Jenerali Sarakikya: Utajiri wa watumishi serikalini unatisha!

Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania. Wameanza malalamiko, thanx, maana maumivu ya kichwa huanza pooole pole!
 
We unamjua huyo sarakikya au unakurupukia tu mambo? Kudi hilohilo na nani? Huyu ndie aliyeweka mwenge juu ya mlima kilimanjaro enzi tunapata uhuru, sasa yukoje kundi moja na hiki kizazi cha nyoka?
Hapana mkuu, aliyeweka mwenge pale kilima cha mungu ni somebody Nyirenda na nadhani kipindi hicho alikuwa kapteni. Pitiapitia vitabu vya Yusuf Halimoja!
 
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya, ameshangazwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kuibuka na utajiri baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi tu. Alisema huko nyuma watumishi waliitumikia serikali kwa miaka mingi na kustaafu wakiwa watu wa kawaida.

Alisema kuwa kwa siku za karibuni amekuwa anashangazwa na baadhi ya watu kujenga majengo makubwa yasiyolingana na mapato halali wanayolipwa na kuongeza kuwa anafahamu mishahara ya watumishi wa umma hakuna mwenye uwezo wa kujenga majengo hayo na kwa muda mfupi.
Jenerali Sarakikya alitoa kauli hiyo mjini Arusha jana, alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata).

“Mimi mwenyewe nilikuwa Mbunge, kisha nikawa waziri na kumalizia ubalozi na kustaafishwa rasmi na Jeshi mwaka 2004, bado sikuweza kujenga nyumba ya kifahari, bali nimejenga kibanda tu cha kuishi tena kwa miaka 10, iweje watu wajenge majengo hayo kwa muda mfupi?” Alihoji Jenerali Sarakikya.

Katika hatua nyingine, Jenerali Sarakikya ameilalamikia serikali kwa kulipa kiwango kidogo cha posho ya pensheni kwa wanajeshi wastaafu ya Sh. 300,000 baada ya miezi sita sawa na Sh. 50,000 kwa mwezi.

Jenerali Sarakikya alisema posho hiyo haiwezi kufanya kitu chochote kulingana na hali halisi ya maisha kwa sasa na wengi wao hujikuta katika wakati mgumu. Alisema kwa mujibu wa taratibu za jeshi, wanajeshi wengi hujikuta wanastaafu kwa vyeo vyao na sio kwa umri, jambo ambalo alisema wengi wao wanastaafu wakiwa bado wana nguvu za kutumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Nipashe

Apeleke ujinga wake huko,ajue m2mish wa uma ni mtumwa hvyo inambidi aanzishe biashara nyngne mitaan na ndo mana anajenga hayo manumba,mfn nina digrii na mshahara wngu n laki 3 za govt,na ugumu wa life unauona,mi tcha je unategemea niwasaport ccm in my life!nyoko
 
Aliongea kitu fulani Mwamunyange yalipotokea maafa ya Gongolamboto, lakini nilimchora kitu fulani kwa kauli ya kwamba wao si wanasiasa na kadiri ya kanuni zao za jeshi hawawezi kulalamikia mambo au kufanya maandamano. Sasa maumivu yakiendelea kuunguza maini ndani matokea yake nini? Elfu hamsini kwa mwezi siku ya leo mtu aliyejitoa maisha kutetea taifa letu wakati huo huo akiwaona wanaofaidi matunda aliyotokea jasho wakitanua kwa mwendo wa kujipangia watakavyo. Inauma na inafikirisha mengi. Wanasiasa wanasahau sehemu nyeti.
 
Gen. Sarakikya alilitumikea jeshi kwa mapenzi na moyo wake wote! Utumishi wake ulitukuka!
 
Tatizo tz bila kufanya kazi ya siasa ni vigumu kufanikiwa, mbunge anafanya kazi ya siasa kwa miaka mitano tu anatoka na pension kubwa zaidi ya mwanajeshi aliyetumikia nchi tena katika mazingira magumu kwa miaka therathini. Jambo hili limesababisha hata wasomi wote hasa doctors(phds) na maprofesa, na wataalam mbalimbali wa fani mbalimbali kuacha kufanya kazi walizosomea na kukimbilia kwenye siasa, na waliobaki kwenye fani zao kuamua kuwa mafisadi sehemu zao za kazi kwa kiwango kinachowezekana. Kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kuirudisha fani ya siasa kuwa kada ya kawaida kama enzi za mwalimu, ili tupate wanasiasa safi, na watu walipwe kutokana na elimu na kazi yake sio kwa sababu ni mwanasiasa ndio alipwe zaidi.
 
aendelee kupiga kelele tu, anaweza undiwa mkoa mpya hata wa tandale na akapewa u-RC ili kumziba mdomo.
 
Hapana; aliyepandisha mwenge ni general Nyirenda aliyefariki miaka michache iliyopita. Hats hivyo, ni keeling kabisa Kuwa yeye ndiye aliyekuwa mkuu wa kwanza wa jwtz wakati linaanzishwa 1964
We unamjua huyo sarakikya au unakurupukia tu mambo? Kudi hilohilo na nani? Huyu ndie aliyeweka mwenge juu ya mlima kilimanjaro enzi tunapata uhuru, sasa yukoje kundi moja na hiki kizazi cha nyoka?
 
Au ndo maana wanageukia siasa baada ya kustaafu?

Lakini wanakumbukwa sana kwenye ukuu wa wilaya, mkoa, na baadhi ya vitengo . Polisi ndo wanasahaulika kabisa wakistaafu.

Bora hata MAGEREZA walalamike ....POLISI ..wanastaafu wakiwa na mikono iliyojaa damu kwa uvunjaji wa haki za binadamu na RUSHWA .....hii ndio inawanyima uhalali wa kurudi kuwa viongozi wa wananchi...mfano ma COMMISSIONER wastaafu...ALFRED TIBAIGANA na JAMES KOMBE ..waliogombea uchaguzi uliopita 2010 ....wananchi wakawakataa kwenye kura za awali.......bosi wao MAHITA alibeep morogoro nadhani state wakamuambia aache asiaibishe cheo cha igp kama MBOMA alivyoaibisha cheo cha CDF kwa kugombe ana kushindwa.....mnajuwa kuna vyeo nchi hii ukishafikia unakuwa juu ya Mbunge ki protocal so haitegewi tena urudi bungeni ie Jaji wa mahakama ya rufaa,jaji mkuu,mkuu wa majeshi,mnadhiu mkuu,mkuu wa polisi ,mkuu wa usalama,mkuu wa magereza ,katibu mkuu wa rais etc...hata Spika aitakiwa asiwe mbunge.....

NDIO maana katiba mpya lazima tufikirie kuwa na bunge mfano wa HOUSE OF LORDS ....litakalohusisha ....watu kama 60....ambapo hapa watachukuliwa wastaafu kuanzia mawaziri wakuu..majaji rufaa,hadi majemedari waandamizi....hili hutumika kutoa ushauri kwa nchi..kuliko kuwaacha watu kama kina Sarakikya wakiwa hawana pa kusemea ........
 
Hapana; aliyepandisha mwenge ni general Nyirenda aliyefariki miaka michache iliyopita. Hats hivyo, ni keeling kabisa Kuwa yeye ndiye aliyekuwa mkuu wa kwanza wa jwtz wakati linaanzishwa 1964

KIELELEZO kingine cha huduma mbovu kwa wastaafu ...Brig[col] Nyirenda ameugua na kupata taabu sana bila kuhudumiwa na JESHI[state]....hadi pale picha yake akiwa amedhoofu ilipotolewa ITV akiwa Tanzania HEART INSTITUTE ...ndipo serikali ijajipeleka pale ikampeleka lugalo then INDIA .......sasa zingatia umuhimu wa Nyirenda kwenye historia.....
Tunataka kuwa na taratibu zinazoeleweka kwa wastaafu ...sio kuwa kupata huduma hadi kuchagua wale wanaoonekana kwenye TV ....serikali ione aibu ndio uwahudumie...JE WALE WANAOUGULIA NA KUISHI MIKOANI........?
 
Hapa kuna point. Lengo la pensheni ni kumuwezesha mustaafu kukidhi gharama ya chakula chake, matibabu, kuvaa na vitu vidovidogo muhimu katika hali ya kawaida kulingana na hgazi yake wakati anastaafu (alikuwa na wajibu wa kuwekeza angalau ajenge kibanda chake). Serikali na waajiri wake wa mashirika ya serikali walifanya makosa kwa wale waliostaafu mwaka 1999 kurudi nyuma kwa kutoku-update viwango vya pensheni kulingana na upandaji wa gharama za maisha ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara midogo sana (watumishi walijitolea sana). Walijali vyongozi wa juu ngazi ya Rais maana nakumbuka kuna wakati Spika wa zamani aliwahi kulalamika pia. Baada ya kuona hivyo uaminifu kazini ukapungua na ufisadi ukaanza wa watu wachache sana wa chukua chako mapema -na kweli hawa ndio Mhe. Sarakikya anazungumzia. Huu niwizi uliofanywa na watu wachache na wizi hauna kiwango na sababu zake ni hizo. Kwa sasa tatizo hili limerekebishwa kuanzia mwaka 2000 hivi yaani anayestaafu serikalini au shirika la umma sasa mambo yake ni mazuri sana kuliko ilivyokuwa. Ni jukumu la serikali na waajiri wote kukomesha wizi au ufisadi unaofanywa sasa bila kuoneana haya; ni uroho, sababu haipo tena for sympathy.

Baada ya kusema hivyo, kuna haja ya kuangalia upya wastaafu wote kutoka 2000 na kurudi nyuma na waliobaki si wengi kwa nia kurekebisha viwango vyao kulingana na vyeo vyao kazini wakati wanastaafu. Serikali iache kubagua mashirika yake kwa sabau sera za kuwabana wafanyakazi zilikuwa hazibagui hivyo. Serikali imerekebisha kima cha chini cha pensheni kuwa TShs. 50,000/= bila kufanya hivyo prorata kwa wafanyakazi wa ngazi za kati. Pensheni ya Shs. 50,000/= ndiyo ilikuwa ya akina Mhe Sarakikya sasa na yeye ana pensheni ya kima cha chini sasa, kweli hiyo?

Mapendekezo. Warekebishe kima cha chini cha pensheni kwa vyeo vyote vya waliostaafu mika ya 1999 na kurudi nyuma kikomo cha juu kiwekwe, mfano shilingi millioni moja. Na kamwe isifanyike tu kwa wale wenye nafasi ya kulalamika (yaani wakubwa tu) ambao mara nyingi hali yao siyo mbaya kiasi hicho.
 
Au ndo maana wanageukia siasa baada ya kustaafu?

Lakini wanakumbukwa sana kwenye ukuu wa wilaya, mkoa, na baadhi ya vitengo . Polisi ndo wanasahaulika kabisa wakistaafu.

Hivi polisi hawaruhusiwi kugombea nafasi za kisiasa kama ubunge nk. Kwa kumbukumbu yangu ndogo sina uhakika kama tuna kiongozi ambaye katika nafasi za juu kuanzia wabunge ambaye ametokea jeshi la polisi isipokuwa tu jeshi la wananchi na usalama wa taifa.
 
Hii ni serekali ya chukua........chako ........mapema . Hata huko jeshini wakubwa ni hivyo hivyo wanachukua mapema (Hamna kulala )buni uchukulie wapi. KALAKABAHO,..:clock:
 
WAnamkumbusha ****** awakumbuke ufalumeni kwake subirini kidogo mtasikia Anawakumbuka:mod:
 
Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya, ameshangazwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa serikali kuibuka na utajiri baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi tu. Alisema huko nyuma watumishi waliitumikia serikali kwa miaka mingi na kustaafu wakiwa watu wa kawaida.

Alisema kuwa kwa siku za karibuni amekuwa anashangazwa na baadhi ya watu kujenga majengo makubwa yasiyolingana na mapato halali wanayolipwa na kuongeza kuwa anafahamu mishahara ya watumishi wa umma hakuna mwenye uwezo wa kujenga majengo hayo na kwa muda mfupi.
Jenerali Sarakikya alitoa kauli hiyo mjini Arusha jana, alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania (Muwawata).

“Mimi mwenyewe nilikuwa Mbunge, kisha nikawa waziri na kumalizia ubalozi na kustaafishwa rasmi na Jeshi mwaka 2004, bado sikuweza kujenga nyumba ya kifahari, bali nimejenga kibanda tu cha kuishi tena kwa miaka 10, iweje watu wajenge majengo hayo kwa muda mfupi?” Alihoji Jenerali Sarakikya.

Katika hatua nyingine, Jenerali Sarakikya ameilalamikia serikali kwa kulipa kiwango kidogo cha posho ya pensheni kwa wanajeshi wastaafu ya Sh. 300,000 baada ya miezi sita sawa na Sh. 50,000 kwa mwezi.

Jenerali Sarakikya alisema posho hiyo haiwezi kufanya kitu chochote kulingana na hali halisi ya maisha kwa sasa na wengi wao hujikuta katika wakati mgumu. Alisema kwa mujibu wa taratibu za jeshi, wanajeshi wengi hujikuta wanastaafu kwa vyeo vyao na sio kwa umri, jambo ambalo alisema wengi wao wanastaafu wakiwa bado wana nguvu za kutumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Nipashe
kweli
 
Back
Top Bottom