Je unaamini ndoto???

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Je! Unaamini ya kuwa Mungu anaweza kusema na watu kwa njia ya ndoto? Najua ni rahisi kuamini kuwa Mungu alisema na watu zamani kwa njia ya ndoto kama tunavyosoma katika Biblia; lakini je! Unaamini ya kuwa Mungu anasema na watu kwa njia ya ndoto siku hizi?
Najua kuna watu wanaoamini na wengine hawaamini. Sijui wewe uko upande gani.
Lakini nataka nikueleze hivi; Kufuatana na Biblia kuna ndoto za aina tatu;
(a) Kuna ndoto kutoka kwa Mungu. Soma kitabu cha Hesabu 12:6, na Yoeli 2:28.
(b) Kuna ndoto zinakuja kwa sababu ya shughuli nyingi. Soma kitabu cha Mhubiri 5:3.
(c) Kuna ndoto za uongo zinazotoka kwa shetani aliye baba wa uongo. Soma kitabu cha Yeremia 23:52 na Yohana 8:44.
Unaweza kutofautisha kwa namna gani tofauti iliyopo kati ya hizi ndoto? Na utajuaje kuwa ndoto uliyoiota imetoka kwa Mungu? Kila ndoto lazima ipimwe na Neno la Mungu. Ikiwa imetoka kwa Mungu, ni lazima utakuta neno la Mungu ambalo linaeleza maana yake. Mara nyingine ndoto toka kwa Mungu huja kama fumbo; lakini Roho Mtakatifu ajuaye kuyafumbua mafumbo ya Mungu (1 Wakorintho 2:10,11), atalifunua fumbo hilo kwa kukuonyesha neno la Mungu linalofanana na ndoto hiyo.
Si busara kuzikubali ndoto zote unazoota bila ya kuzipima katika Neno la Mungu. Na pia si busara kuzikataa ndoto zote bila kuzipima katika Neno la Mungu.
​
 
Bwana Yesu asifiwe! Thanx a lot for the word of GOD.
 
Mimi mwenyewe kuna baadhi ya ndoto huwa naota na baada ya muda nikifuatilia nakuta ni jambo lililotokea kweli au lingetokea na wakati mwingine naota na huwa halitokei
 
Ni kweli mtumishi, kuna mifano mingi ya kibiblia ambayo Mungu alikuwa akiongea na watu wake kupitia ndoto. Ila kunahitajika uangalifu maana shetani naye hupitia huko huko na kukufikishia ujumbe wa ndivyo sivyo ktk maisha yako. Unahitaji kusimama kwenye imani kwa uaminifu mkubwa ili ufikia hatua hiyo ....
Yote yanawezekani kwake yeye aaminiye!
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom