Je, wapinzani ni wakombozi?

Mwanasiasa,
Well said.. Baabu kubwa kuhusu katiba umenipa shibe.
Vipi, Chadema wamepisha tayari mchakato huu?..
 
Kwako Mzee MKJJ
Tukiwa tunapambana kujua namna gani Wapinzani wanaweza kuongezeka Bungeni wewe una madai kwamba hawakubaliki kwa Watanzania mimi nasema wanakubalika ila matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa kura wa CCM ndiyo chanzo kikubwa hadi wao wana dorora soma hii report ni ya siku nyingi kidogo lakini haya haya yalitokea 2005 Oct japokuw watu hawakufa .


http://www.hrw.org/reports/2002/tanzania/
 
Mwanasiasa,
Well said.. Baabu kubwa kuhusu katiba umenipa shibe.
Vipi, Chadema wamepisha tayari mchakato huu?..

Kwa kweli sina uhakika kama umewahi kupitiwa kama chama. Ila najua wanachama wengi hasa viongozi wana subscribe na huu mchakato. CCM wao walishaukataa kwa kusema kuwa una mlolongo mrefu na kwamba katiba ya sasa inatosheleza isipokuwa inahitaji mabadiliko ya hapa na pale!
 
Mwanasiasa,

Nadhani utaona kuwa nimekuwa very fair ktk mjadala mzima na pengine naweza kukushukuru sana wewe.
1. Swala la matumizi ya helikopta wakati wa uchaguzi nimelikubali kutokana na maelezo marefu ya ndugu J J. Mnyika. Sirudi huko tena ila tunasonga mbele na hili jipya la matumizi ya helikopta tena, jambo ambalo limewakimbiza baadhi ya wanachama.
2. Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii umechukua 5 zangu pamoja na kwamba hukunieleza zaidi jinsi gani utaweza kugawa bugdet ya serikali.. Unapoongeza fedha wizara fulani ni lazima upunguze matumizi wizara fulani. Je, ni zipi zinazotegemea kupungua budget yake na kwa nini?
3. Swala la kubadilisha katiba umenipa dawa safi iliyopimwa! ila tu hukugusia upande wa Zanzibar!..
4. Majimbo?... bado kabisa
5. Swala la ndoa na Conservative.... bado!
Hadi hapa nadhani tupo pamoja na yote haya ni ktk kuelimishana.
 
Lunyungu, sijasema wapinzani hawakubaliki, nimesema hawajajifanya waonekane wanahitajika (relevance). Ndio maana swali la msingi la mada hii hapa ni "Wapinzani ni Wakombozi"? Ni mpaka wafanye watu wawaone kweli wanawahitaji wasitarajiekupata viti vingi bungeni. Jinsi gani wanajifanya kuwa wanahitajika?

Kwa maoni yangu, siyo kwa kuonesha mapungufu ya CCM au serikali yote, kwani kila mtu anayajua na matatizo ya wananchi chini ya serikali ya CCM ni dhahiri. Huhitaji kuwa mwanasayansi kuweza kuyafahamu.

Mimi na wengine ambao tunaangalia kutoka nje (ya CCM na Upinzani) bado hatujaona mvuto wa upinzani zaidi ya kuipinga CCM. Upinzani lazima uwe zaidi ya kupinga na kukosoa, lazima wawe wanatuonesha kuwa wanaweza kuongoza na kutawala. Hadi hivi sasa binafsi sijawa impressed kuwa Tanzania inaweza kuwapa uongozi wa nchi wapinzani na matatizo yetu yatakwisha. Matatizo ya Kenya yamekwisha sababu NARC wako madarakani? Je, matatizo ya Zambia yamekwisha? vipi Malawi? Wapinzani watafanya nini zaidi kuliko kile ambacho kinaweza kufanywa au kimefanywa na CCM.
 
Mimi na wengine ambao tunaangalia kutoka nje (ya CCM na Upinzani) bado hatujaona mvuto wa upinzani zaidi ya kuipinga CCM. Upinzani lazima uwe zaidi ya kupinga na kukosoa, lazima wawe wanatuonesha kuwa wanaweza kuongoza na kutawala. Hadi hivi sasa binafsi sijawa impressed kuwa Tanzania inaweza kuwapa uongozi wa nchi wapinzani na matatizo yetu yatakwisha. Matatizo ya Kenya yamekwisha sababu NARC wako madarakani? Je, matatizo ya Zambia yamekwisha? vipi Malawi? Wapinzani watafanya nini zaidi kuliko kile ambacho kinaweza kufanywa au kimefanywa na CCM.

Vyema kabisa! Hawawezi kufanya kitu kwa vile hawajaelimika, na jamii nayo haijaelimika. Na hili ni tatizo la sub-sahara nzima. Kuna watu wanaongelea faida za upinzani kwa kulinganisha na Republican-Democrats au Labour-Conservatives, etc, sio vyema kulinganisha namna hiyo kwani Republicans+Democrats etc, ni watu walewale wanaoelewa wajibu wao, jamii ileile iliyoelimika. Sasa kwa hawa wapinzani wetu wanaogombea ruzuku au tuwaonao kila kukicha wakirudi CCM ili kuongeza ulaji, ni wapinzani kweli?

Kwa mazingira ya sub-saharan Africa ya leo, 'wapinzani wa kweli' ni wale walioamua kujikita kwenye kuelimisha jamii kwa NGO kama za Elimu, afya, wanaojenga mashule na hospitali, etc. Kwani ni kupitia huko ndio jamii itaelimika na kuweza kujua nini inahitaji kwa mustakabali wake kuliko hawa matapeli fisadi wanaopigana vikumbo kuingia ikulu.
 
Vikwazo je toka kwa Serikali zilizoko madarakani ? Maana wakijua wanapigwa bao wana anza kubadili sheria .It has happened in Tanzania the last 3 years ama mimi nakosea kukumbuka?
 
Vikwazo je toka kwa Serikali zilizoko madarakani ? Maana wakijua wanapigwa bao wana anza kubadili sheria .It has happened in Tanzania the last 3 years ama mimi nakosea kukumbuka?

Ni kweli wanawekewa vikwazo (e.g. HakiElimu), ila kuwekewa kwao vikwazo ni uthibitisho tosha kuwa wao ndio wapinzani wenyewe ambao jamii zetu zinawahitaji sasa. Kama watu wanaweza kupaza sauti kushinikiza serikali kwenye mambo kama ya kulilia ruzuku, kuibiwa kura n.k. Hizo sauti zingetakiwa haswa ziishinikize serikali ili wapinzani wa kweli wanaowekeza kwenye maendeleo ya jamii wafanye kazi zao bila vikwazo.
 
Dondola,
Kwa mazingira ya sub-saharan Africa ya leo, 'wapinzani wa kweli' ni wale walioamua kujikita kwenye kuelimisha jamii kwa NGO kama za Elimu, afya, wanaojenga mashule na hospitali, etc. Kwani ni kupitia huko ndio jamii itaelimika na kuweza kujua nini inahitaji kwa mustakabali wake kuliko hawa matapeli fisadi wanaopigana vikumbo kuingia ikulu.[

Hii ndiyo Miujiza ya Mussa na Yesu... sijui kwa nini inaonekana kuwa lugha ngumu sana.

Lunyungu,
Hata Manabii wetu hawakukuta barabara ya lami.. walihenya na kupambana na kilai ufedhuli wa Binadamu pamoja na kwamba wao walikuwa Mitume. Msitegemee kabisa kuwepo kwa ulaini.. Siasa kama Dini ni mchezo mchafu ingawa malengo yake ni kuwakomboa haohao binadamu.
 
Dondola amegusia kitu sahihi kabisa.Mie naami si wanamageuzi wote ni wabovu lakini wanafukikwa na kuchafuliwa na wanamageuzi koko.hivyo basi sehemu kubwa ya watanzania wanashindwa kuwakubali ipasavyo. Upinzani lazima pia usisahau kuwa watanzania wengi wana uvivu wa kufikiri, ukiongeza na umaskini ambao unafanya watumie 99.9% ya muda wao kufikiri jinsi gani ya kuishi, wanahitaji kuwa approached na mbinu zilizokomaa. Wanahitaji kuonyeshwa tofauti kati ya CCM na upinzani kwa vitendo na si kwa maneno .Mfano; Pesa alizotumia M/kiti wa Chadema zingetumika kununua matrekta na pembejeo nyingine za kilimo na tumia katika vijiji watakavyoviteua na kuwa kama miradi ya Chadema kuwalimia wananchi kwa gharama nafuu na kisha kuwatafutia masoko ya mazao yao kwa bei nafuu.Tofauti watakayoiona katika kipato chao itasaidia kuwafanya waamini nini watafanyiwa.Pia upinzani kwa ujumla uelekeze nguvu ktk kuchukua majimbo na si urais.Hizi mbinu za wizi wa kura hazitafua dafu pale watanzania watakapokuwa tayari kuupokea upinzani kwa kishindo.
 
Nyangumi, hicho ndicho CCM imejaribu kufanya.. nacho ni kushika hatamu na utamu wa nchi!! Wao wanajenga, wao wananunua, wanalima na kuvuna!! Mwananchi wa kawaida hahitaji kufanyiwa kila kitu. Tunachohitaji ni kujengewa mazingira mazuri ambapo soko linatuamulia nani afanye nini. Nimeshaeleza toka huko nyuma ni nini wapinzani wafanye. La kwanza, wawe majasiri kusema:

a. Upinzani ukichukua madaraka itaundwa tume huru itakayochunguza mali zote ambazo viongozi waliopita walichuma wakiwa madarakani na kuoanisha na mapato yao. Wale itaoonekana mapato yao hayawiani na mali zao basi mali zao zitafilisiwa! Wasema watalifanya hilo ndani ya miezi sita ya mwanzo ya utawala wao.

b. Wapinzani wawaambie wananchi kuwa kila kijana wa Kitanzania aliyefaulu kwenda chuo Kikuu Serikali itagharimia nusu ya ada zao na matumizi. Anayepata daraja la kwanza kila mhula analipiwa 75% Wanaoenda shahada ya uzamili watalipiwa 75% na wa shahada ya Udaktari 100% Hii ni kuonesha kuwa upinzani unatilia maanani elimu. Na kwenye hilo la Elimu Wapinzani waseme chini ya uongozi wao, Elimu ya Msingi hadi ya Sekondari (O'Level) itakuwa ni ya bure!

Pia waamue kusema kuwa yeyote anayetaka kusomea Udaktari (Utibabu) analipiwa gharama zote! (nafikiri CCM inafanya kitu kama hiki).

c. Wapinzani waweke wazi kuwa pindi wakichaguliwa, watasitisha mara moja mikataba yote ya Nishati na Madini na kurenegotiate na kampuni yoyote ambayo inataka kuendelea kufanya kazi Tanzania. Katika kufanya hivi wawaambie wananchi kuwa Serikali hiyo mpya itawachunguza viongozi wote waliohusika na mikataba hii na wale ambao walinufaika kwa namna yoyote ile watafikishwa mahakamani kwa ufujaji wa mali ya umma.

d. Wapinzani wawahakikishie wananchi kuwa Watadumisha Muungano wetu na umoja wetu wa kitaifa! Hakuna mabadiliko yoyote ya mfumo au utendaji kazi wa Muungano yatakayofanywa pasipo ridhaa ya wananchi.

Hayo ni machache ya kuanzia!
 
Hayo ni sahihi Mwanakijiji,lakini yanaingia kwa watu walikwenda shule.Tunapokuja kwa watanzania ambao sehemu kubwa wanaishia darasa la saba hiyo kwao inakuwa ngumu.Nakupa mfano.Kuna mbunge mmoja wa CCM kule KIbondo,(nimemsahau jina)alichofanya alitafuta soko la kahawa la wananchi wake. Pili, pesa anayopewa ya shangingi na baadhi ya posho zake kwenye hospitali.Wananchi kule walikwishasema hawataki mtu mwingine na huyo ni mbunge wao wa maisha.Akihama chama nao wanamfuata.
 
Akifa watampata atakayewafaa.Hata Yesu aliwalisha samaki na mikate watu waliokuja kumsikiliza.Hivyo aliwaweka fiti kimwili ili waweze ku-concentrate kwenye mahubiri yake.
 
Sio kweli.Ila kwa huyu mbunge, baada ya wananchi kupata matibabu aliwaambia nendeni mkalime,mimi nitawatafutia soko la zuri la mazao yeni lisilo na ulaji wa vyama vya ushirika.Zaidi kibondo wanalisha Mwanza na Shinyanga na Kagera.
 
Mzee Mwanakijiji,

Mzeee chagua mji!...haya ndiyo maneno napenda kuyasikia toka kwa Freeman!..
Atachukiwa na wengi lakini sio walalahoi na hawa ndio wapiga kura!

Unajua mzee siku hizi kuna masoko yameanzishwa yanaitwa Fair Trade?..Sidhani kama wakulima wa Bongo wameisha yashitukia... kahawa inanunuliwa kwa bei nzuri kuliko ile ya soko la dunia na hivi sasa makampuni mengi sana yamejiingiza kununua kahawa hizi kuzisaidia nchi maskini na hasa za Afrika. Tim Hortons, Starbucks ni mojawapo zilizojiunga ktkmashirika haya ya Fair trade... wenzetu nchi kama Kenya na Ethiopia wameisha ingia. Globalexchange ni moja ya wanunuzi wakubwa wa kahawa toka nchi maskini moja kwa moja toka kwa wakulima.
Kwa hiyo Chama kama Chadema (chenye wasomi) kinatakiwa kutafuta vitu kama hivi na kuwapa wakulima somo ama ushauri wa bure.
 
Mkandara

Hawa Starbuck wana ugomvi mkubwa sana na Ethiopia, CEO wa Starbuck alikwenda Addis ili kuweka makubaliano ya kumiliki nembo ya kahawa na hakuna suluhisho mpaka alipoondoka kwa sababu Ethiopia wamekataa udhalimu wa hii kampuni.

Sakata hili bado halijapata ufumbuzi................

Nitajaribu kupata hiyo story kutoka hapa UK
 
Starbucks in Ethiopia coffee row

Starbucks says it has programmes in place to help farmers
US coffee chain Starbucks is denying Ethiopia earnings of £47m ($88m) a year, according to Oxfam.
The UK charity says Starbucks asked the National Coffee Association (NCA) to block the country's bid to trademark three types of coffee bean in the US.

Oxfam says poor farmers would have benefited from the move but the NCA says there is no economic case to support the charity's claims.

Starbucks denies initiating opposition to the trademark application.

'Backwards step'

The Ethiopian government filed its applications to trademark its most famous coffee bean names - Sidamo, Harar and Yirgacheffe - in US courts last year.

This particular scheme is going to hurt the Ethiopian coffee farmers economically

Robert Nelson
NCA

Oxfam claims that Starbucks flagged up the application to the NCA - of which the firm is a leading member.

The NCA then filed its opposition at the US Patent and Trademark Office.

Oxfam's Phil Bloomer said the charity had worked with Starbucks in the past and appealed to the firm to "act responsibly".

"Their behaviour on this occasion is a huge backwards step and raises serious questions about the depth of their commitment to the welfare of their suppliers," he said.

Berhanu Kebede, Ethiopia's ambassador to the UK, said in a statement that the international community should support the country's efforts to ensure farmers got a fair reward for their hard work.

"This campaign has a pivotal role in redressing the unfairness of the international trading system," he said.

'Reduce demand'

Starbucks' senior vice-president of coffee procurement, Dub Hay, denied approaching the NCA to oppose the Ethiopian move.

"We did not get the NCA involved - in fact it was the other way around, they contacted us."

Robert Nelson, head of the NCA, backed Mr Hay's claim, adding that his organisation opposed the Ethiopian move for economic reasons.

"For the US industry to exist, we must have an economically stable coffee industry in the producing world," he said.

"This particular scheme is going to hurt the Ethiopian coffee farmers economically."

He claimed that the Ethiopian government was being badly advised, and the move would price them out of the market.

The trademark move would also reduce demand for the country's coffee, he said.

Oxfam said the NCA and Starbucks should not dictate to Ethiopia how best to sell its products.

Link ya hii news iko hapa:http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/6086330.stm
 
Dua, hilo sakata nimelisikia toka kwa rafiki yangu mchumi Mu-ethiopia!...
Sasa hapa ndio pima akili ya mwafrika utajua kuwa mengi tunafanya kuiga tu.
Wewe mnagombana na kampuni kubwa kwa sababu ya nembo tu. Pili, KULA ya tradefair inakwenda moja kwa moja kwa mkulima haipitii viongozi waserikali yaani hapo hakuna 5%.. mwafrika anatafuta njia za kupinga. Tazama kahawa ya Columbia pamoja na kupewa majina mengi na kutumika kwa kila kampuni duniani yenye trademark zao jinsi inavyotamba!.
Tena basi Starbucks waliipamba kahawa ya Ethiopia kishenzi na wazungu leo wanaamini kabisa kuwa kahawa ilivumbuliwa Ethiopia kutokana na matangazo ya Starbucks!..
Wee unajua kabisa kuwa waafrika hatujui kujitangaza wala fedha hiyo hatuna kwani kutangaza tu kwa mwaka ni budget nzima ya nchi.
Leo umepewa nafasi ya kuendelea kuzalisha wewe kisha mtu atumie jina lake kuitangaza mali yako mswahili unaona umeibiwa hali China wanatumiwa na makampuni yote duniani kutengeneza vitu kwa majina, trademark na kadhalika. Ethiopia wamesajili kweli majina ya hizo kahawa zao lakini kahawa bila matangazo na mkono wa mzungu huwezi kuuza America..Utakuja nambia kama baada ya miaka kumi ijayo hukusikia wenyewe wananyoosha mikono tena basi safari hii Starbuck atakuwa akimiliki mashamba yenyewe!.. Maskini siku zote jeuri sana lakini NJAA humfanya akala matumbo yake kama fisi.
Starbuck sasa hivi wanaonekana waongo kwa kuwalemba ethiopia kwa miaka yote na kuna watu wanaanza ku-question. http://www.poorfarmer.blogspot.com/
 
Back
Top Bottom