Je, wanaohama CCM na kujiunga na CHADEMA wataing'oa CCM madarakani?

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Huko nyuma tumefananisha chama na nchi. Je,
ni jambo jema wewe kuikimbia nchi yako kwa sababu ina matatizo badala ya wewe kushiriki katika kupambana na matatizo hayo?

Tujifunze kutoka kwa wananchi wa Msumbiji na wa Angola na wa Afrika Kusini. Kama wangezikimbia kabisa nchi zao wangefanikiwa kuzikomboa nchi zao?

Kwa hivyo wanachama wa CCM wanaoendelea kupambana na maovu ndani ya chama chao bila
kukikimbia hao ni wanachama halisi wa CCM na wapenzi wa kweli na wa chama chao.

Fikiria, kwa mfano, nyumba yako ni chafu. Badala ya kuisafisha unaamua kuikimbia. Atasafisha nani?
Sababu nyingine ya wanachama wa CCM kukikimbia chama chao hapana shaka ni kutoridhishwa na uamuzi fulani uliopitishwa na chama.

Kwa mfano, kuna wanachama wa CCM
wanaoenguliwa bila haki kwenye kinyanganyiro cha kugombea udiwani au ubunge au hata urais.

Baadhi yao huamini kwamba wakigombea nafasi hizo kwenye chama kingine watafanikiwa. Na hufanikiwa.

Basi sababu mojawapo inayofanya baadhi ya wanachama kukimbia vyama vyao (na hii si
katika CCM tu) ni kukosekana demokrasia ndani ya vyama. Hii inaleta hoja kwa kila chama kuendesha chaguzi zake kidemokrasia.

Lakini ukitaka kusema kweli kitendo cha
wanachama kukimbia chama chao cha zamani huleta madhara makubwa zaidi kwenye chama wanachokimbilia.
Maana kwa sababu tu ya mwanachama kutafuta maslahi yake binafsi anaamua kwenda kujiunga
na chama ambacho haamini masharti yake wala siasa yake wala sera zake. Mtu kama huyo hubaki na mapenzi ya chama chake cha zamani.

Ndivyo anavyoonekana John Shibuda,
Mbunge wa Chadema wa Maswa Magharibi, aliyehamia Chadema ili agombee ubunge.

Hapana shaka kuna viongozi wengi wa CCM waliokimbia chama chao na kujiunga na Chadema wakiamini kwamba mwaka 2015 wagombea uchaguzi wote watakaowekwa na
CCM watashindwa uchaguzi! Kama hiyo si ndoto ya mchana mimi sijui ni kitu gani.

Basi katika suala zima la uchaguzi ni muhimu viongozi wa vyama waepushe mtafaruku ndani ya vyama vyao kwa kuweka mbele matakwa ya
wanachama badala ya kuweka mbele matakwa yao na maslahi yao kwa kuweka wagombea wasiokubalika.
Wakati mwingine mwanachama anaweza kufikiri kwamba chama chake kimekosea kupitisha uamuzi fulani ambao ni sahihi.

Akakikimbia chama chake. Mwishoni akajikuta anajuta. Turudi nyuma mpaka wakati Tanganyika ilipokuwa ikipigania uhuru. Mwaka 1957 serikali ya Mwingereza Tanganyika iliyoongozwa na Gavana Edward Twining, mwana wa Padre, ilitangaza kuwa mwaka 1958 Tanganyika ingefanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa Baraza la Kutunga Sheria (Lejiko).

Uchaguzi huo ulipangwa mpiga kura apige kura tatu kwa mpigo. Alitakiwa amchague mjumbe Mwafrika,
Mwaasia na Mzungu katika karatasi moja ya kupigia kura.

Katika utaratibu huo wa kura tatu Gavana Twining alikuwa anatekeleza matakwa ya chama cha siasa cha Wazungu cha United Tanganyika
Party (UTP).

UTP kilikuwa chama cha pili cha siasa
kuanzishwa Tanganyika baada ya TANU. Lengo la UTP lilikuwa kupigania Tanganyika iwe na serikali ya mseto (mchanganyiko wa mataifa yote).

Baadhi ya wanachama wa TANU hawakutaka TANU ishiriki uchaguzi huo. Lakini Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere, alipendelea TANU ishiriki uchaguzi huo ili ikiingia ndani ya Lejiko ipate nafasi nzuri ya kupambana na serikali ya
Mwingereza.

