Je unakumbuka nini miaka ya 80’s na 90’s.

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Mimi binafsi, nayakumbuka mafuta ya Yollanda yaliyokuwa kwenye mkebe hivi, yamanukia. Nyimbo za bolingo kama za Kanda bongo Man. Tulikuwa tukibadilisha maneno kama Ndee moni, ndee moni, Ukishakulaa ku tingisha kumba. Zamani Rahaa, enzi za mzee ruksa. Blue Blue kibao.
 
Duh Vingi tu RTD saa mbili unasubiri michezo na daftari lako la Hesabu unahakikisha kila kitu umeweka sawa la sivyo mwalimu wa Hesabu ni wa kwanza bakora tu. au Matangazo kama Omari Ngwarangwara, Uzushi wa wanyonya damu mashuleni, nakumbuka Sabasaba ndio Joyce Wowowo anaanza ndio tena kila mwenye makalio makubwa akawa yanaitwa wowowo! nakumbuka KIA za kuangaliana, na nyimbo kama hizi Chaka Demus Na Pliers Murder She Wrote nilikuwa nikisema anakutesa kwa Karataaaa. nyimbo nyengine Ace of base - All that she want, na hiii nakumbuka udogoni ikipigwa Mchana natoka jua kaliiiiiii! -------->>>>>>> Mory Kante kuna wengine najuwa walikuwa wana itafsiri vibaya zaidi ila mie kama hapo.
[h=1]Mory Kante - Yeke Yeke nilikuwa nafikiri inaenda hivi kikuku kinanukiaaaa ahhhhhh kikuku kinanukiaa ahhh.[/h]
 
mi namkumbuka yule jamaa mmoja aliyekuwa anachezesha sanamu la Joyce wowowo na mwingine aliyekuwa albino anachezesha vijisanamu akipiga filimbi
 
Nayakumbuka Mabasi yalio tamba hinzi hizo. Kiswere, Zainabu, Superstar, Urafiki, Amwenye na mengine mengi
 
Mimi nakumbuka miaka hyo ya 90' RTD kipindi cha Majira na kipindi cha Mazungumzo baada ya Habari!
Pia nakumbuka miaka hyo tulikuwa tunaogopa wagonjwa wa Ukimwi kama nini! Yaani ukikutana naye kakondeana unakimbia! Duh!
 
> RTD kipindi cha kombora,majira na malenga wetu,pwagu na pwaguzi. Mchezo wa kuigiza wa mzee jongo na wenzake. Siku ya kutangaza mpira watu nyomi mmezunguka radio moja ya mkulima.
>Huku bush mashamba ya MFUMAKI, Mashuleni E.K,Mzee mnaenda kulima na kuvuna kwenye mashamba ya wa2 kama manamba.
> Raba mtoni babake,walivaa masharobaro (waziri mkuu Salimu Ahmed Salimu).
> Sekondari ,boarding unakutana na vyombo vinaitwa mustin,vimepigwa chata TG ( Tanzania Government) ili visiibiwe. Mnapewa mikate na siagi. Mnalipwa nauli.
> Primary mnalipa ada shs 20.
> Noti ya thamani ya juu ilikuwa noti ya shs 10. Ilipokuja ya shs 50 tukajua sasa uchumi unayumba.
> Sheikh Yahaya akiwa raia mmiliki pekee wa satelite dish bongo. JKN alipotoka ziarani nje alirudi na mikanda ya video ya hotuba za wakomunisti/ wajamaa,anawakusanya Kawawa na wenzake wanacheki picha ikulu.
> Namkumbuka mbunge wangu Padre Supa.
> All in all zamani tuliishi kwa amani tukiwa 'gizani.'
 
Muzee umechapia! Mustin ulikuwa ukipatikana jeshini mazee. Chapa TG: Tanzania Government.
 
Teh teh teh !
Mkuu Osaka pole kwa mionzi ya Cosmo,nasikia saa 6 tu ulizima simu ukaiweka umbali wa mita 10 !... (Just a joke!)
Back to topiki:
Ni kweli mustin ni jeshini pekee. Except shule ya Secondary Kwiro. Aliesoma pale miaka ya 80- 90 aje hapa akanushe ama athibitishe !
 
Katalogi za miaka hiyo ni Snopy Dogy Dogy, Chachacha, Chupi aina ya VIP. Kipindi hicho vijana tulikuwa tukiokata pesa, tunaona kawaida. Toka 2000 to date sijawai kuokota pesa.
 
Duh Vingi tu RTD saa mbili unasubiri michezo na daftari lako la Hesabu unahakikisha kila kitu umeweka sawa la sivyo mwalimu wa Hesabu ni wa kwanza bakora tu. au Matangazo kama Omari Ngwarangwara, Uzushi wa wanyonya damu mashuleni, nakumbuka Sabasaba ndio Joyce Wowowo anaanza ndio tena kila mwenye makalio makubwa akawa yanaitwa wowowo! nakumbuka KIA za kuangaliana, na nyimbo kama hizi Chaka Demus Na Pliers Murder She Wrote nilikuwa nikisema anakutesa kwa Karataaaa. nyimbo nyengine Ace of base - All that she want, na hiii nakumbuka udogoni ikipigwa Mchana natoka jua kaliiiiiii! -------->>>>>>> Mory Kante kuna wengine najuwa walikuwa wana itafsiri vibaya zaidi ila mie kama hapo.
Mory Kante - Yeke Yeke nilikuwa nafikiri inaenda hivi kikuku kinanukiaaaa ahhhhhh kikuku kinanukiaa ahhh.

Kwa kweli we umenikumbusha mbali sana, ngoja na mimi nikumbuke.
 
Nakumbuka gazeti la sani akina kipepe, madenge, pimbi lodilofa, ndumilakuwili, Bob mazishi, omy kiss, linda, obi,mayuku, zumo, Seba, chino,bushi stars, makwekwe united, born town, captain mapung'o,udeze, ibra wa shokera na wengine wengi ilikuwa full Burudani
 
Kweli kipinde kile raha sana. Nakumbuka katika tarafa vijijini, moja akiwa nalo kijiji kizima kitasoma.
 
Nakumbuka gazeti la sani akina kipepe, madenge, pimbi lodilofa, ndumilakuwili, Bob mazishi, omy kiss, linda, obi,mayuku, zumo, Seba, chino,bushi stars, makwekwe united, born town, captain mapung'o,udeze, ibra wa shokera na wengine wengi ilikuwa full Burudani

ndondocha na mwanae Stiki
 
Mimi binafsi, nayakumbuka mafuta ya Yollanda yaliyokuwa kwenye mkebe hivi, yamanukia. Nyimbo za bolingo kama za Kanda bongo Man. Tulikuwa tukibadilisha maneno kama Ndee moni, ndee moni, Ukishakulaa ku tingisha kumba. Zamani Rahaa, enzi za mzee ruksa. Blue Blue kibao.

Mm nakumbuka lile tangazo la Topaz la baba kchonge na mama kichonge. Mida ile ndo napka chai niende skonga. Utoto ule ulikua raha sna, kwa kua hapakua na tv so mda mwng tulitumia kucheza kmama mama na kbaba. Hahahaa halaf mnajfunika kanga baba na mama, watoto wanaenda kuokota kuni.
 
Viatu vinaitwa-DH
CHUPI ZA V.I.P KWA MALES
CHUPI ZA TAIWAN 4 FEMALES
MAGAGULO,Mabalongo,KANIKI,SABUN YA MBUNJU,FOMA,KIPINDI CHA MAMA NA MWANA, BAISKEL ZA SWALA,MADUKA YA RTC,MAFUTA YA RAYS,ASHANTI,NDALA ZA UMOJA,SKY WAY,KITO,
 
Sugu aliimba'HAPO ZAMAN HAPO ZAMAN,MAMBO MENG YALIKUA SAFI,KINYUME NA SASA KINYUME NA SASA,MAMBO MENGI YAMEBADILIKAA'
 
Nakumbuka nguo anaina ya Kamanyora, Buga na Chachacha. Nilikuwa nazivaa Jumapili tu. Siku nikivaa hakuna kucheza mpira wala tayari bado. Ni mwendo wa mikono mfukoni siku nzima. Vinginevyo ni kichapo.

Nakumbuka jinsi nilivyokuwa napuyanga kwenda shule bila viatu. Tunakula gwaride safi, halafu wakati wa kurudi nyumbani ni mnyukano kwa kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom