Jela Miezi Sita Kwa Kukaidi Kuvua Baraghashia Mahakamani

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
Afungwa jela miezi sita kwa kukaidi kuvua baraghashia mahakamani

Tuesday, 31 August 2010
Hadija Jumanne

MSHAURI wa baraza la kata Gongo la Mboto, anayekabiliwa na kesi ya kutishia kuua na kusababisha fujo, Ally Sururu (60) amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, baada ya kukaidi amri ya hakimu aliyemtaka avue kofia aliyokuwa ameivaa kizimbani aina ya baraghashia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, WilbaForce Luhwago, mara baada ya mtuhumiwa huyo kumwambia hakimu huyo kuwa hana maadili kwa kumtaka yeye avue kofia.

Mara baada ya Sururu kutoa kauli hiyo mbele ya mahakama, hakimu Luhwago alimtaka akampumzike kwa muda katika mahabusu ya mahakama hiyo ya Ilala.

Lakini cha kushangaza, mtuhumiwa alikaidi amri hiyo huku akimweleza hakimu Luhwago kuwa baraghashia ni sawa na vazi lolote hivyo hawezi kuivua.

Hakimu Luhwago alimwambia mshtakiwa huyo kuwa kwa sababu hiyo ni tabia yako ya kudharau mahakama ukiachiwa utaendelea na tabia hiyo, hivyo utatumikia kifungo cha miezi sita jela huku kesi yako inaendelea kusikilizwa.

Sururu ambaye yupo nje kwa dhamana , kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho cha miezi sita jela, jana hiyo alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuisikiliza kesi yake.

Kabla ya kupewa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Daniel Buma aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mtuhumiwa kutokana na tabia aliyoionyesha ya kudharau mahakama na kudaia kuwa zikiachiwa tabia hizo mahakama hazitaheshimiwa"alidai Buma.

Awali mtuhumiwa alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ilala akikabiliwa na kesi ya kutishia kuuwa na kutoa lugha chafu ikiwemo usumbufua katika baraza la kata.

Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilikuja katika mahakama hiyo Septemba 15, mwaka jana, na mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 27,mwaka 2008 katika eneo la Ukonga Mzambarauni.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa mtuhumiwa alitoa maneno makali wakati wakiwa katika mashauriano katika baraza la kata na hivyo kusababaisha usumbufu na uvunjifu wa amani katika baraza hilo.

Buma aliendelea kudai kuwa mtuhumiwa katika shtaka la pili anadaiwa kumtishia kumuua Mzee Shija .

Ilidiwa siku hiyo majira ya saa 5 asubuhi mtuhumiwa alimtishia kwa maneno mzee Shija kwa kumwambia "Wewe Mzee Shija nitakushughulikia kisawasawa na kuwa ndio mwisho wako"alisema mtuhumiwa huyo katika baraza la kata na hivyo kusababisha hofu kwa mlalamikaji.

Hata hivyo kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi ulikuwa bado haujakamilika.

Gazeti la Mtanzania
 
Hawa jamaa wakorofi sana hajui kuwa baraghashia nivazi la kidini, na ile si mahakama ya Kadhi wacha apate akili huko jela kwa miezi sita. Safi sana hakimu
 
hawa ndugu zetu wa upande wa pili sijui wanadhani sheria iko juu yao wanafanya kile watakacho, safi sana hakimu hii itakuwa fundisho hata kwa wengine wenye tabia kama hiyo
 
Walidanganywa Mahakama ya kadhi uchaguzi uliopita wanataka halarisha sasa!
 
Najiuliza kama angekuwa ni Sista na amevaa shera angeamulia kuitoa? Na je angekuwa mwana mama mwenye baibui angeitoa? Nadhani kuna jambo hapa!
 
Unatakapotosha! Aliyevaa baraghashia ni mwanaume sasa wewe wajiuliza nini na watu wa jinsia ya kike? Hakuna jambo hapa amedharau mahakama kwisha
 
Hapana jamani wamemuonea sana na kumdharaulisha mzee wa watu, kweni sheria inasemaje kuhusu mavazi mahakamani? Je angekuwa karasinga na kiremba chake wangemwambia atoe? Au angekuwa Kardinali Pengo na kofia yake ingetolewa amri atoe? Au tuseme angekuwa Mufti Simba angeambiwa avue kofia?

Hakimu huyu kaonyesha vile ambavyo watanzania wengi maofisini walivyojisahau wawapo maofisini mwao na kutumia mabavu bila sababu za msingi, hii inanikumbusha yule bwana waliyemfunga na baadaye akatoka kwa ruffaa ...kisa eti kusema Yesu si mtoto wa mungu..acheni kuchanganya udini na kazi...nahisi jamaa hakuwakatia kitu kidogo na sasa wamemaliza kesi kifisadi....njaaa zenu zitawaua...kesi gani toka mwaka jana haijaisha wakati mnaseema alipayuka mbele za watu...

Waislamu amukeni mumtetee mwenzenu bila nyinyi kweli hatapata haki yake...msumeno hukata mbele na nyuma naa kwa hili nalipinga kwa nguvu zangu zote kwani ni maonevu yale yale kwa wanyonge tunayofanyiwa kila siku
 
Ohhhh my GOD! I knew this was coming
 
Ngoja ashitakiwe Singasinga mwanaume tuone...baraghashia sio uislamu...Mrema ni mkatoliki:mad2:
========

Yarabi toba! Ama kwa hakika umenipa somo. Kumbe basi, ndevu chafu si Uislamu wala suruali fupi kwa wanaume wenye ndevu chafu si Uislamu. On that note, nauliza, hivi baragashia kama ni alama ya Uislamu kwa nini watu kama Kikwete huwa wanaivaa kwenye ibada na kwenye misiba tu? Kwa hiyo yawezekana hakimu alikuwa anatuma message kuwa pale si ibadani bali ni mahakamani!? Kuna hatari ya kuchanganya Uarabu na Uislamu na kuchanganya uzungu na ukiristo?!
 
MSHAURI wa baraza la kata Gongo la Mboto, anayekabiliwa na kesi ya kutishia kuua na kusababisha fujo, Ally Sururu (60) amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela, baada ya kukaidi amri ya hakimu aliyemtaka avue kofia aliyokuwa ameivaa kizimbani aina ya baraghashia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, WilbaForce Luhwago, mara baada ya mtuhumiwa huyo kumwambia hakimu huyo kuwa hana maadili kwa kumtaka yeye avue kofia.

Mara baada ya Sururu kutoa kauli hiyo mbele ya mahakama, hakimu Luhwago alimtaka akampumzike kwa muda katika mahabusu ya mahakama hiyo ya Ilala.

Lakini cha kushangaza, mtuhumiwa alikaidi amri hiyo huku akimweleza hakimu Luhwago kuwa baraghashia ni sawa na vazi lolote hivyo hawezi kuivua.

Hakimu Luhwago alimwambia mshtakiwa huyo kuwa kwa sababu hiyo ni tabia yako ya kudharau mahakama ukiachiwa utaendelea na tabia hiyo, hivyo utatumikia kifungo cha miezi sita jela huku kesi yako inaendelea kusikilizwa.

Sururu ambaye yupo nje kwa dhamana , kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho cha miezi sita jela, jana hiyo alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuisikiliza kesi yake.

Kabla ya kupewa hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Daniel Buma aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mtuhumiwa kutokana na tabia aliyoionyesha ya kudharau mahakama na kudaia kuwa zikiachiwa tabia hizo mahakama hazitaheshimiwa”alidai Buma.
Awali mtuhumiwa alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ilala akikabiliwa na kesi ya kutishia kuuwa na kutoa lugha chafu ikiwemo usumbufua katika baraza la kata.

Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilikuja katika mahakama hiyo Septemba 15, mwaka jana, na mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 27,mwaka 2008 katika eneo la Ukonga Mzambarauni.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa mtuhumiwa alitoa maneno makali wakati wakiwa katika mashauriano katika baraza la kata na hivyo kusababaisha usumbufu na uvunjifu wa amani katika baraza hilo.

Buma aliendelea kudai kuwa mtuhumiwa katika shtaka la pili anadaiwa kumtishia kumuua Mzee Shija .

Ilidiwa siku hiyo majira ya saa 5 asubuhi mtuhumiwa alimtishia kwa maneno mzee Shija kwa kumwambia “Wewe Mzee Shija nitakushughulikia kisawasawa na kuwa ndio mwisho wako”alisema mtuhumiwa huyo katika baraza la kata na hivyo kusababisha hofu kwa mlalamikaji.
Hata hivyo kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa kwa kuwa upelelezi ulikuwa bado haujakamilika.

Chanzo Afungwa jela miezi sita kwa kukaidi kuvua baraghashia mahakamani
 
Ya Mungu tumpe Mungu na Kaisari tumwachie yanayomfaa.,hata neno la Mungu linatutaka tuheshimu mamlaka zilizo juu yetu, hata kama ana haki ya kuvaa hiyo kofia kwa mujibu wa dini yake alipaswa kujua kuwa pale ni mahakamani na amri ya mahakama ni lazima iheshimiwe hilo halina mjadala, kinyume na hapo ni Contempt of Court na adhabu yake ndiyo hiyo iliyompata huyo bwana.
 
Acha ujinga wewe Mungu hakusema tuheshimu sheria za kijinga na kijahili hivi unadhani ni sawa kwa sista wa roman akiambiwa atoe kilemba chake? au singa singa avue kilemba chake? mbona nimrod mkono anaingia mahakamani na tarbush yake? tatizo mnalijua mahakimu wengi hawana uelewa.........................
 
Back
Top Bottom