Basi kwa lengo la kufikia mwafaka TANU iliitisha. Mkutano Mkuu maalumu Tabora mwezi Januari 1958. Wajumbe walio wengi wa mkutano huo
walikubaliana na wazo la Mwalimu Nyerere la kushiriki uchaguzi huo.

Ndipo baadhi ya wanachama wa TANU
wakiongozwa na Katibu Mwenezi wa TANU, Zuberi Mtemvu, walijiengua kutoka chama hicho wakipinga TANU kushiriki uchaguzi huo.

Wakaanzisha chama cha African National Congress (ANC) ambacho kauli mbiu yake ilikuwa Afrika kwa Waafrika. Uchaguzi Mkuu ulipofanyika Septemba 8, 1958 yalishindaniwa majimbo kumi ya uchaguzi. Kila
jimbo lilitakiwa litoe wajumbe watatu
(Mwafrika, Mwaasia na Mzungu).
Kwa kuwa mpaka wakati ule TANU haikuwa na wanachama Waasia na Wazungu iliamua kuwapigia kampeni Waasia na Wazungu waliokuwa karibu na wananchi.

Uchaguzi ulipofanyika TANU ilizoa viti vyote thelathini. Ikaingia kwenye Baraza la Kutunga Sheria kwa kishindo.

Ikabadilisha mambo mbalimbali
mpaka uhuru ulipopatikana.
Wale wanachama waliojitenga na TANU chama chao hakikupata kitu. Mwishoni kiongozi wa ANC, Zuberi Mtemvu, alikikimbia chama chake.
Akaajiriwa Ikulu na serikali ya Mwalimu
Nyerere.

Basi si kila uamuzi unaofanywa na chama unakuwa si sahihi. Cha muhimu ni mwanachama kuwa makini.
Wakati huo huo kuna wanachama wa CCM wanaokikimbia chama chao kwa kufuata mkumbo tu. Labda kuikomoa CCM. Na kufuata nyuma yao wanachama hao wanaitwa oili
chafu ambayo haifai kuendelea kutumiwa na CCM!

Kuna wanachama wengine wa CCM
wanaoaminiwa kuwa wanakikimbia chama chao.

Kumbe kule waendako wanakwenda kulinda maslahi ya CCM! Huwezi kuepusha uwezekano huo. Waingereza wamesema, Politics is a dirty
game (siasa ni mchezo mchafu).
 
ADDITION:

TANU ya Mwalimu Nyerere ilijua hilo mapema. Kwa hiyo haikumpokea kwenye TANU Mwaasia wala Mzungu kabla ya kupatikana uhuru.
Kwanza TANU iliona kwamba katikati ya
mapambano ya kutafuta uhuru ilikuwa vigumu
kumjua Mwaasia au Mzungu aliyekuwa na
mapenzi ya kweli na TANU. Pili, TANU ilihofia
kuwa baada ya kupatikana uhuru Waasia na
Wazungu wangeweza kujitapa kuwa bila wao
uhuru usingeweza kupatikana. Tatu, TANU
ilihofia kuingiza kwenye chama watu ambao
wangejiunga na chama hicho kwa lengo la
kupeleleza na kukivuruga.
Kwa hiyo milango ya TANU ilifunguliwa kwa
Waasia na Wazungu mwezi Januari, 1963 baada
ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.
Tofauti na TANU iliyokuwa macho na watu
ambao wangeweza kuivuruga leo Chadema
inapigana vita inayodai kuwa ni ya kuwakomboa
Watanzania kutoka ukandamizaji wa CCM, huku
ikiwaingiza ndani ya chama mamia (kama si
maelfu) ya wanachama wa CCM. Wanachama
wote hawa wa CCM wanatakiwa washiriki vita ya
kuking’oa chama chao cha CCM!
Je, itawezekana? Tusubiri.
 
Wimbi laweza fanya mabadiliko yasiyotarajiwa. Time Will Tell.

Dalili zilizopo zaonesha hili lawezekana, Late JKN alisema Upinzani utakaoizamisha ccm utatoka ndani yake.
 
Was Kanu stronger than CCM?

Kanu ilimegeka coz powerful members walitoka na kuanzisha chama kingine, dont c that happenin here in bongo bt the way things are goin ikifika 2015 cdm wengi watakua either wamekufa or jela ccm wud do all they can to stay in power for whatever cost
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom