Je, unakumbuka ulivyokuwa ukifikiria ulipokuwa mtoto?

mimi nilikuwa nafikiria tukila chakula kinajaa hadi kwenye koo
Mimi nilikua nadhani kwamba tunapokula basi chakula kinaanza kujaa kwenye vidole vya miguu kwanza na kinapanda kidogokidogo kwnye mwili ndipo tunanenepa......na nilifikiri watu wazima hawapigi mswaki..looooh!!!
 
Mbona wote mnakwepa wote tulivyokuwa tunafikiria tulipokuwa watoto? Kwamba Baba anajua kila kitu hapa duniani, pia hakuna mtu anayeweza kumpiga baba, ndio maana kila ulipoguswa tu, "ntaenda kumwambia baba"
 
Kabla sijaanza shule Nilidhani nikianza shule, siku ya kwanza ndo darasa la kwanza, ya pili ndo la pili, ya tatu la tatu ...nk. Nilishangaa sana nilipoanza shule, maana kila siku ninapoenda shuleni bado niko darasa lile lile la kwanza....nilikasirika sana!

da mi sijawahi kuwaza hivyo.
 
Nakumbuka nilipokuwa mtoto kila nilipokwenda stesheni (Tbr) nilikuta injini za tren zipo on muda wote, pia mabehewa yakisukumwa kwenda mbele na nyuma. Hapo nilidhani kwamba injini ya treni ikizimwa basi haiwaki tena, na mabehewa yakikaa muda mrefu bila kupelekwa mbele na kurudishwa nyuma (shanting) hupata kutu na kusababisha injini kushindwa kuyavuta. Je wewe unakumbuka nini ulipokuwa mtoto?
Mie nakumbuka siku mama akipika wali nilikua naoga saa9,lakini siku ukipikwa ugali naweza lala bila kuoga kabisa.
 
mi nilipokuwa mtoto nilidhani jua yako mengi kila sehemu yaani tukisafiri nasema na hawa wana jua lao na nilipoona mawingu kama yameinama nilijua Nndio mwisho wa mawingu,nilipokuwa mkubwa nilijiona nilikuwa mjinga sn!
 
Mimi nilikua nikimganda sana baba. Akiwa anfanya kazi zake za nyumbani niko naye. Hata akilala saa nane za usiku basi ntakaa naye. Sasa akona technique ya kuniambia nikalale mapema ni kuniambia kua nikisikia radio inasema saa tatu kamili usiku basi nikalale.

Sasa kila siku akawa ananiambia hivyo. Na nikweli bwana baada tu ya kuniambia kama dakika 5 tu inachukua kabla ya radio kutangaza.

Basi nikawa namuona baba anaakili kinoma, sasa anajuaje mida namna namna hii...... dah
 
Mi nlikuwa najua 2kiwa 2nasafir kwny basi ikiwa kwny mwendo wa kasi, ile miti na nguzo za umeme vilikuw vina2kimbiza ku2fuata.
 
nilikuwa nasikia watu wakimwita balozi wa kijiji chetu Ngamilo basi nikajua mabalozi wote wanaitwa mangamilo yani ni kama jina la cheo chao..

Dah! Brother ulikuwa kiazi SANA! Ha ha ha!
 
kumi hili nilisahau kulinukuu mwanzo mm wakati niko totoo nilikuwa najua ukipaka pafyumu na ukibana makwapa harufu haisikiki kwa wengine ila ukiachia mikono au ukokaa kawaida ndo harufu inaruka kwa wengine basi bana,
sikui ya siku nakumbuka ilikuwa usiku nishaoga nimevaa night dress mama akanituma rum kwake nikalete kalamu na gazeti coz mum alikuwa anapenda kujaza puzzle games kwene magazeti sasa kwa ufinyu wangu wa akili nikaona pafyum kwene dressing table wajua ilikuwa pafyum gani bana ilikuwa yolanda kopo la bati la rangi ya pinki we acha nikapuliza makwapa yote halafu nikabana makwapa kwanguvu nikapeleka gazeti na kalamu kwa mama huku mikono imebana kwapani kwanguvu ili asisikie harufu nikashangaa akaniambia nani kakwambia upake pafyum yangu weee nilitahayari nikaomba msamaha haraka kabla cjashushiwa kofi coz mum alikuwa mkali balaa lol nikaondoka ila nikajiuliza alijuaje wakati nilibana makwapa sana jibu ckupata now najiona very fun
 
nilikuwa nawaza ikosiku tutakuwa ulaya au america maana dunia inazunguka!
 
Hata mi nilijua wanaume hawanyi wala hawajambi.
Pia nlikua nafikiria watangazaji watu wanaoonekana kwenye tv wamo mulemule ndani na km ukifungua ile screen unawaona
 
mazee mimi nilijua kua ukila tunda na mbegu yake ukaimeza basi mti utaota ndani na kutokea kichwani basi nilikua naogopa kweli kumeza mbegu kama za machungwa hivi yani ilikua nitashikwa na mawazo siku nzima..! na nilikua najua zile plastic za mfano wa mtu zilizokua zinatumika kufundishia wanafunzi wa MATC zilikua ni watu wa kweli waliokufa wakakatwa matumbo yao yani nilikua nina ogopa kweli nikizikuta ofisini kwa dingi..! nakumbuka siku moja dingi alikua hayupo ofisini basi kwa utundu wangu nikafungua kabati nikakutana nalo...! ahahhhhaaaaa aisee nilitoka nduki kama nimeona nini sijui..! tulikutana mlangoni dingi anaingia na mimi ninatoka nduki..!
 
niko na mwenzangu hapa alikua anayasalimia yale maplastic ya kama watu....! yani utoto..!
 
Mbona wote mnakwepa wote tulivyokuwa tunafikiria tulipokuwa watoto? Kwamba Baba anajua kila kitu hapa duniani, pia hakuna mtu anayeweza kumpiga baba, ndio maana kila ulipoguswa tu, "ntaenda kumwambia baba"

aisee huu ni ukweli kabisaaaa...!
 
Kabla sijaanza shule Nilidhani nikianza shule, siku ya kwanza ndo darasa la kwanza, ya pili ndo la pili, ya tatu la tatu ...nk. Nilishangaa sana nilipoanza shule, maana kila siku ninapoenda shuleni bado niko darasa lile lile la kwanza....nilikasirika sana!

Mie nilifikiria,katika gari zile Break lights, taa za indicator na taa zote huwa dereva anaziwasha kwa mikono yake yaani kama vile :disapointed:humo ndani ya gari kuna sehemu nyingi mbalimabli ambazo ili taa za breki ziwake yabidi ubonyeze.
 
Mie nilifikiria,katika gari zile Break lights, taa za indicator na taa zote huwa dereva anaziwasha kwa mikono yake yaani kama vile :disapointed:humo ndani ya gari kuna sehemu nyingi mbalimabli ambazo ili taa za breki ziwake yabidi ubonyeze.

duh!! Hata mimi nilikuwa nafikiri endiketa swichi ni gia ya kukatia kona, yaani gari haiwezi kukata kona mpaka uweke hiyo gia.
 
Nilijiahidi kuwa mume atakae nioa atakuwa yule ambae hanyi wala hakojoi. :bored: Endless search!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom