Jehanamu ipo?

NAOMBENI MAJIBU WADAU KWELI JEHANAMU IPO?KAMA UPO INTERESTED ,THANK YOU.Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu. Tunasoma katika WAEBRANIA 9:27, "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu." Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya Neno la Mungu, hufundisha kwamba mtu anapokufa, analalatu, na hakuna lolote la hukumu mara moja wakitumia maandiko yafuatayo na kuyatafsiri visivyo: MATHAYO 27:52; 1WAKORINTHO 15:20: YOHANA 11:11-14 n.k.; na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba, kinachobaki kaburini ni mwili tu. Roho ya mtu huondoka na kuingia katika mwili mwingine, unaoitwa mwili wa roho Miili tuliyo nayo wanadamu kabla ya kufa, inaitwa miili ya asili. Tunasoma katika 1WAKORINTHO 15:40, 44, "Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani, …Ikiwa uko mwili wa asili, na wa r oho pia uko." Mwili wa asili, ndio unabaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka kama tunavyosoma katika MHUBIRI 12:7, Nayo mavumbi ya nchi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa."Mwili wa asili, ndio unaobaki kaburini, na huo ndio unaotajwa kwamba umelala, haujui lolote, na hauna kumbukumbu; lakini pasipo mwili huo, mtu atamwona Mungu na kukabiliana na hukumu yake dakika ileile baada ya kufa (AYUBU 19:26). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu, mara tu baada ya kufa huchukuliwa mbinguni (LUKA 23:43; 16:22). Ikiwa ameishi na kufa katika dhambi, bila kutubu dhambi zake na kuokoka, hukumu yake mtu huyo, huwa ni kutupwa katika Jehanamu ya moto, mara tu baada ya kufa, kama yule tajiri anayetajwa katika Biblia (LUKA 16:19-24). Mbinguni ni juu (Mbingu ya tatu), lakini kuzimu au Jehanamu ya moto, ni pande za chini zanchi (2 WAKORINTHO 12:1-4; MITHALI 15:1-4; MITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14. Mara mtu anapokufa, hufika kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni kuzuri, hata hivyo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni, huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni. Hali hii wakati mwingine inaweza kuonekana katika mwili wa asili kwa kumwangalia mtu anavyotapatapa na kuhangaika sana katika kufa kwake. Kutokana na mtu asivyopenda kwenda motoni na kutaka kwenda mbinguni asikotakiwa, mtu hulazimika kukamatwa kwa nguvu na malaika wa kutisha, na kutupwa katika Jehanum ya moto; inayojulikana pia kwa jina jingine, giza la nje; kama tutakavyoona baadaye kidogo (UFUNUO 19:20; 20;10; MATHAYO 25:30). Huko motoni Jehanum kukoje? Kunatisha, nashindwa hata nikueleze vipi unielewe. Moto wa milele, hatukuwekewa wanadamu bali shetani na malaika zake (MATHAYO 25:41). Kama utakwenda huko baada ya kusoma ujumbe huu, itakuwa ni kwa sababu ya kiburi chako tu, na kushupaza shingo yako na kukataa kulitendea kazi Neno hili (MITHALI 29:1). Moto wa Jehanum siyo mahali pa mchezo kama walimu wa uongo wanavyofundisha. Waalimu hawa huwafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa na kuangamizwa kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 (kuangamizwa) na YOHANA 3:16 (kupotea). Kuangamia katika maandiko hayo haimaanishi kumalizika kabisa, bali kukabiliwa na mauti (ESTA 4:16). Mauti ya watu walioko motoni, ni mauti ya milele, kama tutakavyoona hivi punde. Kondoo akipotea, haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (ISAYA 57:1-3). Vilevile, neno "Kuharibu" linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele, halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni kuadhibu vikali (1WAKORINTHO 3:16-17. Waalimu hawa wa