Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?

  • Total voters
    111
Yani hakuna kitu wale jamaa yani wakivaa yale manguo yao wanajiiona wako juu ya sheria. Kuna siku nlimuuliza polisi mmoja wewe unaniita mimi Raia. wewe ni nani??... Alishindwa kujibu
 
Nampongeza kamanda Lema (Mb) CHADEMA kwa kutuibulia mjadala wa Jeshi na Siasa. Hebu tujiulize, jeshi letu ni la wananchi kweli au ni la watawala? Ni nini madhara kuwa na jeshi la watawala? Ili kujua madhara ya kuwa na jeshi la watawala tutumia mifano ya mapinduzi ya Tunisia, Misri, Libya na sasa huko Syria.
Katika mapinduzi ya Tunisia watu 200 hadi 300 wanalipoteza maisha, Huko Misri watu 846, wakati Libya inakadiriwa kuwa watu kati ya 30,000 hadi 50,000 na sasa Syria ni takribani watu 45,000 na bado vita inaendelea. Mtakubaliana nami kuwa Tunisia na Misri vifo si vingi kutokana na Jeshi kutambua jukumu la kuwalinda Raia badala ya kuwakumbatia watawala kama ilivyokuwa Libya na sasa Syria.

Hapa kwetu kuna madai ya utovu wa nidhamu kwa Mwanajeshi kupiga picha na Lema, ilihali kuna madai ya mtu aliyekuwa mwanajeshi kupewa nafasi za kisiasa na baadaye kurudishwa jeshini kushika wadhifa mkubwa huko jeshini. Sasa hili letu ni jeshi la wananchi au la watawala? Wananchi tudai jeshi letu, vinginevyo tujiandae kuumia 2015!
Nawasilisha!
 
Ngoja waje
 
Sina Imani na chombo hiki cha usalama wa raia na mali zao....nasema sina!!ebo kwanini kunilazimaisha?!!![QUOTE=Ileje;3374059]Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?[/QUOTE]
 
Jesh la polisi linazidi kupoteza imani kwa wananchi baada ya kufanya madudu katika kazi yao. Hivi kweli ndilo ambalo linasafirisha bangi tena kwa kutumia gari la polisi, leo tena mtuhumiwa atoroka mbele ya mikono ya hao mapolisi, kweli? Wengne tena wakamatwa na fuvu eti hukumu yao ni kutimliwa tu, hapana hi haikubaliki hakika, RPC arusha kumsafisha mkuu wa wilaya, Lukuvi kumsifia Kamhanda kwa kitendo cha vurugu na kusababisha mauaji ya Mwangosi, hoja ya kulifumua ni sasa.
 
Kama umechelewa vile? wenzio imani na jeshi la polisi tena nadhani na serikali yetu kwa ujumla ilisha potea siku nyingi.
 
Police + wanajeshi SIWAKUBALI kabisa, yaani hawana maana yoyote. Nikiwaona huwa nasikia kichefuchefu, Siwapendi KABISA.
 
  1. Polisi hivi sasa wanatembea na mafuvu ya vichwa vya watu kuwavizia watu wa kuwabambikizia kesi za jinai!
  2. Polisi sasa wanasafirisha magunia ya bangi kwa kutumia magari yao na kuyauza nchi za jirani kama hawana akili nzuri!
  3. Polisi wanashirikiana na magenge ya kusafirisha madawa ya kulevya!
  4. Polisi wanalinda mali zinazoingizwa kiharamu ambazo hazilipiwi kodi!
  5. Polisi wanaua raia kwa visingizio mbalimbali!
  6. ​nk
 
Tunawaita polisi kwasababu wanavaa Uniform na wanatembea na bunduki pamoja na virungu lakini mambo wanayoyafanya siyo ya kipolisi, Maana wanapora, wanaiba, wanafanya magendo, wanauza dawa za kulevya wanauwa raia, wanabambikizia watu kesi, kazi ndogo ya kutuliza ghasia ikiwashinda wanita jeshi sasa unaweza kujiula huko CCP moshi huwa wanaenda kupata mafunzo gani kama la kutuliza ghasia linawashinda mpaka jeshi wanaingilia kati.

vitendo viovu
Kwa vitendo hivyo viovu vinavyofanyw na jeshi la polisi vinanifanya nianze kufikiria huenda kile kikundi cha CCM cha ulinzi sasa wanaingizwa kujiunga na jeshi la polisi kupata mafunzo ya kupiga, na kutumia silaha nina mifano mingi inanifanya niamini hivyo.
kitendo cha polisi kuegemea upande mmoja wa chama tawala kukilinda na hata kusimamia maovu yanayofanywa na chama tawala. mfano kubambikizia viongozi wa upinzania kesi za ugaidi, kuuwawa kwa mwandishi wa habari kwenye mkutano wa chadema, vitendo hivi vinaonyesha jinsi gani jeshi la polisi linavyoongozwa na watawala wa ccm na kwa hali hii inanifanya niamini kuwa huenda hawa polisi tunaowaona mtaani hasa hawa wapya ni vijana wa ccm waliongizwa jeshi la polisi.

JWTZ kuingilia kati.
kitendo cha jwtz kuingilia kati kila mara jeshi hilo linapoonekana kushindwa kutuliza ghasia kunanipa shaka juu ya mafunzo ya jeshi la polisi uwezo wake.

Kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani jeshi la polisi lilivyo dhaifu katika kukabiliana na changamoto zinazokutana nazo, pia ni aibu kwa mkuu wa jeshi hilo IGP kwa jeshi lake kushindwa kufanya kazi zao mpaka wapate msaada wa JWTZ.

kitendo hicho kinanifanya niendelee kuamini kuwa huenda hawa polisi wengi ni vijana wa ccm waliongizwa huko ndio maana vurugu zikiwa kubwa wazazi wao wanaomba msaada wa JWTZ ili vijana wao wasipatwe na mazara.
SINA IMANI NA JESHI LA POLISI
 
Polisi ni majambazi wanajua michongo yote ya kijambazi na wao ndo washiriki kifupi polisi ni majambazi na majangili
 
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?

Pamoja na mapungufu makubwa waliyonayo, kwa kiasi fulani wamejitahidi kuzuiya uonevu na matatizo ya jinai yaliyokuwa yanafunywa na Polisi hasa wakati wa Awamu ya Tatu (matatizo kama ya kina Zombe). Aidha, wamejitahidi kuzuia njama kubwa zinazopangwa (Organized Crime). Wanajitahidi kufika kwenye matukio na kuchukua hatua ingawa wakati mweingine hawako effective sana na kwa eleimu kwa jamii pia wamejitahidi. Kwa ujumla ukilinganisha Idara hiyo wakati wa awamu ta Tatu kuna tofauti kubwa. Pia ukilinganisha utendaji wa Polisi ya Tanzania na wale wa nchi jirani kama Kenya utaona kuna afadhali kidogo kwa Polisi wa Tanzania. Pamoja na hayo yote, bado wana safari ndefu ya kwenda haswa kwenye suala zima la kutenganisha utendaji kazi wao na masuala ya siasa.
 
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?

kwakua uzi huu ulianza dec,nami nakumbushia yalojiri ndani ya mei 2013 tu,
-kusafirisha bangi kwa gari la polisi wakat hapo ukiripot uhalifu wanakwambia halina mafuta
-Kutembea na fuvu ambalo hulitumia kubambikia watu kesi(DUMILA MOROGORO)
-KUHUKUMU B4 HUKUMU YA MAHAKAMA
 
Polisi ni majambazi wanajua michongo yote ya kijambazi na wao ndo washiriki kifupi polisi ni majambazi na majangili
kwenye majangili hapo wanaohusika ni JWTZ,,,, ndo maana hata baadhi ya makanali ni majangili,,,,,na wengine walitajwa bungeni
 
Tunawaita polisi kwasababu wanavaa Uniform na wanatembea na bunduki pamoja na virungu lakini mambo wanayoyafanya siyo ya kipolisi, Maana wanapora, wanaiba, wanafanya magendo, wanauza dawa za kulevya wanauwa raia, wanabambikizia watu kesi, kazi ndogo ya kutuliza ghasia ikiwashinda wanita jeshi sasa unaweza kujiula huko CCP moshi huwa wanaenda kupata mafunzo gani kama la kutuliza ghasia linawashinda mpaka jeshi wanaingilia kati.

vitendo viovu
Kwa vitendo hivyo viovu vinavyofanyw na jeshi la polisi vinanifanya nianze kufikiria huenda kile kikundi cha CCM cha ulinzi sasa wanaingizwa kujiunga na jeshi la polisi kupata mafunzo ya kupiga, na kutumia silaha nina mifano mingi inanifanya niamini hivyo.
kitendo cha polisi kuegemea upande mmoja wa chama tawala kukilinda na hata kusimamia maovu yanayofanywa na chama tawala. mfano kubambikizia viongozi wa upinzania kesi za ugaidi, kuuwawa kwa mwandishi wa habari kwenye mkutano wa chadema, vitendo hivi vinaonyesha jinsi gani jeshi la polisi linavyoongozwa na watawala wa ccm na kwa hali hii inanifanya niamini kuwa huenda hawa polisi tunaowaona mtaani hasa hawa wapya ni vijana wa ccm waliongizwa jeshi la polisi.

JWTZ kuingilia kati.
kitendo cha jwtz kuingilia kati kila mara jeshi hilo linapoonekana kushindwa kutuliza ghasia kunanipa shaka juu ya mafunzo ya jeshi la polisi uwezo wake.

Kitendo hicho kinaonyesha jinsi gani jeshi la polisi lilivyo dhaifu katika kukabiliana na changamoto zinazokutana nazo, pia ni aibu kwa mkuu wa jeshi hilo IGP kwa jeshi lake kushindwa kufanya kazi zao mpaka wapate msaada wa JWTZ.

kitendo hicho kinanifanya niendelee kuamini kuwa huenda hawa polisi wengi ni vijana wa ccm waliongizwa huko ndio maana vurugu zikiwa kubwa wazazi wao wanaomba msaada wa JWTZ ili vijana wao wasipatwe na mazara.
SINA IMANI NA JESHI LA POLISI

itafika hatua tutahimili na mikiki ya JWTZ,now ni mara ta 2 wanaingia street tena mikoa tofauti,,,,,so kuwa na subira mdau
 
Back
Top Bottom