Je waweza kupenda pasipo kumwona?

Kiroroma

JF-Expert Member
Feb 6, 2009
370
114
Hii ni habari ya kweli kabisa,Rafiki yangu wa damu walitengana au tuseme waliachana na mkewe miaka mingi iliyopita.

Mkewe huyo akaolewa na kuzaa watoto kadhaa. Sasa rafiki yangu huyu kaniambia nimtafutie mchumba nikamsimulia kuhusu shemeji yangu mmoja yuko upcountry nikampa namba ya simu wakaweza kuwasiliana.

Cha kushangaza ni kuwa rafiki yangu huyu amefikia hatua ya kufanya maamuzi ya kumuoa yule shemeji yangu, hawajakutana hawajuani hata picha yake kila mmoja hamjui mwenzake zaidi ya mawasiliano kwenye simu tuu!!!

Ni mwezi wa tatu sasa unaenda wako kwenye mapenzi moto moto, ila kutokana na wingi wa kazi kila mmoja hapati mwanya wa kwenda kuonana na hasa hasa umbali uliopo kati yao.

Naomba kusikia kutoka kwenu wadau.
 
Dah,Inahitaji Imani kubwa katika hili,Lakini kwa dunia ya sasa,sijui!
Mie nimesoma habari za mtu mmoja kwenye bible anaitwa Isaka alitafutiwa mke ambaye ni Rebeka na mfanyakazi wao na akaletewa tu.Wengine waliona kwanza.Sasa kwa case yako,mhhh! sina majibu kamili
 
kama wanaelewana kwenye simu basi uwezekano ni mkubwa wata click wakikutana!!
Ndoa ni kuelewana na si sura!!
 
Mie naona kawaida sana coz jamaa ana imagination zake kuhusu huyo dada, na huyo dada ana imagination zake kwa huyo jamaa yako, km vile chatting kwenye internet inavyodanganya. wala usiwe na wasi wasi kwa sababu ndoa haifungwi remotely lazima wakutane one day, hapo kila mtu atapima upeo wake na zile imagination kwamba ile expectation ndo hii naiona before my naked EYES? km sawia basi itakuwa jambo la kheri lkn km mmoja hakuridhika basi utaona mawasiliano yanakuwa sio km yale ya mwanzo taratiiibu uhusiano utakoma, hata km watamegana lkn kama no SPARKS flying jamaa yako lzm utamwona atakuwa mzito wa kuongelea uhusiano wao.
 
kaka saluti kwa posti zako!
 
Cha kushangaza ni kuwa rafiki yangu huyu amefikia hatua ya kufanya maamuzi ya kumuoa yule shemeji yangu, hawajakutana hawajuani hata picha yake kila mmoja hamjui mwenzake zaidi ya mawasiliano kwenye simu tuu!!!

Ni mwezi wa tatu sasa unaenda wako kwenye mapenzi moto moto, ila kutokana na wingi wa kazi kila mmoja hapati mwanya wa kwenda kuonana na hasa hasa umbali uliopo kati yao.

its possible lkn washauri wakutane kwanza, wakishakutana muulize huyo jamaa wako mtazamo wake tena kisha utamsikia atakavyosema...
 
ya.....kwani hujawahi uziwa au kuona mtu anauziwa mbuzi kwenye gunia................................kama huamini basi jibu ni kuwa waweza kumwoa bila kumwona..............
 
...KUPENDANA....wamevutiana tu hao hawajapendana, utapenda vp kitu hujajua uzuri wake? utapenda nn sasa pale?...labda amependa sauti!
 
kama wanaelewana kwenye simu basi uwezekano ni mkubwa wata click wakikutana!!
Ndoa ni kuelewana na si sura!!

aha aha aha eti wata click!!!! mouse au sio mkuu,duuh?
kwa kweli hiyo inawezekana kwa wakati huu wa utandawazi,ila tatizo linakuja je ni kweli wataendelea kupendana hata baada ya kuonana? mana hapo wamecope may be kwenye interest,etc,lakini figure,appearance etc bado,lakini uwezekenao wa kuendelea ni upo kabisa,mi naamini hivyo mana nimeshaona watu walianzia hivyo na sasa wako pamoja,na ndoa ina amani kabisa kuliko wewe uliyemfukizia baada ya kumuona
 
inategemea wako honest kiasi gani kwenye hayo mawasiliano, wengine huwa wana kuwa feki sana tu hata kwenye mahusiano ya kawaida tu sembuse kwenye simu? kama sio wakweli basi siku ya kukutana na kuanza maisha ya uso kwa uso watakoma
 
Kama huyo shemeji yako ni demu aliyekamilika na huyo jamaa yako nae yuko kamili hakuna tatizo kwani mwisho wa siku mechi itapigwa na maisha yataendelea. Kikubwa wote mwanamke na huyo jamaa kila mmoja atakachokikuta kwa mwenzake akubaliane nacho...
 
Inawezekana sana tu manake hata mimi nina story ya ndugu yangu walipendana na Msweden mmoja pasipo kuonana for two years wakiwasiliana kwenye email na simu tu. Lakini leo wana ndoa yenye amani na mtoto mmoja. So its very possible Kiroroma
 
..Kiroroma acha jamaa avute mzigo hata kama hajamuona huyo shemejio. Nina imani hata wewe ulichangia kum-brief hatimaye kumpa taarifa zote muhimu kuhusu huyo shemejio that's why akafikia hatua hiyo.Nina imani huyo jamaa yako si mjinga kiasi hicho!!!
 
Back
Top Bottom