kilimomaarifa.tajiri
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 574
- 409
- Thread starter
- #321
NZI WA MATUNDA, Hushambulia matikiti, machungwa, apple, peas, parachichi na nyanya
ThanksBAADHI YA MAMBO MUHIMU KUHUSU PILIPILI KALI (HOT PEPPER)
View attachment 410462
MAELEZO JUMLA YAPO KATIKA PDF HUSIKA
Thanks
Imekaa poa sana kilichobaki nikufanyia kazi...vp kuhusu pilipili mbuzi mkuu?
Habari mkuu.. naomba ushauri wa mambo mawili..
1. Nimepanda mbegu za tikiti na baada ya siku nne zimeota kama 70% hivi. Hizi ambazo hazijatoka niendelee kungoja au nirudishie mbegu zingine..
2. Naomba nishauri nini hii kwenye hizi papai ni ungojwa au? Mwanzo zilikua na wadudu weupe hivi nikatumia Confidor wakaisha wote lakini sielewi huu ni mnyauko wa nini..View attachment 418291View attachment 418293
KARIBU
1. KUHUSU MBEGU ZA TIKITI KUOTA
=Kwa kawaida tikiti zinapaswa kuota ndani ya siku 7. Subiri kwa ziada ya siku 5 kutoka leo, ikifika maximum siku ya 10 tangu ulipozisia na zikawa hazijaota, basi pita katika yale mashimo ambapo hazijaota, kisha fukua kuangalia kama zipo hizo mbegu na zina hali gani, mara nyingi huwa tayari zimebunguliwa na wadudu au ukungu. Hivyo itakupasa kurudia kupanda tena
SWALI; Je ulizitibu hizi mbegu zako kabla ya kuzipanda?? Kuna dawa ambazo ni muhimu kumix na mbegu kabla ya kupanda, ili kuzuia changamoto za nematodes, au wadudu au fanagasi kuzishambulia kabla ya kuota NIMETUMIA MBEGU AMBAZO ZIKO TREATED ALREADY (SUGAR KING) KWAHIO SIKUONA HAJA YA KUZITIBU MBEGU TENA SABABU NIMESOMA MOJA YA MAANDIKI YAKO UMESHAURI HILI
2.KUHUSU MICHE YA PAPAI
Tutakuuliza maswali kadhaa hapo chini, LAKINI
=Kuna baadhi ya matatizo yako wazi
i. Picha ya kwanza ya juu kuna miche majani ya chini (OLder leaves) ni ya Njano, hiyo ni dalili ya wazi kabisa ya upungufu wa Nitrogen (N), na utaona inaanza kuwa ya njano nchani (Tip) mwa jani kushuka chini, angalia miche miwili ya mstari wa mwisho kwenye hiyo picha ya kwanza angalia huo unjano umekolea sana hapo nchani mwa jani kuja chini huku katika kikonyo/mwanzo mwa tawi/jani
ii. Pia kuna miche inaonekana baadhi ya majani yamekauka kabisa, mfano mstari wa pili kutoka kaskazini kuja kusini, angalia mche wa kwanza, wa pili na wa tatu kutoka kulia kuja kushoto, utaona majani yamekauka kwa kuanzia katika ncha kuja chini. Hiyo ni dalili ya wazi kabisa ya upungufu wa Potassium (K). Na utaona hata ukuaji wa hiyo miche si mzuri imedumaa.
ANGALIA PICHA YA PILI (AMBAYO MAJANI YAKE HAYAKO VIZURI-YAMEJIKUNJA/Filiform)
Muda si mrefu sana hayo majani yatakuwa hivi (Unjano katika vena za majani)
View attachment 418426
Huo ni ugonjwa huitwa Papaya Ringspot diseases/Papaya Ringspot Virus
Huenezwa na wadudu waitwao Aphids/Wadudu mafuta
Mche wa namna hiyo hata ukizaa matunda yake huwa na mabaka baka/mashiringi
View attachment 418428View attachment 418436
KABLA HATUJAKUSAHURI CHA KUFANYA, TUNAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO
1. Maganement/Matunzo ambazo tayari umeshayafanya shambani, yaani tangu kuandaa mashimo mpaka sasa umefanya nini na nini, ie. Ulipandia mbolea gani??, umeshaweka mbolea zipi tena mpaka sasa, JE UKIACHA CONFIDOR kuna viuatilifu gani umeshapiga hapo shambani?/
KWAKWELI NIMETAFUTA SANA MASOMO YA KILIMO CHA PAPAI SIJAPATA KWAHIO NLIKUA NAFANYA TU MAJARIBIO. NLIPANDIA SAMADI YA NG'OMBE TOKA HAPO NAPIGA TU MAJI MARA MBILI KWA WIKI. SINA BOOSTER WALA DAWA ZOZOTE NAZOTUMIA ZAIDI YA CONFIDOR NLIPIGA BAADA YA KUONA APHIDS.
2. Je umewahi kupiga booster zozote?? HAPANA
3. Hizo dawa za wadudu unapiga kila baada ya muda gani?? SIPIGI ZAIDI YA CONFIDOR NLIPIGA MARA MBILI
4.Napsack Sprayer (Bomba) unalotumia kupulizia dawa ni lako?/ au unaazima kwa jirani (Eleza ukweli) LA KWANGU
5.Uwekaji wako wa maji ukoje, unaweka mara ngapi maji kwa wiki, na ni wastani wa lita ngapi kwa mche kwa siku/wiki?? etc
KILA SHINA NDOO MOJA YA LITA 10 MARA MBILI KWA WIKI
KARIBU
===================================
kilimomaarifa.tajiri ni kweli African marigold ikipandwa kuzunguka shamba/bustani inasaidia kupambana na wadudu na unaweza acha kutumia dawa za wadudu za viwandani?
ASANTE SANA MKUU. MUNGU ATAKUJAALIA KWA ELIMU HII YA BURE UNAYOTOA KWA WAKULIMA WACHANGA KAMA SIEASHA NGEDELE
SALAMU SANA
ASANTE KWA MAJIBU YAKO
KUNA VITU TUNAKUSHAURI
1. Kuhusu hiyo mbegu yako ya tikiti, ipe muda angalau siku 5 mbele tuone. Zisipooota itabidi urudie kupanda, LAKINI hatuisemi vibaya ila kuna takribani wakulima 15 pia wameilalamikia inaota taratibu, na haiko haraka katika ukuaji. Sijui tatizo liko wapi, au labda watu wameanza kuichakachukua hatujui. Ni vyema hizo mbegu mpya ukaziongezea nguvu kwa kuzitibu zaidi (siku 2 kabla ya kupanda) na moja wapo ya dawa kama Cluiser, Mortano, Seed care, Seed plus, Seed treat, Broad hactare etc, kwa sababu mbegu nyingi hata hiyo uliyotumia naamini iko na Thiram tu ambayo ni non-systemic dimethyl dithiocarbamate fungicide, haina nguvu sana dhidi ya baadhi ya bacteria, na magonjwa mengine (Inafanya kazi vizuri kama Contact fungicides), hivyo bado mbegu inaweza kushambuliwa kabla ya kuota.
2. Tukirudi katika Miche yako ya papai
i. Iongezee lishe, tafuta NPK (17:17:17) ambayo itasaidia kuboost ukuaji, mizizi na kuimarisha afya ya majani
2. Ni muhimu ukatumia tena cofidor ndani yake mix na dawa ya ukungu kama Multi Power 78wp au Azoxtrobin, au Agrifos400, au Ebony 72, ndani yake weka booster kama Supergrow, au Multi K,au Murphy foliar fertilizer au Omex. Lengo ni kusaidia kama kutakuwa na baridi usiku/unyevu mwingi basi mmea usiathirike (Fungus), na pia kuna dalili ya upungufu wa micro elements kama Boron, na Magnesium, hizo utazipata kwa kupitia booster.
ii. Kabla ya kuweka mbolea ile NPK mwagia kwanza maji, kisha weka NPK, kila mche unapaswa kupata gram 300, unaweka pembeni ya shina huku yalipo ya majani (Plant Canopy), huko ndipo root hair ziliko fika, tumia rato kutengeneza sahani kisha weka hizo gram 300 (sawa na maganda 6 ya viberiti, kule kunako kaa njiti,) ukiweka mbolea hiyo unafukia na udongo au kuweka matandazwa,
ii. Kwa upande wa maji si mbaya sana kiwango unachoweka, kwa kuwa bado haijaanza kuzaa angalau lita 25 kwa mche inatosha, ila ikianza kuzaa walau kila mche upate lita 50 za maji kwa wiki 1.
KILA LAKHERI
KABLA HATUJAKUSAHURI CHA KUFANYA, TUNAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO
1. Maganement/Matunzo ambazo tayari umeshayafanya shambani, yaani tangu kuandaa mashimo mpaka sasa umefanya nini na nini, ie. Ulipandia mbolea gani??, umeshaweka mbolea zipi tena mpaka sasa, JE UKIACHA CONFIDOR kuna viuatilifu gani umeshapiga hapo shambani?/
KWAKWELI NIMETAFUTA SANA MASOMO YA KILIMO CHA PAPAI SIJAPATA KWAHIO NLIKUA NAFANYA TU MAJARIBIO. NLIPANDIA SAMADI YA NG'OMBE TOKA HAPO NAPIGA TU MAJI MARA MBILI KWA WIKI. SINA BOOSTER WALA DAWA ZOZOTE NAZOTUMIA ZAIDI YA CONFIDOR NLIPIGA BAADA YA KUONA APHIDS.
2. Je umewahi kupiga booster zozote?? HAPANA
3. Hizo dawa za wadudu unapiga kila baada ya muda gani?? SIPIGI ZAIDI YA CONFIDOR NLIPIGA MARA MBILI
4.Napsack Sprayer (Bomba) unalotumia kupulizia dawa ni lako?/ au unaazima kwa jirani (Eleza ukweli) LA KWANGU
5.Uwekaji wako wa maji ukoje, unaweka mara ngapi maji kwa wiki, na ni wastani wa lita ngapi kwa mche kwa siku/wiki?? etc
KILA SHINA NDOO MOJA YA LITA 10 MARA MBILI KWA WIKI
KARIBU
Asante kwa majibu...hii issue ya marigold ni maelezo ya jamaa wa JKT kwenye banda lao wakati wa nanenane...kwenye shamba darasa lao walisema wametumia african marigold tuu bila dawa yeyote hasa katika kilimo cha kabichi.Bonge
SALAMU KIONGOZI
KARIBU
Ni kweli jamii za Marigold (African marigold (Tagetes erecta Linn.) and French marigold (Tagetes patula Linn). Zinatumika kama fly repellent/kufukuza wadudu hasa Aphids na Thrips, pamoja na fruit flies.
Lakini pia mahali yanapoota Marigold wale Minyoo fundo (Nematodes, wasababishao kuoza kwa mizizi, Root knot Nematodes) hupungua sana. Marigold yanamatumizi mengi sana , baadhi ya nchi kuna namna wanayatumia kuongeza virutubisho kwa chakula cha mifugo na kukiknga mifugo dhidi ya minyoo.
Hakuna uthibitisho wa kisayansi wa 100% kuwa ukitumia Marigold basi uache kutumia dawa za viwandani, Kuna baadhi ya wadudu kama Tuta absoluta (Kanitangaze wa nyanya, au Bakteria i,e Bacteria Wilt, au Fungus (Kuvu/Fangasi)) bado hakuna uthibitisho wa kutosha kuwa wanaweza zuiwa kwa kutumia Marigold.
Lakini ni vyema ukayapanda, yatakupunguzia kiasi fulani gharama za madawa. Hushauriwa kutumika katika kilimo cha Organic (Kilimo hai), maana sumu yake huisha nguvu ndani ya siku 7.
kuna kajistory hapa, unaweza kapitia kutoka kwa mkulima Kenya hapo
Marigold is all I use to stop pests and diseases
Asante kwa majibu...hii issue ya marigold ni maelezo ya jamaa wa JKT kwenye banda lao wakati wa nanenane...kwenye shamba darasa lao walisema wametumia african marigold tuu bila dawa yeyote hasa katika kilimo cha kabichi.
ASANTE SANA MKUU. MUNGU ATAKUJAALIA KWA ELIMU HII YA BURE UNAYOTOA KWA WAKULIMA WACHANGA KAMA SIE