uongo, pia hufundisha pia kwamba, eti watu watatoweshwa kama moshi baada ya kuunguzwa kwa kutumia andiko la ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa na Mungu, kama Adamu na Hawa walivyotoweshwa na kutolewa katika bustani ya Edeni, na hivyo kutengwa na Mungu, Kwa ujumla, mafundisho yote haya yanayotokana na Shetani, yanalenga kuwafanya watu waendelee kutenda dhambi, huku wakipuuza ukweli juu ya Jehanum, kwa kuwaza kwamba watateseka dakika chache na kupotea kabisa na ndiyo mwisho. Hiyo siyo kweli.Ukweli kuhusu Jehanum ya moto ni upi basi? Sikiliza nikuambie! Jehanum ya moto, au Kuzimu, ni shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Wengi tunafahamu jinsi wanawake wanavyouchochea moto wa kuni au mkaa, kwa kuupulizia hewa kwa mdomo, au kipepeo. Sasa basi, moto wa Jehanum nao huchochewa mfululizo, ili usizimike; lakini huchochewa na pumzi ya Bwana, yaani pumzi maalum ya Mungu mwenyewe (ISAYA 14:15; 30:33). Moto wa Jehanum ni mkali sana kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani. Moto wa gesi wa kuunganishia vyuma, unaotokana na kuwashwa mchanganyiko wa gesi ya "Oxygen" na "Acetylene", moto huu unaonekana kwa hapa duniani kwamba ni mkali. Moto huu, siyo chochote, ukilinganishwa na moto wa Jehanum. Katika karakana au viwanda vinavyotengeneza vifaa vya chuma, chuma huyeyushwa na kuwa ujiuji katika matanuru ya moto mkali unaofikia nyuzi joto 2,000 hadi 3,000 na zaidi. Moto huu unaoyeyusha vyuma na ukali wake, huo si chochote! (Kumbuka kwamba maji yaliyochemka sana hufikia nyuzi joto 100 tu!). Moto ulio katikati ya jua linalotuangaza, unafikia nyuzi joto milioni kumi . Moto wa jua nao, si chochote ukilinganishwa na moto wa Jehanum! Ukali wa moto wa Jehanum, unatisha (WAEBRANIA 10:26-27). Siyo hilo tu, moto wa duniani una rangi mbalimbali, njano, bluu, nyekundu n.k. Moto wa Jehanumu ni tofauti kabisa; Ni moto wa rangi nyeusi, unaosababisha giza na kumfanya mtu aliye motoni, awaone wenzake wachache tu wa karibu naye, hivyo hamna faraja ya kusema "tuko wengi!" Moto huu mweusi, ndiyo maana unaitwa "giza la nje" Mathayo 8:11-12, 22:13; 25:30; YUDA 1:6). Siyo hilo tu. Moto huu wa Jehanum, una meno! Hivyo una uwezo wa kuwala na kuwatafuna walioko motoni (KUMBUKUMBU 32:22; WAEBRANIA 10:26-27). Hata hivyo, pamoja na moto huu kumtafuna mtu, bado una sifa ya kumhifadhi mtu huyo na kumfanya asimalizike, kama jinsi chumvi ilivyo na uwezo wa kuizuia nyama kuharibika. Hivyo moto unamtafuna mtu wakati wote, lakini haishi na wala moto wenyewe hauzimiki. Ndiyo maana unaitwa moto wa milele (MARKO 9:43-49; MATHAYO 25:41).Moto huu wa Jehanum, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti au kwa lugha ya kitaaluma, Sulphur." Kwa wale wanaofahamu kidogo somo la shule la "Kemia," au "Chemistry," wanafahamu kwamba madini ya "sulphur" yakiwashwa moto, huwa kama mpira, na hutoa harufu mbaya kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii inafunika kuzimu yote, na watu walioko huko wanahangaika kushika pua zao, lakini hakuna jinsi! Hebu jaribu kuwaza maisha haya, ndiyo yawe ya milele, mpendwa msomaji! Siyo hilo tu! Katika moto huu, wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi makubwa katika miili yao, wakiingia na kutoka, kutoka ubavu hadi ubavu mwingine, kutoka kwenye tumbo hadi mgongoni n.k. Hii hufanya sura za wale walioko motoni, kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Hata kama mtu alikuwa mweupe duniani, huko motoni, huwa ni mweusi tii!Moto wa milele, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Kwa nini huitwa mauti ya pili?

