Jee, huu ndio utawala bora?!

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,266
4,716
Wana jf, nimekuwa nikitazama sakata la mabaraza ya madiwani na watendaji wa halmashauri mbalimbali hasa baada ya ligi ya vikao vya bunge vilivyopita na kugundua kuwa mabaraza ya madiwani yatarudisha maendeleo ya nchi nyuma(i stand to be corrected). Mtazamo wangu ni kuwa nyuma ya kile kinachoelezwa kama utendaji mbovu wa watendaji wa Halmashauri kuna wingu zito la roho ya kifisadi ya madiwani, wenyeviti na mameya wa manispaa na majiji. Tazama haya yafuatayo kwa uchache:

1. Kuvunjwa kwa nyumba za tabata dampo(4 yrs ago). Mkurugenzi wa Manispaa ya ilala pamoja na wasaidizi wake walifunguliwa mashitaka kwa kile kilichoelezwa kama uzembe na kuisababishia serikali hasara. Hata hivyi, ukweli ni kuwa naibu meya ndiye aliyekuwa ameshinikiza utekelezaji wa zoezi hilo, hapa ni nani aliyesababisha hasara?!, ofisi ya meya au ya mkurugenzi?!, je serikali inalichukulia vipi tatizo hili?.

2. Magu. Hivi karibuni baraza la madiwani limeazimia kumchukulia hatua mkuu wa idara ya Kilimo na mifugo kwa kile kilichoelezwa kama kumpitisha mkandarasi kufanya kazi bila ridhaa ya baraza, mhusika alijitetea kuwa kandarasi hiyo ilikuwa na baraka za mwenyekiti, mwenyekiti amekana.

3. Halmashauri ya morogoro. Baraza limewasimamisha kazi watendaji 9 na kuwapa onyo kali wengine 12. MY take- maofisa wa serikali wanaoubavu wa kujitetea mbele ya mabaraza haya yanayoonesha kuwa na uchu wa kujinufaisha kisiasa?, serikali haioni kuwa hali hii inakudumaza maendeleo kwa ku-intertain jazba za madiwani.

4. Manispaa za DSm, kuna rekodi isiyopingika kuwa madiwani na mameya wote wa manispaa za DSM sasa wameamua kuvaa viatu vya wakurugenzi na wasaidizi wao. Madiwani na mameya wa dar sasa hawafuati mwongozo wa utendaji kazi wa madiwani na mameya. Mameya wote na madiwani wote huripoti ofisini kila siku na hutumia mali za halmashauri kila siku. Mwongozo huwataka kuwepo ofisisni kwa siku zisizo zidi 3 kwa wiki. Kwa kufanya hivi ofisi ya meya huwa na matumizi makubwa kuliko bajeti iliyotengewa, hivi serikali hailioni hili?.

Hata hivyo, mameya wa DSM wamejiwekea rekodi ya kuunda tume mbalimbali zisizo na tija ambazo huzigharimu halmashauri fedha nyingi, fedha hizi zingeweza kutumika kwenye shughuli za maendeleo, badala yake hutumika kuwa -entertain madiwani katika vikao/kamati zao amabzo haziko katika mpango wa bajeti.

Karibuni tujadiri hili.
FINALLY; hawa wanasiasa ndio wanaosababisha utendaji mbaya katika halmashauri.
 
tatizo madiwani wamepewa madaraka makubwa ........... Na wengi wanafanya maamuzi ingawa 1.shule hamna au 2. Wanafanya kwa maslahi binafsi......

Too bad wengine ni vifisadi vidogo.....
Na tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuingiza siasa kwenye utendaji, taratibu hazifuatwi badala yake mashinikizo ya kisiasa ndiyo yanayofuata hivyo kusababisha hasara zinazoweza kuepukika, au kusababisha uvunjifu wa taratibu na kuzaa query zisizokuwa na sababu, too bad zikija audit query wao sio wajibuji na wanakana kuwa hawakuhusika.....
 
Kimsingi+kisheria madiwani hawakupewa madarak makubwa, sheria inawapa nafasi ya kushiriki katika maamuzi ya halmashauri zao kwa kusikiliza mipango ya mkurugenzi(katibu wa baraza) na wao kushauri. Sasa hivi wamepoka madaraka ya afisi ya mkurugenzi nasasa wao wameingilia shughuli ya kupanga na si kushauri. Imefikia mahali madiwani hawataki wakurugenzi ama watendaji wanaowakumbusha juu ya kufuata taratibu.
tatizo madiwani wamepewa madaraka makubwa ........... Na wengi wanafanya maamuzi ingawa 1.shule hamna au 2. Wanafanya kwa maslahi binafsi......

Too bad wengine ni vifisadi vidogo.....
Na tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuingiza siasa kwenye utendaji, taratibu hazifuatwi badala yake mashinikizo ya kisiasa ndiyo yanayofuata hivyo kusababisha hasara zinazoweza kuepukika, au kusababisha uvunjifu wa taratibu na kuzaa query zisizokuwa na sababu, too bad zikija audit query wao sio wajibuji na wanakana kuwa hawakuhusika.....
 
Back
Top Bottom