Je umewahi kusikia adhabu kama hii kwa shule za msingi?

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,458
3,209
Waalimu wa shule ya msingi Mbezi Ndumbwi iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, wanawaadhibu wanafunzi wasiofanya majaribio ya kulipia wakati wa asubuhi (speed test) kwa kuwakalisha chini (sakafuni) siku nzima.
Wakati wa kuingia darasani asubuhi, wanafunzi wa darasa la 4, 6 & 7 waliofanya mtihani wa asubuhi, huitwa majina na kuruhusiwa kuingiza madawati watakayokalia. Wanafunzi wasiofanya mtihani hupewa adhabu ya kukaa chini siku nzima huku madawati yakibaki nje bila kutumiwa.
 
nchi hii kila mtu anajiamulia lake, sasa hapo kosa la watoto au wazazi? na ile ruzuku ya wanafunzi ina kazi gani? au wizara haiipi shule ruzuku? au kamradi kwa walimu?
 
Huu ni mradi wa waalimu! Wazazi wamelipia madawati. Wanafunzi wengine wanalazimika kukaa chini kwa kukosa madawati, huku madawati hayatumiwi. Mwalimu Mkuu akiulizwa anakuwa mkali kama mbogo, anawadharau wazazi, shule inapaoromoka, .....
 
Back
Top Bottom