Maneno haya ni ya mtu ambaye ameanza kuchanganyikiwa!!!
 
Thx sana wana jamvi hili wote.
Haya mawazo ya mbingu, jehanamu, dhambi na kadhalika huwa ni mtizamo wa mtu, jamii husika. Ndiyo maana yanatofautiana sana kati ya mtu na mtu.
Kwa mtu ambaye huelewa wake wa mambo ni mdogo sana, picha ya Mungu wake anayemtengeneza kichwani huwa tofauti sana na mtu ambaye huwa ana uelewa wa mambo mengi, na haijalishi hata wakiwa ndani ya dini moja.
Wengi wetu tumekuwa watu wa kupokea taarifa kuyakumbatia bila hata ya kujipa nafasi ya kuyachambua vizuri. haswa linapokuja swala la Mungu, mbingu, na mengineyo.
Kiranga thx sana angalau kwa kuona japo mwanga.
Swali ambayo tunatakiwa tujiulize wote
Je Mungu ni nini?
Ni kitu?, ni mtu?
Je Mtu ni nini?
Je Mungu mungu ana limit/mipaka?
Naombeni sana msaada wenu.
Sorry kama nimewakwaza kwa namna yoyote ile.
 
hakuna mjadala hapa, ngoja tuseme basi jehanamu haipo kuiridhisha nafsi yako kwani wajua fika jehanamu ipo ila hakuna mtu aliyewahi kutupwa humo hata shetani, hata kuonekana, hakuna aliyewahi kuiona kamwe ila itafuniliwa siku ya mwisho na shetani atakuwa wa pili kuingia humo, atakayefungua dimba ni mpinga kristo. baadaye shetani then malaika wa shetani, then hao wanadamu kulingana na maovu yo, waliofanya madhambi mengi na ya kutisha zaidi watakwenda chini zaidi karibu na shetani na walio na ka -unafuu watakuwa huku juu. the more you seen, the deeper you go
 
hakuna mjadala hapa, ngoja tuseme basi jehanamu haipo kuiridhisha nafsi yako kwani wajua fika jehanamu ipo ila hakuna mtu aliyewahi kutupwa humo hata shetani, hata kuonekana, hakuna aliyewahi kuiona kamwe ila itafuniliwa siku ya mwisho na shetani atakuwa wa pili kuingia humo, atakayefungua dimba ni mpinga kristo. baadaye shetani then malaika wa shetani, then hao wanadamu kulingana na maovu yo, waliofanya madhambi mengi na ya kutisha zaidi watakwenda chini zaidi karibu na shetani na walio na ka -unafuu watakuwa huku juu. the more you seen, the deeper you go

Unaanza kwa kusema hakuna mjadala halafu unaanza kujadili, contradictions kila unachosema.

Unakubali hakuna aliyewahi kuiona, halafu unasema itafunuliwa siku ya mwisho. Unataka kutuletea biashara ya mbuzi ndani ya gunia hapa? Kanyaboya ?

Kama hakuna aliyeiona wewe unahakikishaje kwamba ipo ?
 
Nimeuliza hapo juu, biblia hii hii imesema jua linazunguka dunia, je mnaamini na hilo pia?

Mpaka sasa naona jiii. Biblia haina credibility kwenye haya, ni kitabu cha watu, kimetungwa na kuandikwa na watu. Kwa hiyo unless una empirical evidence za kuwepo kwa Jehanam, kama source yako ya info ni biblia, you might as well claim that there is a restaurant at the end of the universe based on a Douglas Adams Sci-Fi novel.

It is all fiction, largely.
69485253.JPG

Huyu bwana huwa anaongea kilicho kichwani kwake, anavyoona vitu namna vilivyo na vinavyoweza kuleta logic kwake na hata kwa watu wengine pia. Ila ukisoma sana post zake, unagundua bado ana wasiwasi kwamba pale aliposimama pengine siyo penyewe, hivyo anahitaji msaada ila kusema waziwazi anashindwa. Siri kubwa moja niliyoigundua pia ni kuwa ukitaka kumsaidia huyu mtu aamini kwamba Mungu yupo, inabidi usitumie Biblia wala Qurani. Kama unaweza kufanya hivyo, is just a matter of seconds. Natamani ningekuwa namfahamu ningewzeza kumsaidia! Na nilishamwambia siku zote kuwa maandiko matakatifu Biblia na Quran, let's say kukosa credibility kwake yeye haku-automate a guarantee ya kwamba Mungu hayupo!
 
Hili swali zuri sana, nitamjibu kwa sababu hukunipa uwezo wa kukujua.

Kama mungu ndiye mtoa vyote, mpaka uwezo wa kumuelewa yeye, ataweza kunilaumu kama sitamuelewa ?

Nimejaribu kwa uwezo wa akili zangu zote kuamini kwamba kuna mungu lakini kila nikijaribu nashindwa, maswali na maswala kibao yananionyesha hakuna mungu.

Hata Yesu kwenye maandiko alisema kwamba manabii waliyatamani kuyaona mambo mengi ambayo sisi twashuhudia kwa wakati huu,binadamu amepewa limitations flani ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuona na kujua zaidi ya wewe uliyesema nimenyimwa uwezo wa kukujua,kumjua Yesu na kujua maandiko hilo ni tosha kwa Mungu.Anachotaka Mungu ni Imani yako tu!
 
Thx sana wana jamvi hili wote.
Haya mawazo ya mbingu, jehanamu, dhambi na kadhalika huwa ni mtizamo wa mtu, jamii husika. Ndiyo maana yanatofautiana sana kati ya mtu na mtu.
Kwa mtu ambaye huelewa wake wa mambo ni mdogo sana, picha ya Mungu wake anayemtengeneza kichwani huwa tofauti sana na mtu ambaye huwa ana uelewa wa mambo mengi, na haijalishi hata wakiwa ndani ya dini moja.
Wengi wetu tumekuwa watu wa kupokea taarifa kuyakumbatia bila hata ya kujipa nafasi ya kuyachambua vizuri. haswa linapokuja swala la Mungu, mbingu, na mengineyo.
Kiranga thx sana angalau kwa kuona japo mwanga.
Swali ambayo tunatakiwa tujiulize wote
Je Mungu ni nini?
Ni kitu?, ni mtu?
Je Mtu ni nini?
Je Mungu mungu ana limit/mipaka?

Naombeni sana msaada wenu.
Sorry kama nimewakwaza kwa namna yoyote ile.

Kisungura hujakwaza baba ni haki yako kujua mambo.

Nitajaribu kukujibu kwa mamchche kuhusiana na maswali yako hapo juu (kwenye red).

Je Mungu ni nini?
JIBU: Ni roho.

Ni kitu? ni mtu?
JIBU: Si kitu wala si mtu.

Je Mtu ni nini?
JIBU: Mtu ni wewe,mimi na wengine (wanadamu),mwenye Roho, Nafsi na Mwili.

Je Mungu ana limit/mipaka?
JIBU: Mungu hana limit wala mipaka, ila kwa upande mwingine Mungu na Dhambi ni vitu viwili tofauti. Kwa hiyo kilicho kichafu(dhambi) kwa Mungu ni kelele na njia moja ya kuiondoa hiyo ni Toba kupitia kwa mwnaye Yesu Kristu.

Nadhani nimekusaidia kwa kadri uwezo wangu,naamini kuna wengine watakujibu vizuri zaidi yangu.
 
Hata Yesu kwenye maandiko alisema kwamba manabii waliyatamani kuyaona mambo mengi ambayo sisi twashuhudia kwa wakati huu,...
Wewe umewahi kushuhudia nini ambacho manabii hawajawahi kukiona, bahari ya Hindi ikitenga njia katikati?

Siri kubwa moja niliyoigundua pia ni kuwa ukitaka kumsaidia huyu mtu aamini kwamba Mungu yupo, inabidi usitumie Biblia wala Qurani. Kama unaweza kufanya hivyo, is just a matter of seconds.
Kama "inachukua sekunde" fanya basi, onyesha kuna jehanam/Mungu/ahera bila kutumia msahafu.

Ni sawa na mtu anakwambia "thibitisha kuwa alichosema Kikwete ni kweli" halafu wewe unaenda kuleta nakala ya hotuba ya Kikwete eti ndio uthibitisho. Hapana, haikusemwa thibitisha amesema, imesemwa thibitisha hajatuongopea. Kwa hiyo usianze na "Mungu kasema yupo kule..." Kamlete!
 
Ipo maeneo ya Misri, ni shimo kubwa ambalo ndani yake uchomwa takataka muda wote na hivyo moto wake hauzimiki! Hivyo kibano cha sinners baada ya kifo kinafananishwa na hilo dampo!
 
Back
Top Bottom