Je ulishawahi pata tatizo kama hili?

Nyati

JF-Expert Member
Mar 6, 2009
2,489
1,813
Heshima mbele wanajamii,

Nimepata tatizo hili juzi na leo. Nina usafiri / gari aina ya Suzuki escudo. Juzi nilipowasha asubuhi nikajaribu kuweka "Reverse gear" ikakataa kabisa. Basi likasukumwa gari nikaendelea. Jana halikutokea hata kidogo. Leo asubuhi halikujitokeza pia, Lakini jioni ikawa kama juzi.
Mafundi wametoa sababu tofauti kama Petrol yenye maji, baridi, bearing zimekufa, Oil ilikuwa mbovu (nilifanya service jumamosi iliyopita), n.k. Lakini yaonekana wengi hawana uhakika.
Kama umeishawahi pata kitu kama hiki naomba ushauri na solution kama mwafahamu.
Natanguliza shukrani.
 
Pole, mimi pia imewahi nitokea gari yangu ni Mitsubishi GDI automatic, na nilikanyaga mafuta zaidi lakini wapi, nikarudisha P nikajaribu tena ikakataa, nilipomwambia fundi wangu akassema yawezekana pipe zinazosukuma mafuta ndio zina matatizo. Amerekebisha na sasa iko poa.
 
Pole ndugu, ila angalia hao mafundi wako, wengine njaa watakuleteaugonjwa uso kuwapo kwenye gari yako. Yaani mara nyingi huwa wanafanya kubabia tu, siyo kwamba wanajua,

ni sawa na mafundi wa computer, walio wengi ukimpa tu, anakimbilia kukwambia motherbody imekufa hata kama ni ka fuse tu ka power! ( angalizo tu mkuu)
 
Magari ya sasa hivi yote yana computer diagnostic terminals.Mafundi wa mitaani watakulia hela yako tu bila hata wao wenyewe kulijua hilo.Watafute wataalam wenye hizo diagnostic computers kabla hujua system ya gari lako.
 
umefanya service wapi? Jaribu kufanya service pale total shekilango. wale jamaa wana oil za uhakika. kwa hiyo kama ni oil watakusaidia.
 
Engine Oil haina uhusiano na gear.
Unamaanisha haiingii gear ya reverse au gear inaingia lakini gari haitembei(nyuma) ukikanyaga mafuta huku engine inachanganya?
 
Engine Oil haina uhusiano na gear.
Unamaanisha haiingii gear ya reverse au gear inaingia lakini gari haitembei(nyuma) ukikanyaga mafuta huku engine inachanganya?

Nashukuru kwa msaada wenu na mawazo yenu wakuu. Gari ni Automatic. Pia tatizo ni kuwa gear nyingine zinafanya kazi vizuri bali ile ya "Reverse' tu ndiyo ina matatizo niliyoeleza (gear inaingia bali gari haitembei) Leo tatizo halikujitokeza kabisa.

Pia naomba anwani ya hao watumiao "Computer" Mimi nafanyakazi hapa Dar Es Salaam (CBD), na makazi ni Kibaha, Pwani.
 
Cheki level ya transmission fluid yako, zaidi ya hapo utakuwa na tatizo kwenye gearbox(transmission) nadhani.

I would first look at the automatic transmission fluid level and make sure it is to the full line.

Most cars require that the engine be running and at normal operating temperature when you check the transmission fluid level. It might tell you how to do it on the transmission dipstick itself.
 
Gearbox ya automatic iko a bit complicated maana ni electronic. Problem hiyo inasababishwa na uharibifu kwenye clutch plates zilizoko ndani ya hiyo gear box. Ni mafundi wachache wanaweza kurekebisha lakini inatengenezeka fresh tu. Just look for the proper mechanics, kuna mmoja namfahamu anaishi Kigoma, itakuwa gharama kumtegemea huyo.
 
Back
Top Bottom