Je,walimu wa sekondari kusimamia mitihani ya kuhitimu....(itv kipimajoto)

jobe ayoub

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
203
99
Je,walimu wa sekondari kusimamia mitihani ya kuhitimu
darasa la saba ni suluhisho ya kuondoa wasiojua
kusoma na kuandika kwa kidato cha kwanza...?

ITV kipima joto......
 
labda itasaidia kupunguza udanganyifu sababu waliokuwa wanafanya hiyo kazi iliwashinda kabisa. lakini tusubiri tuone. kama ni hivo na wa vyuo wasimamie ya sekondari
 
Wamechemka maana hiyo sio suruhu. Hili tatizo ni mwendelezo wa tabia za rushwa ambazo zimekithiri kwenya taasisi na mamlaka mbalimbali za serikali kama njia ya kujiongezea kipato kwa watu wenye dhamana ya uongozi. Walimu walikuwa bado wanaheshimu miiko yao ya kazi, hawakutaka kabisa rushwa. Baada ya kuona watu wa kada zingine wanapokea rushwa na serikali inanyamaza na wakati mwingine inabariki rushwa kwa kuipa majina mapya kama Change, Takrima, Malupulupu, Kifuta jasho, n.k nao wameamua kufunga kibwebwe na kuicheza ngoma kama wengine. Mi naona hapo wanawaongezea ulaji tu waalimu wa sekondari na kuwabania wale wa Msingi
 
Minadhani hilo sio suluhisho nanikutaka kuwagawa walimu kwakuwa wameanza kuonesha mshikamano katika kudai maslahi yao. walimu makini wanatakiwa kulipinga vikali wazo hili, na kwa taarifa kuna walimu waliotoka shule za msingi nakuanza kufundisha sekondari walishazoea kula hizo pesa zakuibia mitihani sasa hivi wameshaanza mipango ili wapate nafasi katika usimamizi huo na kula hizo pesa zinazochangwa na wazazi. suluhisho la hapo nikuwajengea walimu uwezo wakufundisha vyema wanafunzi nakuwaondolea mawazo ya kufaulu kwa kuibia.
 
Back
Top Bottom