Je, wapinzani ni wakombozi?

Ukweli usiopingika kuwa walio wengi wanaamini hivyo ila ukweli ni kwamba CCM imetusaidia sana na kutufikisha hapa tulipo,ww fanya tathmini shule ya msingi umelipa Tsh 200/= kwa mwaka je fedha hii inatosha kumlipa mwalimu anayekufundisha kwa mwezi?jibu hapana basi serikali hii ya CCM tunayoichukia ndio inayojitoa muhanga kwa kuwalipa walimu,ila ni kwamba huwezi pendwa na wote na kuchukiwa na wote

Hizo sio pesa za CCM; ni kodi yangu na wewe. Walichofanikiwa CCM ni kuonesha kuwa kutoa huduma kama elimu na afya ni upendeleo (previledge) na sio haki! Kazi yangu mimi na wewe ni kuwaelimisha wananchi kuwa kazi ya kodi tunazolipa ni kwa ajili ya serikali kutoa elimu, afya na huduma zingine na wala sio kununua ndege ya kifahari, kumfanya Rais atalii dunia nzima, kufanya sherehe kubwa za sikukuu ya uhuru, kugharamia mazishi makubwa ya waziri, n.k.
 
Washawasha,

Ndugu yangu hatuzungumzii CCM hapa wala kulinganisha kati yao kwa sababu Chadema hawajapewa nafasi hiyo....

Kitila,
Kwenye elimu, afya na ustawi wa jamii chukua zangu 5...
Umesema kuwa Chadema:-

1. Mtasema kile ambacho mnataka kukifanya na ambacho mna uwezo nacho...
Nadhani wananchi wanadai kujua mbali na kusema kipi mtakifanya ambacho mtakuwa na uwezo nacho..How? ina maana mtaweza kweli kuwaambia wananchi kuwa Umeme hauwezi kupatikana kutokana na uwezo wetu mdogo ama?..

2. Pia hilo la kuweka misingi imara ya demokrasia ili wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Bila shaka misingi hii inatokana na hoja ya JK kuwaongopea wananchi!
Je, Unaweza kutupa baadhi ya proposal zenu za mfumo huu kutengua nguvu za rais wa nchi!...

Kisha ni sehemu zipi za katiba ambazo mnataka mabadiliko na yepi mapendekezo yenu? Na yalifanyiwa uchunguzi wa kitaalam (takwimu) kupata support ya wananchi walio wengi?
 
Kitila,
Kwenye elimu, afya na ustawi wa jamii chukua zangu 5...
Umesema kuwa Chadema:-

1. Mtasema kile ambacho mnataka kukifanya na ambacho mna uwezo nacho...
Nadhani wananchi wanadai kujua mbali na kusema kipi mtakifanya ambacho mtakuwa na uwezo nacho..How? ina maana mtaweza kweli kuwaambia wananchi kuwa Umeme hauwezi kupatikana kutokana na uwezo wetu mdogo ama?..

2. Pia hilo la kuweka misingi imara ya demokrasia ili wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Bila shaka misingi hii inatokana na hoja ya JK kuwaongopea wananchi!
Je, Unaweza kutupa baadhi ya proposal zenu za mfumo huu kutengua nguvu za rais wa nchi!...

Kisha ni sehemu zipi za katiba ambazo mnataka mabadiliko na yepi mapendekezo yenu? Na yalifanyiwa uchunguzi wa kitaalam (takwimu) kupata support ya wananchi walio wengi?

Naam, maswali yako yote yana akili. Naomba ni kujibu baadaye kidogo, kuna kitu kimenitinga. Ahsante
 
Mie nakubaliana sana na Mwanakijiji. Ni lazima Vyama vya upinzani vikae na vitafakali kwanini mwaka hadi mwaka vinadorola!!Wananchi wanatambua matatizo ya chama tawala, CCM kama mabavyo ninyi mnaelewa.Tatizo hapa ni kuwa upinzani haujajenga mazingira ya kuwa altenative choice kwa watanzania.Wanakurupuka tu unapofika wakati wa uchaguzi wakitegemea wananchi watawachagua kwa kuwa CCM ni maafisadi.
Huu ndo muda wa kutafakari na kuweka mikakati na kuujenga upinzani kabla ya 2010.Ni lazima wajijenge na wawe the right choice.
 
Mzee Mwanakijiji,

Makala yako inachoma!

Kwanini basi? Asilimia kubwa ya waTanzania kwa sasa hivi maisha yao ni hoe hae ukilinganisha na wakati wowote uliowahi kupatikana huko nyuma - hata ukilinganisha wakati ule wa kula unga wa yanga! Nimejaribu kuisoma labda niweze kugundua hasa ni nini unachotuelezea - nimegundua kumbe na wewe pia ni mmoja wetu ambaye unakubali kwamba utawala uliopo umeshindwa kabisa kututoa waTanzania hapa tulipo ila huamini upinzani tulionao unaweza kumaliza matatizo ambayo waTanzania tunayo kwa sasa.

Sitathmini hali ya nchi yetu kwa vigezo vya nchi yoyote kwani matatizo yetu hayafanani na nchi yoyote, haya ni matokeo ya mfumo mzima wa utawala tokea enzi ya uhuru.

Mzee Mwanakijiji, kama upinzani si ukombozi in maana CCM waendelee kuongoza hata kama wanatupeleka mtaroni? Hapo ndipo ninasema makala yako ni kali - inamvunja moyo mtu ambaye anahitaji kusikia maneno ya faraja na yanayotumainisha. Naamini wewe hukai kijijini, na wala hujawahi kukaa kijijini mwaka mzima mfululizo katika utu uzima wako. Ungekuwa ni mtu wa kijijini ningefikiri kwamba tayari umeisha kata tamaa pamoja na kwamba utawala huu uliopo ni wewe uliouweka madarakani.

Upinzani ndio bado ni dhaifu lakini nina imani angalau kwa kiasi fulani ni dira katika utendaji na utekelezaji wa sera za chama kinachoongoza. Hatua moja itafuata na nyingine, usije ukashangaa kusikia vyama vikubwa vinaungana na kuwa na chama kimoja (hapa nakubaliana nawe kwamba viongozi walipo madarakani katika hivyo vyama itakuwa si vyema wasimamishwe kugombea urais).

Mbali ya upinzani nje kuna pia upinzani ndani ya CCM...

Waliokuwa nacho ni wachache ukilinganisha na wasiokuwa nacho mwanya unazidi kukua kila kukicha. UPINZANI MADHUBUTI WENYE DIRA CHANYA (UWE NDANI AU NJE YA CCM) UTATUTOA HAPA TULIPO.
 
Kitila,
Kwenye elimu, afya na ustawi wa jamii chukua zangu 5...
Umesema kuwa Chadema:-

1. Mtasema kile ambacho mnataka kukifanya na ambacho mna uwezo nacho...
Nadhani wananchi wanadai kujua mbali na kusema kipi mtakifanya ambacho mtakuwa na uwezo nacho..How? ina maana mtaweza kweli kuwaambia wananchi kuwa Umeme hauwezi kupatikana kutokana na uwezo wetu mdogo ama?..

2. Pia hilo la kuweka misingi imara ya demokrasia ili wananchi wawe na uwezo wa kuwajibisha viongozi. Bila shaka misingi hii inatokana na hoja ya JK kuwaongopea wananchi!
Je, Unaweza kutupa baadhi ya proposal zenu za mfumo huu kutengua nguvu za rais wa nchi!...

Kisha ni sehemu zipi za katiba ambazo mnataka mabadiliko na yepi mapendekezo yenu? Na yalifanyiwa uchunguzi wa kitaalam (takwimu) kupata support ya wananchi walio wengi?

Naam Mkandara, nimerudi nilitoka kidogo. Haya ni maoni yangu kuhusu maswali yako hapo juu:
1) Ndugu yangu mimi hata mwanangu wa miaka minne huwa simdanganyi. Simuahidi kile kitu ambacho sitamfanyia maana najua nitakosa uaminifu wake kwangu. Sasa hata katika hili mimi nikiwa kiongozi sitaaidi mambo ambayo kwa hakika najua sitayafanya.

2) This a tall order question. Kwa maoni yangu kuna matatizo matatu makubwa kuhusu katiba yetu:

i) Mchakato wa uundwaji wa katiba haukushirikisha wananchi. Kumbuka katiba tuliyonayo ilitungwa kwa tume ya Msekwa kisha ikaenda kwa Mwalimu Nyerere. Kisha ikiapitishwa na NEC ya CCM, halafu ikaenda bungeni lililokaa maalimu kwa ajili ya kupitisha katiba (Constituent Assembly). Bunge lilikuwa na wajumbe 222. 101 kati ya hawa walikuwa wateule wa Rais! Kwa hiyo wananchi wa Tanzania hawajawahi kushiriki kutunga katiba yao. Katiba yeyote ya kidemokrasia utungwaji wake hushirikisha wananchi. Kwamba hatujawahi kushiriki kutunga katiba inaeleza ni kwa nini hatuijali-wote watawala na watawaliwa.

ii) Katiba iliyopo ilitungwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja na ilikuwa inakidhi mazingira haya. Tume ya Nyalali iliweka wazi kabisa bila kutengeneza katiba mpya mfumo wa vyama Tanzania utadorora maana Katiba iliyopo ina-support mazingira ya chama kimoja. Tume ya Nyalali ilisema pia haiwezekani kubadili tu katiba ya sasa ikaleta maana bila kuiandika upya kwa watawala na watawaliwa kushiriki kikamilifu.

iii) Ukiacha mchakato wa utungwaji wake, katiba ya sasa ina kasoro nyingi mno. Kwa mfano, huwezi kuamini nikikwambia kuwa katiba yetu haiongelei chochote kuhusu umilikaji wa raslimali asili ikiwemo ardhi, madini,n.k. Matokeo yake viongozi wetu ndio wenye maamuzi na mambo haya maziti ya nchi. Si ajabu basi tunashuhudia mikataba ya ajabu ajabu inayoambatana na uporwaji wa raslimali zetu, tangu enzi za Loliondo hadi sasa katika madini.

Pia gogoro la Zanzibar kwa kiasi kikubwa linachangiwa na mapungufu katika katiba yetu. Kwa mfano, badala ya serikali kutengeneza utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu nafasi ya Rais wa Zanzibar, wao na CCM yao wakijifungia wakamuengua Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais-which was a terrible mistake. Kisa, waliogopa kwamba Rais wa Zanzibar akitoka CUF itakuwaje! Hii inakuonesha jinsi ambavyo CCM wamejifungia katika box. Yaani hawezi kufikiria in a big picture, wao ni ccm kwanza, nchi baadaye! Matokeo yake ndio hivyo kwamba wazanzibar wanaona kabisa walikuwa cheated katika hili. Hata hatua ya mgombea wa urais kupitia ccm anapitishwa na NEC yenye wajumbe lundo kutoka bara ina matatizo makubwa. Ndio maana Rais wa sasa wa Zanzibar hana moral command ya kutosha zanzibar maana anajua alichaguliwa na wabara na kwamba wazanzibar ndani na nje ya ccm hawakumchagua!

haya ni maoni yangu ya haraka kabisa kuhusu swali lako kuhusu katiba.
 
Kitila,

Nasubiri majibu ya hoja nyingine kabla sijazama zaidi ktk upimaji wangu.

hata hivyo, samahani mkuu nitapenda kufahamu hiyo KATIBA ambayo itawashirikisha wananchi inaundwa vipi? (process yake)..
Pili, hili swala la rais wa Zanzibar bado zito sana kwangu! nakuwa mzito kuamini kuwa Sharrif hamad akichukua urais wa Zanzibar chini ya CUF na bara iwe chini ya CCM, kutakuwepo na mfarakano mkubwa zaidi.

Hofu yangu kubwa ni kuwa vyama hivi vyote vinapigiwa kura sio kwa sababu ya sera zao (CCM) isipokuwa nani kasimamishwa. Na kibaya zaidi ni kwamba wananchi wepesi wa kusamehe chama makosa yake inapofikia kuwepo kwa utenganishi wa rangi.

Kitila, kumbuka tu sisi ni waafrika... tuna vijimila vibaya ambavyo haviwezi kuondoka kirahisi kwa hii demokrasia ya wazungu. Hata kama ndugu yako ni jambazi, siku akikamatwa mshikaji utamtetea kwa kila hali na pengine kuficha hata silaha zake!.. kwetu damu nzito sana na hakuna demokrasia inayoweza kuvunja mila hii kirahisi.. na ndio hapo by extension tunafika hadi kwenye makabila!..sielewi hayo marekebisho ya Katiba yamezingatia kwa kiasi gani mazingira yetu ama ndio sifa za Mzindakaya kuwa na ng'ombe wa kizungu 3,000!

Anyway, yote tisa, kumi hamuwezi kuwa na mabadiliko yoyote ktk katiba bila kuchukua kwanza ushindi bungeni!..

Nasubiri majibu ya hoja nyinginezo
 
wambandwa, sawa nieleze kinagaubaga upinzani utatuoje hapa tulipo.

Mzee Mwanakijiji,

Upinzani siyo tu utatutoa hapa pabaya tulipo ila pia utarudisha maadili mengi ya mTanzania yanayoendelea kupotea kila kukicha! Wanaforum waliomakini humu wameshauri wapinzani kuwa ili kujisafishia njia ya kwenda Ikulu ni bora wakajikite zaidi kuwa na wabunge wengi sana bungeni, angalau hata turufu ya CCM isiwe kabisa na nguvu! Si ni bungeni miswada ya sheria inapitishwa? Kwa namna hiyo wapinzani watakuwa na silaha isiyokuwa butu ya kuweza kuiwajibisha serikali ifanyapo maamuzi yasiyokuwa na maslahi kwa taifa.

Wapinzani wakiwa wengi bungeni, kilio cha kubadili katiba ili iendane na wakati kinaweza kikasikilizwa kama rais hatakuwa dikteta kwa kulivunja bunge.

Nategemea upinzani kuwa na uzalendo mno zaidi ya ubinafsi kinyume na mambo yalivyo sasa. Watawala wa sasa sio siri kwao uzalendo haupo - wanachojua ni wao wenye nchi. Hawana hata ile heshima ya kuweza kuheshimu ushauri wanaopewa na wataalamu waliopo! ili mradi tu yeye ni kiongozi basi anajiona yuko juu ya kila kitu na kila kitu anakijua. Wamekosa uadilifu na pia wamejaa unafiki na ufisadi. Hivi kwa nini CCM hawakurudisha mali za serikali baada ya nchi yetu kuwa na mfumo wa vyama vingi?

HAPO NDO NASEMA BORA UPINZANI KULIKO UTAWALA HUU!
 
Kitila,
Hapo juu ulipozungumzia Constituent Assembly, umenigusa kidogo kwenye suala (au dhana) ambalo huwa najiuliza kama lina maana yoyote, hasa kwenye nchi zetu za Afrika. Nalo ni suala ama dhana ya DEMOKRASIA na (au ya?) UWAKILISHI:

UWAKILISHI maana yake nini?

Kwa mfano wako, Bunge lile la Katiba lilikuwa na wabunge, nusu yao, wakiwa ni wateule wa rais. Kama nimekusoma, wateule hao hawakuwa "wawakilishi wetu".

Je, tunapomchagua rais, si ni kweli kuwa tumempa madaraka atuwakilishe?

Na kwa hivyo, rais anapoteua watendaji mbalimbali, wakiwemo Wabunge, si "anatuwakilisha" pia? Kwani tulishamuamini na labda(?) haiwezekani wananchi wote wakawa wanapiga kura kila rais anapotaka mtendaji na hivyo "mwakilishi" wetu mwingine?

Tuje kwenye wabunge na madiwani, ambao mimi na wewe pia tunawapigia kura. Kwanza kuna mbunge (au diwani for that matter) ambaye mimi sikumchagua au nilimkataa, lakini eti "ananiwakilisha". Sawa, utasema hiyo ndiyo maana ya "demo" katika Kigiriki kuwa ni "wengi"; yaani wengi wapewe kwa vile walimchagua huyo "mwakilishi" wangu. Je, kwa wale waliomchagua ni mara ngapi huyo "mwakilishi" wao wanakutana naye na yeye kuchukua mawazo yao, ili kweli akayawasilishe na hivyo kuwawakilisha vema kwenye hatua mbalimbali za uongozi?

Utakubaliana nami, bila shaka, kuwa mfumo uliopo una udhaifu mkubwa, na kwangu mimi suala au dhana ya UWAKILISHI ni kiini macho. Binafsi, nadhani Watanzania wengi wameanza kuling'amua hilo na ndiyo maana wamekata tamaa na siasa za uchaguzi, kiasi kwamba, licha ya shida (kero!) zao, wako tayari wanywe soda na bia na wale pilau ya mgombea na wavae khanga (na mitumba!) kutoka kwa mgombea, bila kujali kama atawawakilisha, kwa sababu wanafahamu fika hakuna cha UWAKILISHI wala nini! It is just another Mazingaombwe in the name of democracy!

Najua wewe ni Mwanasiasa, na wachambuzi wengine humu ndani pia ni wanasiasa na hivyo watanisaidia kwa hili.
 
Mwanagenzi,

Nina matatizo kidogo na tafsiri yako ya uwakilishi. Rais tunamchagua ndio, lakini siyo kutuwakilisha bali kuongoza na kusimamia utendaji wa kila siku dola. Wawakilishi ni wabunge na ilivyotakiwa nikuwa Rais akitaka jambo alitakiwa aende kwa hawa Wabunge na kuwauliza maoni ya Wadanganyika wenzetu ni yapi kwenye hili suala. Mathalani teuzi kuu zinatakiwa ziidhinishwe na bunge kama ilivyo kwa waziri mkuu. Rais akiteua wabunge wakiidhinisha tena kwa kufuata maoni ya wananchi hapo ndio uwakilishi wenyewe. Siyo Rais anashauriana na mkewe halafu tunambiwa anatuwakilisha.

Demokrasia inafanya kazi vizuri kwenye nchi yenye makundi shinikizi (pressure groups). Hatuwezi watu wote kukutana na kuanza kutoa maoni, lakini tungekuwa na vikundi hivi vya kijamii ni rahisi wawakilishi kupata maoni yao huko. Watawala wetu hawataki haya maana wanajua hali ikiwa hivyo maamuzi yao ya ovyo ovyo yatawafanya wawajibike.
 
Tabasamu,
Nimesoma maoni yako huku natabasamu!

Sawa, hata tumuite rais KIONGOZI (naamini hata Wabunge nao ni viongozi wetu), si bado anatuwakilisha? Anapokutana na viongozi wa mataifa mbalimbali, au anaposaini mikataba au sheria, si pia ANATUWAKILISHA? Mimi nilidhani hivyo ndivyo.
 
Tabasamu, yote inategemea ni nini Katiba inasema. Rais hawezi kushauriana na mkewe kuhusu uchaguzi wa kama Waziri (atakuwa anavunja Katiba). Rais anatakiwa kwa mujibu wa sheria kumteua waziri mkuu ambaye atapigiwa kura na Bunge, na kisha kushauriana na Waziri huyo mkuu kuteua mawaziri wengine.

Hata hivyo ni lazima tuelewe tulikotoka. Baada ya Uhuru na Baada ya Muungano tuliweka nguvu nyingi na madaraka makubwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kwa maoni yangu ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kuimarisha umoja wa nchi na kuzuia nchi kusambaratika. Ni kwa sababu hiyo tumeweza kuepuka matatizo ya Nigeria (ambapo Rais wa Shirikisho hana madaraka makubwa ya kuzuia majimbo kujifanyia yatakakavyo) n.k

Hii iliahisisha upatikanaji wa viongozi wapya, na ilimpa uwezo Rais kubadilisha kiongozi yeyote atakavyo (at his pleasure). Hata hivyo, kufanya hivyo kulitupa tatizo moja kubwa nalo ni undugunization na urafikinization. Badala ya kutupa viongozi wanaojali maslahi ya nchi Marais wetu walianza pole pole kuanza kutoa nafasi kwa kuangalia maslahi yao na hapa na pale wakitupa mazingaombwe ya kiongozi tusiyemtarajia!

Udhaifu huu basi unalazimisha haja ya kubadilika ili kuhakikisha kuwa viongozi wanaopatikana hawana maslahi mengine bali mafaa ya Watanzania wote na siyo viongozi waliowateua. Hapa ndipo nakubaliana na wewe na wengine kuwa kuna haja ya lazima na ya mapema ya kubadilisha Katiba Yetu (suala la kuandika upya halitatokea hadi CCM ikubali au wapinzani wachukue Bunge na kulazimisha hoja hiyo!). Hivyo tunaweza kuwa na mabadiliko ya Katiba ambayo yatapunguza madaraka ya Rais katika uteuzi wa viongozi na hivyo kuweka uwiano wa madaraka (balance of power) katika ya Bunge, Rais na Mahakama.

a. Inawezekana kuwa na options mbili kwa upande wa uteuzi wa mawaziri.

- Rais amteue Waziri Mkuu kutoka chama chenye Wabunge wengi na Waziri huyo Mkuu ateue Mawaziri wote na Rais awakubali au awakatae wote na si mmoja mmoja. Kwa jinsi ilivyo sasa kuna tatizo kubwa. Katiba inasema Waziri Mkuu atatoka chama chenye Wabunge wengi. Sasa hivi ikitokea kuwa TLP ikawa na wabunge wengi Bungeni itabidi watoe Waziri Mkuu, lakini Katiba hiyo hiyo inamtaka Rais kushauriana na Waziri Mkuu kuteua wabunge. Itakuwaje kama Waziri Mkuu kutoka TLP kupendekeza majina ya Wabunge wa TLP kuwa mawaziri na Rais hawataki anataka majina ya wana CCM? Kwa vile Katiba haimlazimishi Rais kukubali mapendekezo ya Waziri Mkuu basi Rais ataweka Mawaziri wa Chama chake au atalazimisha kuunda serikali ya mseto! yatakayotokea hapo unaeweza kufikiri!!

au,

- Rais ateue Waziri Mkuu, na pamoja naye wateue Mawaziri na Manaibu wao ambao watapigiwa kura na Bunge na kupitishwa na Bunge kabla hawajachukua nafasi hizo. Mawaziri wasiwe wa Bunge ili wawe na jukumu moja nalo ni kuangalia Wizara zao badala ya kuhangaikia kampeni au majimbo yao wakati huo huo kama ilivyosasa.

- Katiba itaje idadi ya Wizara zinazoweza kuundwa ikitaja Wizara za lazima kuwepo na kuacha nafasi moja au mbili za Wizara mpya kabisa. Ina maana, Wizara kama Ulinzi, Usalama, Afya, Elimu, Nishati na Ufundi, n.k zilizo za lazima zitajwe. Kwa mfano, Katika iseme Rais anaweza kuunda hadi Wizara Ishirini na tano na kati ya hizo 20 zimetajwa wazi na tano ataachiwa Rais aunde kwa kuangalia haja ya wakati huo. Hii itapunguza gharama zisizo za lazima, itaendeleza mwendeleo uliopo, na itaondoa hali ya kutokujua Rais mpya atakuja na mambo gani mapya! Pia itaondoa haja ya kuunda Wizara ili kulipa fadhila za kisiasa! Itakuwa vizuri pia kusema idadi ya Manaibu waziri isizidi mara tatu ya idadi ya Mawaziri! (ina maana kila Wizara inaweza kuwa na manaibu hadi wawili)

b. Viongozi wenye kusimamia sehemu nyeti za serikali au idara nyeti za serikali ni lazima wapitishwe na Bunge. Hivyo wakuu wa Majeshi wote, Majaji wote wa Mahakama Kuu na ya Rufaa wateuliwa na Rais lakini lazima wajadiliwe na kupitishwa na Bunge. Wakuu wa makampuni au vitengo wasiteuliwe na Rais wala waziri, bali nafasi hizo zigombaniwe kwa kutuma maombi kupitia bodi za mashirika hayo na bodi hizo ziamue ni nani apewe nafasi hizo!

Hata hivyo katika haya yote, kiongozi yeyote anayeteuliwa na Rais ukiondoa wale ambao kwa mujibu wa Katiba nafasi zao ni za kudumu, basi watapoteza madaraka yao pindi rais ataondoka madarakani au atakapoamua kuwabadilisha.
 
Mwanry akamia kumfuatilia Mbowe


Na Raymond Mihayo, Kahama (Majira)

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM anayeshughulikia itikadi na uenezi, Bw. Aggrey Mwanry, amesema atahakikisha kila atakakokwenda Mwenyekiti wa CHADEMA yeye atafuatilia nyuma kulinda sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliyasema hayo juzi wilayani hapa, katika mkutano wa hadhara alipokuwa akikanusha kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa CCM inanunua wapinzani kwa lengo la kijinufaisha.

"Nimechukizwa na kitendo cha Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe kusema kuwa CCM inanunua wapinzani na ninakilaani sana na nitahakikisha kuwa kila atakapokwenda Mwenyekiti huyo wa CHADEMA na mimi nitakuwa nyuma yake," alisema Bw. Mwanry.

Katika mkutano huo, wananchi walishuhudia aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kahama kwa tikiti ya CUF, Bw. Ezra Machogu, akirudisha kadi ya chama hicho na kurudi CCM.

Kabla ya kurudisha kadi hiyo, Bw. Machogu alisema ameamua kurudisha kadi hiyo baada ya kushauriana na familia yake ikiwa ni pamoja na kubaini kuitumikia CUF bila mafanikio yoyote.


Huyu mpinzani alitegemea mafanikio gani akiwa anatumikia CUF?
 
Huyu mpinzani alitegemea mafanikio gani akiwa anatumikia CUF?

Hawa ndiyo wale wanaoingia kwenye vyama kwa kufuata masilahi, kumbe unatakiwa uingie kwa lengo la kuwasaidia au kuwatumikia watu. Kwa hiyo hapo inaonesha jinsi CCM wasipoangalia wanaokota makombo !!! Nikijaribu kiuangalia tangu wameanza kuwachukua hawa wapinzani tukianza na Lamwai, Marando wote sioni kama wana msaada wowote huko walioupeleka zaidi ya kukishusha chama, kwani leo hii Lamwai au Marando hata wakigombea ubunge na Mtoto mdogo anayeanza siasa muda huu, hawatapa kushinda. Hiyo yote ni jinsi walivyojishushia heshima katika jamii kwa kuwahadaa. Leo unasema hiki kizuri, ukikosa masilahi unabadilika!!! Je tukikupa nchi si utatumaliza!! Zaidi utatuletea akina Richmonduli na akina Netgroup Problems kibao.

Nawasihi kama umeamua kuwa mpinzani basi uwe kweli mpinzani wa kweli, na kama umeamua kukaa CCM basi ukae huko kiukweli siyo kufuata masilahi. Wananchi siyo watoto wa kuwadanganyia pipi. Na nyie mnaohamahama ndiyo mnaua upinzani na siasa kwa ujumla. Mnasababisha watu wanaona kuwa kumbe hata chama kikibadilika hakuna maana , watu wale wale sana sana tutaongeza matumizi kwani lazima na wao waibe kwanza ili wawe richmonduli then ndipo wawasikilize nyie. Kwa hiyo wanaona is better kuwa na walewale wa zamani ambao wameshakuwa richmonduli.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM amekasirishwa (au ametahayari?) na kitendo cha mwenyekiti wa CHADEMA kuwaambia waTanzania ukweli kwamba CCM inanunua wapinzani kwa lengo la kuuua upinzani wenyewe! Hasira hizi si kwa sababu Mbowe anaongopa na kukipaka CCM matope, hapana, hasira hizi ni kwa sababu CCM wanachelea ni nini itakuwa hatima yao kama wananchi watafumbuliwa macho.

Wasiwasi wangu ni kwamba sehemu nyingi za huko vijijini ambako umeme, maji na barabara zinazopitika kwa urahisi hakuna, bado watu wa huko wanaamini kwamba CCM ni mkombozi na wapinzani ni wasaliti!! Kwa mfano huko ninakotoka bado wazee wanajua rais wa Tanzania ni Nyerere! Hivyo basi Mwanry akienda sehemu kama hiyo kwanza atapokewa na uongozi mzima wa Wilaya nzima pamoja na kuimbiwa nyimbo na watoto wa shule za misingi - wanafunzi ambao shule yao ni mabanda yaliyokandikwa kwa udongo! Atakachosema ndicho wananchi wataamnini kwa sababu anawakilisha CCM.

Kuamini huko nako vijijini kunaanza kupungua kwa sababu kaul;i mbiu haitoki kwa viongozi wa upinzani tu hutoka pia kwa wakereketwa kama sisi tupatapo mwanya wa kwenda kijijini.. Beba redia kubwa na kanda za hotuba za viongozi wa upinzani, betri ya gari halafu wewe kila joni wakusanye wazee nyumbani kwako mbadilishane mawazo.. Ukiondoka unaona kuna ujumbe umeacha.

Ni vyema vita ya kupingana bila ya kupigana imeanza, ingawa CCM hilo hawalioni ila ni wajanja kuweza kuona mpinzani yupi yu kama wao - yaani 'mlafi', 'mnafiki' na mfisadi! Akionyeshwa pesa kidogo anasaliti chama chake. Ndugu zangu mlio upande mwingine, waangalie saana hao ambao macho yao siku zote ni kutaka kujua ruzuku ni kiasi gani imetoka... hawakitakii mema chama wala taifa letu....

UPINZANI NI UKOMBOZI WA MBONGO nina imani safari ya ushindi imeanza..

Mwanry hakugusia (hatagusia) katika ziara zake wizi wao wa kura
 
Kilio upinzani: JK leo kupokea vinara wengine

2007-01-10 16:43:47
Na Mary Wejja, Jijini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Bwana Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kupokea vinara waliotimka kutoka vyama mbalimbali vya upinzani.

Waliza wapinzani kwa kuwapokea rasmi vinara kadhaa wa kambi hiyo walioamua kutimkia CCM.

Hatua hiyo inatarajiwa kuibua kilio kingine kizito kwa kambi ya upinzani ambayo hivi karibuni, imeripotiwa ikitoa shutuma nzito kwa CCM, kwamba inawarubuni watu wake muhimu kwa nia ya kuisambaratisha kambi yao.

Malalamiko hayo mazito ya upinzani, na ambayo yamekuwa yakikanwa na CCM, yameibuka hivi karibuni baada ya vinara wao kadhaa kutimka upinzani na kwenda CCM, wakiwemo Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Tambwe Hiza na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Dk. Walid Amaan Kabourou.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, amewahi kukaririwa katika moja ya mikutano yake, akimtaka Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Mstaafu Yusuph Makamba kuacha kuwa `bize` katika kuwanunua wapinzani na badala yake, afanye kazi ya kumkumbusha Rais Kikwete juu ya ahadi walizotoa kwa wananchi wakati wa Uchaguzi Mkuu na kuzitekeleza.

Hatahivyo, CCM, kupitia kwa Katibu wake wa Uenezi na Itikadi, Bw. Aggrey Mwanri, wakatoa ufafanuzi wa madai hayo mazito, wakisema kuwa sera zao nzuri na mipango bora iliyonayo ndiyo ndoano yao katika kuwanasa wapinzani kila kukicha.

Akizungumza na Alasiri jana, Kada wa CCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk. Lenny Kasoga, amesema Rais Kikwete atapokea vinara 11 wa upinzani `waliojisalimisha` katika tawi lao la Chuo Kikuu na pia, atawapokea wananchi wengine kadhaa walioamua kutua CCM baada ya kuvutiwa na sera nzuri na zinazotekelezeka za chama chao tawala.

``Mbali na shughuli hiyo ya kuwapokea wanachama wapya wanaotoka upinzani, pia Mheshimiwa Rais atazindua Tawi la CCM la Chuo Kikuu huria,`` akasema Dk. Kasoga.

Bila ya kutaja majina ya vigogo wa upinzani watakaopokewa rasmi na Rais Kikwete leo, Dk. Kasoga amesema shughuli hiyo itafanyika katika viwanja vya CCM Mwinjuma na zimeandaliwa na Tawi la CCM Chuo Kikuu cha Dar es salaa, likishirikiana na wanachama wengine wa CCM wilayani Kinondoni.

SOURCE: Alasiri

Hapa sasa hawa wapinzani wanamaanisha nini? Je, ni wapinzani wa kweli!! Je, bado wanasingizia CCM amwarubuni!!! na kama CCM anawarubuni basi hawa si wanasiasa tunaowataka wabadilishe hili taifa lililooza, Maana hata wakishika maradaka mtu yeyote anayejiita mwekezaji atawarubuni ni kusign mikataba feki kama ya madini, ya akina Stewat na rafiki zake. Hivyo naomba rais Kikwete uwe mamcho na watu hao wanaokimbia kwa mwenzako na kujifanya wao ni wazuri kwako , huku wakivizia vyeo vya kuteuliwa kama u DC na u RC
 
Back
Top Bottom