Je wana jf wanatosha kuwakilisha mawazo ya watanzania? (kama iliwahi kujadiliwa samahani)

mbogo31

JF-Expert Member
Nov 28, 2008
711
173
Ningependa kufahamu mawazo yenu, je sisi ambao tumepata nafasi ya kuchangia katika hoja mbali mbali humu kwenye JF na forums nyingine, je tunaweza kubeba mawazo ya watanzania wote?, je ndizo hasa hisia za watanzania wote?, kama ndio na nionavyo mimi wengi wetu tunaunga mkono CHADEMA, nini kifanyike sasa katika kufikia lengo, maana haina maana kujadili bila sisi wenyewe kufanya vitendo!
 
Kwa mtizamo wangu, JF ina:
-watu wa mikoa yote Tanzania.
-Watu wa dini zote Tanzania, pia wasio na dini kabisa.
-Wasomi na wasio wasomi,
-Wakulima na wafanyakazi(najua hii inahitaji moyo wa mwendawazimu kuimeza)
-Wazee na vijana
-wake kwa waume
-Masikini na matajiri.
Hivyo kwa dhana hiyo tu, JF inawakilisha kundi kubwa la watanzania, na mawazo yetu ni mawazo ya Tanzania nzima.
Hiyo habari ya CDM mimi sitaisemea!
 
Kwa mtizamo wangu, JF ina:
-watu wa mikoa yote Tanzania.
-Watu wa dini zote Tanzania, pia wasio na dini kabisa.
-Wasomi na wasio wasomi,
-Wakulima na wafanyakazi(najua hii inahitaji moyo wa mwendawazimu kuimeza)
-Wazee na vijana
-wake kwa waume
-Masikini na matajiri.
Hivyo kwa dhana hiyo tu, JF inawakilisha kundi kubwa la watanzania, na mawazo yetu ni mawazo ya Tanzania nzima.
Hiyo habari ya CDM mimi sitaisemea!

Short & clear clarifications, nimefurahishwa nayo PJ.
 
Binafsi sielewi swali hili lina pima kitu gani kwa sababu uwakilishi hauhitaji idadi fulani ya wahusika..

Leo hii Tanzania tuna wabunge wetu sijui kama idadi yao inatosha kuwalisha mahitaji na mawazo ya wananchi wote, pia sijui ni idadi ipi haswa inatakiwa kwa mtazamo wa hoja hii...

Na hata huko UN ni rais wetu hutuwakilisha sasa sielewi kama marais mmojammoja wa kila nchi wanatosha kuowakilisha dunia nzima..
 
kwa mtizamo wangu, jf ina:
-watu wa mikoa yote tanzania.
-watu wa dini zote tanzania, pia wasio na dini kabisa.
-wasomi na wasio wasomi,
-wakulima na wafanyakazi(najua hii inahitaji moyo wa mwendawazimu kuimeza)
-wazee na vijana
-wake kwa waume
-masikini na matajiri.
hivyo kwa dhana hiyo tu, jf inawakilisha kundi kubwa la watanzania, na mawazo yetu ni mawazo ya tanzania nzima.
hiyo habari ya cdm mimi sitaisemea!

well said mkuu
 
Mkuu JF ni moja ya majukwaa ya kujadili hoja na changamoto mbalimbali za Tanzania na dunia kwa ujumla, naamini inawakilisha mawazo ya watanzania kwani mada hujadiliwa kwa mitazamo tofauti. Pili JF haina uhusiano wa moja kwa moja na Chadema, ingawaje kuna wanachama, viongozi na mashabiki wa chadema katika Hf, kama ilivyo kwa vyama vingine hususan CUF na CCM. Kama una jambo unataka kuwaambia chadema ili kukijenga zaidi nadhani sehemu sahihi ni website ya www.chadema.net itasaidia sana.
 
Tunawakilisha mawazo ya wengi ila sio wote.
Pakajimmy ameelezea vizuri.
 
Ningependa kufahamu mawazo yenu, je sisi ambao tumepata nafasi ya kuchangia katika hoja mbali mbali humu kwenye JF na forums nyingine, je tunaweza kubeba mawazo ya watanzania wote?, je ndizo hasa hisia za watanzania wote?


Kwa mtazamo wangu jf haiwezi kubeba maoni wala kuwakilisha mawazo ya wa tz WOTE bali ya majority ya wa tz. So far nakubaliana na pakajimmy kaelezea kwa uzuri zaidi
 
kuna wanasiasa kama mnyika,mtema,zitto ambao wameingia na ID zao halisi lakini pia kuna wanasiasa walioingia na ID fake kam J.Makamba,tambwe hiza,salva rweyemam na wasomi vichwa na vijana kama kitila mkumbo..
 
kuna wanasiasa kama mnyika,mtema,zitto ambao wameingia na ID zao halisi lakini pia kuna wanasiasa walioingia na ID fake kam J.Makamba,tambwe hiza,salva rweyemam na wasomi vichwa na vijana kama kitila mkumbo..

Napenda kujua ID ya Makamba,Tambwe Hiza na huyu bwana Rweyemamu.........na hamu nao sana.....ni moja ya watu wanaongea bila kutafakari.Na inawezekana wapo hapa kutuvuruga wapiganaji wa kweli wa Taifa letu....
 
Hata wakificha ID zao tutapima hoja watakazoleta
Kama ni pumba tutajua,ukweli utashinda siku zote
Jamii forums ni ya kila mtu mwenye mapenzi mema na TZ,haina ukanda,rangi,uwezo wa uchumi,chama cha siasa nk
 
Back
Top Bottom