Je, Zanzibar inasonga mbele au nyuma?

Mauza uza,
Tuje katika takwimu, asilimia 95% ya wazanzibar wanaishi uk kwa benefit, sample kila wazanzibar 10, tisa wanaishi kwa benefiti.Na ulaya nzima bw. Mauza uza ukaitembea ukafanya takwimu zako hukusema sample za wazanzibari wangapi umechukuwa na ukaona wangapi wanaishi kwa benefit ila ukaja na 90% sawa,

Halafu unaashria kusema kuwa kutoka na takwimu zako, zanzibar ni nchi ya benefit haiwezi kuendelea kana kwamba uchumi wa zanzibar unategemea maisha ya wazanzibar walioko nje, na kusahau kuwa idadi ya wazanzibar walioko nje ni nduuchu ukilinganisha na wale waliopo zanzibar na tzbara ambao wanachangia moja kwa moja pato la uchumi wa taifa kupitia biashara wanazofanya kwa kodi wanazolipa.

Kama sample zako za kila wazanzibari 10, tisa wanaishi kwa benefit ndizo zinazo determine maendeleo ya taifa zima kwa ujumla, basi tukubaliane katika hili kuwa hapa Ujerumani kuna wavulana na wasichana wengi kutoka tz bara wengine wanafunzi, bila kutoka hapa nilipo kwenda kuwahesabu maeneo mbalimbali walipo,shughuli wanazofanya za kuuza miili yao na madawa ya kulevya, zinawapatia kipato si haba, mm siiti hii ni benefit kwa sababu wenyewe wanaiita kazi, wala siwezi kusema kuwa tz ni nchi ya biashara ya ukahaba na madawa ya kulevya, kwa kuwa baadhi ya raia zake walioko nje huku wanapata kipato kwa njia hiyo.Nnachoweza kusema ambacho ni sahihi kuwa bado nchi yetu yote ni tegemezi kwa kuwa hata bajeti yake ni tegemezi, inategeme msukumo mkubwa kwa mataifa hayo hayo ambayo upo ww huko bw. Mauza uza na aidha uwe unategemea benefit au la, lakini nchi yako bado inategemea sehemu kubwa misaada ya nje ili bajeti yake ya kuwapa tonge jamaa zako huko Tz isomeke.

Kuhusu uvivu, bw. Mauza uza wazanzibar uvivu wao kuishi na mke mmoja tu, hawatosheki wanata nyama nne, ila kwa kuhangaika maisha hili usiseme wenyewe watajisemea. Nilikuwa mashariki ya Kati (Israel n Palestina) nimewakuta wazanzibar wakifanya kazi mpaka katika makambi ya wakimbizi (red cross and crescent), achilia mbali huko Tz kila pahala wametawanyika wanahangaika maisha, pengine kwako ww hii ni ivivu, haya nakubali, lakini wenzako tunahangaika ww endelea na matusi, bezo na dharau.
 
Junius,
Mkuu nimekuelewa ila mie nimechukulia majority yao huko Uk/Europe kwa hivyo basi unavyosema na wabara wako vile kwangu mie hao ni Minority.Wabongo (Bara) wanajulikana na wanasfika na waafrika wengine kuwa ni wachapa kazi.Suala la uvivu hilo halina mjadala....angalia maendeleo tulio nayo bara then linganisha na Unguja/Pemba kwa ujumla wao.
Nawakilisha mkuu.
 
mkuu nimekuelewa ila mie nimechukulia majority yao huko Uk/Europe kwa hivyo basi unavyosema na wabara wako vile kwangu mie hao ni Minority.Wabongo (Bara) wanajulikana na wanasfika na waafrika wengine kuwa ni wachapa kazi.Suala la uvivu hilo halina mjadala....angalia maendeleo tulio nayo bara then linganisha na Unguja/Pemba kwa ujumla wao.
Nawakilisha mkuu.

Mauza uza,
Ndo nakushangaa hao majority wa huko UK/Europe, wanachangia vp, maendeleo yanayochangiwa na majority wa kule visiwani,au nifahamishe vizuri katika maendeleo ya huko tz hao wabara unaowachukulia minority au hata hao majority uanaowajuwa ww,wamechangia asilimia ngapi ya bajeti alau ya mwaka huu,

Mauza uza, pengine kweli bara imeendelea kuliko zanzibar.

Lakini sababu ya maendeleo hayo nakataa kuwa kwa kuwa bara ni wachapa kazi na wazanzibar si wachapa kazi, ndo wakawa hawana maendeleo hayo.

Hatuna haja ya kuendelea kuseama kuwa udogo wa visiwa vya zanzibar na uchache wa rasilimali zake ni disadvantage kulinganisha bara yenye ukubwa wa vitu kama hivyo.

Zanzibar imepigana kufa na kupona kujitafutia way out ya hali yake ya kudorora uchumi. Rasilimali zake chache inazotegemea alau za kuiingizia kipato zinafisidiwa na muungano, kila zanzibar ikitaka kujipapatua Muungano unakuwa tatizo. Hata ikitaka kujitafutia marafiki(OIC) wanaofanana nao na ambao wapo willing bila masharti kuwasaidia katika nyanja za teknolojia na elimu, umuungano unakuwa tatizo, uliza komandoo povu lilivyomtoka mapaka zanzibar ikapata chuo kikuu kwa mbinde, kisa kinajengwa kwa msaada wa taasisi ya kiislamu, leo bado mme'nga'ngania, mnalazimisha tu Zanzibar iingie katika EAC, kwa mwamvuli wa muungano, bila kujali masalahi yanayotofautiana na memba wengine ambayo yanasimamiwa na SMZ tu na si serikali ya muungano.

Kwa hiyo nakubaliana na ww bara itaendelea milele so long as zanzibar itaendelea kuwa koloni lao.
 
Hivi ni kweli Tz Watu wa Pwani: Zanzibar, Tanga, Lindi, Coast ni wavivu ktk kazi za shurba ukilinganisha na watu toka bara- Wasukuma, Wahaya, wachaga?? Je kuna ukweli ktk hili??
 
Hatima na mustakabari wa Zanzibar hipo mikononi mwa Wazanzibar wenyewe...!
Enzi ya M'Mungu kuleta mitume imeshakwisha. Akili wanayo, siasa wanazijuwa, niya wanayo, sababu wanazo, uwezo wanao.

Swali linakuja... Wapo tayari kukaa pamoja na ndugu zao wa upande wa pili wa visiwani? Maana tumeshuhudia mengi sana jinsi wanavyo watetendea ndugu, jamaa na marafiki kutoka upande wa pili wa Zanzibari.
 
Hivi ni kweli Tz Watu wa Pwani: Zanzibar, Tanga, Lindi, Coast ni wavivu ktk kazi za shurba ukilinganisha na watu toka bara- Wasukuma, Wahaya, wachaga?? Je kuna ukweli ktk hili??

Mkuu kwani Tanga, Lindi na Coast siyo watu wa Bara? Au una changanya maana ya neno pwani?
 
Zanzibar -wazanzibar ni WAVIVU...Period!!!wapi ulishaona nchi ya wavivu ikaendelea???Angalia hii takwimu:::asilimia 95% ya wazanzibar waishio UK wanaishi kwa benefits,asilimia 90% ya wazanzibar wote waishio Europe wanaishi kutegemea benefits.
Sasa mlishaona wapi nchi ya wa benefits ikaendelea????Na wakibahatika kupata vijisent wanajenga bongo sio kwao madongo kuinama Pemba.
Habar ndo hio......

Data please?? Tunataka link to the FACT. Sio unatuambia twakimu. Kuna watu waongo sana humu! I can make up any statistic ku-support argument yangu. Sasa ivi nataka kuona links tu. Sio kunipa maneno.
 
Namna Zanzibar ilivyofilisiwa mali zake na Tanganyika, maoni ya Juma Duni

Sipingi amri ya uongozi, na nathamini sana umoja wa Waislam kuliko “persona freedom and intellectual exercise, lakini kwa faida ya watafiti haya yanaweza kuwafass.

3.0 Kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania

3.1 Benki kuu ya Tanzania iliundwa kwa sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya 1965. Kabla ya hapo nchi zote za Afrika Mashariki zilikuwa zikipata huduma za ki-Benki Kuu kutoka Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki “The East African Currency Board” ambayo ilikuwa na Makao yake makuu mjini Nairobi Kenya. Sarafu (currency) ya Afrika mashariki ndiyo iliyokuwa ikitumika kwenye nchi zote zilizokuwemo kwenye Bodi hiyo. Mbali ya Kenya, Tanganyika, Uganda na Zanzibar, Somalia na Aden (Yemen ya Kusini) nazo zilikuwa wanachama. Lakini kabla ya uhuru wa Tanganyika nchi hizo zilijitoa, zikasalia nchi nne (4) nilizotangulia kuzitaja. Kila nchi ilikuwa na mwakilishi wake kwenye Bodi hiyo kuangalia maslahi ya nchi yake.

3.2 Baada ya uhuru wa Tanganyika, katika mwaka 1961, ambao uliutangulia ule wa Uganda (1962), Kenya (1963) na Zanzibar (1963) kukawa na haja ya kufikiria muundo mpya wa Bodi kwani kabla ya hapo mtawala wa nchi hizo, Muingereza ndiye aliyekuwa akiendesha na kusimamia Bodi hiyo. Sera za mambo ya fedha na Uchumi (fiscal and monetary policies) za nchi hizo zililingana kwa kuwa mtawala alikuwa ni mmoja. Ndiyo maana kukawa na haja baada ya uhuru kufikiria vipi Bodi hiyo itaendeshwa kwani sera za nchi hizo changa zinaweza kutafautiana sana na hivyo kufanya mifumo ya kiuchumi nayo kutafautiana.

3.3 Tanganyika wao wakamuajiri Dr. Erwin Blumenthal wa Bundesbank ya Ujerumani kuwa mshauri wake juu ya mfuko mpya wa Bodi hiyo. Wenzetu wa Uganda nao wakamuajiri bwana mmoja anaeitwa Newton kufanya kazi hiyo. Kenya na Zanzibar wao hawakuwahi kuajiri washauri wao. Dr. Erwin Bluementhal alipendekeza kuwepo kwa East African Central Bank ambayo iwe na State Banks kwenye miji mikuu yote ya nchi wanachama. Hivyo basi kungekuwa na State Bank ya Tanganyika, Kenya na Uganda na ya Zanzibar mbali na hiyo Central Bank ya Afrika Mashariki. Newton yeye alipendekeza kuwepo na Benki Kuu ya kila nchi. Wakati Watanganyika wanatafakhari mapendekezo ya Blumenthal, Uganda ikakubaliana na mapendekezo ya Newton, hivyo wakaanza utaratibu wao kuanzisha Benki Kuu yao. Kenya pia walifanya hivyo na Tanganyika nao wakaamua kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania, BoT. Kwa mukhtasari hii ndio historia fupi ya Bodi ya sarafu ya Afrika Mashariki ilivyobadilika.

* Kuchukuliwa kwa Rasilmali za Zanzibar kwa nguvu kinyume na Makubaliano ya Muungano ya 1964

3.4 Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (EACB) iliendelea kutoa huduma huku wakisaidia uanzishwaji wa Benki Kuu ya kila nchi za Afrika Mashariki huku wahusika wakiendeleza utaratibu wa kuifunga Bodi hiyo. Mambo yalichanganyika pale Uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963 ulipofuatiwa na Mapinduzi na baadae Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar miezi mine tu iliyofuata. Hata hivyo Zanzibar iliendelea kuwa mjumbe kwenye Bodi hii na Tanganyika pia ilibaki kuwa mjumbe hata baada ya Muungano. Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (kwa kuwa hapakuwepo na Serikali ya Tanganyika) ndiyo ikiiwakilisha Tanganyika.

3.5 Wakoloni waliokuwa wanaendesha Bodi hiyo pamoja na Watanganyika waliokuwemo kwenye Bodi hiyo akiwemo Mwenyekiti wa wakati huo wa Bodi hiyo ambae nae alikuwa Mtanganyika, hawakufurahi na kuendelea kuwepo kwa mjumbe wa Zanzibar. Kuitoa Zanzibar haikuwa tabu kwani hata Idara ya Sheria ya Jumuiya ya EACB walipania kusaidia mbinu za kuitimua Zanzibar itolewe kuwa mjumbe kama maelezo yafuatayo ya Katibu wa Bodi hiyo yalivyo kwenye kumbukumbu.

“Indeed it could be highly embarrassing as a measure likely to give further encouragement to the separatist elements on the island” (Inasema barua ya J.B. Loynes ya 1st June 1964 akiandika kumueleza muwakilishi wa Tanganyika.)

3.6 Kwa sababu suala la sarafu, mambo ya fedha na Mabenki hayakuwa mambo ya Muungano Waziri wa Fedha wa Tanganyika J.D. Namfua alijibu kwa EACB kwamba lazima muwakilishi wa Zanzibar aendelee kuwemo kwenye Bodi hiyo.

“As you will appreciate the Act of Union between Tanganyika and Zanzibar does not specifically transfer matters relating to currency to the Union Government, and pending any relevant modifications as may be agreed, the membership of Zanzibar in the Currency Board remains unaffected”. (Inasomeka barua ya J.D. Namfua ya 9th June 1964) akijibu barua kutoka kwa katibu wa Bodi hiyo alietaka kujua nafasi ya Zanzibar baada ya Muungano).

3.7 Baada ya barua hii Bwana Loynes mzungu wa kingereza alijitokeza wazi wazi kutopenda kwake kuiona Zanzibar kuendelea kubaki mjumbe wa Bodi hiyo na aliandika barua fupi kumwambia katibu wa Bodi hivi.

“We clearly do not want Zanzibar at our next meeting and I should hope that ways should be found of keeping them out. All I should like to do now is to remind you on this point so that no papers are sent across the water until we are clear where we stand”. (Inasomeka barua ya J.B Loynes 8th September 1964 akimuandikia Katibu wa EACB Bwana Hirst baada ya kuagizwa na Mwenyekiti wa Bodi)

3.8 Kwa hivyo baada ya hapo kilichobaki ilikua ni kubadilisha katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano ili iingize masuala ya fedha na mabenki kuwemo katika orodha ya mambo ya Muungano wakati uamuzi wa kutengwa Zanzibar kutoka EACB ulishachukuliwa zamani tangu 1964 hata Benki kuu yenyewe haijaanzishwa.

Fedha za Zanzibar Zaibiwa Kijanja (Makubaliano ya Muungano yachezewa tena)

3.9 Kazi ya kwanza ya Tanganyika ikawa kuingiza shughuli za matumizi ya sarafu ya Tanganyika na utawala wa mabenki ya Tanganyika kuwa ni shughuli za Muungano. Kwa kutumia katiba ya muda ya Muungano (1965), sheria Na 43 ya 1965 (1965 Act. No. 43 of 1965), Mwalimu alipeleka Bungeni marekebisho ya kifungu Na. 85 cha Katiba hiyo na kuongeza kifungu kidogo Na.XII cha orodha wa Makubaliano ya Muungano kinachohusu masuala ya fedha, mabenki, sarafu, fedha za kigeni na udhibiti wa fedha za kigeni kuwa katika orodha ya mambo ya Muungano kama inavyosemeka.

“The following matters are hereby reserved to the Parliament and Executive of the United Republic and declared Union matters: currency, coinage and legal tender (including paper money; banks (including saving banks) and banking; foreign exchange and exchange control; and subsection (1) of the section 68 of the Interim constitution is hereby amended by adding the said matters as a new item (xii) to the definition of “Union matters” therein.” (Interim Constitution 1965)

3.10 Gazeti la Serikali ya Muungano la tarehe 18 Juni 1965 ndilo lililotangaza kufanyika marekebisho hayo ambayo ni kinyume kabisa na makubaliano ya Muungano ya 1964. Baada ya kufanyika marekebisho hayo Mzee Mtei aliandika barua rasmi kwa katibu wa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki EACB na kumueleza kwamba kuanzia tarehe 29.12.1965 yeye ndiye atawakilisha Tanzania katika Bodi hiyo, jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa sana na Bodi hiyo na kujadiliwa katika vikao jinsi ya kuitoa Zanzibar.

3.11 Pamoja na maelezo hayo bado Mzee Mtei alikubali kwamba haki na mgawanyo wa faida za Bodi hiyo ubaki kama ulivyokua na kwamba Zanzibar iendelee kupewa haki zake na faida yake kutoka Bodi kama zamani. Baadhi ya maneno ya barua hiyo inasomeka hivi:

“ One of the effects of this Act is that I will represent the whole United Republic on the board, but as it was recognised at the meeting, this will not effect the reckoning of the distribution of profit or the purchase of treasury bills or other securities in respect of Zanzibar.”

(Barua Ref. TYC.46/01/582 ya Mzee Mtei kwa Katibu wa Bodi ya 29th December 1965)

3.12 Kumbukumbu tulizokusanya zinaonesha mawasiliano marefu kati ya Dar Es Salaam na Nairobi kujadili njia sahihi kisheria itakayoweza kuzichukua fedha za Zanzibar na kuziingiza katika Account za Tanganyika maana katibu na Mwenyekiti wa Bodi EACB hawakutosheka na barua ya Mzee Mtei kama inaweza kuwalinda Bodi wasidaiwe baadae. Bodi ililazimika kuwapelekea Dar Es Salaam Rasimu (draft) ya barua ambayo ikipelekwa kwenye Bodi itawalinda Bodi baadae wasije kudaiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kuungana (au wasije kudaiwa na Serikali ya Mapinduzi iliyokuwepo Zanzibar kabla kuungana na Tanganyika.)

