Je wana jf huu ni wizi, ujinga, au wendawazimu kwenye baadhi ya wizara za sirikali ya tz?

Mboja

Senior Member
Sep 29, 2010
157
23
26th February 2012


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni





headline_bullet.jpg
Wakamilisha ripoti, waipeleka kwa Spika
headline_bullet.jpg
Mwenyewe asema hatma anayo Spika



ChamiCyrl(13).jpg

Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami


Wabunge wamependekeza kusimamishwa kazi Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, ikiwa ni utekelezaji wa azma ya kuliepusha taifa na upotevu wa fedha unaotokana na tozo za ukaguzi wa magari kabla ya kuingizwa kutoka nje ya nchi.
Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili umebaini kuwa agizo la kusimamishwa kazi kwa Waziri huyo linatokana na ‘madudu’ yaliyobainika katika Shirika la Viwango nchini (TBS), wakati wajumbe wanne wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), walipofanya ziara katika nchi za Hong Kong na Singapore mwaka
jana.
Ziara hiyo iliyoanza Augusti 16, 2011 ililenga kuthibitisha ikiwa wakala walioshinda zabuni ya TBS iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, kuhusu ukaguzi wa magari wanakidhi vigezo vinavyostahili ikiwemo kuwa na ofisi, wafanyakazi na vifaa vya ukaguzi katika nchi hizo.
Kampuni sita zilizoshinda zabuni hizo ni Jabal Kilimanjaro Auto Electric Mechanical and Paints na Jaffer Mohamed Ali Garage zilizopangiwa Dubai na WTM Utility Services kwa Uingereza, zote zikipewa leseni zilizoanza Mei 14, 2007.
Kampuni nyingine ni Planet Automotive PTE Limited kwa Singapore (leseni ya Novemba, 6, 2007), East Africa Automative Services Company Limited kwa Japan (leseni ya Desemba 24, 2007) na Quality Motors kwa Hong Kong (leseni ya Desemba 15, 2008).
Leseni hizo zilikuwa na ukomo wa mwaka mmoja, muda ambao uliruhusiwa kuongezwa ikiwa utendaji kazi ungekidhi matakwa yaliyopo. Wakala hao walishinda zabuni hizo zilizotangazwa na TBS Novemba 22, 2007, ambapo pamoja na mambo mengine walitakiwa kufanya ukaguzi wa magari, kukusanya mapato yanayotokana na ukaguzi huo na kuilipa serikali kupitia shirika hilo.
Ziara ya wabunge hao huko Hong Kong na Singapore, ililenga kuzikagua shughuli za wakala ambao ni kampuni za Quality Motors na Planet Automotive PTE Limited.
Wabunge hao walipofika nchini humo, wakilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege na Mkurugenzi wa Udhibiti wa ubora wa shirika hilo aliyetajwa kwa jina moja la Katabwa, hawakukuta ofisi, wafanyakazi wala vifaa vya ukaguzi vinavyomilikiwa na mawakala wanaotambuliwa na shirika hilo kwa ukaguzi wa magari.
Wajumbe wa kamati hiyo waliokwenda Hong Kong na Singapore ni Makamu Mwenyekiti wake, Deo Filikunjombe, Mbunge wa Mwibara (CCM), Alphaxard Kangi, Christowaja Mtinda (Viti Maalum-Chadema) na Felister Bura (Viti Maalum-CCM).
Hata hivyo, kutokana na ukubwa wa athari zinazolikabili taifa kuhusu ulaghai uliofanywa na TBS, wabunge wameandaa ripoti itakayowasilishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda, ikipendekeza, pamoja na mambo mengine, kuziagiza mamlaka husika kumsimamisha kazi Waziri mwenye dhamana.
“Tumekamilisha ripoti yetu kwa Spika na moja ya mapendekezo ni kutaka Waziri mhusika asimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi na akibainika kuhusika kwa namna yoyote, hatua zaidi zichukuliwe,” kilisema chanzo chetu ndani ya kamati hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, ripoti ya kamati hiyo inapendekeza pia ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, kushirikiana na Mamlaka ya Mapato (TRA) kukagua hesabu za fedha zilizostahili kupatikana kwa ukaguzi wa magari yaliyoingia nchini tangu wakala hao walipoanza kazi.
“Tumesema kwenye ripoti yetu kuwa Mkurugenzi wa TBS na washirika wake watakaobainika kuhusika na upotevu wa fedha zilizostahili kuingia serikalini lakini haikuwa hivyo, wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kushitakiwa na kuzilipa fedha hizo,” chanzo chetu kilieleza.
NIPASHE Jumapili ilipozungumza na waziri Chami juu ya sakata hilo kwa njia ya simu jana, alisema Kamati ya Bunge imeshapeleka taarifa kwa Spika. Kuhusu pendekezo la kamati hiyo kwamba waziri mwenye dhamana naye ajiuzulu kuhusiana na sakata hilo alisema kuwa kazi ya kamati ya bunge ni kutoa ushauri na siyo kuiagiza serikali hivyo pendekezo lao litategemeana na jinsi Spika atakavyoliamua.
Aidha alisema Spika baada ya kupokea taarifa hiyo kwa utaratibu ataiandikia Serikali ambayo itaona hatua za kuchukua dhidi ya Mkurugenzi wa TBS.
Waziri Chami alisema lazima ieleweke kwamba Serikali haipo kwa ajili ya kumlinda mtu au kutaka kumwangamiza hivyo mara baada ya Spika kutoa maelekezo hatua za haraka zitachukuliwa dhidi ya Mkurugenzi wa TBS.
Aidha aliwaondoa hofu wananchi kwamba hakuna njama zozote zinazofanywa na Serikali kutaka kuzima suala hilo kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.
Taarifa zaidi juu ya sakata hilo zinasema miongoni mwa sifa zilizoanishwa wakati zabuni hizo zikitangazwa (ingawa zilibainika kukiukwa) ni muombaji kuwa na mitambo ya ukaguzi iliyosajiliwa kwenye nchi husika na kuwa na uwezo wa kuwagharamia watalaamu wawili wa TBS kuhakiki mitambo hiyo.
Sifa nyingine ni kuilipa TBS Dola 6,250 za Marekani zikiwa ni ada ya mwaka na Dola 20 kwa kila gari litakalokaguliwa kwa ajili ya mambo ya utawala.
Aidha, palikuwa na masharti kadhaa kwa leseni zilizotolewa, yakiwemo ukaguzi kufanyika kwa kiwango cha kitaifa cha TZ S698:2003, kutuma ada ya Dola 150 za ukaguzi kwa kiwango kitakachokubalika kila mwezi, kuomba kibali kutoka TBS ya ada ya tozo kwa kila gari na kutuma idadi ya magari yaliyokaguliwa kila mwezi.
SAFARI YA WABUNGE:
Agosti 16, mwaka jana wabunge hao waliondoka nchini kwenda Hongkong, wakapokewa na Mkurugenzi wa TBS, Ekelege akiwa na Katabwa.
Mmoja wa wabunge waliokuwa kwenye ziara hiyo, Alphaxard Kangi, aliiambia NIPASHE Jumapili kuwa baada ya kufika Hongkong, Ekelege aliwapeleka kwenye ofisi iliyodaiwa kuwa kampuni ya Quality Motors ambapo walipelekwa kwenye ‘ofisi hewa’.
“Tulipoingia kwenye hizo ofisi hatukukuta chapisho lolote kama cheti cha usajili, vipeperushi vinavyoonyesha nembo za wakala, wala picha ya kiongozi kama Rais ama Baba wa Taifa inayoonesha kuwa waliopo pale ni Watanzania,” Kangi alisema.
Mbunge huyo ambaye huu ni msimu wake wa kwanza kuiwakilisha Mwibara, alisema pamoja na udhaifu huo, mtu aliyendaliwa kutoa maelezo ya wakala na shughuli zake, hakuwa na uelewa, ndipo ikabainika kwamba hakuwa mmoja wa watendaji wa Quality Motors.
“Tulimbana Mkurugenzi Mkuu wa TBS hadi akakiri kwamba mtu yule alikuwa ahusiki na kwamba Mkurugenzi wa Quality Motors alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Appolo nchini India,” alisema.
Wabunge hao waliwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutaka kujua ukweli kuhusu kuwepo mgonjwa huyo nchini India, na baada ya mawasiliano na ubalozi wa Tanzania nchini humo, ilibainika kuwa hapakuwa na mtu aliyelazwa hospitalini hapo kwa jina la Mkurugenzi wa Quality Motors.
Hata hivyo, wabunge walitaka kuonyeshwa mitambo inayotumika kukagua magari yanayingizwa nchini, huku wakiomba gari walilokuwa wakilitumia litumike kwa upimwaji, lakini mashine iliyokuwepo ilibainika kuwa ya kupiga injini za magari tu, huku ikiwa haifanyi kazi.
Pia wabunge hao waliomba kuona nakala ya vyeti vinavyotolewa kwa magari yenye viwango yanayoingizwa nchini, lakini hawakufanikiwa.
“Tulijisikia vibaya sana kwa usumbufu na ubaridhifu ulioonekana kwa maana kiasi cha asilimia 75 ya mapato yaliyostahili kuingia serikalini, hakikuonekana, lakini hata mazingira yenyewe yakadhihirisha kutokuwepo kampuni rasmi za uwakala,” alisema Kangi.
Kwa mujibu wa Kangi, hata mchakato uliotumika kutoa zabuni kwa wakala hao, uligundulika kutawaliwa na ‘usanii’ kiasi cha kukiuka sheria ikiwemo ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004.
Tutaendelea na taarifa zaidi za sakata hilo Jumapili ijayo



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


 
Back
Top Bottom