Je viongozi wetu wanapata commission kwa kuhakikisha muundo wa muungano haubadiriki?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Mimi naanza kuwafikiria viongozi wetu vibaya, inawezekana wananufaika kwa kupata fedha za comission kwani kama wananchi wa pande zote mbili za muungano wanaona muundu huu wa muungano hautufai lakini viongozi wamekataa kata kata, zaidi ya yote wanataka kupitisha sheria itakachokifanya kitendo cha kuujadili muungano kuwa kosa la jina sawa sawa na wizi, mauaji, uhaini, n.k.

Haiingii akilini kwa mtu ambaye hana manufaa na kitu fulani kulazimisha kitu hicho kuendelea kuwepo hata kama kitu hicho kinamgharimu kuwa nacho... Ukimuuliza mtu yeyote mwenye uelewa wa Muungano wetu atakwambia kuwa Tanzania Bara inagharamia shughuli zote za kuendesha mambo ya muungano na kwa maana hiyo hakuna manufaa yoyote kwa wananchi wa Tanzania Bara isipokuwa misifa (kuwa nchi iliyodumisha muungano) BASI!

My theory of things:
Kama kuna pesa inatumwa na serikali ya mapinduzi kwa ajiri ya kuendeshea serikali basi pesa hiyo huishia kwenye mifuko ya wajanja (wanaotaka muungano huu uendelee kuwepo au kuna pesa huwa zinachotwa kutoka benki kuu ya Tanzani kupelekwa Zanzibar ambazo huishia kwenye mifuko ya wajanja) .... Hawa kwa namna yoyote ile watasisitiza kuwa muungano huu uendelee kuwepo kwani unawanufaisha! .... Vinginevyo watuache tujadili na tukubaliane muundo wa muungano tunaoutaka!
 
Back
Top Bottom