyosema Ulimwengu?Acheni porojo zenu za kibongo na kiswahili swahili.WTF is the solution?Eti mwingine anadai kuwa "kama wameweka nta masikioni sahuri yao" na mwingine eti "Its the cruel truth" WTF? How is that going to help the cause?JF ni sehemu ya kuja na solution si blah blah na ushabiki.Toa thans,like the posting,move on and contribute to the issue na si vijiposting vya kishabiki. Nyie sijui ndo kizazi kipya ama vipi?Ndo mnaanza kusoma makala maybe coz bongo flavor imekufa?Pambaf kabisa.Jenerali yuko long time na makala zake kama hizi.Fanyeni something na muache ujinga wa Isidingo hapa.
 
Mkuu, mbona na wewe unafall kwenye the same trap unayowa accuse wenzio?... Wengine tulikua tunasubiri kusoma part 2 ya hiyo haluli(laxative)
anayoipendekeza Jenerali, ili kama kuna haja tuongezee mawazo. Ila nawewe ungepaswa uoneshe njia kwetu sisi uliotuita bongo falva kwa kutoa solutions badala ya kujaza pages tu.
 
Bravo Jenerali! lakini hawa jamaa hawaambiliki wanajiona much know sana, umeshawaasa sana lakini hawashauriki, endelea kuwapa dozi na usichoke wala kukata tamaa na siku watakapoangukia pua ndipo watakapo review makala zako na ku regret
 
Mkuu, mbona na wewe unafall kwenye the same trap unayowa accuse wenzio?... Wengine tulikua tunasubiri kusoma part 2 ya hiyo haluli(laxative)
anayoipendekeza ili kama kuna haja tuongezee. Ila nawewe ungepaswa uoneshe njia kwetu sisi uliotuita bongo falva kwa kutoa solutions badala ya kujaza pages tu.
Alwatan,
Frustrations ni mojawapo ya dalili kuwa una akili timamu....If something doesnt work out,its obvious you can get frustated..Ni muhimu pia kutambua kwamba doing the same thing over and over again,expecting different results is one of the insanity indicators....My hope is that this is not what we are doing.Naona pia unasubiri version mpya (2) ya msiisimko AKA laxative version.I did enjoy this one and ofcourse the next it if it is just for the sake of entertainment.
Nisome hapo nyuma.Whts nxt?Ama tunajidhihirishia ukichaa kwa kufanya yale yale na kutegemea matokeo ya tofauti?
 
Kudo for you Jenerali,Huyo Nyerere mpya tunamsubiri coz kwa sasa naona wanasiasa wengi ni wafanyabiashara au makuwadi wa wafanya biashara hata CCM ikiondoka watakaokuja watakua business as usual believe it or not!!!
 
Nchi imeoza lakini cha ajabu ujuwe tuko shimoni na mbali sana kuelekea uhuru wa kweli.Mtu akidai nchi imeoza basi anakuwa shujaa.Hapo utajuwa kuwa siasa za ccm zimetulemaza akili,na hilo wanalifurahia sana.

Yes nchi imeoza,sasa kazi ni kuuondoa huo uoza!Naomba pia nisieleweke vibaya na wanamapinduzi na wanaofurahia makala kama hizi kutoka kwa wanamapinduzi kama hawa.Ni kweli zinatia moyo.However ninaomba pia mtambue kuwa wengine tumechoshwa.

Nothing personal.So ninaomba kuendelea kujadiliana na wale wanaotaka kuhoji whats next.Honestly wengi wetu tunajuwa ccm imetuangusha na kutusababishia haya yote ie umasikini wa kutupwa.Inasikitisha ninaposoma hapa watu wazima wakilalamika kila siku kuwa hakuna umeme,maji nk.
Hayo mambo yalishatuchosha wengine wetu ndugu zanguni,hayakuanza jana wala leo.Just imagine wale tuliosukuma gari ya Mrema na kula mabomu ya machozi tukiwa very young.Put yourself on my shoe, and imagine kama hutajikuta na wewe pia umechoshwa.

Kuna mjadala mwaka jana kabla ya uchaguzi na Dr Slaa alikuwa akichangia.Nilisema kuwa kama mnajuwa hakuna haki na wizi wa kura upo,why waste your time before making sure kuwa mazingira ya ushindani ni ya haki na kwamba uchaguzi unakuwa huru na wa haki?Alinijibu kwa kusema tusikate tamaa na kwamba maneno kama hayo yanaweza kuwakatisha tamaa wengine.Nilikubali nikakaa kimya.However everything happened the way i predicted it to be.Sasa tumerudi pale pale,and sad enough tunacheza nao kiduku kwa raha zetu.

CDM na wao nadhani waligundua hilo na ndio maana wanaandaa maandamano every now and then.Hiyo ni hatua.Mapambano ya katiba mpya yaendelee kwa kasi.Tunataka mabadiliko ambayo yanaweza kufafana na mapinduzi in one way or another.Otherwise ni versions after versions kama nilivyosema hapo nyuma.Na situations kama hizi zinapelekea hata wale waliokuwa wakijali kutojali mara baada ya kupata nafasi ya uongozi nk.
Imagine hizo posho na mishahara ya viongozi wa wananchi amabo wengi wao ni masikini wa kutupwa!Hatua zinazoendelea kuchukuliwa mfano Zitto na Mbowe ni only the begining and definetly just a tip of an iceberg.

Tunahitaji mapinduzi.Na baada ya hapo tutawapa kina Ulimwengu nafasi za kuandika namna ya kusonga mbele na si how we cant do something,or how viongozi wetu walivyo corrupt,foolish,stupid and everything bad you can name.Tunajuwa wako hivyo because thats the way they have been,even behind the back of mwalimu back in a day,walikuwa hivyo na wataendelea kuwa hivyo since hawana sababu za kutokuendelea kuwa wanavyotaka kuwa...Hatujawapa sababu ya kutokuendelea kuwa jinsi walivyo kwasababau hawaogopi maneno ama just makala.....Hawalkuogopa makemeo ya mwalimu ndo wataogopa haya?

Hazikuwatisha kipindi cha nyuma na hazitawatisha kipindi hiki kama tunazifurahia tu na halafu hatuchukui hatua yoyote constructive amabayo itawatisha kuwa sasa wanaweza kuodolewa madarakani, hivyo na wengine tumekuwa allergic hata kuwepo hapo na kuongozwa na mawazo yao yenye kuchefua,mioyo isiyojali,wenye roho mbaya na matendo yao yenye kutia hasira ya hali ya juu.Wamelifikisha Taifa hapo lilipo na siasa wanazozitumia hazitoi nafasi kwa mabadiliko ama viongozi wapya wenye maono mapya ya Taifa hili.Inatia hasira kweli kweli!

Tunaomba Mungu atupe uzima ili kabla ya kuondoka hapa duniani,basi tutoe mchango wetu wa ukombozi.Hilo nimeapa kulifanya!I will contribute to the cause,its just the matter of time.Kwa wale wenye nafasi kwa sasa,basi endeleeni.Hii ni changamoto tu.
 
Big up Jenerali,Pinda hawezi kupata makala kama hii,nafikiri haya magazeti hayafiki ofisini kwake kwa sababu yanawakosoa
 
Big up Jenerali,Pinda hawezi kupata makala kama hii,nafikiri haya magazeti hayafiki ofisini kwake kwa sababu yanawakosoa
Nyie watu wa wapi?Magazeti yanawafikia sana tu,tena pengine kabla hujayapata wewe.Mnadhani hawayasomi?Kweli kuna watoto humu.Hatuwezi kurudia rudia haya mambo ndugu zanguni halafu tudai tunasonga mbele.Wenye kutakiwa kuyasikia haya ni wananchi na wanatakiwa kuchukua hatua.Msitegemee eti mafisadi watasikiliza haya!Zamani mwalimu ndo tulikuwa tukimtegemea atusemee.

Wanamapinduzi walimwandalia majukwaa na conferences aweze kutusemea mara baada ya kung'atuka.Na udhaifu huu wa kutokuwa na sauti inayosikilizwa ni kosa, hilo ni kosa lake pia kwasababu tumekuwa kukimtegemea sana kiasi cha kwamba ameondoka na sasa ni kama wanatukomoa....Tumekuwa kama yatima!...Hakuna anayesikilizwa,kuna pengo ambalo halizibiki.

We should re examine our means and fighting tactics.Again,i agree...Big Up Ulimwengu,lakini tunataka muda si mrefu uanze kuandika makala ya namna ya kuanza kulijenga Taifa.Na kama hutakuwa na passion nyakati hizo.Basi utaandika makala ya how everything went down.Hili litasaidia kizazi kijacho wasije kurudia makosa.
 
Jenerali hakumung'unya maneno. Amesema wazi li mwenye masikio na asikie. Kama alivyosema Ulimwengu,wanachokifanya CCM ni kujaribu kutibu ugonjwa bila kutafuta na kuharibu chanzo cha ugonjwa huo.

Bravo Ulimwengu, no wonder serikali iliwahi kukuzushia eti wewe sio raia wa nchi hii kwa sababu tu wakufunge mdomo usiseme ukweli.

Tiba
 
Mawazo haya CCM hawawezi kuyakubali maana si wazalendo .Sasa wataanzaa kumuuliza uraia tena
 
This is very good analysis!

Kwa kweli mtu unashindwa kuelewa mtu amelipwa mshahara wa kazi anayofanya, amelipwa perdiem/posho ya kuwa nje ya kituo eti unamlipa tena sitting allowance kwa kazi hiyo hiyo! Hiki kitu ni vigumu sana kukielewa na huenda ndiyo maana wengi wataendelea kuwa maskini wakati wachache wanaendelea kuneemeka. CCM na walioko kwenye serkali yetu wanapaswa kuliona hili na kuwahurumia wananchi ambao leo hawana maji, umeme, hospitali n.k na huku yuko mtu anayelipwa kwa njinsi hii ya Mshahara mkubwa, posho ya kuwa nje ya kituo na sitting allowance.

Nawasilisha
 
Alwatan,Frustrations ni mojawapo ya dalili kuwa una akili timamu....If something doesnt work out,its obvious you can get frustated..Ni muhimu pia kutambua kwamba doing the same thing over and over again,expecting different results is one of the insanity indicators....My hope is that this is not what we are doing.Naona pia unasubiri version mpya (2) ya msiisimko AKA laxative version.I did enjoy this one and ofcourse the next it if it is just for the sake of entertainment.Nisome hapo nyuma.Whts nxt?Ama tunajidhihirishia ukichaa kwa kufanya yale yale na kutegemea matokeo ya tofauti?
Well said jmushi tunaomba mwongozo what next kwani wtz wote wamechoka na hizi sinema
 
Duh! naona Jamaa ametumia Staili ya Kambarage katika kujenga hoja yake.
Ukisoma kitabu cha Uongozi wetu na hatma ya Tanzania style yake na hii vinashabihiana sana. Kudos sana Jenerali kwa hoja Mujarrabu.
CCM ni gari bovu, ni mzigo kwa Taifa. Sisi kama Taifa tunahitaji gari jipya ili Tusafiri salama!
 
Back
Top Bottom