Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Safi sana jamaa umenikumbusha mbali mimi nakumbuka JKT Msange oparation miaka 20 ya Azimio la Arusha.Mbali na mitulinga,mitikasi na taabu JKT.JKT kwa namna moja au nyingine ilikua na umuhimu wake mafunzo ya ukakamavu,uvumilivu pia hapa JKT ilikua unawakutanisha watu mbalimbali wenyevipaji mbalimbali bila kujali unatoka katika familia gani na wote kua katika kivuli kimoja.

Kwa Msange kombania B ilikua na maafande poa na tulikua tukishinda kila mashindano kuanzia kwata na shughuli nyingine nyingi namkumbuka Afande Sijali,Afande,Mrope,Swai.Pia namkumbuka Afande Wela wa kombania D huyu jamaa alikua katili wa kupindukia.Kwa upande wa wimbo naukumbuka wimbo huu oo msange...msange malaika....oo msange nitarudi
 
JKT ni heri irudishwe tuu bse vijana wa leo ndo maana wanaaribika ukakamavu sifuri mara ooh mtoto si rzki.
Wale wa Mafinga mpo?
 
Kombania A kulikuwa na kiafande kinaitwa Mwashamba..ebwana hiki kijamaa noma kweli.

.Kwa Msange kombania B ilikua na maafande poa na tulikua tukishinda kila mashindano kuanzia kwata na shughuli nyingine nyingi namkumbuka Afande Sijali,Afande,Mrope,Swai.Pia namkumbuka Afande Wela wa kombania D huyu jamaa alikua katili wa kupindukia.Kwa upande wa wimbo naukumbuka wimbo huu oo msange...msange malaika....oo msange nitarudi

Duu, Mwashamba. Jasha kama unakumbuka, Msange pia alikuwepo Mwashamba Kombania A. Hawa ni mtu na ndugu yake. Mwashamba wa Msange alikuwa akipiga NYUMA GEUKA, anazunguka zaidi ya degree 180 halafu anarudi kwenye hiyo 180, na anapiga mguu. Huyu wa Msange alikuwa kaowa na hivyo hakuwa anajionyesha kupenda chini.

Msange nilikuwepo Operation ya Chama. Nilikuwepo Komb. A kwa Mohamed. Kama unakumbuka Makonde walikuwepo wawili, Mrope na Mohamed. Pia yule mchaga sijui Majani (walikuwa hawajaowa). Sisi tulikuwa 89/90. Tulifika CO akiwa Sanga na baadaye akahashimishwa na kuwa yule M-Mbulu nani sijui.

Afande wera, Muha yule lohhhh. Sisi tulipofika alikuwa kapoa sana. Nasikia alimfanyia unyama kijana fulani kumbe jamaa ni Medical Assistace, na jamaa akapangiwa kazi Kitete. Wera akaugua jino akaenda pale Kitete na kijana akamtoa jino zima akaacha bovu. Wera kichwa kikavimba na next day akarudi tena na jamaa ndiyo akatoa bovu. Ila mwaka wetu nakumbuka siku ya sherehe ya kutuaga walikosana na jamaa anayeitwa Shelukindo kwenye Disco.

Wera akachukua Ma-MP asubuhi na kwenda kumkamata. Basi ilianza urukushani na kwa sababu Shelukindo alikuwa kapanda, basi kazi ilikuwa ngumu. Shelukindo akiwa ndani la shati la kijana Mataka (Kijana wa Movie) alichaniwa lile shati, na Shelukindo alimchania Wera Suruali na tukagundua kuwa alikuwa ndani ya chupi VIP. Ila bahati haikuachia ipande kifuani.

Waikumbuka Mihogo ya pale Msange? Zile Zambarawe na Maembe ya pale? Kwa taarifa yako, unaweza kuiona Msange JKT ndani ya GOOGLE Earth. Na juzi nilicheka kusikia kuwa JOHN LEGGEND yule mwanamziki kutoka USA aliyekuwa Tanzania, kumbe alienda Mbola. Waikumbuka Mbola lakini??
Mrope nakumbuka alienda Dar, na kurudi akawa anasikiliza nyimbo za Reggae. Nikamuuliza hivi huyo ni Tosh? Akanijibu bila mkwara "Hapana, huyu ni Lucky Dube....."

Hivi ndivyo nilivyokuja msikia Lucky Dube. Niliporudi Dar, cha kwanza ni kwenda nunua Kaseti ya Lucky Dube. Mrope alikuwa hana shida na mtu. Mmakonde kapanda wala huwezi amini ni Makonde. Wamkumbuka Ngoma? Alimsotesha jamaa yangu mmoja aitwaye Sepetu hadi leo hii yule anasema akimuona atamdunda. Jamaa likuwa kaficha godoro msituni. Akirudi kikosini, Ngoma anampa Drill, jamaa akitoka hapo analala msituni wiki. Akirudi tena anapata Drill, na jamaa analala msituni wiki........ hadi akamaliza. Ehh, pia alikuwepo Afande Magwega. Siku za mwanzo unamuona usiku tu maana alikuwa anapenda sana kuimba. Magwega wa Chiguru...

Namkumbuka sana Kepteni Mrimba. Mkuu huyu wa Mafunzo ya kijeshi alikuwa very up-to-date. Mafunzo yake na lugha yake imefanya hadi leo hii nikumbuke alivyosema. Mkifika siku za mwanzo, Mpoleeee. Mkianza mafunzo ya kijeshi anakuwa Mbogo. Pana wakati ilikuwa tuende kuhudhuria mazoezi ya kijeshi ya DIvision ya Mirambo. Basi tukaanza tizi la kukimbia.

Tunakwenda hadi Miyemba na kurudi. Jamaa wakasema tuongeze Mbio ili tumkomoe. Basi yeye si kuwa alikuwa akikimbia kama sisi. Alikuwa akienda kama mwendo wa nyoka. Yaani akienda kichaka cha kulia, baadaye cha kushoto. MWisho wa safari akawa kakimbia zaidi kutuzidi sisi. Looo, kutoka hapo tukajua kweli Mzee hatumuwezi na cheo alikipata kwa haki.
 
Kwa wale waliopitia Oljoro miaka ya 1989/90/91/.. watakuwa wanaijua "SINDANO YA GANZI" ni Koplo mmoja alidumu sana pale A coy. Dah kumbukumbu ni nyingi, nazitafutia muda nije na mkanda wote.
 
JKT kweli kulikuwa na ubunifu. Alikuwepo rafiki yangu mmoja makutupora (mlinzi wa shamba la zabibu) alikamatwa na afande anakula zabibu. Afande akamchukua pamoja na zabibu zake kuelekea kwa ma MP kule "kota gadi". Jamaa njiani akabuni mbinu ya kujiokoa. Ghafla alichomoka mbio, akiruka miuzio ya minyaa, watu we we weee.

Afande alikuwa akienda naye sambamba, cha kushangaza jamaa alikuwa akielekea katikati ya kikosi badala ya kukimbilia msituni! e bwana jamaa alikimbia moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi ya CO. Wakati huo alikuwa Rajab mzanzibar bonge la mtu. Afande kuona jamaa anaingia mbio kwa CO..yeye kala kona shaaa.

Kruta aliishia tu pale nje kwa maofisa wadogo akawauliza kama wamemuona afande mwingine, akajidai alimtuma. Basi alipoambiwa hayupo akatoka na adui yake alisha tokomea. Aliporudi shambani akamkuta afande aliyemshika kesha rudi huko. Afande hakuwa na noma tena wala hakumuuliza kitu, akaishia kupangia vikazi vya kawaida na life ikasonga mbele, kuruta Haji akawa amepona lupango na drill za ma MP.

Moja mbili, jambo afande
moja mbili, jambo afande.....mnaruka nonstop
 
Staff Sgt. Chisanza wa A coy pale Oljoro JKT, anakuuliza umeona ukisema ndio basi ujue kazi unayo, kama hujaona basi endelea mbale.
 
Mwashambwa aka LB (Last born). Haka ka bwana kalikuwa kanapenda chini ile mbaya........

Kina mkwara wakati kijitu chenyewe kidogo! Kilitukamata mnadani, tukakinunulia nyama, wakati kinakula tukakitoroka. Kufika kambini ati kinasema tumetoroka mara mbili..kikosi na mnadani..tena tulikitoroka mnadani bila kulipia nyama kilizokula.

Nakumbuka nilikuwa mpishi mkuu, nikapiga stop ya maafande kuchukua pororo...looh walinitimua jikoni nikapelekwa kwa mbuzii. Ukienda kuchunga mimbuzi hata nane inaweza zaa machungani basi taabu kuvibeba kurudi zizini.
 
Kwa wale waliopitia Oljoro miaka ya 1989/90/91/.. watakuwa wanaijua "SINDANO YA GANZI" ni Koplo mmoja alidumu sana pale A coy. Dah kumbukumbu ni nyingi, nazitafutia muda nije na mkanda wote.


Capt Mrimba alihamia Oljoro baadaye miaka ya 90.. kama sikosei na huko pia aliendeleza "tifu". Nakumbuka tukiwa kwenye "range" pana service mmoja alirusha "grenade" likashindwa ku-explode! Na kama ilivyo sheria ni lazima li-explode... Capt Mrimba alilifuata lile "grenade" akajaribu kulipiga bastola haliku-explode, hivyo ikabidi aliokote na kurirusha tena (by the moment kila mtu alisubiri li-explode mikono mwake), kwa bahati aliporirusha mara ya pili "booom". Huyu mzee alikuwa balaaaaaa kwelikweli.......

Watu wa oljoro mpooooo? Afande Tyetye mnamkumbuka? huyu sajenti alukuwa balaa wakati wa "guard".. alikuwa anakagua malindo kuanzia CTS mpaka "farming". Kwa walikuwa oljoro kati ya CTS na farming kulikuwa na pori kubwa kiasi!

Bahati tulipigwa bogi kutoka CTS tukapelekwa makuyuni (hapa usiku tulikuwa tunapishana na wanyama wa mwitu - kama fisi, e.t.c) ambako siku tunafika tulikuta "wamepiga" nyati waTATU, usiku huo tulikesha tunachoma nyama and kesho yake tulishinda "zahanati" - matumbo hoi. hapa life ilikuwa kama vile upo uraiani tu, zaidi ilikuwa ni kuchunga mifungo ya Mh Makame R.

Baaadaye tukahamishiwa Mto-wa-Mbu tukiwa kama 40 hivi. Kazi kubwa hapa ilikuwa ni kuchimba mtaro wa maji ya kumwagilia maji kutoka ukingo wa mto wa mbu (mto unaopita katika kitongoji cha Mto wa Mbu) hadi kikosi, trust me ilikuwa kama 5km lakini within 30 days maji yalikuwa yamefika kwenye mashamba ya jeshi! Maisha ya hapa yalikuwa mazuri sana, maana kazi iliisha saa nne asubuhi, baaada ya hapo unatinga "combat" unaingia down-town mto wa Mbu - mpaka majogoo - kulikuwa na ukumbi wa disco pale na tuliingia bila kulipa kiigilio...

I miss JKT!
 
Ah...sisi tuliolikosa tumekosa uhondo kwelikweli...ninaposikia stori za jeshi natamani namimi ningepitia huko
 
Capt Mrimba alihamia Oljoro baadaye miaka ya 90.. kama sikosei na huko pia aliendeleza "tifu". Nakumbuka tukiwa kwenye "range" pana service mmoja alirusha "grenade" likashindwa ku-explode! Na kama ilivyo sheria ni lazima li-explode... Capt Mrimba alilifuata lile "grenade" akajaribu kulipiga bastola haliku-explode, hivyo ikabidi aliokote na kurirusha tena (by the moment kila mtu alisubiri li-explode mikono mwake), kwa bahati aliporirusha mara ya pili "booom". Huyu mzee alikuwa balaaaaaa kwelikweli.......

Baba Enock,
Nakubaliana na wewe kabisa. Huyu Mzee tulikuwa hatujui kwa nini ni Captain na wala siyo Major. Alikuwa akisema hayo maneno nilikuwa nafikiri anadanganya. Alisema kuwa kama grenade likianguka karibu basi yeye kama kama Afande wajibu wake ni kulirukia na kuhakikisha linamlipua yeye bila ya kuuwa makuruta. Nilivyokuwa nasoma nikafikiri umeandika "akafa".

Kama ni mafunzo ya kijeshi, basi huyu mzee alinipa. Pana wakati alitufundisha hadi mbinu wanazotumia makomandoo au Sniper kuuwa vitani huku wakiwa mita kama 20 mbele. Hivi kuna mtu anakumbuka maneno ya Mrusi aliye-retreat vitani na akapona hukumu ya kifo?

Mrimba alituambia ila sikumbuki. Mrusi yule aliulizwa sababu yake kurudi nyuma wakati wa vita wakati sheria inasema "milele ni kwenda mbele.." Jamaa nasikia akasema (Maneno ya Mrimba) " .. We ware not retreating, but we was" Hapa ndipo nimesahau.

Nasikia Mageneral kutoka wakati huo wakaanza kufunza mafunzo ya ku-retreat wakati wa vita mambo yanapokuwa magumu.
 
Yaani hivi Visa vya JKT, kila unaposoma simulizi zake ni burudani tosha . . . . .

Kuna afande moja alihukumiwa na Court Marshall kisa kamlazimisha kuruta kushika kinyesi . . . . .

Nadhani JKT inaweza kufanywa kwa sasa kuwa Chuo Cha Mafunzo ya jeshi na Ujasiliamali wa Vitendo yaani kama Incubators.
 
Tutaongelea mazuri yote ya JKT lakini tusichopenda kukiongelea ni msambazo wa UKIMWI na wenzetu (sana sana akina dada) waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi na maafande wa darasa na saba. Hatutaki tuongelee juu ya ubakaji uliokuwa unafanywa na maafande ambao kwa namna moja au nyingine uliahalalishwa na serikali.

Ukiuliza takwimu za waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi wakiwa JKT zinatisha, uliza takwimu za maafande wanaokufa kwa ukimwi..mbaya mno...Hongera kwa aliyeamua kutoendelea na taratibu za JKT....we have lost enough manpower for our country.
 
Wanataaluma mnanikumbusha mbali sana tena . . .

Nakumbuka wakati wa kwata na kunyakua, kuna afande alikuwa analala chini kabisa akidai anataka kuhakikisha kuwa miguu yote inaenda na kushuka pamoja bila kupinda.

Ilikuwa balaa . . . Kunywa uji mwendo wa kunyakua, kula mwendo wa kunyakua nk.

Jamani tunatoka mbaaaaali kweli kweli. Sijui kama watoto wetu watakuja kupata hii experience . . . .
Hizo zilikuwa za Nyundo C coy Ruvu. Thank God mie nilikuwa Danger, na on top nilikuwa naq kitengo cha kudumu garage.
 
Tutaongelea mazuri yote ya JKT lakini tusichopenda kukiongelea ni msambazo wa UKIMWI na wenzetu (sana sana akina dada) waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi na maafande wa darasa na saba. Hatutaki tuongelee juu ya ubakaji uliokuwa unafanywa na maafande ambao kwa namna moja au nyingine uliahalalishwa na serikali. Ukiuliza takwimu za waliokufa kwa kuambukizwa ukimwi wakiwa JKT zinatisha, uliza takwimu za maafande wanaokufa kwa ukimwi..mbaya mno...Hongera kwa aliyeamua kutoendelea na taratibu za JKT....we have lost enough manpower for our country.

Hakuna kitakachoachwa hapa. Ndiyo maana niliandika hapo mwanzo kuwa JKT kumbukumbu yake ni mchanganyiko. Uzinzi, uasherati, UBAKAJI, Ubakwaji, ukuwadi, uonevu, rushwa, mabavu na mengine mengi yote yalijiri. The only important thing to observe confidentiality. Yaani hakuna kutaja mjina ya wahusika live hasa KURUTAS! AU SERVICEMEN/WOMEN.

Pale Ruvu maafande kabla ya kumlia dili kuruta wa kike, basi kwanza wanauliza umesoma wapi.
waliokuwa rahisi ni Uhazili
then Walimu
halafu form six leavers at least maafande walikuwa hawapaparikii hao. they were known as wagumu. sijui kambi zingine how was it?

Maafande wengi wamaeondoka kwa ajili ya Ngoma. wakipata mshahara basi afande yuko radhi ampe mwanamke mshahara wote halafu yeye anahemea pororo na kula kikosini. Mwee!! Nilikuwa nawaonea huruma waliobakwa especially wakidakwa wakati wanajongo!!
 
Hizo zilikuwa za Nyundo C coy Ruvu. Thank God mie nilikuwa Danger, na on top nilikuwa naq kitengo cha kudumu garage.

Mimi nilikuwa na kitengo pale Ruvu. Lakini baadaye kitengo kilini-bore. Wenzako wako kwenye minazi wewe huko kitengoni.
 
1985/1986 Ruvu!

Kwa Babu mbali . . kwa Babu mbali tukumbukane kwa barua . . . Vibwende mbali vibwende mbali tukumbukane kwa barua . . .

Mhando . . . Wapi uko?
Sebastian?
Nyange?
Bagenda?
Halima?
Viviane?
Liberata?

NK . . . I miss all of you guys!
 
Yaani hivi Visa vya JKT, kila unaposoma simulizi zake ni burudani tosha . . . . .

Kuna afande moja alihukumiwa na Court Marshall kisa kamlazimisha kuruta kushika kinyesi . . . . .

Nadhani JKT inaweza kufanywa kwa sasa kuwa Chuo Cha Mafunzo ya jeshi na Ujasiliamali wa Vitendo yaani kama Incubators.


Sanctus Mtsimbe:

Uite mpera mpera na wala sio mchungwa. Wanajeshi watakufundisha jeshi tu na sio ujasiliamali.

Kama kuna nia ya kufundisha watu ujasiliamali, sehemu zitafutwe zingine na sio jeshi.
 
Dakitari Major Omar alihisi tunamuingilia himaya zake (Alikuwa mpenda vimwana sanaaaa, akitoa "C" 100, 98 za wana-serengeti). Siku moja mi na mshakji wangu mmoja Mangi. Tuko zahanati kwenye foleni tunafukuzia "C". Tulikuwa na apointmenti hewa Muhimbili. Jamaa akatushtukia, Siku ya pili Guard-phase two; kudadadeki!!!!!

Weekend moja, tuliishia dar kiaina, tukiwa bado makuruta. Wakati tunajikusanya kariakoo kuchukua Coaster ili turudi RUVU, Co (Urio) akatuona. Tulipoondoka akafunga tera na Land Rover yake huku akiwa ameshawataarifu ma MP kule camp wakae mkao wa kula. Kufika vigwaza, tukamstukia. Mpaka anasimamisha gari kabla ya main gate, ktk coaster alibaki dereva na utingo tuuuu!!!!

Nilikuwa Combania ya MRA WATU!!!!
Wapi Tungaraza!!!!
 
Back
Top Bottom