Jeetu Patel ashinda zabuni ya matrekta!

Mwache ayalete huenda tutafaidika nayo katika kilimo chetu duni.....

Huu ujinga wa kusema tumwache ndo umetupelekea tukitanga tanga kila siku bila kujua adui yetu ni nani kumbe ni sisi wenyewe tunajiloga kama wewe hapa duh kweli Miafrika ndivyo ilivyo.
 
Si mpaka ayalete. Utashangaa hizo bilioni 50 atalipwa, matrekta hayatakuja na deni hilo itabebeshwa serikali ya Tanzania!

Kama mnabisha mtaona!
 
Hivi hakuna wajasiriamali ambao wanaweza kuwekez ana kuagizaaa hayo ma trekta????????huyu hajamalizana na kesi yake leo anapewa tender kubwa namna hiyo tz hii hakua nchi ingine bla bla kama hii

Tatizo kubwa ni "information". Watanzania wengi ni wajasiamari kwenye maduka ya stationery na saloon na kunyoa nywele tu! Halafu wepesi sana wa kuridhika.

Wahindi wana taarifa zote za pesa zilizotengwa na serikali kwa ajili ya maendeleo na wako bize mchana na usiku kutafuta namna ya kuzipata. Si ajabu hata hii ya matrekta Jeetu alikuwa ana taarifa zake, akaenda India ku-rob na serikali ya kule (usishangae kusikia pengine aliongozana na Waziri wa Kilimo). Kisha tukapewa mkopo usiokuwa na riba!

Sasa niambie hiyo tenda unataka apewe nani? Lazima atashinda yeye!
 
Hiyo tender aliyoshinda Jeetu ilimfanya Manji abwabwaje kwenye vyombo vya habari kwamba Jeetu kapendelewa au kapindisha mambo hadi hiyo tender ashinde.

Ajabu Manji alilalama kwamba sheria za manunuzi ya serikali hazikufuatwa: moja kuu likiwa 'TENDER WAS NOT ADVERTISED IN ANY MEDIA' Tunashangaa kama ni hivyo manji yy alipataje tender document na ku - bid?

Tuna mzigo wa viongozi wanaoamua mambo ki siasa kwa sababu hapa kinachoangaliwa ni mwaka 2010 wapi pesa ya kampeni itapatika. Haya matrekta yanakuja kwa mgongo wa kilimo kwanza na si ajabu hata bei itakayonunuliwa hayo matrekta tutakuja kuumia watumiaji. HIVI NI LINI INDIA WAKATENGENEZA TREKTA IMARA?
 
Hii ni Bongo bwana. Wanakuja maskini wanatajrika katika masaa, tena tunawalilia wachukue haraka na watuachie chenji tu. Wahindi wote wanaokuja Afrika hawaji kuhubiri Uhindu, ni biashara. Afanyaye biashara lazima awe mjanja. Hujasikia marehemu wa miaka 20 kapanda cheo serikalini?

Leka
 
Nimesoma habari kuwa Jeetu Patel ameshinda zabuni ya kuleta matrekta yenye thamani ya bilioni 50 toka ambayo ni mkopo wa serikali ya India kwa Tanzania. Mkopo usio na riba. Sikuelewa hapo inamaana ni Jeetu Patel yule aliye kwenye kesi ya EPA au mwingine?? TUTAFIKA katika mapambano ya makali haya ya kuwabana watu walionatuhuma za kukwapua mablioni ya TZ!! Je si vema kususa hata biashara nao?? :confused:
We susa wenzio wale!!
 
Huu ujinga wa kusema tumwache ndo umetupelekea tukitanga tanga kila siku bila kujua adui yetu ni nani kumbe ni sisi wenyewe tunajiloga kama wewe hapa duh kweli Miafrika ndivyo ilivyo.
Mi africa mijinga kweli ndivyo ilivyo,sasa asingeshinda hiyo zabuni ulitaka ashinde nani?yupi mwenye nia ya kujitoa kibongo bongo,hao baba zetu wenyewe dili wanaona nyumba ndogo na kununua majini,huyu mtu hakuja kusoma kutembea bongo embu mwacheni afanye lilomleta."Siku zote maendeleo ya mvivu yapo kwenye njozi(kitandani)".
 
Habari za siku,jamani ki ukweli sometime nashindwa hata kufikiri sijui nimekuwa mvivu wakufikiri ama no ukali wa maisha hata nikisikia jina la mmoja kati ya Wale walioko kwenye kesi anajaribu kutoa ushauri juu ya lolote lile nahisi kama nataka kumfuata Mwalimu Nyerere.Kwa vile JEET amekuwa akijipatia mahela toka kwa wadanganyika basi hata hilo pia linawezekana.Hebu wale waliowahi kwenda India hivi trekta toka India nakumbuka SWARAJ ndio trekta toka India.linauwezo wa kushindana na FORD,MASSEY , KUBOTA.
 
Huyu jamaa ni mtuhumiwa na si-muhalifu, Tanzania ni inchi inayofuata sheria...innocent til proven guilt.

Kwani nani kasema ni muhalifu!! Alafu anaweza akashinda hiyo kesi kwa sababu CCM hawana ubavu wa kumfunga baada ya kumuagiza akachukue hizo ela BOT. Na hata wasipomtia hatiana haibadili ukweli kuwa huyu jamaa ni mwizi tu.
 
Kama viungo vyako vyote sba vya fahamu vipo makini, uwezi kushangaa mtuhumiwa wa EPA "Jitu" ameshinda zabuni .....hicho ni kitu kidogo sana kwa zabuni za Serikalini ndugu yangu. Wajuzi wa mambo wanasema ni zabuni chache na "uchwara" kama za ununuzi wa vifaa vya ofisi na kufanya usafi maofisi au kupika na kupamba kwenye dhifa za Serikali ndizo zinazotoka kwa "wabongo wenye urai wa kuzaliwa"

Hii "sisitimu" yetu "wa-tz wenye asili ya Mumbai au Uta-pradesh" na wale wanaoishi Canada na Tz kwa wakati mmoja " wameikaba kila kona!...... Hakuna zabuni itakayotolewa na Serikali usikute sura ya "huko" hata akiomba "Mpori Mnyakyusa", yeye atakuwa kivuli tu anatumika, ukichimba zaidi utakuta nyuma yake yupo "Mwenye asili ya huko......!!!" (ndani naeleweka!)

Jitu asilalamikiwe sana, yeye ni mwakilishi tu wa kampuni ya Escot toka " In -dia" ambayo kisheria inatambulika kama "legal body". Aidha, hta kama "Jitu" hasingehusika moja kwa moja kwenye zabuni aidha kwa jina lake au jina la kampuni yake, bado hakuna Mtanzania anayeweza kujua hiyo ya India ni ya nani kama tusivyojua ya Shirika letu la Reli "TRC" kwenda mdudu "TRL"..Kwani Jeetu ni mwenye asili ya wapi??????? au angepata Manji nae ni wa wapi!!!!!! labda tungekuwa "confortable" angepewa "Mzee wetu wa IPP Media" tungejua labda kama sio wa Kibosho basi wa Huru kishimundu.........Oh, vpi kama angepewa "mzee wetu wa Waraka" (anaye endesha sasa standi kuu ya Mabasi - Ubungo Terminal) tungefurahia?????????...

Inawezekana hata hyo ya India ikawa ya familia ya mmoja kati ya wale wenye asili ya huko au pia ikawa ya mmoja kati yetu (nani alijua yule Yuda wa Isikaliot aliyekuwa anakula na kunywa bure mvinyo ambao Wagalatia, Warumi na Wayunani wenye dhambi walikuwa wakimletea Mwalimu (Yesu Kristu)angefikia siku akubali kubadili fikra na kuanza kutafuta "vijiseti!" wakati akiwa "kundini" na akiwa na uhakika wa ufalme wa mungu wa bure kabisa ambao wengi walikuwa wakiutafuta kwa kusali na kulia kila siku???? Huyu YUDA sijui tumfananishe na nani katika Serikali yetu, ambaye ana acha kuambatana na Bwanake (yule aliyemwita kundini) na kwenda kutafuta "dili" za hela tena za kutoa uhai....(anyway).......

Labda kwa mfano unaoonekana, nani alijua mtu aliyepewa dhamana ya kumshauri Mkuu wa Nchi kwenye masuala yote ya kisheria (Chief Legal Advisor) na ambaye alikuwa akila na kunywa mezani kwa mkuu wa nchi muda anaotaka angeweza kuingia kwenye mtego na kishawishi kibaya cha "kupenda sana vijisenti kuliko nafasi yake na nduguze (Watanzania)....??????? ......

Nadhani mnyororo wa watu hawa wenye asili ya huko ambapo mshinda zabuni ametokea kila mtu anaufahamu !. Kwa taarifa za uhakika, tokea Serikali yetu ilipojitoa kufanya biashara, kumekuwa na utitiri wa makampuni hapa nchini ambayo yamefunguliwa na watanzani wenye asili ya .......(huko mnakomanisha) tena nyingine ni za watoto ambao hata miaka kumi na nan hawajafikisha. Kuna kampuni moja maarufu hapa nchini oofsi zake zipo hapo "Barabara ya Marehemu Baba wa Taifa -Mungu" amrehemu!, hiyo kampuni inakaba uchumi wa nchi kila kona kuanzia inalima, inanunua mazao, inatengeneza na kuagiza toka nje baadhi ya zana za kilimo, inasindika na kuuza au kuleta toka nje mazao an vyakula (mpaka tandare ina meza!), inafuga, inatengeza maji, itatoa huduma za benki, inauza daftari na vifaa vingine vya maofisi, ina maduka ya simu za mikononi, inamiliki timu ya soka, ipo kwenye biashara ya siasa kupitia mmoja wa wakurugenzi wake, inauza vipuri (spear parts), ina maduka ya vifaa vya ndani na samani (fenitures) na maduka y kubadilishi fedha, inafanya biashara ya kusafirisha abiria, inaagiza toka nje madawa ya kilimo na mbolea, ........sina shaka itakuwa na saluni na kumb za starehe pia..... Kwa tetesi toka ndani ya ofisi za umma inasemekana hiyo kampuni ndani yake ina kampuni dada "sister companies" zaidi ya Ishirini na hilo ni uhakika kabisa.

Inapotokea zabuni, kampuni hiyo kubwa na yenye jina huhakikisha kila kampuni yake inaomba ili kuhakikisha ushindi wakati wote na pengine unaweza kukuta ni kampuni za mtu mmoja tu zimeomba zabuni (!!!!!!)........Inasemekana kuwa zabuni nyingi ambazo kampuni hiyo na makampuni yaliyo chini yake imehusika sana Serikalini ni zile za sekta ya kilimo na ununuzi wa vifaa vya ofsi ambapo inadaiwa kuwa nyaraka za zabuni (bidding documents) huwa zinatofautiana kidogo sana hususan kwenye jina la mwomba zabuni, bei, jina la mkurugenzi anaye mweka saini kwenye nyaraka husika na stairi ya maandishi (font type/ size). Ila maelezo mengine yote ndani ya zabuni huwa ni sawa sawa kabisa (copy and paste). Aidha, inadaiwa kuwa hata kwenye barua za kulalamikia pale inapotokea jambo ambalo kampuni hiyo na makampuni yaliyo chini yake yatakuwa hajaridhishwa, mwandishi wa barua husika kwenda Serikalini huwa ni mmoja na unaweza kuona tofauti kwenye jina la kampuni na mtia saini tu.

Katika hali hii wanajamii mnategemea nini kwenye zabuni zinazotangazwa Serikalini????????.... TUNAHITAJI MUDA WA KUJIFUNZA KWA YALE TULIYOAMBIWA TUTATEKELEZEWA, TUSIPOYAJUA LOLOTE LAWEZA KUWA JIBU.............
 
Kaka maelezo yako ni makali kama hiyo rangi ya damu uliyotumia lol!
 
Mnasahau kwamba mwaka 2010 ni kampeni na CCM ndiyo zao hizo ? Vigari vile vya CCM nilitolewa India na sasa wanataka pesa waingie uchaguzini mwakani nk . Mikataba ya nyuma sijui inasemaje hadi tunashangaa Jeetu Tapeli kushinda hii . Wahindi wana lalamika kwa nini afungwe na lazima naungana na wale wanaosema hakuna kesi ya EPA ni kuzugana .
 
Jamani kumbukeni huyu ndiye aliyewanunulia CCM mahindra za kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2005, kwa nini wasimpe tenda ili awaletee magari mengine ya uchaguzi 2010? Hiyo ni Kasi mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya katika kuleta maisha bora kwa kila MTZA Hongera kwako JK kwa mbinu zilizochakaa! Siwaelewi wTZA wanaowapitisha CCM bila kupingwa kabisaaaaa. Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.
 
Nimesoma habari kuwa Jeetu Patel ameshinda zabuni ya kuleta matrekta yenye thamani ya bilioni 50 toka ambayo ni mkopo wa serikali ya India kwa Tanzania. Mkopo usio na riba. Sikuelewa hapo inamaana ni Jeetu Patel yule aliye kwenye kesi ya EPA au mwingine?? TUTAFIKA katika mapambano ya makali haya ya kuwabana watu walionatuhuma za kukwapua mablioni ya TZ!! Je si vema kususa hata biashara nao?? :confused:
Huyu dawa yake ni kumwacha ayalete hayo matrekta kisha yachukuliwe bure kufidia pesa yetu ya EPA
 
mwenzio mjanja, hayo matrekta yanaletwa kutokana na mkpo toka serikali ya india na sirikali yetu ndio inatia saini kwenye huo mkopo, jeetu hapa anapromote biashara ya nyumba zake mbili ya tz na ya india, na kamisheni anakula kote kuwili(tanzania na India)
 
Nashangaa wanaodai eti Jeetu ndo analeta matrekta,sasa huo mkopo nani atalipa?Ukweli ni kwamba watakaolipa mkopo ndio walioleta matrekta,isipokuwa ni via Jeetu,kama this is the way we think then kazi ipo,what kind of mentality is this?Yani tunalipa kufisadiwa?Wengine wakidai eti "Wacha ayalete" nk. Kama mambo yangekuwa yanaendeshwa kiuadilifu,then tungesubiri baada ya tuhuma kumalizwa kwenye vyombo vya sheria then apewe consideration kama ni proved innocent beyond reasonable doubt.
 
Mkuu heshima mbele kidogo sasa kama serikali ya India inaipa mkopo nafuu serikali ya Tanzania huyu Jitu anaingiaje kwenye deal au Serikali ya Tanzania haiijui serikali ya India ingawa ni nchi rafiki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom