Je wanafunzi wa sekondari wanaomiliki simu za mkononi,je wazazi wanafanya vyema

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
5,818
11,001
Madenti wengi wavulana kwa wasichana wanamiliki simu za mkononi'je wazazi ndo wanawanunulia na kama ndio jeni vema
 
Watanzania inabidi tubadirike kwa maana kutumia kifaa chochote cha teknolojia kwa nia njema si vibaya,kwahiyo kitendo cha dent kumiliki simu sio tatizo na ni vema mzazi akamnunulia.
 
Ni mfumo wa maisha kwa hawa wanafunzi wa sasa kipindi cha jeykey hasa hawa wa sekondari za kata wanatumia mfumo wa Utandauchi na sio utandawazi
 
kwanza mtoa mada mwenyewe ni {via mobile} then ana blame kuhusiana na wanafunzi kumiliki simu?
Cha msingi cha kujiuliiza matumizi ya kifaa hiki.je wanakitumia vizuri,au wanakitumia tofauti?
 
Madenti wengi wavulana kwa wasichana wanamiliki simu za mkononi'je wazazi ndo wanawanunulia na kama ndio jeni vema

Naam, tena kila mzazi anatakiwa kumnunulia mtoto wake cell phone. Lakini mwanafunzi akiwa darasani, namshauri a-seti simu kwenye silence au vibration
 
Madenti wengi wavulana kwa wasichana wanamiliki simu za mkononi'je wazazi ndo wanawanunulia na kama ndio jeni vema

hili jukwaa si la wahuni. Nini maana ya madenti! Sema wanafunzi ili kila mmoja akuelewe.
 
Kwa karne hii kumzuia mtoto kumilki simu ni ujinga.
Nashauri:

1. Mzazi/Mlezi amuelimishe madhara na faida za kutumia simu. Kumiliki simu si kosa, kosa ni baadhi ya matendo yanayofanyika kwenye simu. Mtoto aelezwe.

2. Unapomnunulia simu mtoto wako jitahidi umtumie na vocha. Hii itampunguzia tamaa za hapa na pale hasa kwa hawa mabinti zetu.
 
Naam, tena kila mzazi anatakiwa kumnunulia mtoto wake cell phone. Lakini mwanafunzi akiwa darasani, namshauri a-seti simu kwenye silence au vibration

bora zaidi ni kuzima simu. Kwani akiwa darasani anaweza kupokea sms ambayo itamfanya apoteze network. Mf. Sms za mapenzi, misiba n.k.
 
mnaodai kuwa simu zinaongeza uhuni ...hivi kabla ya simu hizi kuwepo mbona mabinti walikuwa wanatoroka wanaenda kukaa kwa mabasha hata zaidi ya wiki moja ?
 
Simu ni njia mojawapo ya mawasiliano hivyo ni muhimu kwa mwanafunzi lakini cha muhimu ni kubudget muda wa simu pamoja na muda wa masomo
 
Back
Top Bottom