3.13 Baada ya kukamilika kufanyika marekebisho haya ya katiba ya muda ya Jamhuri ya Muungano, Waziri wa Fedha wa wakati ule Mhe. Amir H. Jamal alimuandikia barua (Kumb.Na. TYC.46/01 ya tarehe 22 Machi, 1966) Mwenyekiti wa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na kumuagiza rasmi kwamba haki zote na amana zote (assets) za Zanzibar zilizokuwemo katika Bodi hiyo zipelekwe katika Benki Kuu chini ya Serikali ya Muungano na kwamba kuanzia pale ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania pekee ndiye tu ataeiwakilisha Tanzania katika Bodi hiyo. Haya yalifanyika baada ya kulazimisha kuingizwa kifungu Na .(xii) katika orodha ya mambo ya muungano ambacho hakikuwemo kabisa katika makuabaliano ya Muungano ya 1964. Baadhi ya maelezo ya barua ya Mhe. Amir H. Jamal yanasomeka hivi:

“On behalf of the Government of United Republic of Tanzania (hereinafter referred to as “the Government”) I have to say that in view of sub-clause xi and sub-clause xii of the definition of “Union matters” in section 85 of the Interim Constitution of Tanzania 1965 (No. 43 of 1965) barua inaendelea

—— (a) —-,

(b) all distributions of capital or profits made by the Board in respect of Tanzania including any share which but for the provisions of the Interim Constitution, referred to above, would be payable direct to the Executive for Zanzibar, are due and payable only to the Government

3.14 Huu ni wizi wa kalamu. Kwanza kuongezwa masuala ya fedha kuwa ya Muungano ni kosa la kisheria na kikatiba maana halingeweza kufanyika kwa idhini ya upande mmoja pekee. Lakini sababu ya pili ni kwamba Waziri wa fedha wa Serikali ya Muungano hakuwa na wala hajawa “Waziri wa fedha wa Muungano” na ndiyo maana hadi leo kuna Wizara za fedha mbili .

3.15 Wizara ya ulinzi au ya Mambo ya nje au ya Mambo ya ndani ni ya Muungano hasa maana hatuna Waziri wa Wizara hizo Zanzibar, lakini siyo ya fedha. Kwa hivyo si waziri wa fedha wa Tanganyika wala Gavana wa Benki Kuu angeweza kuamrisha chombo kinacho mahusiano ya kifedha na Serikali ya Zanzibar kwamba atoe amana za Zanzibar na kuzipeleka katika hazina ya Benki Kuu au hazina ya Muungano.

3.16 Kilichofanywa kuwa cha Muungano baada ya marekebisho ya katiba ya muda ni usimamizi wa taratibu na utoaji wa sarafu, na pili udhibiti wa mwenendo wa kubadilisha thamani ya shillingi ya Tanzania (currency and exchange rate control).

3.17 Tafsiri hii siyo maana yake kuchukua amana za Zanzibar. Maana huko EACB kulikua na amana za nchi nne, lakini wangereza walijua hazikua zao zilikua za Makaloni yake na ndiyo maana kila mmoja ya nchi hizo alipewa fedha (amana zake) baada ya kuvunjwa Bodi au baada ya kupata uhuru.

3.18 Kama kazi ya AECB ilikua ni kumiliki amana hizo basi waingereza wasingekuwa na sababu kuzigawa kwa makoloni husika baada ya kupata uhuru wake. Barua ya Serikali ya kingereza wakati ikijitoa kwenye shughuli za kuisimamia EACB ilieleza wazi kwamba inakabidhi dhamana za uwakilishi wa Bodi kwa Makatibu wakuu wa Wizara za fedha na siyo kwa Gavana wa Benki na barua hiyo ilitumwa na ikaagizwa kutangazwa rasmi katika magazeti ya Serikali (official Gazette) . Barua hiyo Ref. LEG/199 ya 13/9/1963 imepelekwa kwa makatibu wakuu fedha wa nchi zote tano, Kenye, Uganda, Tanganyika, Aden na Zanzibar baada ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo kutoa Notice yake juu ya uamuzi wa waziri wa Makoloni wa Uingereza.

3.19 Kwa nini Serikali ya Muungano wakazichukua amana za Zanzibar na pia kuingiza kifungu katika sheria ya Benki Kuu kwamba haki na amana hizo zote ziwe za Benki Kuu. Huu ni ushahidi mwengine wa kukosa nia njema, na ni ushahidi unaothibitisha kwamba tangu awali dhamiri ni kufuta utaifa wa Zanzibar kihadaa.

3.20 Kama kulikuwa na nia nzuri, si ingekua vyema kwa Tanzania kuwa na wawakilishi wawili kwenye Bodi moja? Kwa nini iwe sisi wenyewe kwa wenyewe tunaojiita ndugu ndio tulofanya jitihada ya kuitoa Zanzibar na kuitaka Tanganyika ibaki peke yake kuiwakilisha Zanzibar wakati rasilmali fedha (assets) si Muungano?

3.21 Kulikuwa na mawasiliano makubwa kati ya Serikali ya Muungano na Bodi hii hata kufikia kufanikisha nia yao ya kuing’oa Zanzibar kwenye Bodi. Kuna wakati “Prospective Governor”(Mkuu wa Benki hiyo mtarajiwa) aliwasiliana na uongozi wa Bodi akiwashauri kikao kilichopangwa kufanyika Dar es Salaam, kihamishiwe mji mwengine kwa hofu kuwa Wazanzibari huenda wakapata taarifa kwa urahisi juu ya kikao chao hicho cha siri.

3.22 Bila kujua nini kikifanyika nyuma ya mgongo wake, Waziri Abdul AzizTwala ambae wakati huo wa 1964 ndiye aliyekuwa waziri wa fedha wa Zanzibar aliandika Barua nyingi kupinga hatua za Waziri Jamal za kuanzisha Benki Kuu bila kwanza kukubaliana juu ya mahusiano ya benki hiyo yatakavyokua na Serikali ya Zanzibar, hasa juu ya haki na amana (assets) za Zanzibar zilizokua katika EACB. Vikao mbali mbali vilifanyika kati ya Zanzibar na Dar es Salaam kujadili masuali hayo bila mafanikio.

3.23 Kwa sababu tayari uamuzi wa kuzichukua amana (assets) za Zanzibar ulishafanyika tangu 1964, kwa makusudi kabisa Waziri Jamal na Balozi Nsekela pamoja na Mzee Bomani wakatayarisha sheria ya Benki Kuu iliyoacha kwa makusudi kuyalinda maslahi ya Zanzibar. Sheria hiyo iliingiza kifungu kilichoshusha hadhi ya Serikali ya Zanzibar kuwa sawa na Baraza la Manispaa na pia kuingiza kifungu kwamba haki zote za Zanzibar zilizokuwa katika EACB zihamishiwe katika BOT bila Zanzibar kulipwa chochote.

3.24 Katika tafsiri ya neno Public Authority ya sheria hiyo (hapo 1966) limepewa maana kwamba “Public Authority means any political subdivision of the United Republic including the Executive for Zanzibar.” Maana ya maneno haya ni kwamba kwa Mzee Mtei na Marehemu Amir Jamal Serikali ya Zanzibar ni sawa na Serikali ya mtaa au Baraza la Manispaa mbele ya Benki Kuu hiyo na hivyo hawana tena nafasi kama nchi au Serikali yenye mamlaka ya Kidola kama ilivyokua chini ya EACB.

3.25 Leo munaposikia Mhe. Pinda akisema Zanzibar si nchi maana yake ni hiyo kwamba Zanzibar ni sawa na Serikali ya mtaa tu. Kwa muda wote wa Muungano. Mwalimu na vijana wake wakijua wanalofanya. Wazanzibari tumesalitiwa na tukakubali kuhadaiwa na wale wanaojiita ndugu zetu bila kujua.

3.26 Hakuna mahala popote katika makubaliano ya Muungano panapotoa amri kwamba fedha za kigeni zichanganywe au zitakua za shirika. Hata baada ya kuandikwa Katiba ya Muungano ya kudumu bado fedha za kigeni ziliendelea kuwa ni za nchi mbili mbali mbali. Wapi walipata madaraka ya kuichukua amana ya fedha iliyomo EACB zichukuliwe na Tanganyika?

3.27 Maana kubadili katiba hakukutoa madaraka ya kumiliki mali za Zanzibar. Kilichofanyika ni kwamba kuanzia pale utawala wa fedha ni suala la pamoja na kwamba Zanzibar hawatakua na sarafu yake ya ndani wala ya kigeni kama vile ilivyo Marekani au Uingereza. Haikua na maana kwamba fedha za kigeni ni zetu shirika au zichanganywe. Fedha za Zanzibar zikaibiwa kimachomacho na baada ya hapo wizi huo ukahalalishwa kwa kuingiza kifungu katika sheria ya BoT kwamba mali zote za Zanzibar ziingie huko. Tunaposema hakuna nia njema ya Muungao huu, hivi ni baadhi ya vigezo vya ushahidi unaoonesha hadaa iliyofanyika tangu kuasisiwa Muungano huu.

3.28 Baada ya kukamilisha wizi wa kalamu, Waziri Jamal alimuandikia Waziri Twala juu ya maamuzi yake hayo siku moja tu baada ya kwisha kuiagiza EACB kuhamisha haki za Zanzibar kwenda BOT huku sasa akidhania kwamba ana nguvu za kusema suala hilo ni la Muungano.

3.29 Wakati anapoandaa rasimu ya kuongeza kifungu Na (xii) kupeleka Bungeni apate mabadiliko ya katiba Waziri Jamal aliacha kuwasiliana na Waziri Twala kwa sababu alikua hawezi kuchukua fedha za Zanzibar wakati hana kinga ambayo angeitumia kama kisingizo chake. Ndiyo maana barua ya kuhamisha fedha za Zanzibar kuingiza BOT iliyopelekwa EACB iliandikwa tarehe 22 March 1966 (Ref Na. TYC.46/01) na ile ya kujibiwa Mheshimiwa Twala ikaandikwa tarehe 23 March 1966 (Ref Na. TYC.46/08/01).

3.30 Prof. Shivji anasema hatua zote zilizofanyika za kuhamisha fedha hizi hazikua hatua zenye uhalali wa kikatiba wala kisheria. Prof. Shivji anasema kwamba kuongeza kifungu cha 12 katika katiba ya muda ni kinyume na makubaliano kwa hivyo haikua halali kikatiba na hivyo hata sheria ya fedha za kigeni kutumika hadi Zanzibar pia si halali.(Shivji :2005)

3.31 Katika kufanya marekebisho haya ya kisaliti Mwalimu pengine kwa maksudi alitafuta safari ya nje akajiondoa ili ije ionekane kwamba Mzee Karume alikubali mabadiliko hayo maana aliyeweka saini yake kwenye sheria hiyo ya mabadiliko ni Mzee Karume. Huu ulikua ni mpango mahsusi wa usaliti na hadaa iliyokua ikifanywa na Mwalimu nyuma ya mgongo wa Rais mwenzake.

3.32 Pamoja na Mzee Karume kuweka saini, Prof. Shivji anasema saini hiyo haitowi uhalali wa jambo lenyewe maana tangu awali lilikua ni kinyume na makubaliano ya Muungano.

“Clearly therefore the list of the union matters could not be amended during the interim period and neither the President nor the Parliament had the power to do so. It could therefore be argued that the addition of item 12 on the list was in breach of Articles and Acts of Union and therefore invalid.
“None of these laws could be considered legitimate either.The Zanzibar side did not then or later accepted, by conduct or otherwise the twelth item or exchange control ordinance. The powers to extend relevant Tanganyika laws to Zanzibar were in respect of Union Matters only.” (Prof. Shivji 2008:140)

3.33 Kwa hivyo katika Benki Kuu ya Tanzania kuna mchango wa Serikali ya Zanzibar ambao kwa muda mrefu Serikali ya Zanzibar ilipokuwa ikidai ikipata hujuma eti inahatarisha Muungano. Si hivyo tu ila pia kumbu kumbu zinaonesha kwamba wakati wa kuanzisha Benki Kuu za kila nchi ulipofika, Bodi hii iliamua kutoa fungu kuzisaidia nchi hizo kuanzisha Benki Kuu zao. Tanganyika ilipewa Paundi za Kiingereza 668,884 sawa na Kenya na Uganda

3.34 Zanzibar kwa vile ilikua imeungana na Tanganyika haikupewa chochote wakati ule, kwani uongozi wa Bodi ya sarafu tayari ulishaambiwa kwamba Tanganyika ndiyo Tanzania kwa maelezo hayo hapo juu, uliona kuwa kutaanzishwa Benki Kuu moja, hivyo watoe mchango kwa Benki kuu moja ya Tanzania “by virtue of being partners in the Union”

3.35 Bahati njema Bodi ilipeleka Paundi za kiingereza 82,840 kama ni mchango wa Zanzibar katika uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania. Fedha hizo zilimezwa na Tanganyika na kuundwa Benki Kuu moja, The Bank of Tanzania (BOT) kwa mtaji wa Paundi za Kiingereza milioni moja wakati huo ikiwa ni sawa na Shilingi milioni ishirini (20,000,000) za Afrika Mashariki (East African Shillings) Kasoro ya kufikia pauni 1,000,000 ilijazwa na Serikali ya Muungano. Kwa urahisi zaidi tazama hesabu hizi chini:

Mchango wa Serikali ya Tanganyika ni Pound za Kingereza 668,884
Mchango wa Serikali ya Zanzibar ni Pauni za Kingereza 82,840
Jumla ndogo (ST + SMZ) ni pauni 751.724
82,840*100 /751,724 = 11.025%
82,840 *100/668,884 = 12.388482%
3.36 Muda wote ule wa uhai wa EACB, Zanzibar ilikuwa ikipata si chini ya asilimia 12.40 (12.4 %) ya mgao wowote ule unaotolewa na Bodi kwa Tanganyika. Ukweli huu unathibitishwa kwa kuangalia mgao uliofanyika wakati zikigawiwa fedha za mwisho zilizobaki katika Account za Bodi hiyo kama zilivyooneshwa katika kumbu kumbu ya Bodi hiyo za (21st August 1972 zilizoandikwa na Mr. A.C.C.Roberts).

—–“Shs. 10,120,000 apportioned according to the Board’s distribution formula would be:-

Accounts with Cenntral Bank of Kenya shs. 3,239,169
Accounts with Bank of Uganda shs. 3,239,169
Accounts with Bank of Tanzania shs. 3,641,662
shs.10, 120,000

Fedha zilizopelekwa Benki Kuu ya Tanzania ziko tafauti na zile za Kenya na Uganda kwa (shs. 3,641,662 – 3,239,169 = 402,439). Fungu hili ni ziada kwa Benki Kuu hii kwa sababu ni fedha za Zanzibar. Kima hiki ni sawa na asilimia:

402,493*100 / 3,239,169 = 12.42581%
402,493*100/3, 641662 = 11.0525 %

Sawa na ile iliyotolewa kwa ajili ya kuanzisha Benki Kuu hapo juu.

3.37 Barua Ref. No.INV/EA/F/196 ya 21st March 1964 iliyoandikwa na H.R.Hirst kumpelekea Mr. J.H. Butter inathibitisha Formular iliyokua ikitumiwa kugawa faida na fursa za huduma za Bodi hiyo kwa nchi wanachama wote.

“It is stated in the 1961/62 Reports that the Board agreed a new formular for sharing of dstributable profits. The same formular is applied to fix the Government portions of the fiduciary issues and that Tanganyika, Kenya and Uganda have been given precisely equal shares.——My own view, therefore, is that it would probably do more harma than good to “hedge” on the percentages which are of course 28.1/6 % each for Tanganyika, Uganda and Kenya. 12% for Aden and 3 1/2 % for Zanzibar.”

Kumbukumbu hizi ni sawa na kusema:

Kenya 28.1667 %
Uganda 28.1667 %
Tanganyika 28.1667 %
Jumla 84.5001 %
Aden 12. 0000
Jumla 96.50001 %
Zanzibar 3.50000 %
Jumla 100.00000 %

Na ndio maana utaona kuwa hata kwenye mchango wa uanzishaji wa Benki Kuu ya Tanzania, Zanzibar ilipewa asilimia yake kwa mujibu wa Formular ya kugawana kati ya nchi hizo nne kuingizwa katika kuanzisha Benki hiyo. Mlinganio wa sehemu ya Zanzibar na ile ya Tanganyika ni 3.50/28.16667 ni sawa: 12.426%, sawa na mgao uliotolewa hapo juu wa sh. 10,120,000 za mwisho.

3.38 Amana za Zanzibar katika Benki Kuu, zipo si kwa sababu Zanzibar ni partner wa Muungano tu bali zipo amana zetu kama wana hisa wa Benki hiyo (shareholders). Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania haikutaja kabisa kama Zanzibar ni mmoja ya wenye hisa wala haikutaja kwamba Tanganyika nayo ina hisa. Kinyume chake mwenye hisa 100% kwa sheria hiyo ni Serikali ya Muungano peke yake. Si Serikali ya Tanganyika wala Serikali ya Zanzibar ingawa sheria ile ikijua kwamba Tanzania maana yake Tanganyika kama nitavyonesha baadae.

3.39 Lakini kwa mujibu wa hesabu hizo hapo juu wenye hisa katika B.O.T ni watatu, Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano. Kila moja ikiwa na hisa zifuatazo:-

Mchango wa Serikali ya Tanganyika ni Pound za Kingereza 668,884
Mchango wa Serikali ya Zanzibar ni Pauni za Kingereza 82,840
Jumla ndogo (ST + SMZ) ni pauni 751.724
82,840*100 /751,724 = 11.025%
82,840 *100/668,884 = 12.388482%

Kwa sababu katika hizi Paundi 248,264 asilimia 11.02 ni za Zanzibar basi, 11,02% x 248,246 = 27,356.71 ni za Zanzibar. Jumla ya fedha za Zanzibar katika uanzishwaji wa Benki Kuu ni 110,196.7 ambazo ni sawa na 110,196.7 x 100 / 1,000,000 = 11.02% kama ilivyochambuliwa hapo juu.

3.40 Pamoja na ukweli huo bado, Serikali ya Zanzibar haikutajwa kabisa kwenye sheria hiyo. Badala yake sheria ya Benki Kuu iliingiza kifungu ambacho kiliiteremsha hadhi Serikali ya Zanzibar kwa kuilinganisha kuwa sawa na Serikali ya Baraza la Manispaa.

3.41 Matokeo yake ni kama Serikali za mitaa zisivyoweza kukopeshwa na Benki Kuu, vivyo hivyo na Zanzibar nayo haikuweza kukopeshwa. Kama Serikali ya Zanzibar inahitaji kukopa, basi inabidi ifanye hivyo kupitia Serikali ya Muungano. Mtiririko wa mawasiliano na mijadala mikubwa kati ya Mhe. Waziri Twala na Amir Jamal inathibitisha wazi kwamba kulifanyika njama za makusudi kuuwa uchumi wa Zanzibar ili usiweze kujitegemea wenyewe. Huu ni usaliti dhidi ya Zanzibar

3.42 Hali hiyo ndiyo inayojitokeza hivi sasa na pamoja na madai mengi ya SMZ kutaka kufanyike mabadiliko ya sheria hiyo ya Benki Kuu lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa. Katika haja ya kuzibwa macho SMZ, Viongozi wa Serikali ya Muungano wamefanya ujanja wa kuiingiza kifungu ndani ya katiba kinachosema kuwe na Tume maalum ya fedha kushughulikia masuala ya Muungano. Hali imeachwa hivyo kwa makusudi kwa sababu wenzetu hawakuwa na nia njema tangu awali hapo 1965.

3.43 Mtu anaweza kusimama na kauli kwamba Sheria ya Benki Kuu iliitambua Serikali ya Muungano pekeee kama mwenye hisa. Kwa nini Serikali ya Muungano ya Tanzania, baada ya kupokea “Divedends” (faida za Benki hiyo), wakiweka wao tu bila ya kugawana na Zanzibar, wakati wao ndiyo waliopokea fedha kutoka EACB, fungu la Tanganyika na la Zanzibar kuanzisha Benki hiyo?

3.44 Kwa miaka 31, Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa ikitoa “Dididends” kwa Serikali ya Muungano bila ya Serikali ya Zanzibar kupewa chochote. Baada ya vita vya maneno na baadhi ya viongozi wa Zanzibar kutafsiriwa kwamba ni maadui wa Muungano na kutolewa kejeli kwa wazanzibari kuonekana wasaliti wasokwisha kunung’nika, kwenye mwaka 1996, ndiyo IMF imependekeza eti SMZ ilipwe na Serikali ya Muungano 5% tu ya “ Dividends“ kuanzia mwaka huo.? Sura hii inatoa picha ya wazi kwamba Benki hiyo wenyewe ni Watanganyika na kwamba Wazanzibari eti wanajipachika tu.

3.45 Hali ya ubishani wa aina hii umeshajitokeza tena hivi sasa juu ya suala la mafuta ambalo nalo liliingizwa kinyemela na matokeo yake kutoa tafsiri kama kwamba mafuta hayo ni ya Tanganyika.

3.46 Hali hii iko kwa kila taasisi ya Muungano. Na ndiyo maana nikasema kwamba hakuna nia njema, Sheria zote za Muungano zinatungwa kama kwamba ni za Tanganyika siyo za shirikisho na Zanzibar. Huu ndiyo udhaifu wa Muungano unaofichwa usisemwe. Huu ndiyo usaliti na hadaa za Mwalimu Nyerere dhidi ya Zanzibar. Mwalimu alifanya haya kwa sababu alikusudia kujenga Tanganyika mpya yenye jina jipya na mipaka mipya. Nina sababu ya kusema hivyo.

3.47 Hapo 1964 neno “Jamhuri” lilitafsiriwa kisheria kwa maana kwamba kila lilipo katika katiba ya Tanganyika lisomeke kwa maana ya “Jamhuri ya Muungano”. Lakini neno hili hili lilibadilishwa maana na kutakiwa litafsirike kila penye neno Jamhuri katika katiba na sheria zote zilizopitishwa baada ya Novemba 1972 lijulikane kwa maana yake mpya ambayo ni Jamhuri ya Tanganyika maana hiyo inajumlisha popote pale palipoandikwa Jamhuri ya Muungano. Katika sheria hiyo Na. 30 ya 1972 inasomeka hivi:

All acts and all Public documents made or issued before or after November 1972 “ The Republic means the Republic of Tanganyika and including “United Republic” (Section 3 of the Interpretation of Laws and General Clauses Act 1972 (No. 30 1972)

Kwa mujibu wa sheria hii, Jamhuri tuliyonayo sasa si Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, bali ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika.

Jee tunakosa gani tukisema kwamba dhamiri halisi ilikua ni kuunda Tanganyika mpya yenye jina jipya na mipaka mipya. “The United Republic of Tanganyika”?


Author: Unknown
 
Hizi habari za seif, Duni..za kunyonywa Zenj sii mpya hapa!

Dawa Visiwani wafanye tu kazi kwa bidii..au wakipenda wahamie bara kuna opportunities kibao!
 
Namna Zanzibar ilivyofilisiwa mali zake na Tanganyika, maoni ya Juma Duni
Author:

Hizi habari za CUF zimepitwa na wakti......kwa kifupi Zanzibar hawaendi mbele wala hawarudi nyuma na pia hawako pale pale, bali wanaruka ruka mbele na nyuma kutafuta sababu pa kutokea lakini ndo hivyo tena wameshindwa.HATOKI MTU HAPA WALISHASAINI PAPERS KWA HIO LAZIMA KIELEWEKE HAKUNA PA KUTOKEA IMEBAKI KELELE ZA WAPANGAJI.........
 
Last edited by a moderator:
Mauza uza,
tutaona kama kuna refu lisilokuwa na mwisho.Time will tell, tuombe uhai...
 
Mauza uza,
tutaona kama kuna refu lisilokuwa na mwisho.Time will tell, tuombe uhai...

uhai upi ndugu yangu junius??mkivunja muungano bila kufuata utaratibu Tanganyika inaivamia Zanzibar kinguvu ...tuone mtatokea wapi.Itakuwa utawala wa mabavu,amri amri tuu...hakuna ooh yakhe ..
 
uhai upi ndugu yangu junius??mkivunja muungano bila kufuata utaratibu Tanganyika inaivamia Zanzibar kinguvu ...tuone mtatokea wapi.Itakuwa utawala wa mabavu,amri amri tuu...hakuna ooh yakhe ..
Dunia ipi hiyo unayoizungumzia ww ya kutumia nguvu utakavyo? kama ingekuwa hivyo ndo ndivyo, basi mpaka leo East Timor ingekuwa sehemu ya Indonesia au Singapore ingekuwa bado katika muungano tatanishi wa Malay.Bado AU isingelishughulika kumfurusha kanal Moh'd Bakar alietaka kuwagawia wafaransa kisiwa cha Anjouan kwa mabavu. Dunia hii nyengine bwana mkubwa.

Comrade Fidel Castrol alikuwa na maneno yake akimkumbuka Comrade "che" Guevara, husema " hakuna silaha yeyote wala nguvu zenye uwezo wa kubadilisha ukweli wa historia".

Watu wakishaamua kusema basss hakuna cha nguvu tena hapo, kwani wakoloni hawakupiga, kuua , kufunga watu magerezani, kuwatisha n.k? upo wapi sasa ukoloni? Nna hayo yalikuwa enzi hizooo dunia imejaa dhulma na maonevu lakini bado watu walipigana na kudai walichokion haki na kikipata. Kiongozi wa harakati za kupinga uvamizi wa Italia nchini Libya 1920s, Umar al Mukhtar alipokamatwa na wataliano na kumpeleka pahala kunyongwa mbele ya watu wake, aliwambia kuwa "msisahau kuwa mnamuua mwanamapinduzi mmoja na vitoto vinashuhudia, they will letter on rise after me.." nini kimetokea?

Ndg. yangu Mauza uza we, makataba wa muungano si maandiko matakatifu ambayo agano lake lazima litimizwe milele, ni mkataba wa kimataifa wenye ridhaa tatanishi kati ya dola mbili, zinazodaiwa kuungana kwa hiari, kama dola moja itaona hakuna maslahi katika muungano, nafasi ipo ya kurekebisha au ku terminate mkataba, na hili ni jambo la kawaida tu.

Mambo ya amri amri sisi wazanzibar si watumwa kama wenzetu kule nanihii, sisi tumezoewa kuamrisha tu na kama haliwezekani, tunaamua tu POTELEA MBALI...
 
hata singapore ilijikwamua kwa kutegemea bandari tu ......
si dhani kama tatizo ni soko la karafuu. kurudi nyuma kwa zanzibar kumesababishwa na utawala mbaya wa ccm.
 
uhai upi ndugu yangu junius??mkivunja muungano bila kufuata utaratibu Tanganyika inaivamia Zanzibar kinguvu ...tuone mtatokea wapi.Itakuwa utawala wa mabavu,amri amri tuu...hakuna ooh yakhe ..

Kama munataka kuigeuza Tanganyika kuwa Somalia basi kakivunjika haka kaji muungano kenu ivamieni rasmi Zanzibar, patakuwa hapatoshi.
 
uhai upi ndugu yangu junius??mkivunja muungano bila kufuata utaratibu Tanganyika inaivamia Zanzibar kinguvu ...tuone mtatokea wapi.Itakuwa utawala wa mabavu,amri amri tuu...hakuna ooh yakhe ..

Man this is wrong.....mimi ni mbara but this is wrong. Kama kweli unaona Zanzibar siyo muhimu kwa nini ukaevamie tena? Sijui hata nianzie wapi maana fikira zako wazijua mwenyewe.
 
Kama munataka kuigeuza Tanganyika kuwa Somalia basi kakivunjika haka kaji muungano kenu ivamieni rasmi Zanzibar, patakuwa hapatoshi.

Usijidanganye wewe...bongo haiwezi kuwa Somalia hata siku.HAITATOKEA KAMWE HIZO NI NDOTO ZA MWENDA WAZIMU.Mna ubavu nyie wa kupigana na bara...rojorojoo.
 
Usijidanganye wewe...bongo haiwezi kuwa Somalia hata siku.HAITATOKEA KAMWE HIZO NI NDOTO ZA MWENDA WAZIMU.Mna ubavu nyie wa kupigana na bara...rojorojoo.

Kwani kupigana na Tanganyika kunataka ubavu - kwa nguvu gani mulizo nazo? hizo Mig 24 tano na mabomu yaliyopitwa na wakati yanayokuripukieni Mbagala? pamoja na tanks zilizopitwa na wakati kutoka Urusi? hizo tanks zilitumiwa kwenya 2nd world war - angalia takwimu ya silaha za Tanzania na ni aibu tupu, kama ubavu tu ndio unaamua mapigano Mmarekani angelikuwa keshaiweka sawa Afghanistan zamani tu. Acheni njozi hizo hamuwezi kupigana na nchi yoyote, vita vya Uganda tu na mpaka leo uchumi umeyumba seuze leo mukiwa na civil war na Wazanzibari mutakuwa kuliko Somalia. Hebu anzeni muone.
 
mkuu nimekuelewa ila mie nimechukulia majority yao huko Uk/Europe kwa hivyo basi unavyosema na wabara wako vile kwangu mie hao ni Minority.Wabongo (Bara) wanajulikana na wanasfika na waafrika wengine kuwa ni wachapa kazi.Suala la uvivu hilo halina mjadala....angalia maendeleo tulio nayo bara then linganisha na Unguja/Pemba kwa ujumla wao.
Nawakilisha mkuu.

Mauza Uza unaelewa kitu human nature ?kima mahali katika dunia hii watu waiashi katika mazingira waliyo jichagulia kama vile maisha ya kimakabila ,sasa unapokuja na hoja za kuwasema watu fulani unatakiwa kwanza utowe uovu wako binafsi ,hapa bara kuna maneno mengi kama yako huwambiwa waisilamu kuwa wavivu hawana elimu nk ,na ukija kwa upande wa zanzibar kuna maneno kama hayo lakini cha kushangaza umewataja wazanzibar waishio ulaya na namna gani wanaishi,huku ukijifanya umehafilika kueleza kiwango kikubwa cha wanawake wanaotoka Tanganyika wanaoishi UK na German wengi wao wanajishuhulisha na kazi za kuuza mili yao,wamechukuwa nafasi iliyokuwa ya wa ghana,ukienda HUMBUG ni aibu hata kujiita MTanzania,kule Uk wamekuwa ndio tambara bovu la wanigeria (watu wakale)na mataifa mengine.
 
Back
Top Bottom