Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane

Status
Not open for further replies.
kilimomaarifa.tajiri thanks sana kwa uzi huu. Hakika unastahili pongezi sana kwa elimu hii unayotoa hapa jukwaani bure...
 
Habarini wanajamvi naomba mwenye uzoefu kuhusu kilimo cha mboga mboga hasa chinese au spinach atupe elimu ya utunzaji, madawa ,ikiwezekana kuhusu soko hata maeneo pia ningependa kujikita katika kilimo hicho
Nipo mkoa wa Dodoma. Nawasilisha
 
Ungepita pitia jukwaa LA Kilimo kule Kuna Kuna wadau na pia wataalamu wengi.
 
mkuu pole na majukumu, naomba kuuliza, matikiti yangu yanashambuliwa sana na konokono, wanakula majani na wakati mwingine hufikia kukata mmea, sumu ya wadudu ninayotumia ni IMIDA, pia matikiti yangu yana shida moja, baadhi ya matunda hunyauka hasa yakiwa na ukubwa wa au chini ya ngumi, afya ya mmea huonekana safi tu na ndani ya kile kitunda hakuna mdudu anayeonekana, naomba msaada wako...
 
Tatemahunda
POLESANA MKUU

-NAOMBA KUFAHAMU MAENEO SHAMBA LILIPO KUNA UNYEVU MWINGI/MVUA?

KWA KONOKONO, MARA NYINGI TUMEKUWA TUKISHAURI MCHANGANYIKO WA SUMU YA CYPERMETHRIN NA IMIDACLOPLID/CHLOROPHRIVOS ZITUMIKE, (UNACHANGA PAMOJA) KISHA UNASPRAY JUU YAO) HUWA WANAKUFA

KWENYE MATUNDA KUNYAUKA, ANGALIA UWEPO WA WADUDU NYUMA YA MAJANI,AU KATIKA KIKONYO CHA MMEA WA TIKITI NA TUNDA LA TIKITI, AU CHUNGUZA CHINI KULIWA KWA MIZIZI, HUENDA KUNA SHIDA. KWA MAANA KAMA MZIZI/MAJANI YANASHAMBULIWA MAANA YAKE MMEA UNASHINDWA KUTENGENEZA CHAKULA, HIVYO TIKITI HUKOSA CHAKULA, NA MIZIZI KAMA IMELIWA BASI INASHINDWA KUFYONZA VIRUTUBISHO CHINI NA KUVILETA JUU NA KUVISAMBAZA KWA MMEA, PIA KAMA KIKONYO (KISHIKIO) KIMESHAMBULIWA MAANA YAKE KUNAKOSA MUUNGANIKO KATI YA TUNDA NA MMEA, HIVYO TUNDA KUNYAUKA KWA KUKOSA MAJI/LISHE/VIRUTUBISHO.

mkuu pole na majukumu, naomba kuuliza, matikiti yangu yanashambuliwa sana na konokono, wanakula majani na wakati mwingine hufikia kukata mmea, sumu ya wadudu ninayotumia ni IMIDA, pia matikiti yangu yana shida moja, baadhi ya matunda hunyauka hasa yakiwa na ukubwa wa au chini ya ngumi, afya ya mmea huonekana safi tu na ndani ya kile kitunda hakuna mdudu anayeonekana, naomba msaada wako...
 
Mkuu naomba kujua mimea kama hoho, pilipili mbuzi na ngogwe inahitaji maji kiasi gani kwa wiki,? Kwa kila mmea .aksante
 
Mkuu kilimomaarifa.tajiri habari za siku? Naomba kujua je ninaweza kuchanganya mbolea ya samadi ya kuku pamoja na urea? Lengo ni kufanya mmea upate virutubisho vya urea kwa haraka wakati ikisubiria virutubisho vya samadi vianze kufanya kazi.
 
mkuu
naomba nikuongezee kitu hapa najua wengi wamekariri mbolea zile zile ,hebu piga hii number katika laini yoyote ile,halafu leta mrejesho
*149*50*31#
 
mkuu pole na majukumu, naomba kuuliza, matikiti yangu yanashambuliwa sana na konokono, wanakula majani na wakati mwingine hufikia kukata mmea, sumu ya wadudu ninayotumia ni IMIDA, pia matikiti yangu yana shida moja, baadhi ya matunda hunyauka hasa yakiwa na ukubwa wa au chini ya ngumi, afya ya mmea huonekana safi tu na ndani ya kile kitunda hakuna mdudu anayeonekana, naomba msaada wako...
mkuu
kuhusu wadudu na magonjwa ya aridhini,tafuta dawa ya inayokinga na kutibu,mfano huwa mimi naipenda confidor
 
Habarini wanajamvi naomba mwenye uzoefu kuhusu kilimo cha mboga mboga hasa chinese au spinach atupe elimu ya utunzaji, madawa ,ikiwezekana kuhusu soko hata maeneo pia ningependa kujikita katika kilimo hicho
Nipo mkoa wa Dodoma. Nawasilisha
unataka kujua nini hasa katika hilo mkuu?
 
DE FULE
ASANTE SANA NDUGU
Habari mkuu!!

Leo nimekutana na mmea mmoja umeanguka shambani.... Cheki hii picha mkuu...

a044d53a60d57009dea029c8f62d6ce4.jpg
e7826817228007efe7774934cddd4d88.jpg

Naona kama shina limeoza au kukauka! Sijui tatizo ni nini!!

Naomba uangalie na hayo majani labda kama utakua na ushari zaidi mkuu wangu!!
 
Kwa macho yangu hiyo ni kata k au kata kiuno,wazungu huita dumping off,tumia milraz ,,ukiiikosa nambie nikuunganishe na wadau

jw library
 
NimeSubscribe kabisa huu uzi, nimesoma hadi page ya 25, ntaendelea kusoma na kujifunza. Nimeelewa common mistakes ambazo huwa nazifanya sometimes. Shukrani mleta uzi.

Post sent using JamiiForums mobile app
Mimi niliusoma mwanzo mwisho!! Nikiwa na kalamu na daftari pembeni!! Hii ni elimu kubwa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom