Habari kiongozi. Majani ya nyanya kujikunja kama kujifunga vile inasababishwa na nini? Unakuta ni karibu shamba lote. Pia naweza tumia mbolea ya SA kwa kupandia na wakati wa maua na matunda?
Asante kiongozi.Chief
Salaamu
Pole kwa hizo changamoto
1.KUJIKUNJA MAJANI KWA KUJA JUU
Hiyo inaitwa Leaf Curing, sababu ni virus wanaoenezwa na wadudu hasa white flies (vipepeo weupe)
Tumia dawa za wadudu, kama abamectin, au Dimethoate (Kama mmea hauna maua), au duduall, au Nimbecidine, kuangamiza hao wadudu, kisha piga booster (Multi K, Omex, au Murphy au Potphos etc) ili kuichangamsha
2. Mbolea ya SA
=SA siyo ya kupandia, hiyo ni Sulphate of Ammonia, hiyo ni ya kukuzia, naomba kujua upo mkoa gani, kwa sababu hiyo SA kuna mikoa hasa ya kuanzia Iringa kuja mpaka katavi (Mikoa 5 ya nyanda za juu kusini) haifai kutumika kukukuzia, kwa kuwa yenyewe huongeza acid katika udongo, wakati tayari udongo wa mikoa hiyo ni too Acidic (PH 4-6). WAKATI WA MAUA NA MATUNDA KUZIA NA CAN/NPK/YARA NITRABOR/MOP/ UREA-kama unamaji ya kutosha, na juu katika maua piga booster (Multi K, Omex, au Murphy au Potphos, Wuxal Macromix, Yara Vita tracel Biz etc). SA inafaa sehemu zenye magadi kama Arusha au Moshi huko (Chekeleni, Rundugai etc)
===================
Asante kiongozi.
Daaah.. Kwa uzoefu wa wakulima wenzangu tulijua hiyo ni Ukungu.
Nimechukua namba yako nitakutafuta kwa mazungumzo zaidi. Pia tulikuwa tunahitaji documenti ya nyanya na viungo(karoti, hoho)
Naomba utaalamu wa ulimaji wa giligilani maandalizi, matunzo nk.
ASANTE MKUU KWA TAARIFA HII.BAADHI YA AINA ZA MAGONJWA YA MAZAO MBALI MBALI
1. Ubwiri Unga/Powdery Mildew
View attachment 421114 View attachment 421115
Chanzo kikubwa ni fangasi
Ugonjwa huenea zaidi wakati wa unyevu mwingi, majani/matunda huwa na vidoa doa vyeupe
TIBA. Tumia dawa zenye Metalaxyl au Azoxtrobin au Myoxin au Hexaconazole kutibu ugonjwa huu
Baadhi ya dawa hizo ni Ebony 72 WP, Amista Xtra, au Power 78WP, au Xantho
===========
2.Bacteria Angular Leaf spot (Madoa ya bakteria kwa majani)
View attachment 421117
Husababishwa na Bacteria (Pseudomonas Spp)
Bacteria Husababisha madoa doa ya rangi ya brown kwa majani,majani huchakaa, na kisha majani hufa na kisha mmea wote hufa pia
Hutokea zaidi wakati wa unyevu mwingi na katika udongo kichanga
Tiba tumia dawa za ukungu zenye Copper kuzuia mashambulizi zaidi
Dawa kama vile, Bluu Copper/Tan copper/Nordox/ Funguran etc
=================
3.Bacteria Fruit Blotch
View attachment 421118
View attachment 421120
Husababishwa na Bacteria
=Ugonjwa huenea zaidi wakati wa unyevu mwingi
Matunda hutobolewa, huwa na madoa doa na kuoza kwa ndani
Mashambulizi yakizidi hata matunda hupata nyufa (Fruit Cracking)
View attachment 421123
Tumia dawa zenye Calbendazim na copper mapema baada ya kupanda miche, kumbuka kutibu mbegu na udongo kabla ya kupanda mazao
=====================
4.Bacteria Wilt
View attachment 421125
View attachment 421126View attachment 421127
Ugonjwa husababishwa na Bacteria
Huenezwa na Kobe wa Matunda (Erwinia Tracheiphila) wa mazao ya Tikiti/Tango/Maboga
Mmea huaanza kwa kushambuliwa majani machache, mmea husimama kukua, kisha majani yote huanza kunyauka, mmea hufa
Tumia dawa za kutibu mbegu (Seed plus, seed plus, Seed care etc), na udongo (Fungicides +Insecticides) mapema kabla ya kusia/kupanda mbegu/Miche
=================
Itaendelea.............
ASANTE MKUU KWA TAARIFA HII.
KUNA JANI LA TIKITI NIMEKUTANA NALO LINA SHIDA MBILI;
1. KWENYE NCHA YA KILA JANI KUNA RANGI YA NJANO ALAFU YANI UJANI WAKE NI KAMA UNA WEUPE KWA MBALI
2. CHINI YA JANI KUNA WADUDU WADOGO WADOGO SANA NAFIKIRI WANAFYONZA MAJANI
Huyo mdudu wa tuta absoluta si anatokea wakati wa matunda? Je kuna ulazima wa kutumia dawa ya Belt toka kitaluni au kabla ya matunda kutoka?USHAURI KWA WAKULIMA WA NYANYA
Wakulima wengi waliozalisha nyanya na kuingiza sokoni kuanzia mwezi wa 6 hadi wa 10, bei imedondoka sana, lakini walio wengi wamevamiwa sana na Tuta absoluta (Kanitangaze), hivyo hata mavuno yamekuwa hafifu.
Nawapa pole kwa hizo changamoto
LAKINI, kama unamtaji usikate tamaa, rudi tena shamba kwani, wakulima wengi sana hawatalima nyanya kwa msimu huu wa November-May, hasa kwa sababu ya ukata na maumivu waliyoyapata, hivyo kusababisha uhaba mkubwa sana wa nyanya huenda kwa mwaka mzima.
UZOEFU UNAONYESHA KUWA mara nyingi wakulima wengi wanapopata hasara msimu fulani, basi msimu mwingine/ujao walio wengi huacha kulima kulima hilo zao, na hivyo wale wachache wanaothubutu kulima hupata bei nzuri (Demand/Supply theory).Lakini pia kwa kawaida nyanya hupata bei nzuri sana kuanzia November (Kidogo),,, zaidi huchanganya January hadi May.
TIBA ZA MDUDU KANITANGAZE ZIPO
Hizi ni baadhi tu ya dawa za kutumia huangamiza, mdudu, mayai na kiwavi, zitumie mapema tangu kitaluni.
1. Nimbecidine
2.Belt
3.Colagen
4.Evisect
5.Proove
Baadhi ya mbegu za kutumia kwa wakati huu wa masika ni
1. Eden F1
2. Shanty F1
3.Milele F1
4.Kipato F1 etc
=========================
Huyo mdudu wa tuta absoluta si anatokea wakati wa matunda? Je kuna ulazima wa kutumia dawa ya Belt toka kitaluni au kabla ya matunda kutoka?
ASANTE.Gody87
Tuta absoluta (Kanitangaze) Hashambulii matunda tu
Tuta absoluta anashambulia miche tangu kitaluni, hushambulia majani ya miche machaga juu ya majani huoeneka kama alama ya kaki iliyokuwa covered na nailoni, ni vyema kumdhibiti tangu kitaluni, unapoona matunda yameanza kugongwa na kuliwa ujue alishaingia siku nyingi tangu kitaluni. Tumia dawa nilizozielewa tangu kitaluni.
Tazama hapa chini mzunguko wa maisha yake, angalia picha no 3 ambayo kiwavi hushambulia majani
View attachment 427065
Tizama hapa chini, namna Tuta absoluta anavyoshambulia sehemu mbali mbali za mmea ikiwemo majani
View attachment 427067
ASANTE.
Natumia metakan kwajili ya wadudu na ridomil gold kwa ukungu kila siku saba. Pia nilitumia Actara mara moja kitaluni. Na match mara moja baada ya miche kupata ugonjwa wa leaf miner kitaluni. MICHE INA WIKI MOJA SHAMBANI BAADA YA KUKAA KITALUNI KWA SIKU 28.
MASWALI
1. JE METAKAN AU ACTARA INAWEZA ZUIA WADUDU WANAOLETA TUTA ABSOLUTA KWENYE MICHE?
2. JE KAMA NI LAZIMA KUTUMIA BELT AU HIZO DAWA NYINGINE UPIGAJI DAWA UTAKUWAJE KULINGANA NA RATIBA AMBAYO NIMEITAJA?
3. JE TUTA ABSOLUTA AKISHAINGIA IWE KWENYE HATUA YA KITALU, MAJANI AU MATUNDA INATIBIKA? KWA MAANA NYINGINE DAWA KAMA BELT NA NYINGINE ZINAZUIA UGONJWA AU KUTIBU UGONJWA PIA KAMA USHATOKEA?
ASANTE
MASWALI
1. JE METAKAN AU ACTARA INAWEZA ZUIA WADUDU WANAOLETA TUTA ABSOLUTA KWENYE MICHE?
=Fahamu kuwa Tuta abasoluta (Kanitangaze/Dengue etc) ni mdudu na siyo ugonjwa
=Hizo dawa ulizozitaja ni vyema ukizitumia kama kinga lakini siyo kama tiba, tumia kitaluni na unapohamisha miche shambani, lakini matunda yakianza tumia moja wapo ya dawa nilizozitaja kwenye uzi wangu wa kwanza (Nimbecidine, Evisect, Proove, belt , coragen et al)
2. JE KAMA NI LAZIMA KUTUMIA BELT AU HIZO DAWA NYINGINE UPIGAJI DAWA UTAKUWAJE KULINGANA NA RATIBA AMBAYO NIMEITAJA?
=Kama hakuna mashambulizi unashauriwa kupiga dawa za ukungu/wadudu/booster / (Zoote kwa pamoja kila baada ya siku 14), Labda kuwe na mashambulizi sana ndipo unaweza piga kila baada ya siku 5-7.
3. JE TUTA ABSOLUTA AKISHAINGIA IWE KWENYE HATUA YA KITALU, MAJANI AU MATUNDA INATIBIKA? KWA MAANA NYINGINE DAWA KAMA BELT NA NYINGINE ZINAZUIA UGONJWA AU KUTIBU UGONJWA PIA KAMA USHATOKEA?
=Tuta absoluta ni mdudu siyo ugonjwa
=Dawa nilizokutajia kama Nimbecidine, Proove, au Evisect au Belt humaliza mayai, buu, kiwavi mpaka mdudu mwenyewe
==========================================
ASANTE.
KWAHIYO MATUNDA YANAPOANZA UKITUMIA MOJA WAPO YA HIZO DAWA ULIZOTAJA KILA BAADA YA SIKU 7, DAWA NILIZOTAJA NAACHA KUTUMIA AU NATUMIA SAMBAMBA NA HIZO ZA KUTOKOMEZA TUTA ABSOLUTA?
PIA KAMA NILIVYOSEMA ACTARA NILITUMIA MARA MOJA, JE KUNA UMUHIMU WA KUENDELEA KUITUMIA KWA KUCHANGANYA PAMOJA NA METAKAN NA RIDOMIL GOLD?
ASANTE.