Je Ungependelea Muundo Gani wa Muungano au Hautaki, Piga Hapa

Huu ni upepo utapita tu, na lazima upite, kasi yake ikiwa kali, utaondoka na katiba mpya
 
Nataka serikali moja tu. Watu wote ndani ya muungano tuwe treated equally kama raia wa nchi moja. Raia wawe na uhuru wa kwenda popote na kufanya lolote ndani ya muungano chini ya sheria. Sitaki muungano huu ambamo wazenji wanapendelewa sana kiasi cha kuruhusiwa kwenda popote na kufanya lolote ndani ya Tanganyika lakini Mtanganyika anabanwa sana anapokwenda Zenj au akiamua kufanyia shughuli zake Zenj.
 
Serikali moja, nchi moja, taifa moja< vinginevyo muungano uvunjike zanzibar wachukue chao bara wabaki na chao!
 
kwanza nakupongezeni kwa kuwa na hii forum 2napoweza kuchangia mawazo ye2 though cjajua kama kwa namna yoyote ile yanafikia wahusika au yanaishia hapahapa. ila kwa mtazamo wangu muungano una mapungufu mengi sana na sidhani kama ni jambo la busara kuendelea na mchakato wa katiba ya jamuhuri wakati hili halijakaa sawa tutakuja kuumia baadaye. mimi nadhani muungano ungekuwa wa serikari tatu lakini serikari hizi mbili (serikari ya Tanganyika na serikari ya Zanzibar) zisiwe na maraisi bali kuwe na makamu wa pili wa rais kila upande huku serikari ya muungano ikiwa na rais na makamu wa kwanza wa rais watakao shughulika na masuala ya taifa zima.

Kazi yetu ni kutuma maoni kwa tume, na haya yameshafika, wakikataa shauri yao. Historia huwa inahukumu.
 
Ningependa kuwe na mfumo wa states,na ili hili lifanikiwe Zanzibar kwanza wakubali kuondoa katika katiba yao kuwa Zanzibar ni nchi,pia kuwe na states of Tanganyika na States of Zanzibar, muungano ujulikane kama United states of Tanganyika and Zanzibar hii italeta mantiki kidogo kuwa kuna nchi mbili ziliungana,viongozi wa hizi states wajulikame kama magavana siyo Rais ila kuwe na Rais Mmoja wa USTZ na katiba iwe moja itakayoelezea jinsi kila states itakavyojiendesha.
 
ninapendelea muungano hubaki kama ulivyo ila kasoro ndogo ndogo zilizopo zirekebishwe kwa wananchi wa pande zote husika kushirikishwa ipasavyo. Kwani wananchi si kama hawaupendi ila ni hizo kasoro tu!
 
Ningependa kuwe na mfumo wa states,na ili hili lifanikiwe Zanzibar kwanza wakubali kuondoa katika katiba yao kuwa Zanzibar ni nchi,pia kuwe na states of Tanganyika na States of Zanzibar, muungano ujulikane kama United states of Tanganyika and Zanzibar hii italeta mantiki kidogo kuwa kuna nchi mbili ziliungana,viongozi wa hizi states wajulikame kama magavana siyo Rais ila kuwe na Rais Mmoja wa USTZ na katiba iwe moja itakayoelezea jinsi kila states itakavyojiendesha.
Naona mawazo yetu yanafanana.
 
Back
Top Bottom