Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 333
Jenerali Mboma aendelea kuula TPDC
Na Mwandishi wetu
16th September 2009
Jenerali Mstaafu, Robert Mboma.
Rais Jakaya Kikwete amemteua tena Jenerali Mstaafu Robert Mboma kuendelea kuwa mwenyekiti mpya wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kipindi cha miaka mingine mitatu.
Kikwete amemteua Mboma, aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati wa uongozi wa Serikali ya awamu ya tatu kuendelea na wadhifa huo kuanzia Julai mwaka huu hadi Juni mwaka 2012.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Alyoce Tesha, inasema kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Wizara hiyo, William Ngeleja amewateua wajumbe tisa kuunda bodi hiyo.
Wajumbe hao ni Emanuel Ole Naiko ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha uwekezaji, Ngosha Magonya, Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Maduka Kessy Meneja Uhusiano wa Sekta Binafsi na Serikali kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC), wabunge Gosbert Blandes (Karagwe) na Mudhihir Mudhihir (Mchinga)
Wengine ni Faida Bakari (Viti Maalumu), Prosper Victus Kamishna Msaidizi wa Mafuta na gesi wa Wizara ya Nishati na Madini, Mwalimu Mwalimu, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi (MUNA) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na William Haji (Mhasibu) ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Ndege Tanzania (ATC).
CHANZO: NIPASHE
Maoni yangu: Je nilini wazee watastaafu?. Ni nini maana ya neno kustaafu? Ni lini vijana watafanya kazi mchanganyiko na wazee? Ni lini wabunge wataendelea kuwa wawakilishi wa wananchi na baada ya Bunge kurudi majimboni mwao na kuwahudumia wananchi ana kwa ana badala ya kuendilea kuwepo mjini kwa sababu wanahudhuria vikao vya bodi?