je unaweza kuwawakilisha watu wasiokuchagua uwawakilishe katika kikao cha wawakilishi

fige

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
376
61
Kitendo kilichofanywa na ccm Arusha kimeleta picha mpya kuhusu chama hiki.Tunaambiwa kuwa Mary Chitanda ana haki ya kuingia katika wawakilishi wa watu wa Arusha wakati yeye alichaguliwa mbunge Tanga.

Nimejiuliza maswali mengi ambayo nakosa majibu labda wenzangu humu jamvini mnayaelewa.

Maswali yenyewe ni haya hapa
1. Je ni nani anayetakiwa kuingia kwenye vikao vya
halmashauri ?

2. Je Chitanda atatumikia wapi ubunge wake katika miaka mitano hii ?
3. Kama Chitanda alipenda na ana hakika watu wa Arusha wanampenda awawakilishe kwa nini hakugombea kupitia Arusha ?

Yapo maswali mengi lakini yaliyo akilini mwangu ni hayo kwa sasa .

Nijuavyo;
Kuna wawakilishi wa aina mbili wanaoingia kwenye vikao kama hivi, moja ni madiwani na wabunge ambao huwakilisha wananchi waliowachagua, pili ni viongozi wa serikali kwa madaraka na vyeo vyao k.v mkurugenzi.
Nimesikia Mary si kiongozi wa serikali na wala si mbunge aliyechaguliwa huko Arusha ndipo ninaposhangaa na kujiuliza maswali hayo.

Swali la nyongeza,je Tanga wakiandamana kumtaka mbunge wao ,je watapigwa mabomu ?

Naomba kwasilisha
 
lengo lao nikutaka kuficha maovu yao na kwa utaratibu wa namna hiyo wanajiweka katika nafasi mbaya sana kwa miaka mitano ijayo watakuwa na hali mbaya sana hawa ccm kwa sababu wamepora haki ya wana arusha tena wazi wazi kwa kweli naumia sana na siasa za ccm za kizamani kwa sababu awajui kuangalia alama za nyakati
 
Back
Top Bottom