Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?


  • Total voters
    111
Kwa mwendo wa mauaji ya raia wasio na hatia unaofanywa na jeshi la polisi; nashindwa kuendelea kuwa na imani na chombo hiki,
Zamani wakati upinzani unaanza kushika kasi, walimfukuza afisa usalama wa taifa mstaafu na kummiminia risasi hadi akapoteza maisha, walotekeleza hilo walishaachiwa,
Hivi sasa imekuwa ni jambo la kawaida kwenye vyombo vya habari kusikia wakitangaza kuwa polisi wamemuua mtu waliyemuhisi kuwa ni jambazi.

Sasa kama wanaua kwa hisia tu; siku wakihisi kwamba kusanyiko fulani ni majambazi si wataua tu? Mwana JF wasemaje!
 
Sasa kipi kifanyike, toa mapendekezo yako ili kuzuia hali hiyo badala ya kulialia!
 
Hao jamaa wasubiri tu mda si mrefu chadema tunachukua na tunaanza na wale wanao waamuru mapolice kuua hovyo labda wakimbie nchi hii mapema na tunawajua.
Zamani wakati upinzani unaanza kushika kasi, walimfukuza afisa usalama wa taifa mstaafu na kummiminia risasi hadi akapoteza maisha, walotekeleza hilo walishaachiwa,
Hivi sasa imekuwa ni jambo la kawaida kwenye vyombo vya habari kusikia wakitangaza kuwa polisi wamemuua mtu waliyemuhisi kuwa ni jambazi.

Sasa kama wanaua kwa hisia tu; siku wakihisi kwamba kusanyiko fulani ni majambazi si wataua tu? Mwana JF wasemaje![/QUOTE]
 
Nadhani si jeshi la polisi la kulaumiwa issue hapa ni Serikali iliyopo madarakani kwani Polisi huwa wanachukua order kutoka kwa wakubwa wao.
Na cha kusikitisha jinsi system nzima ya sheria inavyopindishwa na hawa wanaoitwa wakuu,Juzi wale watu waliokamatwa kwa tuhuma za kumuua Mwenyekiti wa chadema Usa-r-River marehemu Msafiri Mmbwambo wameshaachiwa na hawana kesi ya kujibu eti ushahidi umeonyesha hawakuwa wahusika.Majamaa wapo mtaani tu hawana hata wasi.Imagine.....


Na itabidi Mheshiwa Nassary aje atupe update ya kesi ile na kama yupo aware kuwa watuhumiwa wote wameshaachiwa?

Hii ndiyo Bongo bana
.
 
Nadhani si jeshi la polisi la kulaumiwa issue hapa ni Serikali iliyopo madarakani kwani Polisi huwa wanachukua order kutoka kwa wakubwa wao.

Hapa hatupaswi kulaumu; inatubidi tutafute njia ya kuiondoa Serikali madarakani iwezekanavyo - ikibidi hata kabla ya 2015.
 
Something must be done kuwaonyesha Polisi kuwa raia hatukubaliani na vitendo vyao!
yaani full bored! wamempiga risasi mwandishi wa Tanzania Daima! wanamsingizia eti alikuwa alikuwa anapambana nao kwa kutumia panga!
cha ajabu hawakukamata hilo panga kama ushahidi! wamemua kijana mdogo wa watu eti wakituliza vurugu! kila kona mauaji!
 
Hata paka ukimbana zaidi kwenye kona hugeuza kibano, tuendako ni kubaya sana maana Utafika wakati raia watalazimika kulipa

visasi mitaani na hapo polisi walia na kusaga meno maana wanaishi mitaani wanatekeleza order za wanaoishi uzunguni kwa lugha nyepesi.
 
Mimi nilishasema hata majambazi wakiingia ndani kwangu ntapambana nao mwenyewe hadi dakika ya mwisho bila kuita polisi labda waje wenyewe, na kwa tabia za polisi wa bongo nasema hata nikute polisi anapambana na nyoka mie namsaidia nyoka, polisi wanakera hawa acha tu
 
Nadhani si jeshi la polisi la kulaumiwa issue hapa ni Serikali iliyopo madarakani kwani Polisi huwa wanachukua order kutoka kwa wakubwa wao.
Na cha kusikitisha jinsi system nzima ya sheria inavyopindishwa na hawa wanaoitwa wakuu,Juzi wale watu waliokamatwa kwa tuhuma za kumuua Mwenyekiti wa chadema Usa-r-River marehemu Msafiri Mmbwambo wameshaachiwa na hawana kesi ya kujibu eti ushahidi umeonyesha hawakuwa wahusika.Majamaa wapo mtaani tu hawana hata wasi.Imagine.....


Na itabidi Mheshiwa Nassary aje atupe update ya kesi ile na kama yupo aware kuwa watuhumiwa wote wameshaachiwa?

Hii ndiyo Bongo bana
.
na hii ndio hali ilyopelekea hata vibaka kuanza kubanikwa wakiwa wazima.

 
Jeshi letu la polisi lina matatizo makubwa sana na haya matatizo ni tokea jeshi hili lilipoundwa.

Muundo wa jeshi lolote la polisi utapekea jeshi hilo kuwa la kitaalam na kujitambua kuwa ni chombo pekee chenye kuaminika kulinda usalama wa raia na mali zao.

Pia muundo wa jeshi hilo utalifanya jeshi hili kutunga sera zake na namna ya kuzitekeleza, pia kutoa maamuzi kulingana na chagizo mbalimbali zinazotoka kwenye jamii ambayo ndio inawategemea.

Ntatoa mfano wa sehemu za muundo wa jeshi hilo na mojawapo ni idara ya habari. Idara ya habari ni tofauti na idara ya uhusiano au (directorate of public affairs) ambayo kazi yake ni kuelimisha jamii na kuishirikisha jamii kwenye mambo mbalimbali ambayo yanahusu uhusiano mwema kati ya chombo hicho na raia wake.

Idara hii au (Directorate of information) ina kazi ya kuelezea kitaalam namna uchunguzi au upelelezi wa kesi kama ya Dr Mwakyembe unavyoendelea na sio bwana Manumba kuja na taarifa mbovu kabisa ambayo ina lengo la kuwachanganya wananchi. Pia katika taarifa ambayo Manumba alitoa, palipaswa pia kuwepo mmoja wa wataalam ambao wanamshughulikia Dr Mwakyembe ambae nae angekuwa anamsaidia Manumba kufafanua mambo kadhaa kuhusu ugonjwa wa ngozi ambao unamsumbua Dr Mwakyembe.

Idara ingine ambayo inaundwa na mfumo imara wa jeshi hilo ni ile ya uendeshaji au (directorate of operations). Hii idara ni muhimu sana katika jeshi la polisi na uendeshaji wowote wa operesheni katika tukio lolote lile, ndio utatoa hasa picha halisi ya jeshi hilo kama limeundwa kukung'uta watu na hata kuua tu au la.


Kwa matukio ya taarifa mbovu ya DCI Manumba, vurugu za kule Songea na matokeo yake ambapo kuna raia wameuawa na mambo mengi tu yatayoweza kujaza sehemu hii inaonekana kabisa kwamba imani kwa jeshi hili inakuwa ni vigumu kujengwa au kufanyiwa ukarabati.

umeeleza vyema, na daima polisi ikipendwa basi ujue taifa hilo, viongozi, ni wakweli kwa wananchi wao na wanatekeleza kile walichowaahidi na kutatua matatizo yao pindi yanapojitokeza, kinyume cha hapo polisi hawezi kupendwa kamwe, Mf; suala la Mwakyembe lipo wazi yy mwenyewe hakuwahi kusema kuwa anaumwa sababu ,kawekewa sumu, bali rafiki zake kisiasa ndo walieneza hayo, na yy mwenyewe kukaa kimya, mwandishi wa habari kamuuliza Swali DCI juu ya ugonjwa wa Mwakyembe asijibu, aeleze siasa , alichojibu ndo lilikuwa jibu sahihi na hata MHmwakyembe alilithibitisha hilo, baada ya kupona kuwa tatizo lake halikuwa sumu,ktk jamii endapo Tanesco, Idara ya maji, hospitali, halmashauri na kwingineko haki isipotendeka fujo itatokea , polisi wataitwa na lawama zote zitabebwa na polisi. leo hii huko kwenye vyuo vya elimu ya juu, polisi ni wabaya kuliko , bodi ya mikopo, wakati bodi ni wabaya kuliko polisi.
 
[h=5]kweli serikali imeshindwa kuzuia ajali za barabarani ? eti wana mpango wa kujenga hospital ya majeruhi kibaha, hii ni kuwaambia madereva sababisheni ajali hospital ipo.[/h]
 
Limekisili kwa rushwa ni aibu kabisa, sasa wana fashion ya kuzunguka mjini na gari au bodaboda kuwanyanyasa wafanyabiashara na wao huwa wanadil na TRA, hata kama umepakia betr ya gari kwenye bodaboda wanakusumbua.
 
Ni muda mrefu sasa tangu kuwe na malalamiko mbalimbali kutoka kwa raia wa nchi hii juu ya utendaji na uadilifu wa jeshi la polisi. Jeshi la polisi limekuwa likituhumiwa kwa mambo mengi sana kama vile RUSHWA, UKANDMIZAJI WA HAKI ZA RAIA, KUSINGIZIA KESI, KUUA RAIA BILA HATIA na KUSHABIKIA SIASA kinyume na maadili ya jeshi hilo.Tuna mifano mingi sana ya ukiukwaji wao wa sheria na maadili yao ya kazi wenzetu hawa, ikiwa ni pamoja na ile ya jumla ambayo imeweza kuripotiwa na vyombo vya habari vya ndani na nchi na mifano mingine ikiwa hairipotiwi hata kwenye vyombo vya habari lakini tukiyaona, yakitutokea kwetu au kwa ndugu au jamaa zetu.

Kwa mfano, ndani ya mwaka huu pekee, jeshi la polisi limelalamikiwa kwa mambo makubwa katika maeneo mbalimbali kama vile, Mauaji yaa raia aliyesemekana alikuwa anauza magazeti wakati wa maandamano ya CHADEMA kule morogoro, mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi, kashfa ya Babarini Dar. mauaji ya wamachinga mwanza, Rushwa, na sakata lingine la ngara.

Lakini lilonisukuma ni hili jipya kabisa la majuzi kariakoo ambapo majambazi walivamia gari lililokuwa na watu waliokuwa wakipeleka fedha benki kiasi cha shlilng. milioni 150, ambapo jambazi mmoja alikamtwa aliwa na majeraha kidogo lakin jana tunaambiwa kafariki, na kwa mujibu wa raia walioshuhudia tukio wanadai kuwa kifurushi cha pesa kilidondoshwa chini na askari mmoja mnene alikiokota na kukiweka kwenye gari la polisi ambalo kwa wakati huo raia wanasema hawakutilia maanani kunukuu namba zake.Cha ajabu hadi sasa tunaambiwa zile pesa polisi hawajui zilipo.

Swala hili linaibua maswali mengi, na habari za chinichini zinadai kuwa polisi walienda kujawana pesa hizo maeneo ya jangwani, kwa haya na mengine mengi je polisi kwa nini sisi raia tuendelee kuwaamini? Je yule jambazi ambaye tulimuona akiwa na majeraha kidogo haiwezekani ikawa nyie mlimpe mateso makali ili afariki na kupoteza ushahidi wa ni wapi hasa pesa zimekwenda?

Na imekuwa ni kwaida kwa viongozi wa jeshi hilo kukanusha ukweli wa mambo na kuwa na ripoti za uongo, kaa mkijua haiwezi tokea ukweli ukashiundwa kwa uongo japo hata kama itachukua muda, imefika mahala imjisafishe raia tuanze kuwaamini tena, hebu fikiria raia waliojitokeza kupambana na majambazi wale halafu manafanya uhuni huu je tuendelee kuwapa ushirikiano, kiufupi polisi wamegeuka majambazi, wapolaji hata ukikamatwa na kitu chako wakaenda polisi kukifanyia uchunguzi hata ukupeleka ushahidi kudhibitisha umiliki wako wakikipenda kitu hicho utakiacha tu!
 
Ndo maana IGP anatakiwa aunde jeshi hili upya na kusimamia nidhamu!
 
atakayemchukia askar labda ana matatizo binafsi
kwanza anatulinda ucku mchana lakini haandamani kama wengine
analipwa mshahara wa kiasi tu lakini anaridhika
askari hana rushwa hata anayo lakini kiasi cyo epa na dowas
kama kuna mtu hana imani na askari wetu tumpe awe askari aone ugumu wake labda ataacha kulalamika
 
1. IGP kama IGP hana makosa: Jiulize wewe ukiteuliwa utafuata matakwa ya nani? Hata sijui kama Said Mwema alikua tayari kuwa IGP. Hata sijui kama alikua na mission ama vision yoyote. Alichoropolewa huko Nairobi akaambiwa shemejiee njoo bana uwe IGP. Bila kuulizwa kama ana uwezo au la. Bila kuulizwa kama ana nia au la. Bila kuangaliwa utendaji kazi wake hapo kabla.

THE PROBLEM IS WITH THE SYSTEM. Let us have a vetting committee..kila anayetaka kuwa IGP anakuwa vetted. Wana apply among the commissioners tunapata mtu mwenye nia na uwezo. Huyo hata akiharibu tunaweza kusimama tukasema atoke na anatoka.


2. Hali ya uchumi ya askari Polisi: lazima tukubali ni duni kupita maelezo. juzi nimekaa na jamaa mmoja wa JWTZ huyu ni Form Four....akaniambia posho yake ni 240,000/- na soon itakuwa 300,000/-.POSHO!!! Nikamuuliza baba yangu (SSGT wa polisi), Je mshahara wa konstebo form four failure ni how much akaniambia 290,000/- kabla ya makato.

Tujiulize je, ni kwa sababu kazi ya polisi ni ya kipuuzi hivyo au? Je mtu unayemlipa peanut unatarajia aproduce product ya quality ipi?

Chukulia mfano wa mbwa unayemfuga na kumpa makoko kama chakula (ndiyo 180,000/- per month ni ukoko tu) halafu unatarajia unapomfungua usiku abaki getini akikulinda dhidi ya wezi na majambazi. Kweli? Mbwa huyo kesho ukimkuta kwa jirani utamlaumu? Mbwa huyu ukiibiwa leo utamwona mbaya na kumuua?

Oh kabla sijasahau...askari Polisi wanakatwa GEPF/PSPF kwa ajili ya pensheni jambo ambalo JWTZ hawakatwi. Jamani hawa watu wanaishi nchi moja wanafanya kazi moja iweje wengine wajihudumie pensheni ilhali wenzao wanalipwa kutoka mfuko maalum wa Raisi?

Point yangu hapa ni: Kuwe na usawa kwenye hivi vyombo vya usalama..hakuna kilicho bora kuliko mwenzake

3. Posho: Posho za askari polisi zinatolewa ka asilimia. Mfano mzuri na unaouma ni wa posho ya pango...ebu niambie 15% ya 290,000/- ni sh ngapi??! Kwa askari anayeishi tuseme jiji la Dar anapata nyumba ya aina gani hapo? Kwanini posho hizi zisilipwe kutokana na market value?

4. Procurement: Jeshi la polisi (na hata majeshi mengine) linatumia fedha nyingi katika ununuzi wa magari ya maofisa wao. Naomba kuiba siri ya mama mmoja aliyekuwa akigombea post ya IGP huko nchini Kenya..alisema akiteuliwa atahakikisha kila ofisa anayestahili kuwa na gari anakopeshwa fedha kwa ajili ya kununua gari analotaka.

Hizo fedha nyingine zinanunua magari kwa ajili ya kazi hasa za kipolisi kama doria na hata kuongezewa kwenye bajeti ya mafuta. In this way hata atakapostaafu afisa huyu hatakufa kwa dhiki kisa alizoea dezo ya gari la ofisi. Anastaafu anaondoka na gari lake.



5. Mafunzo (Recruits Training): bajeti ya mafunzo ya Polisi siifahamu ila kwa trend ya askari tunaowaona mtaani inaonyesha ni ndogo hivyo hupitishwa tu ili wamalize but not ili waelewe.


- Naombeni sana Watanzania wenzangu na waandishi wa habari let us go deep kwenye research tujue hasa tatizo lipo wapi na tutoe solution yakinifu. Tuwe famous kwa kutoa solutions na sio kuonesha matatizo yalipo.

- Honestly Said Mwema namsifu maana ni kama mtu aliyekuwa amelala akaamshwa akambiwa kuna vita akapewa bunduki aongoze. He was not prepared for that. Tusimlaumu he has done a great deal kwa Jeshi la Polisi. Ndiyo alichofanya hakitoshi kwa kuwa kawekwa...sasa akitolewa si atawekwa mwingine? What will it change?


Let us fight then in unison on improving/changing:

A. The system of hiring officials in charge of the police force (Vetting)

B. The Training and Recruitment of Police recruits ( ref. Jeshi la Ujerumani)

C. The Welfare of the Police Force.

D. Priorities za procurement items.



Naomba kuwasilisha.

Mentor..Mtoto wa Polisi.
 
Kwa mauaji na mateso wanayofanya dhidi ya raia wasiokuwa na hatia sina imani kabisa na polisi. Kwangu mimi ni bora nikutane na simba mwenye njaa kuliko kukutana na polisi mwenye silaha. Hawakawii kusema aliuwa baada ya kurushiwa kitu chenye ncha kali au alikuwa anataka kumnyang'anya polisi bunduki au aliuawa katika majibizano ya risasi. Polisi 'wanamhoji' mtu mpaka anakufa utawaamini vipi?
 
Jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na tuhuma nyingi kwa kushindwa kuchukuwa hatua stahili na kwa wakati kudhibiti na kuzuia jinai mbalimbali. Mifano michache ni kama ifuatayo:

  1. Wizi wa EPA, Dowans, Kagoda, Meremeta, Tangold nk.;
  2. Sakata la mmoja wa wabunge kufanya vitendo vya kishirikina ndani ya ukumbi wa bunge ;
  3. Tuhuma kuwa vyombo vya dola vinafanya njama za kuwaangamiza viongozi na watu mashuhuri;
  4. Kutoa pongezi na zawadi kwa watuhumiwa wa rushwa na ujambazi walioko ndani ya jeshi hilo;
  5. Kutoa siri za wanaotoa taarifa nyeti kwa vyombo vya habari na mafisadi;
  6. Kutumia nguvu kubwa kupita kiasi kukabiliana na raia; nk
Je nini imani yako kwa jeshi la polisi?
7. Baadhi ya polisi kushiriki katika ujambazi!
 
Back
Top Bottom