Je Zanzibar imewahi kuwa Koloni la Waarabu au la Watanganyika?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
WAnasema Zanzibar ni koloni la TAnganyika; wanatuita watu wa bara kuwa ni "wakoloni"; wanasema bila hata kufikiria kuwa ati Muungano hauna uhalali kwa vile hakukuwa na kura ya maoni; kwamba ati "watu waulizwe" kwanza ili wajue wanataka nini. Hawa hawa hawaelezikama Sultani alipigiwa kura na Wazanzibari kuwa SUltani wao? Hawa wanaamini Sultani alikuwa na uhalali wa kutawala Zanzibar hata kama Sultani huyo hakupigiwa kura, wala wananchi wake kuulizwa kama wanataka aendelee kuwatawala.

Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?
 
Wazo kwamba Tanganyika ni watawala wa kikoloni wa Zanzibar ni wazo kutoka katika vichwa vya Wazanzibari MISUKULE wa Sultani aliyehamisha makazi yake kutoka jangwani Oman na kuja Zanzibar kuliko na neema tele kisha kupinduliwa na kupoteza kiti.

Kwa kudhani kwamba Sultani akirudi matabaka yatarudi na wao kwa Nasaba yao watakuwa mahali fulani pa neema chini ya miguu ya Sultani wanavalia njuga ishu ya muungano kikengekenge.

Wazanzibari hawa wanahusudu Utawala wa sultani raia wa Oman kuliko Uzanzibari wao.

Sultani wa Omani ni muarabu wa kuja, Zanzibar si kwao hakujawahi kuwa kwao na kamwe hakutakuwa kwao.

Sultan Shamsh anaiona zanzibar kama Koloni wazanzibari na zanzbar ni mali yake binafsi iliyoshuka toka juu mbinguni kwa ahadi kedekede kwa mashoga zake, anawatongoza baadhi ya wazanzibari kumpigania kwa kila hali arudi.

Anakipande cha ardhi yake huko jangwani Omani huyu, alipopinduliwa alitakiwa aenda huko cha ajabu alikimbilia UK na sasa maswahiba wake wanapigana kufa ili arudi awatie utuwani tena.

Utumwa wa kuchagua bwana wa kumtumikia wakati mwingine ni mtamu kama ziwa la mama.

Muungano una matatizo kibao la kwanza likiwa mkataba wa muungano wenyewe.

Hata hivyo Usultani hata unoge vipi haufikii hata robo ya Uhuru wa Wazanzibari uliopo leo hii.

Ni ujinga kudhani Zanzibar ni koloni la Tanganyika wakati Tanganyika yenyewe hata katika ramani ya dunia au ya kisiasa haipo. Kinacho wapa tatizo wazanzibari leo hii ndicho hicho hicho kilicho iua Tanganyika.

Ni haki kudai kura ya maoni juu ya muungano lakini si haki kudai utawala wa Sultani Zanzibar ulikuwa halali.

Huyu mjinga kutoka Omani tunajua tarehe aliyokuja Zanzibar rasmi na kujiita Sultani.

Sijui waungwana wanaodai Uhalai wa Sultani wanaweza kutuambia ni Sultani gani duniani anayepigiwa kura??

Masultani hutembeza mkong'oto wa nguvu na kumwaga damu ya wengi ndipo kwa ubabe hujitangaza kuwa Masultani.

Sultani aliyeshikishwa kichapo na kukimbia kigoda chake cha wizi ni vipi adai kurudi kwa kutumia uhalali wa kujitangaza sultani?

Naanza kuona jinsi hekima inavyochujuka kila kukicha pia nahisi kuna agenda ndani ya agenda ya kudadisi uhalali wa muungano huku Usultani ukikumbatiwa kwa HUG kubwa na mololo ya kiBEAR
 
Chondechonde wasije kuigusa Dar es salaam, mambo yao yaishie hukohuko. Tuombe kura za maoni na sisi mji wetu uitwe Mzizima, mji wa Pazi huu bwana siyo wa Majid. Jina la Dar es salaam liko kisultani mno kama wa Brunei vile.

Tuige mfano wa Oagoudougou na Harare au Maputo.
 
WAnasema Zanzibar ni koloni la TAnganyika; wanatuita watu wa bara kuwa ni "wakoloni"; wanasema bila hata kufikiria kuwa ati Muungano hauna uhalali kwa vile hakukuwa na kura ya maoni; kwamba ati "watu waulizwe" kwanza ili wajue wanataka nini. Hawa hawa hawaelezikama Sultani alipigiwa kura na Wazanzibari kuwa SUltani wao? Hawa wanaamini Sultani alikuwa na uhalali wa kutawala Zanzibar hata kama Sultani huyo hakupigiwa kura, wala wananchi wake kuulizwa kama wanataka aendelee kuwatawala.

Hivi, kabla ya uhuru wa 1963 Wazanzibar walipiga kura ya maoni kuhusu kuendelea kwa Sultani kama "constitutional monarchy" au nani aliamua hili?
Kwa hiyo kama Sultan aliwatawala kinguvu ndio kunaipa haki Tanganyika nayo iwatawale kinguvu?
 
Ni Sultani wa Zanzibar aliyeleta jina la Daressalaaaam kwa ulaini aloukuta kuburuza watumwa. Wazanzibar mpaka weusi wanajiita waarabu, kama sifa, wanajutia mabibi zao hawaja wahi kubakwa na waarabu ili nao wapate rangi kama wapemba
 
Jamani tuwe wa kweli sioni uhalali wa ZANZIBARI kulundikwa huku BARA ktk bunge letu kama vile sisi hatujiwezi kiakili! kuna wabunge 80 kutoka Zanzibar wa nini wote hao? Wizara ya AFYA wamepewa bila sababu yeyote? Hazina usiseme wako kibao kazi yao kubwa kutukwamisha katika mipango makini Kama muungano unaweza kujadiliwa basi haya yote yazungumzwe. ZANZIBAR kwetu ni mzigo! Waondoke tuliwapenda lkn hawabebeki
 
Chondechonde wasije kuigusa Dar es salaam, mambo yao yaishie hukohuko. Tuombe kura za maoni na sisi mji wetu uitwe Mzizima, mji wa Pazi huu bwana siyo wa Majid. Jina la Dar es salaam liko kisultani mno kama wa Brunei vile.

Tuige mfano wa Oagoudougou na Harare au Maputo.

wewe unatafuta ugomvi mwingine kabisa; ila pendekezo lako zuri sana... "Mzizima".. sidhani kama wazee wa Dar watakataa
 
Wale watu wamedumazwa na dezo dezo kutoka uarabuni,na sasa wanajiona wao kama waarabu nakuanza kuwatenga wanyamwezi wasukuma na wengine weusi wakijisahau kuwa kile ni ardhi ya mtu mweusi,waarabu wanawadumaza sana hawa jamaa.
 
Mzee,

Maswali la kizushi;
(a) Hivi wao hawana haki ya kuukana uafrika na kuukumbatia uarabu?
(b) Is blackness synonymous with "Africanness"?
(c) Kama wanajisikia wako karibu zaidi na uarabu kuliko uafrika/ubara/weusi who do we blame?
(d) Them or?
(e) Are we Tanganyikans (or more appropriately their supposed "colonisers") to decide for them where to pledge their allegiance, katika Muungano au kwa uarabu/usultan au uzanzibari?
 
Nadhani wajiite wanavyotaka, ili mradi wasije kuunguza bar huku. Hakutakalika huko walipo na mmanga hata mmoja hawezi kulizimisha nyomi la wanywa bia wa Dar, I mean mzizima.
Kaeni huko huko msituletee balaa huku.
 
Mwanakijiji hizi thread za kuhusu zanzibar unazimwaga Kama vua kila baada ya siku moja lazima uchomoe moja kwenye archives yako kwi! Kwi! Kwi! Kwi!

Huyu mzee namkumbuka wakati wa mchakato wa serikali ya umoja wa kitaifa alikuwa hivihivi! Anaonekana anaumri mkubwa lakini anashindwa kusoma alama za nyakati, anatimia mida wake mwiingi kwa vitu vya fitna fitna, kizazi kilichopo sasa zanzibar hakijui chochote na wa hakina haja ya kujuwa kuhusu sultani wala mapinduzi, wanachohitaji mi mabadiliko tu! Wanachokioma wao kuwa nchi yao imekaliwa na Tanganyika.
 
Nadhani wajiite wanavyotaka, ili mradi wasije kuunguza bar huku. Hakutakalika huko walipo na mmanga hata mmoja hawezi kulizimisha nyomi la wanywa bia wa Dar, I mean mzizima.
Kaeni huko huko msituletee balaa huku.
Hivi ukivunjika hawa wapemba walioko Huku tandika itakuwaje?
 
Back
Top Bottom