Jela Miezi Sita Kwa Kukaidi Kuvua Baraghashia Mahakamani

mi sijaelewa hivi ni kosa sheria mtu kuvaa kofia mahakamani? na kama ni kosa kuna kofia zinaruhusiwa na zingine haziruhusiwi?
 
Acha ujinga wewe Mungu hakusema tuheshimu sheria za kijinga na kijahili hivi unadhani ni sawa kwa sista wa roman akiambiwa atoe kilemba chake? au singa singa avue kilemba chake? mbona nimrod mkono anaingia mahakamani na tarbush yake? tatizo mnalijua mahakimu wengi hawana uelewa.........................
Acha jazba! mtu akitoa maoni siyo mjinga mjibu kwa hoja
 
Nilisoma last week mahali hili swala nikashindwa kuelewa. Kama kesi ni kuvaa kofia mahakamani mmmmh! Nina mashaka na haki za kimsingi
 
Itakuwa huyo kijana hakutoa rushwa suala lake liishe na hakimu kuamua kumkomoa.....nadhani si kwa misingi ya ubaguzi wa kidini...hakuna derss code mahakamani...labda uingie ukiwa uchi...
 
tuwe wapole kwa hili.... Hakimu kachemsha tu.Kibaraghashia sio helmet..tusilipeleke mbaali zaidi kwenye ubaguzi wa Kidini likatuletea uvunjifu wa amani

Kuchemsha kupo tu
 
kila mahala kuna taratibu zake, msikitini huruhusiwi kuingia na viatu, baadhi ya makanisa hayataki vimini na mengine yamekuwa hata yakichukua hereni, mikufu ya waumini. Mahakama nayo ina taratibu zake, ni vema tukazingatia hili na sio kuanza kuchochea chuki na jazba zisizo na msingi. Kama alikaidi amri ya kuvua kofia mvua ya miezi sita aliyonyeshewa halali yake kabisa. Alidharau mahakama ambalo ni kimbilio la waumini wa dini zote,labda ingekuwa mahakama ya kadhi angekuwa na hoja. hakimu yuko sahihi kabisa
 
Hapa napata utata kidogo, hivi amefungwa kwa kuvaa hiyo kofia kizimbani au amefungwa kwa kukaidi amri ya hakimu alomwamuru avue hiyo kofia? Nahitaji ufafanuzi manake kisheria ni hali mbili tofauti. Kama ni kwa kuvaa kofia basi inamaana alipoingia tu kizimbani akiwa ameivaa moja kwa moja alihukumiwa kwa kuivaa. Kama ni kukaidi amri ya hakimu inamaana alipoingia kizimbani akiwa ameivaa hiyo kofia basi ukaanza mjadala baina yake na hakimu, akiambiwa aivue naye akakaidi? Fuatilia kiasi halafu urudi!
 
jee watu wanuliza ndio sheria au jazba za kidini za jaji? kama hakuna sheria hiyo na jaji ambae kwa jina ni mkristo haimaanishi kwamba amaetumia imani yake? jee mbona mrema anaingia na kofia hiyo hiyo hataujasikia? jee hii sheria ni mpya? kwani tuapte uhuru hatujasikia sherria kama hizi. kuwa mple unapojadili hoja

Mahakama ni mahala pa ajabu sana kwa sababu Hakimu anao uwezo wa kimaamuzi...unaweza kwenda jela hata kwa kutabasamu au kucheka tu...na haijaandikwa mahala popote kisheria...umedharau mahakama.....yuko hakimu alipata kumtupa mumewe ndani kwa kupiga honi eneo la mahakamani....wakati mwingine hutgemea hakimu kaamka vipi
 
inaelekea alikuwa amekaa mkao wa kujilipua lipua huyo....baraghashia mbona watu wanavaa tu mahakamani ....
 
usilete kizunguzungu. hoja kafungwa kwa kuvaa kofia. fullstop.

Narudi kule kule, anyways naona umeileta hiyo yako "argumentum ad bacullum" sina mchango tena. Hapo kwenye Red wengine wanasema" Roma locuta causa finita". Thanx!
 
Safi sana Mods kwa kuziunganisha hizi threads nadhani sasa tunapata ukweli wa original, used na feki. Hii ya Mh Masanilo inakuwa a little bit more viable!
 
mzeze kwa maana mrema anaponingia na kibaraghashia huwa mdini? jee jaji katoka vatican karibuni? mbona hatujasikia kitu kama hicho tz? usiichukie kitu mpaka kila mtu akakujua moyoni mwako, ni hatari kwa tiafa hili.

Unataka jilipua?
 
huyu hakufungwa kwa kuvaa kofia ila kwa kupinga amri ya hakimu iliyotaka avue kofia (kutokana na kuonekana ni dalili ya kuvunja heshima)

kwa mahakama za nchi za kimagharibi iko wazi kuwa hairuhusiwi kuvaa kofia (hats) na wapo watu waliofungwa kwa kukiuka amri hiyo

(kuna aliyefungwa siku sita kwa kuchelewa kuivua cowboy hat yake alipoamuriwa kufanya hivyo na hakimu).

suala linakuja jee hali ikoje kwenye mahakama za Tanzania? sheria au taratibu zinasemaje kuhusu suala hilo?

na suala jengine linakuja jee miezi sita ni hukumu stahili kwa kosa kama hilo?
 
Back
Top Bottom