Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Tume ya uchaguzi nchini Sudan imemtangaza Rais Omar Albashir kuwa mshindi katika uchaguzi uliogomea na baadhi ya vyama vya upinzani nchini humo. Albashir ambaye amekuwa akituhumiwa kwa makosa ya kukiuka haki za binadamu na hasa katika eneo la Darfur nchini Sudan amewabeza wale wote waliosusia uchaguz huo na kuwaita ni vibaraka wa nchi za magharibi. Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa kwa Omar Albashir. Je kutangazwa kuwa mshindi kunafuta uhalali wa hati ya kukamatwa kwake??