Je! umaskini unasababishwa na nini?

Mimi nimejibu swali la "chanzo cha mtu kuitwa maskini" na si lazima awe fukara, kumbuka umaskini na ufukara ni vitu tofauti, unaweza kuwa na mali lakini huwezi kujisaidia kwa mali yako, kwa hiyo wewe ni maskini na wakuonewa huruma. Ufukara ni kitu kingine, sasa kama mnatalka tuibadili mada haya, na ndio maana nikatowa mfano wa niliouona Saudia. Ufukara ni kitu kingine, mfano mzuri ni Tanzania, tunaitwa nchi maskini, lakini tuna mali za kutosha, kwa nini? ni wakuonewa huruma umaskini wetu, kwa ujinga wetu, lakini si wakukosa mali na rasilmali.

Twende pole pole kidogo ndugu yangu hao kina mama wanaovaa gold kwanini wanaomba hawawezi kupata chakula, kazi au hawawezi kufanya kazi...? na kwa definition ya kwamba unaweza ukawa ni maskini wa macho, mume, mtoto akili n.k. (basi tunaweza tukasema kila binadamu ni maskini sababu hakuna mtu ambae ana kila kitu..)

kwahiyo ili twende vizuri naomba kwanza tu-dadavue maana ya ufukara na umaskini.... (definition..) alafu uniambie kwanini wale mama wa Kule Saudia ni maskini..?
 
Kwani huyu jamaa katakajua maana ya umaskini au jinsi ya kujiendeleza maana mi hata sielewei haya mambo ya maduka na mikopo yanahusiana vipi kwenye tafsiri ya umaskini anyway nauliza tu.
Ndugu hiyo ilikua ni example tu, ya namna gani kua proactive kunasaidia kubadilisha maisha. Haitoshi kufikiria tofauti, unatakiwa pia kuact tofauti na nikaweka mfano (ukiangalia hapo juu utaona kuna (EX:)
 
kwa mawazo yangu unaskini unatokana na vitu viwili vikubwa kwanza ubinafsi, hatuko tayari kugawana tulicho nacho hata kama ni mawazo tu! na tukiwa kwenye nafasi huna sababu ya kuangalia mwingine itakuwaje no matter yu win. chapili hatujiamini mawazo tunayo shule tunazo na kila kitu tunach lakin hatuko tayari kujaribu na kutoka tulipo ndo mana kila kukicha tunatafuta kazi mpya ya maslahi mazuri.
haya mawili tukiyaweza tunaweza kusonga mbele.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom