je?wewe ungemfanyaje.

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Unakaa kijjni na shughuli zako ni kupeleka jongoo mjn,lkn ukiondoka mkeo naye anagawa uroda kwa jamaa, jirani mwema akaamua kukuambia kuwa unaposafiri mkeo anatoa uroda,hukumuamini na kuamua kufanya uchunguzi mwenyewe, ukamdanganya mkeo kuwa unasafiri ili umfumanie,ukaenda kujificha kwa jirani,usiku wa saa 3 jirani anakuambia kuwa mume mwenzio kashafika nyumbani kwako,ukaamua kwenda kufumania huku ukiwa na ghadhabu tele ile unabisha hodi tu hamadi!ukavamiwa na Simba ila wao walikusikia ukibisha hodi pia wakamsikia Simba anakuvamia,jamaa akatoka na Mchi na kumpiga nao Simba,Simba akakuacha na jamaa akakuingiza ndani kukuokoa na akaufunga mlango kwa ndani ili Simba asiweze kuingia,unajikuta mko watu wa3 unamuangalia jamaa ana kanga 1 ya mkeo na nguo za jamaa ziko chini unamuangalia mkeo naye ana kanga 1 kufuli na jeki zake ziko juu ya kitanda,je?ingekuwa wewe ungemfanyaje jamaa.
 
Duh, mkuu hii ungepeleka jukwaa la mahusiano ingenoga kwei kwei kwani haionekani kama joke joke hv,lol...
 
nadhani ni hadithi ya kutunga, lkn niruhusunisema iliyyomtokea kaka yangu ambayo ni kweli kabisa na shemeji alikuwa bomba sn, lkn alitoka mkoa wa pwani walikuwa wakiishi Gmboto alikuwa ni mlinzi wa kanisa la Lutherani pale Ukonga, akienda usiku kazini mama anaingiza jamaa, jirani wema kwa maneno niwengi lkn wakukupa mshiko uanze mradi wachache sn.
jamaa kajifanya anaenda kazini karudi saa 7 kamkuta jamaa, kubisha hodi mama akatafuta mahali pakumuweka akaona ni uvunguni alipofunguliwa akasema washataa mama akawa anawasiwasi, yeye akawasha, akachungulia uvunguni akamuona jamaa, akamwambia toka jamaa alipotoka kaka akasema mama lete chakula, kamkaribisha jamaa akasema nimeshiba, alipomalia kula akamwambia mkewe twendetusindikize mgeni, wakaenda umbali kama wa mita 200 akamwmbia karibu tena ndug yangu, hakumpiga mkewe wala hakumuuliza , siku yatatu mke akaenda kwa wazazi
 
Alipowaambia wazazi wake wakamwambia anajiandaa kukumalia usikubali kurudi huko tena, ndugu zake wakaenda kuchukua nguo ake, siku chache mkewe akaolewa, je ingekuwa wewe ungefanyaje?
 
Alipowaambia wazazi wake wakamwambia anajiandaa kukumalia usikubali kurudi huko tena, ndugu zake wakaenda kuchukua nguo ake, siku chache mkewe akaolewa, je ingekuwa wewe ungefanyaje?
1.kaolewa bila kupewa talaka kwanza na mumewe? 2.aliyemuoa ni yule mgeni au?
 
Ningemshukuru Jamaa kwa kuokoa Uhai wangu na kisha namkabidhi mke kama zawadi yake, ili wakale uroda kwa kujinafasi vizuri...
 
Mimi binafsi hapo sina la kujibu sababu ukisema kumsamehe maana yake unamruhusu kuendelea na uchafu wake kwingine, na ukisema umwadhibu yawezekana ukasababisha maafa kwa upande mmoja la msingi ni kumuachia MUNGU ndiye atajua lipi la kuwatenda
 
Mimi binafsi hapo sina la kujibu sababu ukisema kumsamehe maana yake unamruhusu kuendelea na uchafu wake kwingine, na ukisema umwadhibu yawezekana ukasababisha maafa kwa upande mmoja la msingi ni kumuachia MUNGU ndiye atajua lipi la kuwatenda
M/mungu hataki kiumbe wake awe mnyonge kiac hiko,ww ndiye unayetakiwa kuanza kutoa hukumu halafu Mungu atakusaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom