Je, una imani na Jeshi la Polisi?

Una imani na utendaji wa Jeshi la polisi?

  • Total voters
    111
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri.. "Liars must have a good memory"
Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya kuuawa kwa kijana Yahaya Omary mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu Arusha. Polisi wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mguuni na kwenye ---- alipokua akijaribu kukimbia.

Lakini picha ya marehemu iliyoonekana baadae inaonesha kupigwa risasi ya tumbo. Sasa kwanini Polisi wamedanganya ni mguu na ----?? Wanataka kuficha nini?

Bila shaka Polisi walidhani picha ya mtuhumiwa akiwa kauawa haitaonekana.. hivyo wakaamua kudanganya ili kuhalalisha mauaji. Lakini hatimaye picha imeonekana akiwa kapigwa risasi ya tumbo, Polisi wameumbuka.

Pili, hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma si tumboni.

Lakini hii si mara ya kwanza jeshi la Polisi kuingia kwenye tuhuma za kuua watu wasio na hatia na kushindwa 'kujustify' mauaji hayo.

Mwaka 2006 aliyekua kaimu RPC wa mkoa wa Dar, Bw.Abdalah Zombe aliorganize mauaji ya wafanya biashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro na kusingizia ni majambazi. Akafika mbali zaidi na kudai walikua wanarushiana risasi na Polisi.!

Lakini ripoti ya Tume ya Jaji Kipenka ikawaumbua Polisi maana ripoti ilionesha watuhumiwa wote walikua wamepigwa risasi visogoni. Ikabainika pia si kweli kuwa walikua wakirushiana risasi na polisi.

Huwezi kurushiana risasi na Polisi then upigwe risasi kisogoni.. Jaji Kipenka akawaumbua Polisi kwa kueleza kuwa wafanyabiashara wale walifungwa kamba mikono na miguu, kisha wakafungwa vitambaa vyeusi machoni ndipo wakapigwa risasi.

Halafu baada ya kuhakikisha wameuawa Polisi wakawapora jumla ya sh. mili.200 na madini waliyokua nayo. Kisha Zombe akaita mkutano na waandishi wa habari akasema kuna majambazi yameuawa yakijaribu kurushiana risasi na Polisi.

Ukatili, ukatili, ukatili wa kiwango cha kutisha. Yani uwakamate watu wasio na hatia, uwafunge vitambaa usoni, uwapige risasi, kisha uwapore mali na fedha walizonazo.. halafu bado uwasingizie ujambazi.. Kwa kweli Mungu wetu ni wa huruma sana lakini hii dhambi sijui kama inasameheka.

Mazingira ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale yanafanana na mazingira ya kuuawa kwa kijana Yahya Omary anayedaiwa kulipua mabomu Arusha.
Kwanza inadaiwa alikua anakimbia, lakini risasi kapigwa tumboni. How comes? Mtu anayekimbia tulitegemea apigwe risasi mgongoni au maeneo ya nyuma ya mwili lakini si tumboni. Huu ni uongo wa kitoto kabisa.!

Polisi wanadai eti mtuhumiwa alikua mcheza karate na judo, hivyo alitumia mbinu zake za karate ili kuwakimbia Polisi.

Cha ajabu mtuhumiwa alikua hajafungwa Pingu mikononi wala miguuni. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo" halafu umsafirishe bila kumfunga pingu? Hizi ni hekaya za Abunuasi.!

Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu?? Uongo wa kitoto kabisa huu.!
Nashauri Rais Kikwete aunde tume kuchunguza mauaji ya kijana huyu kama alivyounda Tume ya Jaji Kipenka kuchunguza mauaji ya wale wafanya biashara wa Mahenge. Huenda kijana huyu ameuawa ili kupoteza ushahidi.!

Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.

Nimeona vyombo vingi vya habari vikiandika habari hii kwa ushabiki. Vingi vimeonesha kufurahishwa na mauaji ya kijana huyu. Gazeti moja limeandika "ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AUAWA".

Hili gazeti sijui kama lina Mhariri, maana hii si habari. Huwezi kusema "aliyelipua mabomu arusha..." wakati haijadhibitika kama ni kweli alihusika au lah.!

Yahaya alikua mtuhumiwa tu na angefikishwa mahakamani ukweli ndio ungejulikana. Huenda si yeye aliyehusika na mabomu na labda hata hajui lolote kuhusu mabomu.. Labda Yahaya alikua na ugomvi na kiongozi wa serikali ndo akaamua kumbambikia hii kesi.

Na chombo pekee cha kusema ukweli ni mahakama.. Lakini serikali kwa kujua kesi ikienda mahakamani wataumbuka na itajulikana Yahaya hakuhusika na mabomu ya Arusha wakaamua kukatisha maisha.

Wakamuua kikatili kabla kesi haijaenda mahakamani. Wawakamsingizia eti alijaribu kukimbia. Kivipi alijaribu kukimbia wakati kapigwa risasi ya tumbo.?
Lakini magazeti yamemhukumu.. yamemuita muuaji.. mrusha mabomu.. mengine yamemuita jambazi sugu..

Nayaogopa magazeti ya Tanzania. Ni magazeti hayahaya yaliyowahukumu wale wafanyabiashara wa Mahenge waliouawa na Polisi wa Zombe. Magezeti yakaandika "MAJAMBAZI KUTOKA MORO YAUAWA DAR."

Lakini ilipokuja kubainika hawakua majambazi magazeti hayohayo yakaandika "KASHFA NZITO JESHI LA POLISI; WADAIWA KUUA RAIA WASIO NA HATIA NA KUWABAMBIKIZIA KESI YA UJAMBAZI"

R.I.P Yahaya Omary, binafsi siwezi kukuhukumu kama magazeti yanavyofanya, maana sijui kama ni kweli ulihusika na mabomu ya Arusha au lah.
Labda mahakama ingeweza kutuambia ukweli.. lakini kwa kuwa umetangulia MUNGU pekee ndio anajua ukweli.

Pumzika kwa amani Yahaya.. Hata waliokuua ipo siku nao watakufuata. Duniani sote tunapita.. hakuna atakayeishi milele.. ipo siku ukweli utafahamika na itakuwa kilio na kusaga meno kwa wote walioshiriki mauaji haya ya kinyama dhidi yako.!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.

Attachments

  • 1011245_725102064248155_4921767149713166530_n (1).jpg
    1011245_725102064248155_4921767149713166530_n (1).jpg
    38.4 KB · Views: 572
ninayo imani kubwa sana na mapolisi wadogo wadogo hawa wa kuanzia inspectors kuja hadi chini kwa constable , MATATIZO YA HAWA NI NJAA TU , BALI SINA IMANI KABISA NA WALA SITAKUJA KUWA NA IMANI NA VIONGOZI WA JESHI LA POLISI , YAANI WALE WOTE WALIO JUU YA HAWA NILIOWATAJA HAPA .
 
Hii ni hatari, ccm na jeshi la polisi wanatafuta pakutupia kashifa inayowakabili ya kuuwa na kutesa wapenzi na wanachama

wa chdema kwa kumsingizia kijana wakiislam marehem yahaya. Mungu awalaani wote wanaosingizia raia wasio na hatia na kuwauwa.

attachment.php
 
Hivi huyu Marehemu alikuwa tayari yupo Sero au ndo ilikuwa mara ya kwanza kukakatwa....Hapo issue ni kwa nini mtuhumiwa wa Ugaidi hakufungwa PIGU. Kuna kitu yawezekana kitakuwa kimefichwa."Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu" Hii hapa inatupa kuamini hiki alichokiandika mtoa mada kwamba "Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.
 
Halafu nisipoelewa mimi ni kuwa inakuaje eti Marehemu akachukia
1. Makanisa na Maaskofu
2.Misikiti na Mashehe
3.Vyama vya siasa(CHADEMA)
4.Watalii
Maana tumeambiwa marehemu alikuwa ni muhusika wa matukio hayo yote
Naomba mnieleweshe jamani
 
Great thinker..thumb up!
 
Halafu nisipoelewa mimi ni kuwa inakuaje eti Marehemu akachukia
1. Makanisa na Maaskofu
2.Misikiti na Mashehe
3.Vyama vya siasa
4.Watalii
Maana tumeambiwa marehemu alikuwa ni muhusika wa matukio hayo yote
Naomba mnieleweshe jamani
hata mm nimeshangaa sana yeye ndo amehusika na matukio yote haya bado wamemuuwa kwa sababu alikuwa anataka kuwatoroka polisi chini ya ulinzi mkali hii aibu kubwa sana kwa jeshi la polisi
 
Hawakuanza leo hawa..yalianza zamani sana..wakaja wakina zombie, yaliomkuta Ponda na yule mwandishi wa chanel ten alouawa na hawa majanjaweed!
Ipo siku ukweli utawaumbua tu..na hawa mapoliccm wenye akili za kushikiwa na kutumika bila ya kuhoji wala kuelewa sababu.aisee inatisha..
Big up mkuu PISTO LERO kwa kuleta mada
 
Hivi huyu Marehemu alikuwa tayari yupo Sero au ndo ilikuwa mara ya kwanza kukakatwa....Hapo issue ni kwa nini mtuhumiwa wa Ugaidi hakufungwa PIGU. Kuna kitu yawezekana kitakuwa kimefichwa."Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu" Hii hapa inatupa kuamini hiki alichokiandika mtoa mada kwamba "Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.
hii itaingia kwenye rekodi za duniani
 
Naomba tumuachie yote Mwenyezi Mungu mana atawahukumu wote na wengi watenda maovu wanaamini kua maisha ya duniani ni ya milele na hamna kufa wala kwenda kokote na ndio mana wengine wanajilimbikizia mali lyk kama wakifa wataondoka nazo.

Tumuachie yote Mungu
 
BIG UP sana PISTO LERO kwa kuleta uzi huu uliojaa hali halisi ya Uhuni unaofanywa na jeshi pumbavu la polis linaloua watu wasio na hatia kwa kuwatetea wakubwa wao ambao ni magaidi no1.. Mungu akujalie maisha marefu..kuanzia sasa uitwe msema kweli..tunawahitaji sana watu kama wewe kuliokoa Taifa hili lilititia kwenye tope yowevu...
 
hivi huyu mtuhumiwa alikua mikononi mwa polisi kwa siku ngapi?
jee alishapelekwa mahakamani kushtakiwa? au hata kutajwa kesi yake?
kama alishapelekwa mahakamani huyu anakua chini ya magereza , jee kuna kibali cha mahakama kuruhusu polisi kumbeba ?
tumeona mara nyingi washukiwa wa ugaidi wanachukuliwa wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi na pingu za miguu na mikono na pamoja na mateke na marungu
kwa polisi wetu wanavopenda kutesa hasa waislam sidhani huyu kama alikua na nguvu tena za hata kutembea, sote tunaelewa ni kina uamsho walivo onesha usaha matakoni kwao.hiyo huyu mpaka hapo kukubali ati ana bomu ana enda kuwaonesha basi kichapo alichopata ni cha paka mwizi
polisi walikuisudia kufanya mauaji period....
 
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri.. "Liars must have a good memory"
Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya kuuawa kwa kijana Yahaya Omary mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu Arusha. Polisi wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mguuni na kwenye ---- alipokua akijaribu kukimbia.

Lakini picha ya marehemu iliyoonekana baadae inaonesha kupigwa risasi ya tumbo. Sasa kwanini Polisi wamedanganya ni mguu na ----?? Wanataka kuficha nini?

Bila shaka Polisi walidhani picha ya mtuhumiwa akiwa kauawa haitaonekana.. hivyo wakaamua kudanganya ili kuhalalisha mauaji. Lakini hatimaye picha imeonekana akiwa kapigwa risasi ya tumbo, Polisi wameumbuka.

Pili, hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma si tumboni.

Lakini hii si mara ya kwanza jeshi la Polisi kuingia kwenye tuhuma za kuua watu wasio na hatia na kushindwa 'kujustify' mauaji hayo.

Mwaka 2006 aliyekua kaimu RPC wa mkoa wa Dar, Bw.Abdalah Zombe aliorganize mauaji ya wafanya biashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro na kusingizia ni majambazi. Akafika mbali zaidi na kudai walikua wanarushiana risasi na Polisi.!

Lakini ripoti ya Tume ya Jaji Kipenka ikawaumbua Polisi maana ripoti ilionesha watuhumiwa wote walikua wamepigwa risasi visogoni. Ikabainika pia si kweli kuwa walikua wakirushiana risasi na polisi.

Huwezi kurushiana risasi na Polisi then upigwe risasi kisogoni.. Jaji Kipenka akawaumbua Polisi kwa kueleza kuwa wafanyabiashara wale walifungwa kamba mikono na miguu, kisha wakafungwa vitambaa vyeusi machoni ndipo wakapigwa risasi.

Halafu baada ya kuhakikisha wameuawa Polisi wakawapora jumla ya sh. mili.200 na madini waliyokua nayo. Kisha Zombe akaita mkutano na waandishi wa habari akasema kuna majambazi yameuawa yakijaribu kurushiana risasi na Polisi.

Ukatili, ukatili, ukatili wa kiwango cha kutisha. Yani uwakamate watu wasio na hatia, uwafunge vitambaa usoni, uwapige risasi, kisha uwapore mali na fedha walizonazo.. halafu bado uwasingizie ujambazi.. Kwa kweli Mungu wetu ni wa huruma sana lakini hii dhambi sijui kama inasameheka.

Mazingira ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale yanafanana na mazingira ya kuuawa kwa kijana Yahya Omary anayedaiwa kulipua mabomu Arusha.
Kwanza inadaiwa alikua anakimbia, lakini risasi kapigwa tumboni. How comes? Mtu anayekimbia tulitegemea apigwe risasi mgongoni au maeneo ya nyuma ya mwili lakini si tumboni. Huu ni uongo wa kitoto kabisa.!

Polisi wanadai eti mtuhumiwa alikua mcheza karate na judo, hivyo alitumia mbinu zake za karate ili kuwakimbia Polisi.

Cha ajabu mtuhumiwa alikua hajafungwa Pingu mikononi wala miguuni. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo" halafu umsafirishe bila kumfunga pingu? Hizi ni hekaya za Abunuasi.!

Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu?? Uongo wa kitoto kabisa huu.!
Nashauri Rais Kikwete aunde tume kuchunguza mauaji ya kijana huyu kama alivyounda Tume ya Jaji Kipenka kuchunguza mauaji ya wale wafanya biashara wa Mahenge. Huenda kijana huyu ameuawa ili kupoteza ushahidi.!

Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.

Nimeona vyombo vingi vya habari vikiandika habari hii kwa ushabiki. Vingi vimeonesha kufurahishwa na mauaji ya kijana huyu. Gazeti moja limeandika "ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AUAWA".

Hili gazeti sijui kama lina Mhariri, maana hii si habari. Huwezi kusema "aliyelipua mabomu arusha..." wakati haijadhibitika kama ni kweli alihusika au lah.!

Yahaya alikua mtuhumiwa tu na angefikishwa mahakamani ukweli ndio ungejulikana. Huenda si yeye aliyehusika na mabomu na labda hata hajui lolote kuhusu mabomu.. Labda Yahaya alikua na ugomvi na kiongozi wa serikali ndo akaamua kumbambikia hii kesi.

Na chombo pekee cha kusema ukweli ni mahakama.. Lakini serikali kwa kujua kesi ikienda mahakamani wataumbuka na itajulikana Yahaya hakuhusika na mabomu ya Arusha wakaamua kukatisha maisha.

Wakamuua kikatili kabla kesi haijaenda mahakamani. Wawakamsingizia eti alijaribu kukimbia. Kivipi alijaribu kukimbia wakati kapigwa risasi ya tumbo.?
Lakini magazeti yamemhukumu.. yamemuita muuaji.. mrusha mabomu.. mengine yamemuita jambazi sugu..

Nayaogopa magazeti ya Tanzania. Ni magazeti hayahaya yaliyowahukumu wale wafanyabiashara wa Mahenge waliouawa na Polisi wa Zombe. Magezeti yakaandika "MAJAMBAZI KUTOKA MORO YAUAWA DAR."

Lakini ilipokuja kubainika hawakua majambazi magazeti hayohayo yakaandika "KASHFA NZITO JESHI LA POLISI; WADAIWA KUUA RAIA WASIO NA HATIA NA KUWABAMBIKIZIA KESI YA UJAMBAZI"

R.I.P Yahaya Omary, binafsi siwezi kukuhukumu kama magazeti yanavyofanya, maana sijui kama ni kweli ulihusika na mabomu ya Arusha au lah.
Labda mahakama ingeweza kutuambia ukweli.. lakini kwa kuwa umetangulia MUNGU pekee ndio anajua ukweli.

Pumzika kwa amani Yahaya.. Hata waliokuua ipo siku nao watakufuata. Duniani sote tunapita.. hakuna atakayeishi milele.. ipo siku ukweli utafahamika na itakuwa kilio na kusaga meno kwa wote walioshiriki mauaji haya ya kinyama dhidi yako.!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!

Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.

Maadam hakuna uchunguzi utao fanyika basi tuifanyie postmorten hii picha..
angalia mabaka na alama za mateso maeneo ya tumbo lake
ukiukuza utagundua ana majaraha na michubuko mingi kwenye mwili wake.
jee alishauawa wakati wa kuteswa?
hapa kuna shaka aliteswa akakata roho then wakachukua maiti wakairushia marisasi na kudanganya alitaka kuawa.
postmorten inaweza kuonesha muda gani alifariki.
jamaa zake wasikimbilie kuzika walete uchunguzi wa maiti ufanywe na watu wa nje.itajulikana kama alikufa wakati gani
 
HAPANA IPO HIVI KWANINI WATANZANIA WAMEPOTEZA IMANI KWA JESHI LA POLISI?

Kumekuwepo na matamko mbalimbali kwa Jeshi la Polisi juu ya utendaji kazi kwa raia , kwanini jeshi limepoteza imani kwa raia ambao ndio jukumu lake kubwa kuwalinda raia hao , katika mkutano na Rais Samia leo amewaambia kuwa Jeshi la Polisi limepoteza umalidadi wote na kufanya kwa kuwakandamiza raia ambao ndio msingi wa wao kuwepo kazini .

Leo katika la mtu asiyejulikana ameua askari wawili lakini raia waliokuwa wapo katika daladala , bodaboda na wale waliopo katika vituo vyao vya kazi hajaangaika nao , hii imeonyesha hali halisi baina ya imani na polisi imefikia hatua watu wanafuraia askari kuuawa.

Hii inatafakarisha nini kwa usalama wa taifa letu, je Raia wanaweza kuungana na adui katika kukamilisha misheni, kwasababu raia wamewachoka polisi?
 
Back
Top Bottom