Je wewe ni mwana hiphop wa bongo?

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Kama wewe ni mwana hiphop wa bongo basi unaobwa kutoa/kuchangia maoni yako katika mradi mpya wa kuandika waraka wa wana hiphop kwa wapiga kura wa TANZANIA.mradi huu mpya unalenga kutoa elimu ya uraia na jinsi ya kuchagua viongozi Tanzania, Uamuzi huu umekuja baada ya kuona jinsi viongozi wetu wasivyowaadilifu,ni watumiaji wabaya wa madaraka na wasiopenda kuwajibika. Hivyo basi sisi kama wanahiphop hatuwezi kukaa kimya na kuacha mambo haya yakiendelea,sisi kama wapiganaji wa kweli ni mwiko kukaa kimya.Tanzania bila mafisadi inawezekana kama sote tukiungana na kuwaambia kuwa hatuwataki basi tutafanikiwa.Wote mnaona jinsi lasilimali zetu zinavyopotea na kuisha huku wajanja wachache wakinufaika,basi ni jukumu letu wanahiphop kukaa mstari wa mbele kupinga mambo haya.kama uko tayari kwa mradi huu basi toa maoni yako namna unavyotaka huu waraka uwe kupitia barua pepe ya mnyikungu@gmail.com na sisi tutaufanyia kazi ushauri wako.
 
Back
Top Bottom