Je, wajua: Nyerere aliiogopa ccm?

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,027
1,299
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa
CCM, kwa nia njema ya
kuendeleza mapinduzi katika
nchi yetu, miaka ilivyozidi
kwenda Mwalimu Nyerere
alishuhudia jinsi CCM
ilivyobadilika na kuwa mzigo
kwake na pia tishio kwa usalama
wa Taifa.
Mwaka 1993 Mwalimu
alichapisha kitabu kiitwacho
Uongozi Wetu na Hatima ya
Tanzania (Harare: Zimbabwe
Publishing House, 1993). Pamoja
na mambo mengine katika
kitabu hiki, Mwalimu alisema
kuwa kuna kansa katika uongozi
wa CCM. Nanukuu baadhi ya
maneno yake:
Chama cha Mapinduzi, kwa
sababu ya uzito wa historia
yake, hadhi ya jina lake, mfumo
wa wavu wake, mazoea ya
watu, na ubovu wa Vyama vya
Upinzani, kinaweza
kuchaguliwa na Watanzania,
pamoja na kansa ya uongozi
wake. Au watu wanaweza
wakachoka, wakasema,
"potelea mbali:" wakachagua
Chama cho chote, ilimradi tu
watokane na kansa ya uongozi
wa CCM. Hainifurahishi
kuyasema haya, lakini uhai wa
Nchi yetu unataka yasemwe.
(Ukurasa 61)
Mwalimu hakuishia hapo, bali
aliongezea namna hii:
Nilisema awali kwamba kansa
ya uongozi ndani ya Chama cha
Mapinduzi isingekuwa ni jambo
la kutisha sana kama
tungekuwa tumeanza kuona
Chama kizuri cha upinzani
kinachoweza kuiongoza Nchi
yetu badala ya CCM. Ubovu wa
uongozi ndani ya CCM ndio
uliofanya nikapendekeza
tuanzishe mfumo wa Vyama
Vingi. Nilitumaini kuwa
tunaweza kupata Chama
kingine kizuri ambacho
kingeweza kuiongoza Nchi yetu
badala ya CCM; au ambacho
kingekilazimisha Chama cha
Mapinduzi kusafisha uongozi
wake, kwa kuhofia kuwa bila
kufanya hivyo kitashindwa
katika uchaguzi ujao. Lakini
bado sijakiona Chama makini
cha upinzani; na wala dalili zo
zote za kuondoa kansa ya
uongozi ndani ya CCM. Bila
upinzani mzuri wa nje, na bila
demokrasia halisi ndani ya
Chama cha Mapinduzi, Chama
hiki kitazidi kudidimia chini ya
uzito wa uongozi mbovu. Kwa
hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini
hili si jambo la kutarajia bila
hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)
Ni wa-Tanzania wangapi wenye
utamaduni wa kusoma vitabu? Ni
wangapi wanaosoma vitabu vya
Mwalimu Nyerere? Ni wazi kuwa
umbumbumbu miongoni mwa
wa-Tanzania ni neema kwa CCM.
 
"...kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi"

Baadaye Nyerere alikiri kwamba angalau Chadema ndio walionekana kuwa na sera zenye mshiko, na maneno ya Nyerere leo hii yanatimia kwani wananchi wengi wameona hivyo.

Hivi kwa nini kitabu hiki alikichapishia Harare, Zimbawe badala ya hapa Tanzania...aliogopa kuchakachuliwa nini! Maana Tanzania bwana kwa uchakachuaji, ni kila kitu!
 
Nakubaliana na maneo ya Nyere kuwa umbubumbu wa watanzania ndio mtaji wa ccm ktk kushika dola. Ndio maana serikali ya ccm inaendelea kujenga shule za kata kibao zisizo na walimu, vifaa vya kufundishia wala uwezo wa kumkomboa mtanzania ili waendelee kukuza mtaji wao kwa kuongeza idadi kubwa ya mbumbumbu. Ukachana na sekondari za kata, pia wamejenga vyuo vya kata kibao, bila ya shaka kila mmoja atakubaliana nami ktk suala la vyuo vya kata kwa maana haiwezekani kwa msomi anayemaliza chuo kikuu halafu aunge mkono chama na sera za ccm ambazo zinatuongezea umaskini na ujinga kila kukicha.

Nyerere ni kiongozi na mwanaccm pekee aliyekuwa na akili na hatatokea mwingine kama yeye, wamebakia zero-brain tupu ktk safu ya uongozi, hakuna hata mmoja anayeweza kuona uozo wao wanaofanya.
 
"...kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi"

Baadaye Nyerere alikiri kwamba angalau Chadema ndio walionekana kuwa na sera zenye mshiko, na maneno ya Nyerere leo hii yanatimia kwani wananchi wengi wameona hivyo.

Hivi kwa nini kitabu hiki alikichapishia Harare, Zimbawe badala ya hapa Tanzania...aliogopa kuchakachuliwa nini! Maana Tanzania bwana kwa uchakachuaji, ni kila kitu!

Namwamini Nyerere, aliwahi kusema kusema kama umependa sura za wagombea kanywe nao chai.... leo tunashuhudia vituko. Pia aliwahi kuwakataa wagombea kadhaa akiwemo huyu anayeutaka urais 2015 Mr, Lowassa, lakini kwa vile Wa Tanzania tu mabwe-ge basi tutamchagua.

Chadema ilitabiriwa mema na Mwalimu JK Nyerere
 
"...kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi"

Baadaye Nyerere alikiri kwamba angalau Chadema ndio walionekana kuwa na sera zenye mshiko, na maneno ya Nyerere leo hii yanatimia kwani wananchi wengi wameona hivyo.

Hivi kwa nini kitabu hiki alikichapishia Harare, Zimbawe badala ya hapa Tanzania...aliogopa kuchakachuliwa nini! Maana Tanzania bwana kwa uchakachuaji, ni kila kitu!

surely yanatimia
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom